Wednesday, November 2, 2016

ELIMU YA MPANGO MKAKATI WA UTEKELEZAJI BARAZA LA WATOTO KITAIFA YAENDELEA MKOANI IRINGA

1
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendelewo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Christopher Mushi akifafanua jambo wakati wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
2
Mwezeshaji kutoka shirika lisilo la Kiserikali  kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akiwasilisha mada wakati wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la 
Watoto 2017-2020
3
Mwakilishi wa  Katibu Tawala Wilaya ya Iringa Menrad Dimoson akifungua Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
4
Meneja Mradi kutoka shirika la Ukatili wa Kijinsia na Ulinzi wa Mtoto(GBV) akichangia mada wakati wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
5
Baadhi ya Washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
Na Anthony Ishengoma
Idara zinazoshughulikia masuala ya watoto pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Iringa zinakutana katika kikao kazi cha siku mbili kupata mafunzo ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Baraza la Watoto Kitaifa.
Kikao kazi hiki kuhusu Mkakati wa Baraza la Watoto wa miaka mitano wa 2017-2020  kinaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Christopher Mushi amesema kuwa Mkakati huu kimsingi unatokana na katiba ya Baraza la Watoto ambayo inataka kuwepo kwa mkakati huu ili kuwawezesha watunga sera kutekeleza kwa vitendo haki za watoto.
Mwezeshaji kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Koshuma Mtengeti amesema Serikali ya Tanzania  imeishatimiza malengo makubwa ya kisera kuhusu watoto hapa Nchini lakini bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sera hizo ndio maana Wizara imeandaa Mkakati huu ili kukabiliana na changamoto za utekelezaji.
Amesema katika uhandaaji wa Mkakati huu mambo yote ya msingi kutoka Wizara na Wadau yaliangaliwa kiundani ili kuhakikisha Mkakati unazingatia masuala yote ili kujenga uwezo kwa watoto na masuala mtambuka kuhusiana na haki na wajibu watoto Nchini.
Masuala mbambali zinazowakabili watoto Nchini nia pamoja na janga la ukimwi, umasikini, ujinga, maradhi na uelewa mdogo wa masuala ya watoto kutoka jamii inayowazunguka.

No comments :

Post a Comment