Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez
akizungumza kuhusu mradi ambao una malengo ya kurejesha watoto wa kike
shuleni. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi
akizungumza kuhusu mipango ya serikali kukabiliana na tatizo la watoto
wa kike kukatishwa masomo.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum
akizungumzia sababu ya watoto wa kike kutokuwepo shuleni na jinsi
ambavyo UNWOMEN watashiriki katika mradi wa kusaidia watoto wa kike
kurudi shuleni.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watu Duniani (UNFPA), Maria
Karadenizli akielezea takwimu za watoto wa kike ambao hawapo shuleni.
Mkuu
wa Ofisi wa Shirika hilo la Maendeleo la (KOICA), Joosung Park
akielezea ushiriki wa KOICA katika kusaidia mradi huo kukamilika sawa na
mipango iliyowekwa.
Na Mwandishi wetu
Katika
kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na hatimaye kumaliza masomo
yao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) limetenga Dola 1,605,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za
Kitanzania ambayo zitatumika kuwasaidia watoto wa kike nchini kurejea
katika shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Akizungumzia
mradi huo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira
Rodriguez alisema kuwa Tanzania bado inaonekana kuwa na tatizo la watoto
wa kike kuachishwa masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo
kupata mimba za utoto na ndoa za utotoni hivyo kupitia mradi huo
wataweza kuwasaidia watoto hao kuendelea na masomo.
Bi.
Rodriguez alisema UNESCO imeamua kushirikiana na serikali ili
kuwasaidia watoto wa kike kurejea masomoni na utafanyika kwa uhakika
bila kumwacha mtoto yoyote na wana matumaini utaweza kusaidia watoto wa
kike ambao wamekatishwa ndoto zao kimaisha kutokana na kukatishwa
masomo.
“Tanzania
kuna tatizo la watoto wa kike kusahaulika katika elimu na UNESCO
imejitoa kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kusaidia kukuza elimu
ya watoto wa kike, “Baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuchangia ni
pamoja na mambo ya asili, wamekuwa wakiwaozesha ndoa za utotoni na na
watoto wengine wamekuwa wakipata mimba za utoto na hivyo kuacha masomo …
mradi huu ni wa uhakika na utasaidia kukuza elimu,” alisema Bi.
Rodriguez.
Kwa
upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi.
Maimuna Tarishi alisema serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hizo na
imekuwa ikifanya jitihada ili kuhakikisha kuwa matatizo ya watoto wa
kike kukatishwa masomo yakimalizika.
Alisema
kuwa makabila mengi ya Tanzania yamekuwa yakiwaona watoto wa kike kama
watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto lakini kama jamii ikiwa na
mtizamo tofauti na kuwawezesha watoto wa kike basi wanaweza kusaidia
nchi kukuza uchumi.
“Tumeona
kazi ambayo wameifanya UNESCO hata machifu huko Ngorongoro wameanza
kuelewa umuhimu wa watoto wa kike kuwa shuleni na kwa mpango huu
matarajio ya serikali ni kumaliza changamoto iliyokuwepo awali,
“Serikali
inafahamu kuna changamoto nyingi ambazo zinawakuta watoto wa kike na
sio katika elimu pekee bali ni maeneo mengi … serikali inataka kukuza
thamani ya elimu kwa watoto wa kike ambao wengi wao wanakatishwa kwa
sababu ya mimba na ndoa za utotoni,” alisema Bi. Tarishi.
Nae
Afisa Mradi wa Maswala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana (UNFPA), Fatina
Kiruviya alisema mradi una malengo ya kuhakikisha watoto wa kike
wanakuwa shuleni na kwa kuanza wanataraji kufanya mradi Ngorongoro,
Pemba, Geita na Sengerema.
POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imewaonya
wazazi kuwa makini na mienendo yawatoto wao, baada ya kubaini baadhiya vijana
kuendesha mazoezi ya kareti na matumizi ya silaha misituni.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Polisi (CP),
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, wakati akionyesha “shehena” ya
silaha zilizokamatwa na polisi kufuatia operesheni ya kimyakimya inayoendelea
hivi sasa kwenye viunga vya jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
“Niwaombe wazazi wenzangu kufuatilia mienendo ya
vijana wetu, kwani kutofanya hivyo kunaweza kupelekea mzazi kutojuavitendo
viovu vinavyofanywa na mototo wako, utakuta watoto wanajifunza kareti na
matumizi ya silaha, hii sio dalili njema hata kidogo,” Alionya Kamanda Siro
huku akiwaonyesha waandishi wa habari silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi
kwenye operesheni hiyo.
