NA
K-VIS MEDIA
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo
la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana
na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza
na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya Shirika hilo, Makao Makuu jijini Dar es
Salaam leo Agosti 30, 2016, katizo hilo la umeme litaanza rasmi Septemba 3 na
umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu
na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na
Septemba 24-25, 2016.
Taarifa
hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na eneo lote
la katikati ya jiji (City centre), Maeneoyote ya Upanga, maeneo yote ya
Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Mbagala, Maeneo yote ya
Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Maeneo yote ya Chang’ombe, Maeneo ya Temeke,
Uwanja wa Taifa, Unilever, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality
Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate pamoja na maeneo ya jirani.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa ili jiji la Dar es Salaam lipate umeme ulio bora na wa uhakika,
Shirika laUmeem Tanzania (TANESCO), limemruhusu mkandarasi, (TAKAOKA),
kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa za njia mbili (Two-lines)
za Msongo wa Kilovolti 132.
Kuboresha
vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Ubungo kwa kuweka nyaya zenye
uwezo mkubwa zaidi.
Kubadilisha
vifaa vya kupima umeme kwenye njia mbili (Two-lines) za Ubungo-Ilala.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi
yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho
hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili
kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya
kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na
kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho
na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven
Mlote, (pichani juu), amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “Tanzania kuelekea
kuwa nchi ya uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanda: nini jukumu la wahandisi”.
“Tumejipanga
Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya
kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya
viwanda” amesema Eng. Mlote.
Maadhimisho
ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni
kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi
wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.
Takribani
wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo
likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato
cha kati ifikapo mwaka 2025.(PICHA NA BENJAMIN SAWE-MAELEZO)
Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
Familia ya
marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura
pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na
Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa
upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika
kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo
(pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi,
kwa ajali ya gari.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano ya madawati 235
kwa shule za msingi mkoani Kagera toka kampuni ya simu za mkononi
Tigo.
|
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati
kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.
|
Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbeneakipokea Risala kutoka kwa Ocd Wilaya Ileje
Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akikabidhi Laptop kwa OCD wa Wilaya ya Ileje kw ajaili ya kusaidia kazi katika Wilaya hiyo
Mbunge wa Ieje , Mh Janet Mbene, akikabidhi Matairi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo
Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akipokea
mkono wa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude mara baada
ya kukabidhi laptop, Photocopy Mashine, Matairi na lim tano
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina
Nkurlu,(katikati), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa
kuchezesha droo ya wiki ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Hassan Mfaume, mkazi wa Mwananyamala jijini
Dar es Salaam aliibuka mshindi wa wiki wa kitita cha shilingi Milioni 5/-
kupitia promosheni hiyo inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa
kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 224 wamepatikana tangu
kuanza kwa promosheni
hiyo.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa
moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na
mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Wengine katika picha kushoto ni Ofisa
msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa huduma
za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe.
Bw . Mohamed Seif Ofisa kutoka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo akikabidhi kwa
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa
Samora jijini Dar es salaam.
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa
Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa
Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015
Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka
madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya
kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa
chini wakiwa darasani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa
makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na
Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali
ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba
na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe
amesema
kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa
ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na
wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500
hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo
hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika
Halmashauri za Singida na Manyoni.
No comments :
Post a Comment