Friday, December 30, 2016

Mbunge CCM Kigoma atuhumiwa kushiriki kumn’goa Meya wa Halmashauri

ccm
Mbunge wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephine Gezabuke ametuhumiwa na viongozi wa chama hicho wilaya ya Kasulu kushiriki kutaka kumn’goa Meya wa Halmashauri ya Kasulu, Twaribu Mangu licha ya kuwa chama kimoja kwa kile kinachotajwa kuwa ni meya huyo kukataa kutekeleza matakwa ya mbunge huyo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya ya Kasulu, Masoud Kitowe kuwa mbunge Gezabuke aliwatumia madiwani wa Halmashauri ya Kasulu kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu kuwa hawana imani na meya wa halmashauri hiyo, Mangu ili meya atolewe katika nafasi hiyo.
katibu-mwenezi-wa-ccm-wa-wilaya-ya-kasulu-masoud-kitoweKatibu Mwenezi wa CCM wa wilaya ya Kasulu, Masoud Kitowe akizungumza kuhusu Mbunge wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephine Gezabuke kutaka kumtoa madarakani Meya wa Halmashauri ya Kasulu, Twaribu Mangu.
Kitowe alisema katika barua hiyo kulikuwa na saini za madiwani 13, 11 wakiwa wa CCM na wawili wakiwa wa upinzani na baada ya kuwahoji madiwani hao, madiwani sita walisema walishajitoa katika jambo hilo na hawana hofu yoyote na meya na wengine watano wakikubali kushiriki na wapo tayari kupewa adhabu na chama.
“Wahusika walipewa onyo kali na Kamati ya Uongozi na Maadili ya wilaya lakini pia wakiwa katika kipindi cha uangalizi kwa kipindi cha miezi 18 lakini baada ya kuchunguza nani yupo nyuma yao tuligunduakuwa mbunge wa viti maalumu Kigoma, Josephine Gezabure ndiyo anahusika, tulimwita tukamhoji na yeye akapewa adhabu ambayo mpaka sasa anaitumikia,” alisema Kitowe.
mbunge-wa-viti-maalum-kigoma-kupitia-chama-cha-mapinduzi-ccm-josephine-gezabukeMbunge wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephine Gezabuke akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipotembeleaa kijiji cha Nyumbigwa kwa ajili ya kukagua mradi wa maji, Aprili 9, 2014. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Dk Aman Walid Kabourou.
Alisema walifanya uchunguzi na kubaini sababu za Gezabuke kutaka meya wa Kasulu avuliwe madaraka kuwa ni kukataliwa kushiriki vikao vya Baraza la Madiwani la Kasulu kwasababu alishashiriki kupiga kura katika Baraza la Madiwani la Kakonko na kukataliwa na meya kumwita Diwani wa Heru, Avelin Charles katika kikao kutokana na kuwa na mgogoro wao binafsi, lengo lake ikiwa ni diwani huyo avuliwe udiwani.
“Tunazo sauti anasema kuwa hata kama tunamzuia lakini mapambano yataendelea na mpaka tunaamua kutoa taarifa hii tayari tumeshamwambia sana lakini hasikii na anasema ana watu ngazi za juu na atapanda kwa viongozi wa juu ili hata adhabu aliyopewa itenguliwe,” alisema Kitowe.
Nae Josephine Gezabure alipotafutwa kwa njia ya simu ili azungumze kuhusu tuhuma ambazo zinatolewa dhidi yake hakuwa tayari kuzungumza kwa muda huo.

No comments :

Post a Comment