Mwezi uliopita, polisi wanne waliuawa kwa kupigwa
na risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, kwenye eneo la tawi la benki ya
CRDB, Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilifuatiwa na tukio linguine la kuuawa
kwa afisa mwandamizi wa polisi wa kikosi cha kudhibiti majambazi, wakati polisi
wakiwa kwenye jitihada za kuwasaka wahalifu hao huko Vikindu wilayani Mkuranga
mkoa wa Pwani.
Baada ya tukio hilo, polisi walizidisha msako mkali
dhidi ya wahalifu hao na hatimaye katika kipindi cha siku 10 tangu kutokea kwa
matukio hayo mawili ya kusikitisha,
Polisi ikiwatumia watuhumiwa watatu ambao
walikwisha tiwa mbaroni na polisi, na ambao waliwachukua polisi ili kuwapelekea
kwenye ngome yao kwenye msitu wa Mbande, ambako wakati wanakaribia eneo hilo,
huku polisi wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa mbele, walishitukia mashambulizi
ya risasi yakielekezwa upande wao na ndipo polsi wakalala chini ili kujihami na
mashambulizi hayo na kuwaacha hao watuhumiwa watatu wakishambuliwa na risasi ambapo
walipofikishwa hospitali, Daktari alitangaza kuwa wamekwishakufa.
Katika operesheni hiyo, Kamanda Siro anasema, jumla
ya bunduki 23 za aina tofauti tofauti zilikamatwa, ikiwa ni pamoja na risasi
835, fulana za kuzuia risasi kupenya mwilini (Bullet Proof), Sare za polisi,
pingu 48 na Redio za mawasiliano za polisi (Radio Call) 12.
NA
K-VIS BLOG
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, (pichani),
amekanusha taarifa kuwa ameomba kujiuzulu wadhifa wake.
Taarifa
iliyosambazwa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam
leo Septemba 6, 2016, imekanusha vikali habari zilizozagaa kwenye mitandao ya
kijamii zikisema, Mama Samia amemuandikia barua Rais John Pombe Magufuli,
akiomba ajiuzulu wadhifa wake.
“Ofisi
ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla wake kupuuza
taarifa hizo ambazo zinalenga kuupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo
baina ya viongozi wetu,” taarifa hiyo imesema.
Taarifa
hiyo imeendelea kufafanua kuwa, wasambaza taarifa walilenga kuliweka taifa
kwenye taharuki na kuwahakikishia wananchi kuwa Makamu wa Rais yuko bega kwa bega
na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kufanya kazi zao
kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Taarifa
hiyo imehitimishwa kwa kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vinavyolenga
kuvuruga amani na utulivu wa nchi.
Hii ni mara pili, Makamu wa Rais kuzushiwa habari
ambazo si za kweli. Mnamo Februari 8, 2016, Ofisi ya Makamu wa Rais, ilikanusha
taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii kuwa Makamu wa Rais, Mh. Samia
Suluhu Hassan, AMEANZISHA SACOS, VICOBA na vitu vingine kama hivyo na kwamba atatoa
mikopo kwenye vikundi hivyo.
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jafo
Selemani Said, (picha ndogo kulia) amenusurika kifo baada ya gari lake kugongana na gari dogo eneo
la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.
Polisi
wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilihusisha gari la Mh. Naibu
Waziri aliyekuwa akitokea Tukuyu mkoani humo kikazi, akielekea Mbeya njiani
kwenda Dodoma, wakati gari hilo aina ya Toyota lilikuwa likitokea Mbeya kwenda
wilayani Rungwe.
Picha zilizopigwa kwenye eneo la ajali,
zinaonyesha sehemu iliyogongwa ni upande aliokuwa amekaa Naibu Waziri
na kutokana na mshindo wa ajali hiyo, kitufe cha usalama (kinachokaa
mbeleya abiria), kilifyatuka ili kumuhami abiria asepatwe na madhara
makubwa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema gari la Naibu Waziri kulikuwemo
watu watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka
salama katila ajali hiyo.
Alisema
baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo
walifanyiwa uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa. Hata
hivyo taarifa za Daktari zimethibitisha kuwa wote watatu wako salama. Naibu Waziri na wenzake waliruhusiwa kuondoka baada ya uchunguzi huo.
(PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU)
Hii ndiyo sehemu ambayo iligongwa, upande ambao Naibu Waziri alikuwa ameketi.
