Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipokea Tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi
Mkuu Bw. Eliud Sanga wa ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka 2015 kutoka
kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Shogolo Msangi.
LAPF iliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA
Pro. Isaya Jairo kwa ushindi wa kwanza wa ufungaji bora wa mahesabu ya
Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Tuzo hizo zilitolewa tarehe 03
Disemba, 2016.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko Bw.
John Kida akiwa ameshikilia Tuzo, pamoja nae ni timu ya Kurugenzi ya
Fedha ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo ilifanikisha ushindi huo wa
ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka wa fedha 2014/15 LAPF imekuwa
mshindi wa kwanza mara sita kati ya mara nane tangu kuanzishwa kwa Tuzo
hizo zilizoasisiwa na NBAA mwaka 2008.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF Bw. John Kida aliyeshikilia Tuzo katika picha ya pamoja
na watumishi wa Mfuko mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya ushindi wa
kwanza ya Ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Hafla ya kukabishi tuzo hizo zilifanyika tarehe 03/12/2016 jijini Dar
es Salaam.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washindi mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao.
No comments :
Post a Comment