Friday, December 2, 2016

SERIKALI YASHAURI MAJINA YA WAHASIBU WEZI YAWEKWE HADHARANI


 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

 Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
 Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
 Katika hafla ya kufungua kituo hicho nyama choma zilikuwepo ingawa mimi sikubahatika kupata walau finyango moja.
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na 
wageni waalikwa.
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wengine akitoka kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
 Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
 Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani 
kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
 Mkutano ukiendelea.
 Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa bodi ya NBAA na Mfuko wa GEPF
Picha ya pamoja.


Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na  Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.

"Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.

Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.

"Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.

Aliwataka wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.

Mpango alisema kuwa serikali itaendelea kuwatumbua watumishi wasio waaminifu na wahasibu bila ya kumuonea muhusika huruma na kuwa atakayebainika atapelekwa mahakama ya mafisadi iliyofunguliwa.

 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA Pius Maneno alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia sh. biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia kumbi hivyo ujenzi wa kituo hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa kitakuwa ni chanzo cha mapato.

Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.

Alisema awali walikadiria ujenzi huo ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14 lakini kutokana na sababu mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh. bilioni 33 zaidi ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.

Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi aliishukuru serikali kwa ushirikiano na mifuko ya jamii na NBAA  hasa katika suala zima la kusukuma maendeleo ya nchi ikiwa na kuzitaka taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho cha kimataifa ili kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.


 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake Dk.Elihuruma Mangawe (katikati), akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick Goodluck.
 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi uliompa nafasi hiyo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano huo.
Usikivu katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.

Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.

Katika nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey Swai aliibuka kidedea dhidi ya Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura tisa zilikataa ambapo katika nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa wawili Elizabeth Nchimbi aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.

Katika nafasi ya Mtunza Fedha licha ya kuwepo na ushindani makali aliyeibuka mshindi ni Mwanahamisi Hassan ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya mgombea mwenzake Violeth Shirima aliyepata kura 24.

Nafasi ya Katibu wa Mipango ilikwenda kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata kura 38 dhidi ya Othman Shem aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi na Dismas Vyagusa wakishinda nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.


Wakati wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi. Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu ya watu wake ni vijana hivyo wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi kushawishi wengine kuhuisha maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku huku wakitunza mazingira. Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa mengi wakati yale ya Milenia yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema kwamba suala si uwingi wa malengo bali maana yake na haja ya utekelezaji. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema MDGs (Malengo ya Millennia) iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake kunahakikisha uwapo wa maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea sana mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Alisema ni matumaini yake kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto hizo za sasa za dunia. Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na wanachuo hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya sasa na kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo na mabadiliko.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.

Kwa kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa asilimia 75 ya vijana wanaishi vijijini, itakuwa heri kama walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa kupeleka salamu vijijini ili kukabiliana na tatizo la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanafumua misimu ya kilimo na upatikanaji wa mvua. Kushirikisha vijana ni suala la msingi sana, hasa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini ambako malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema Kidai Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia (Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Amesema amefurahishwa mno na mpango huo wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa basi atahakikisha anawaelimisha wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo hayo. Akirejea mazungumzo ya mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake. Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko wa vijana wa kutaka kujua malengo hayo na ni imani yake kwamba kwa kuwakujua wao basi jamii itaerevuka mapema zaidi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya wakati wa semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro akiuliza swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni hapo, Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani) wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).



Mmoja wa washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Pichani juu na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (hayupo pichani).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Manafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss Mbeya 2016, Eunice Robert.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa mabalozi hao.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya wakiwa wameshikilia baadhi ya SDGs.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akielezea mipango aliyonayo ya kuinua uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia) nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: 'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.
-- Zainul A. Mz

No comments :

Post a Comment