Polisi wa usalamabarabarani, akifanya uchunguzi sehemu ambayo gari la Mh. Naibu Waziri liliathirika
Polisi wa usalama barabarani, wakifanya vipimo kwenye eneo la ajali
Gari lililogongana na gari la Naibu Waziri Jafo, likiwa
nje ya barabara baada ya ajali hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tigo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita. Ramos yuko nchini kutembelea kampuni ya Tigo na miradi yake.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga ,Bi Zainab Telack (aliye vaa ushungi) akiongozwa
na Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii wa Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila (kushoto kwake) wakati
wakielekea uwanja wa Taifa wa mjini Kahama kwa ajili ya makabidhiano ya
Madawati kutoka kampuni ya Acacia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akihutubia wananchi
katika uwanja wa Taifa Kahama wakati wa zoezi la Kukabidhiwa madawati
kutoka kwa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia, Bulyanhulu.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,kutoka kushoto ni Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Elias Kasitila, Afisa Miradi
Mzee Hamisi, Afisa Mahusiano ya Jamii William Bundala Chungu pamoja na Afisa
Mahusiano ya Jamii David Magege, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kabla ya zoezi la Kukabidhi
Madawati .
Baadhi
ya waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga wakichukua taarifa kwa
ajili ya kuuabarisha umma juu ya tukio la makabidhiano ya Madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia.
Na Dixon Busagaga,Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack
amekabidhiwa madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi 240,800,000/= na Mgodi wa
Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya
Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Makabidhiano yamefanyika leo mjini Kahama.
Akimkabidhi madawati hayo Meneja wa Ufanisi wa
Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, “hii ni awamu ya nne
kwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu kukabidhi madawati ndani ya mwaka huu katika
kipindi ambacho taifa linaendelea kutekeleza kampeni ya kitaifa ya dawati kwa
kila mwanafunzi iliyoagizwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu nchini
Tanzania.”
Ameongeza kuwa, “licha ya Mgodi wa Dhahabu wa
Acacia Bulyanhulu kuchangia madawati pia inachangia miradi mingine kwenye jamii
lakini kwenye sekta ya elimu mgodi unashirikiana na jamii kuitekeleza miradi
kama vile ujenzi na ukarabati wa nyumba, ofisi za walimu madarasa, maabara za
sayansi na udhamini wa masomo kwa wanafunzi.”
Miradi ya Madawati 2016 kutoka Mgodi
wa Acacia Bulyanhulu
- Mei tulikabidhi madawati 380 kwa Halmashauri ya Msalala yenye thamani ya shilingi 28,500,000/=
- Juni tulikabidhi madawati 1,000 kwa Halmshauri ya Msalala yenye thamani ya shilingi 88,500,000/=
- Julai tulikabidhi madawati 500 kwa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita yenye thamani ya shilingi 37,500,000/=
- Na hii leo Agosti tunakabidhi madawati 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga yenye thamani ya shilingi 240,800,000 /=
- Aidha mwaka 2013 mgodi wa Acacia Bulyanhulu pia ulikabidhi dawati 1,389 kwa Wilaya ya Kahama
Mchango wa Miradi ya Madawati Kwenye
Ajira
- Katika kipindi cha miezi minne, utengenezaji wa madawati yenye thamani ya shilingi 393,800,000 umewezesha kutolewa kwa tenda za kutengeneza madawati kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo na kuwawezesha vijana kujipatia ajira.
Wanafunzi ambao Wamenufaika
- Mradi wa Madawati wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu umewaondelea adha jumla ya wanafunzi 5,040 ya kuketi sakafuni wakati wa kupokea masomo yao, baada ya kupata madawati 3,880 bora ya kudumu ambayo yametengenezwa kwa awamu nne hadi sasa.
Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
na Sekta ya Elimu Nchini
Mgodi wa Bulyanhulu unaamini kwamba elimu ni msingi
wa maendeleo ya jamii na unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine
wa maendeleo katika ngazi mbalimbali kuendeleza shughuli za uboreshaji wa elimu
hapa nchini kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mgodi kupitia Mfuko wa
Maendeleo wa Kampuni ya ACACIA, (ACACIA Maendeleo Fund).
Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi Zainab Telack amesema, “ Tukio hili la
kukabidhiwa madawati ni tukio kubwa, nimefurahi sana na ninajua furaha ya
watoto watakaotuhmia madawati haya itakuwa mara mbili yake, kwa hivyo kwa niaba
ya Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa
kututengenezea madawati elfu mbili, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na upungufu wa
Dawati elfu 7000 lakini sasa kupitia mchango wa leo kutoka Bulyanhulu na wadau
wengine sasa mkoa wetu unamaliza kabisa upungufu wa madawati.”
No comments :
Post a Comment