Tuesday, July 26, 2016

TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa, inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti nchini Brazil.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki.
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 

WANAUME WA KIDACHI NA WANAWAKE WA LATVIA WAONGOZA KWA UREFU DUNIANI

MICHELLE OBAMA AMPONDA DONALD TRUMP, NA KUMUUNGA MKONO BI. CLINTON

Michelle Obama mke wa rais wa Marekani amemponda mgombea urais wa Republican Donald Trump, na kumuunga mkono Hillary Clinton katika mkutano wa Taifa wa Chama cha Democratic huko Philadelphia.

Huku akishangiliwa na kupigiwa makofi na wajumbe wa mkutano huo Michelle Obama amesema lugha za chuki zinazotolewa na watu mashuhuri kwenye TV, haziwasilishi moyo wa uzalendo wa taifa hilo.

Kama hiyo haitoshi Michelle amewataka wafuasi wa chama cha Democratic kutojishusha sawa na wapinzani wao, kwani kauli mbiu ya chama hicho ni “Wao wakijishusha, sisi tunakwenda juu”.
Awali aliyekuwa mshindani mkuu wa Bi. Clinton, Seneta Bernie Sanders amewasihi wafuasi wa chama cha Democrat, kumuunga mkono Bi. Hilary Clinton.
Wanachama wa Democrat wakimshangilia Michelle Obama wakati akitoa hotuba yake
Michelle Obama akionyesha ishara ya vidole gumba baada ya kumalizi kutoa hotuba yake
Rais Obama alishindwa kujizuia na kutuma twitti ya kumfagilia mkewe Michelle Obama kwa hotuba nzuri aliyoitoa

MTU AWAUWA KWA KUTUMIA KISU WAGONJWA WA AKILI 19 NCHINI JAPAN

MILIPUKO MIKUBWA YATOKEA KARIBU NA UWANJA WA NDEGE WA MOGADISHU

MAALIM SEIF KUNGURUMA TENA MAREKANI

Maalim Seif Sharif Hamad akiwasili katika uwanja wa ndege, Philladelphia. 

Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.

Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwahutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston.  

Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja.
Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uingereza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali.

Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia. 


Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.

Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar. 

Maalim Seif ambaye anafuatana na Mkuu wa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Bwana Issa Kheir Hussein, yupo nchini Marekani kuitikia mwaliko wa kuhudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democratic ulioanza jana jijini Philladelphia, mkutano ambao unatazamiwa kumpitisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa kuoitia tiketi ya Chama hicho. 

Katika mkutano wake wa hadhara na Watanzania, Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, anatazamiwa kuzungumzia zoezi zima la uchaguzi huo uliofutwa, na kusisitza madai ya Chama chake ya kurejeshewa haki yao waliyoporwa katika uchaguzi huo, na mwenendo mzima wa Demokrasia nchini Tanzania.

Itafaa kukumbusha kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kuzuru Marekani katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Mwezi uliopita, Maalim Seif alikuwepo nchini humu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kisiasa na mashirika binafsi, na kutembelea Umoja wa Mataifa ambako alifikisha madai ya Chama chake ya ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania. 

Aidha alizungumza na Watanzania waishio nchini Marekani katika jiji la Washington

No comments :

Post a Comment