Wezi
walivunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa mshambuliaji wa
Manchester City Carlos Tevez viungani mwa mji wa Bueno Aires nchini
Argentina siku ya Jumapili na kuiba wakati nyota huyo alipokuwa nchini
Uruguay kufunga ndoa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa
Tevez hakuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu wizi huo hivyobasi
haijulikani ni nini kilichoibiwa.
Tevez na mke wake tayari wameondoka na kuelekea Mexico kwa fungate yao.
Polisi wanasema kwamba waligundua
kuhusu wizi huo siku ya Jumanne baada ya kuwaona wanahabari
wamekusanyika nje ya nyumba hiyo ya nyota huyo wa Argentina.
Wanasema kuwa wezi wengi waliingia
katika nyumba hiyo ambayo Tevez na familia yake walikuwa wamekodi huku
wakisubiri nyumba yao ambayo ilikuwa inafanyiwa ukarabati.
Inadaiwa wezi hao waliingia nyumba hiyo kupitia eneo ambalo ukarabati huo ulikuwa ukifanywa.
Baada ya Tevez kuarifiwa kuhusu wizi huo, alirudi nyumbani kwake kwa helikopta .
Aliukuta mlango wa nyumba yake uko wazi huku vitu vikiwa vimepekuliwa.
Tevez baadaye alisafiri kuelekea Mexico kama alivyopanga kwa fungate yake na mpenziwe wa utotoni Vanesa Masilla.
Wawili hao waliokutana wakiwa na
umri wa miaka 13 na ambao wana wasichana wawili, walifunga ndoa katika
sherehe ya kawaida siku ya Ahamisi mjini Bueno Aires.
No comments :
Post a Comment