Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi
Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mkurugenzi wa
Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha
Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo, Dar es Salaam leo
asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku
saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto),
akizungumza na wajumbe hao.
Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya
picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyochorwa
na kikundi cha Angavu Youth Group leo Novemba 28, 2016 jijini Dar es Salaam. Picha hiyo
imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba
ya Mhe. Rais. kushoto ni Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na
kulia ni Katibu wake Bi. Oliver Charles.
(PICHA
NA ANITHA JONAS – MAELEZO)
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia)
akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth
Group Bi.Oliver Charles (katikati) wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea
picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka
kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia) leo jijjini Dar es
Salaam. Picha hiyo imechorwa kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group.
Wanafunzi
wa shule ya Academic International school, Harshvardhan Kabla (kushoto)
ambaye ameshika nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa
wanafunzi wa “A Level” kwa mitihani ya Cambridge na Abishek
Sankaranarayanan(kulia) ambaye ameshinda nafasi ya kwanza kwa somo la
hisabati kwa mitihani ya Cambridge kwa wanafunzi wa kidato cha nne
wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe maalum ya kuwapongeza.Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na
kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Harshvardhan Kabla
(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta
kwa wanafunzi wa “A Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na
kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Abishek
Sankaranarayanan(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika
somo la Hisabati kwa wanafunzi wa “O Level” kwa shule zinazofuata
mtahala wa Cambridge.Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar (kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na walimu wawili wa shule ya Academic International,
Walter Mlowe ambaye anafundisha somo la Hisabati na Thadei Mwinuka
ambaye anafundisha somo la kompyuta. Walimu hao walitunukiwa vyeti kwa
kazi nzuri ya ufundishaji.Mkurugenzi
wa shule ya Academic International, Yusuf Kalindaga akizungumza katika
hafla maalum ya kuwapongeza wanafunzi , walimu na wafanyakazi wa shule
hiyo kwa kufanya vyema katika mitihani ya Cambridge.Mkuu wa shule ya ya Academic International, Shyama Santhosh ( wa kwanza kushoto) akisema jambo katika sherehe hiyo ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Academic International wakishiriki katika hafla hiyo.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule ya Academic International wakiwa katika hafla hiyo
Wanafunzi
wawili wa shule ya Academic International ya Tanzania wameweka historia
katika mitihani ya mtahala wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya
kwanza duniani katika masomo ya hisabati na kompyuta.
No comments :
Post a Comment