Thursday, December 29, 2016

JESHI LA POLISI ARUSHA:WATAKAOCHOMA MATAIRI,FAINI MILIONI NNE,MADEREVA WALEVI KUKAMATWA NA KUNYANG’ANYWA LESENI,WAZAZ I/WALEZI WATAKAOWAACHA WATOTO WAKAZURURA OVYO KUSHTAKIWA,WENYE VIBALI VYA KUFYATUA FATAKI KUTUMIA DAKIKA TATU TU


polii
Na.Vero Ignatus,Arusha.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kuwa katika kusheherekea mwaka mpya ,kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya watu kufanya matukio ya kuhatarisha usalama kwa kuchoma matairi,kupanga mawe barabarani,na hata kuwarushia mawe askari pindi wanapothibiti matukio hayo,haswa maeneo ya majengo,kwa mrombo,kwa mrefu huku
wengine wakitumia mwanya huo kufanya uhalifu.
 
Kwa wale
watakaochoma na watakaokamatwa wamechoma matairi barabarani,wakumbuke kwamba
watashtakiwa kwa sheria za Tanroad, ambapo watatakiwa kulipa faini isiyopungua
milioni nne
 
Lakini pia
baadhi ya madereva huwa wanatumia vilevi kupita kiasi katika majumba ya starehe
inapofika saa 00:00 usiku unapoanza mwaka mpya huwa wanashangilia kwa kuendesha
vyombo vyao kwa mwendo kasi na kupiga honi mitaani huku wakiwa wamepakia watu
kwa kuwaning’iniza milangoni kama njia ya kuonyesha furaha
zao.
 


Uzowefu unaonyesha
kwamba maeneo ya sakina mpaka kwa iddi baadhi ya madereva wanatuamia magari
aina ya altezana Subaru huwa wanafanya maonyesho kwa kuendesha mwendo kasi
vyombo hivyo huku vikitoa sauti kama risasi.
 


Kwa upande
wa wamiliki wa bar wazingatie masharti ya leseni zao ambazo zinaonyesha muda
halisi wa kufunga na wasiwe na tama ya kuendelea kupata pesa baada ya
kuona wateja
wengi katika biashara ,hali kadhalika wamiliki wa kumbi na maeneo mengine ya
starehe wanatakiwa kuzingatia usalama katika maeneo yao hasa kwa kuweka
wasimamizi na kutojaza watu kupita kiasi.
 


Aidha
wazazi na walezi tunawakumbusha pamoja na kusheherekea mwaka mpya wa 2017
wasisahau majukumu yao ya kuwa makini na watoto kwa kutowaacha peke yao na hata
kutoacha mtu yeyote katika majumba ili kuondokana na matukio yanayoweza
kuepukika sambamba na kuangalia watoto wao katika maeneo ya round about hasa
kijenge mnara wa mwenge,wasizagae barabarani
 


Jeshi la
polisi linatoa onyo kwa baadhi ya watu watakaofanya makosa yaliyoorodheswa hapo
juu ,tutawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wawe wahalifu ,wamiliki wa
bar na kumbi nyingine za starehe pamoja na wazazi au walezi na madereva walevi
ambao pia watapima na ikithibitika wamevuka viwango tutawafungia
leseni.
 


Kwa upande
wa waaliomba vibali vya kufyatua fataki ,watatakiwa watumie dakika tatu na wote
kwa pamoja watatakiwa kufyatua saa 00:00 na pia hawataruhusiwa kufyatua katika
makazi ya watu.
 


Tutahakikisha
nyumba zote za ibada ,kumbi za starehe na maeneo mengine kutakuwa na ulinzi wa
kutosha ambapo askari watakuwa katika doroa za miguu na doria za magari kila
kona ya jiji la Arusha na wilaya zote za mkoa huu ,hivyo waumini wa dini
mbalimbali wasiwe na hofu pindi watakapokuwa wanaendelea na
ibada.
 


Kama ilivyo
kwa nyakati zote tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana nasi katika
kuwabaini na kuwafichua wahalifu na uhalifu ili kuimarisha amani na utulivu
uliopo.
 


Mwisho
tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari
radio,magazeti,blogs,televisheni,kwa
ushirikiano mkubwa mnaotoa kwa jeshi la polisi mkoa wa Arusha kwa kuwa
mbele katika kufichua, kuelimisha,na kuhabarisha umma juu ya
uhalifu.
 


Jeshi la
polisi mkoa wa Arusha tunawatakia heri ya mwaka mpya wa 2017 wakazi wote wa
Arusha .
 


       IMETOLEWA
NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA



NAIBU
KAMISHANA WA POLISI



(DCP)CHARLES
MKUMBO

No comments :

Post a Comment