Mzee wa Kijiji cha Murangi- Musoma
Vijijini, Clifford Biseko (kulia) akifungua rasmi mkutano wa kujadili
uchumi na maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni
Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo.
Baadhi ya wananchi wa Musoma
Vijijini waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Mbunge wao, Profesa
Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo akitambulisha watendaji mbalimbali kutoka kwenye halmashauri hiyo.
Madiwani wa Musoma Vijijini
wakijitambulisha wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya
Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wadau wa maendeleo ambao pia ni wazaliwa wa Musoma Vijijini lakini wanaishi nje ya hapo wakijitambulisha.
…………………
Wananchi wa Jimbo la Musoma
Vijijini wamempongeza Mbunge wao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo kwa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ndani ya
mwaka mmoja.
Pongezi hizo zimetolewa na
wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na
Uchumi ya jimbo uliofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Murangi,
Musoma Vijijini na kushirikisha wananchi wa jimboni humo, madiwani,
wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.
Awali akifungua mkutano huo mzee
wa Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini, Clifford Biseko alisema
wanamusoma vijini wanajivunia maendeleo yanayodhihirika kila kukicha
kutokana na mchango wa mbunge huyo.
Aliongeza kwamba Profesa Muhongo
ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kuwa hawajuti kumchagua na wanamwombea
afya njema ili azidi kushirikiana nao katika kusukuma gurudumu la
maendeleo jimboni humo.
Alisema katika kipindi kifupi cha
uongozi wake, wameshuhudia masuala makubwa ya maendeleo kwenye sekta
mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, sanaa na michezo.
Akizungumzia suala la afya, Biseko
alisema, Musoma Vijijini haikuwahi kuwa na gari hata moja la wagonjwa
lakini tangu Profesa Muhongo awe Mbunge tayari jimbo hilo linayo magari
manne.
Aliongeza kuwa Musoma vijijini
haikuwahi kupata ugeni wa madaktari bingwa kwa ajili ya vipimo, ushauri
na matibabu lakini kwa Profesa Muhongo hilo liliwezekana kwani
alikaribisha madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi ambao walitoa
huduma bila malipo.
Kuhusu suala la kilimo, Biseko
alisema, tangu Profesa Muhongo achaguliwe, alisambaza tani kadhaa za
mbegu za zao la mihogo na alizeti ili wananchi wajikwamue kwenye
umasikini.
Aliongeza kuwa, Profesa Muhongo
alipeleka wataalamu mahiri wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili
kufanya tathmnini ya kilimo bora ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa
kilimo bora.
Aidha, suala la elimu, Biseko
alisema kuwa kulikuwa na uhaba wa madawati 8,000 kwa shule zote zilizomo
jimboni humo na hilo lilitatuliwa bila wao kuchangishwa pia kusambaziwa
shehena ya vitabu vya sayansi kwa shule zote.
Biseko alimalizia kwa kuzungumzia
sekta ya michezo na sanaa alisema kuwa Mbunge ameandaa mashindano
mbalimbali na vilevile kugawa vifaa vya michezo kwenye vijiji mbalimbali
jimboni humo jambo ambalo alisema limehamasisha sekta husika.
Regards
Mohamed Saif
Communication Officer
Ministry of Energy and Minerals
Ministry of Energy and Minerals
P.O.Box 2000
Dar Es Salaam
Tanzania
+255 712 969626
No comments :
Post a Comment