Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo
wakati alipokutana na ujumbe kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani
(AWEB) kushoto.Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura,
Mhandisi Manyiri Isack na Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na
Mifumo ya Kijiografia Adolf Kinyero.Ujumbe huo umekuja kujifunza mambo
mbalimbali ikiwemo mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) na
kutambulisha Teknolojia mpya ya mashine ya Kuandikisha Wapiga Kura.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango
na Operesheni wa Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Lee Ju-Hwan
(katikati) akimueleza jambo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani wakati walipotembelea Ofisi za NEC
jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mtafiti wa chama hicho, Moon Jueun.
Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga
Kura, Mhandisi Manyiri Isack (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani
(katikati) kamera kwenye mashine ya kuandikisha wapiga kura wakati
ujumbe kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) ulipotembelea
Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kulia ni Mtafiti wa chama
hicho, Moon Jueun, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni, Lee
Ju-Hwan, Mtaalamu wa Uchaguzi Park jae Sung kutoka AWEB
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akiweka kidole
kwenye mashine ya kuandikisha Wapiga kura huku Mkuu wa Sehemu ya
Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia Adolf Kinyero akishuhudia.
Kulia ni Mtafiti wa Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Moon
Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park jae Sung (aliyevaa miwani).
Mtaalamu
wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae
Sung (aliyeshika mashine ya kusajili wapiga kura) akieleza utendaji kazi
wa mashine hiyo kwa baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) (kulia).
Mkuu
wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Adolf Kinyero (kulia) akimuonesha Mtaalamu wa
Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung
(katikati) na Mtafiti wa Chama hicho, Moon Jueun, jinsi BVR inavyofanya
kazi.
Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama
cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (katikati) akiwaeleza
baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kifaa
kinachotumia Teknolojia ya Kuandikisha wapiga Kura.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (wa tatu kushoto) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi
Duniani (AWEB).Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na
Operesheni, Lee Ju-Hwan, Mtafiti, Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi,
Park jae Sung.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura,
Mhandisi Manyiri Isack na Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na
Mifumo ya Kijiografia, Adolf Kinyero.
Mashine
inayotumika kuandikisha Wapiga kura inayotumia Teknolojia ya Kisasa
ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejifunza jinsi mashine hiyo
inavyofanya kazi.
Picha na Hussein Makame, NEC.
………………………….
Christina Njovu, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC
imepokea ujumbe Taasisiya Tume za Uchaguzi Duniani(AWEB)
uliokujakujifunza na kubadilishana uzoefu katika masualambalimbali ya
uendeshaji Uchaguzi.
Ujumbe huoumekujakujifunza kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masualambalimbali ya uendeshaji
Uchaguzi nchiniikiwemomatumizi ya vifaa vya kuandikishiawapigakura.
Mkurugenzi wa Mipango na
OparesheniBw. Lee Ju-Hwan alisema kuwa yeye na ujumbe wake
wamekujakubadilishana uzoefu katika technolojiaya Kuandikisha Wapiga
Kura.
Ujumbe huoumekutanana Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na kufanya
mazungumzonayeofisinikwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa
Menejimenti ya tume hiyo kutembeleaofisimbalimbali za Tume hiyo na
kujifunza.
Wakiwa katika kikao na baadhi ya
Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ujumbe huo wa watu
watatuulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR)
inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyowezakuandikisha Wapiga Kura wengi
kwa kutumiamashinetechnolojiahiyo nachangamoto zake.
Aidha ujumbe huoumekuja na aina
mpya yatechnologia ambayo inauwezo wa kuandikisha Wapiga Kura, kutuma
taarifa za Wapiga katika kanzidata kutoka katika kituo cha
kujiandikishia na kuhakiki Wapiga Kura siku ya Uchaguzi .
Mashine hiyo ambayo
nindogoukilinganisha na ile BVR inauwezo wa kutumiwa na
mtummojaambayeatawezakumuandikisha Mpiga Kura katika hatua zote hadi
kupata kitambulisho cha mpiga Kura na inabebeka kirahisi.
Ujumbe huoumeongozwana Mkurugenzi
wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa
Uchaguzi Park Jae Sumg.
Technologiahiyo
mpyainawezakurahisishautendaji kazi katika masuala ya uandikishajiwapiga
Kura, kuhakikiwapigakura na kutuma taarifa katika kanzidara.
No comments :
Post a Comment