Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa
Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Edwin Ngonyani (kushoto)na Katibu Mkuu
wa Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (kulia) baada ya mazungumzo
kati ya wizara hiyo na Viongozi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya
Airtel, Sunil Colaso ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (wapili kushoto) na
Beartice Singano.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
SERIKALI YAMILIKI HISA ZA TTCL KWA ASILIMIA 100
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria (aliye
kaa katikati) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina ( aliye kaa
wa kwanza kushoto) wakiweka saini ya kuiwezesha Serikali kumiliki hisa
za TTCL kwa asilimia 100. Dkt. Injinia Maria Sasabo, Kaimu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (aliyesimama nyuma
katikati), Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL
(aliyesimama wa tatu kushoto) na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji
Mkuu wa TTCL (aliyesimama wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
Msajili
wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa utiaji saini na Bharti Airtel kwa niaba ya Serikali
ili iweze kumiliki hisa 100 za TTCL
Kaimu
katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)
Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel ya kuuza
hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha TTCL.
Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia) na
Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto)
wakifuatilia tukio hilo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya makabidhiano ya
hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za Kampuni ya TTCL kwa
asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya
Bharti Airtel.
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Afisa
Malalamiko wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. James Katubuka (kulia)
akihudumia mteja katika Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2016 iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi
wa Umma leo.
Mhasibu
Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Victor Gideon (kulia) akihudumia
mteja katika Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo.
Wateja
wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma 2016.
Picha na mpiga picha wetu
TBA yakusanya Bil. 2.6 kwa kipindi cha miezi mitatu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Bw. Elius Mwakalinga wa
kwanza kushoto akiwaongoza wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya usafi
jijini Dar es salaam katika kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa
Umma.
Wafanyakazi
wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) wakishiriki katika kufanya usafi
jijini Dar es salaam ili kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa
Umma.
————————————————————————
Na Ally Daud-Maelezo
Wakala
wa Majengo nchini (TBA) wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
bilioni 2.6 sawa na asilimia 43 kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo
wapangaji wa nyumba hizo kushindwa kumalizia madeni wanayodaiwa
Akizungumza
hayo katika kilele cha kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga amesema kuwa
wamefanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha kutoka kwa wateja wao
waliowapangisha majengo na bado wanaendelea kukusanya mpaka
watakapomaliza.
“Kutokana
na mkakati wa kukusanya mapato na kutoa huduma bora kwa wateja wetu
tumefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.6 katika kipindi cha miezi
mitatu tuliyowapa wateja wetu kuweza kukamilisha malipo hayo” alisema
Bw. Mwakilinga
Mbali
na hayo Bw. Mwakilinga amesema kuwa wameamua kutumia siku hiyo kufanya
usafi kwenye makazi ya watumishi wa umma na wakazi wengine ili kuweka
mazingira bora kwenye miradi yao na jamii nzima kwa ujumla.
“Siku
ya leo tumeamua kuitumia kufanya usafi kwenye maeneo ambayo tumeweka
miradi yetu kwa watumishi wa umma pamoja na mazingira mengine ili
kuepuka na magonjwa yasababishwayo na uchafu” alisisitiza Bw.
Mwakilinga.
Aidha
Bw. Mwakilinga amesema wanampango wa kupanua wigo wa huduma yao kwa
kuwapangisha watumishi wa umma ambao wanastaafu waendelee kukaa kwenye
nyumba hizo ili wasipate shida mara baada ya kustaafu.
Mbali
na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo amesisistiza kuwa wataendelea na
utaratibu wao wa kukusanya kodi na kuchukua nyumba zao kwa wale ambao
wamekaidi amri yao ya kutolipia kodi nyumba hizo ili wapewe wengine
ambao wana huitaji .
Wiki
ya utumishi wa Umma imeadhimshwa kwa kila taasisi ya kiserikali
kusikiliza na kutatua kero zinazowapata wateja wanaoutumia huduma za
taasisi husika ili kuipeleka nchi katika utendaji bora na mafanikio kwa
ujumla.
RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
Rais
wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akitoa
hutuba yake mbele ya viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje
baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es
Salaam leo
Rais
wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akipokea
Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania(NEC) kutoka kwa Jaji Mstaafu wa Tume hiyo Mhe,Damian Lubuva
mbele ya Viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje katika ukumbi
wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,[Picha na Ikulu.] 23/06/2016.
Rais
wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli na
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe,Jaji Mstaafu Damian
Lubuva wakionesha Ripoti ya Tume hiyo Juu baada ya kukabidhiwa rasmi leo
katika ukumbi wa mikutano Ikulu ya Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]
23/06/2016.
Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya
Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa hutuba
yake mbele ya viongozi hao na waalikwa wakiwepo mabalozi wa nchi za nje
baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es
Salaam leo
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Pili Mzee Ali
Hassan Mwinyi (kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
awamu ya Nne Mhe,Jakaya Mrisho Kikwete(katikati)na Waziri Mkuu mstaafu
Mhe,Ahmed Salum(kulia) wakiwa katika hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika
ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiteta jambo na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe,Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi
wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,
MIAKA 10 YA UMOJA SWITCH WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Akizungumza na Vyombo vya Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya UMOJASWITCH.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Amezindua Amezindua Rasmi Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch..Katika Hotuba yake aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari Amesema Miaka 10 iliyopita Benki ndogo zilikuwana Changamoto Kubwa ya kuweza Kupatia Huduma za ATM wateja wao kwani Mitaji na Gharama za uwekezaji,Uendeshaji wa ATM na Wigo wao wa utoaji wa Huduma hii Uliwapa Changamoto kubwa.Kutokana na ChangamotoHizo Mabenki Sita Yaliamua Kuanzisha Umoja wao ili Yaweze Kuweka ATM na Kuwezesha Benkihizo Kushirikiana katika Utoaji wa Huduma a ATMKWA Wateja wao,Umoja huo Ndio uliozaa UMOJASWITCH.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Amezindua Amezindua Rasmi Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch..Katika Hotuba yake aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari Amesema Miaka 10 iliyopita Benki ndogo zilikuwana Changamoto Kubwa ya kuweza Kupatia Huduma za ATM wateja wao kwani Mitaji na Gharama za uwekezaji,Uendeshaji wa ATM na Wigo wao wa utoaji wa Huduma hii Uliwapa Changamoto kubwa.Kutokana na ChangamotoHizo Mabenki Sita Yaliamua Kuanzisha Umoja wao ili Yaweze Kuweka ATM na Kuwezesha Benkihizo Kushirikiana katika Utoaji wa Huduma a ATMKWA Wateja wao,Umoja huo Ndio uliozaa UMOJASWITCH.
Akielezea
Zaidi Bw Danford Mbilinyi Amesema kwa Sasa Umoja Switch Ina Jumla ya
Mabenki 27 Yanayoshirikana katika Utoaji wa Huduma za Kibenki Kupitia
ATMzaidi ya 250 Nchi nzima.Kupitia Umojaswitch Mteja wa Benki Yenye
Tawi Moja Inamwezesha Mteja wake Kupata Huduma Sehemu Yoyote Tanzania.
Mafanikio
ya Umojaswitch ni Mafanikio ya Ushirikiano na Mabenki Pamoja na
Mzingira Wezeshi yaliowekwa na Serikali Kuptia Benki Kuu.Wakti Umoja
Huo Ulioanzishwa na Kuanza kutoa Huduma zake Jumla ya Benki sita tu ndio
walikuwa wanachama wa Umoja Swich Pamoja na ATM 27 tu.Tofauti na Ssas
umoja huo una Wanachama 27 unaotoa Huduma kwa zaidi ya wateja Milionoi 2
kupitia Zaidi ya ATM 250.Mafanikio ya Umoja Huo yanachangiwa na Ubunifu
na Huduma zitolewazo na Umojaswitch kama Kuhamisha Fedha Kutoka Benki
moja kwenda Nyingine zilizopo ndani ya Umoja huo Kupitia ATM Pamoja na
Huduma za Kununua Luku Mpesa pamoja na Kulipia Huduma Mbalimbali Kupitia
Hudama za Mobile Banking na zile za Uwakala.
Katika
Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch ni Kutoa Elimu kwa
Wananchi Kuhusu Umuhimu wa Mtandao huu na Technolojia kwa Ujumla Katika
Kukuza na Kuendeleza Sekta ya Kibenki na Mchango wake katika maendeleoa
ya Maisha ya Kila siku, Pia katika Maadhimisho haya Wanategemea
Kufanya Shuguli Mbalimbali ikiwemo kuchagiza Matumizi ya Technolojia
na Ubunifu Kwenye Vyuo vikuu hapa Nchini kwajili ya kuwa Kichocheo
muhimu Katika Maendeleo ya Sekta ya Kibenki
ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WAMKUBALI RAIS MAGUFULI, AWAPIKU JK NA LOWASSA; UTAFITI WA CZI WABAINISHA
Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafitiunaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya uchumi na nidhamu.
David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi |
Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKABIDHIWA MAGARI TISA
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo
jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye
thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP
Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania
utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni
Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatuma Mrisho akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye
thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kati ya Ofisi ya Taifa ya
Takwimu na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria
na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi
Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu
Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na
kulia kwake ni Dkt. Michelle Roland Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya
Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and
Prevention – CDC).
Mkurugenzi
Mkaazi wa Shirika wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa –
(Centre for Disease Control and Prevention – CDC) Dkt. Michelle Roland
akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari tisa yenye thamani ya
Shillingi Millioni mia nane na kumi kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa
ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania
utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa pamoja na
mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Claud Kumalija wakionyesha ufunguo wa gari mbele ya
waandishi wa habari na wageni waalikwa kuashiria kupokea magari tisa
yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa
Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia
mwezi Septemba, 2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasha gari kama
ishara ya kupokea magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia
nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa
Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia
mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Umma waaswa kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao
Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma
—————————–
Watumishi wa Umma waaswa kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao hasa wanapowahudumia wananchi ili kuongeza tija.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali
ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Akifafanua
Mhe. Majaliwa amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa
watumishi wote wa Umma wanazingatia uadilifu, uchapakazi, sheria,
taratibu na kanuni zinazosimamia Utumishi wa Umma.
“Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaotumia madaraka yao vibaya bila kujali vyeo vyao” alisisitiza Mhe. Majaiwa.
Katika
hatua nyingine Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali hivi karibuni
itawasilisha Bungeni muswaada wa Sheria utakaosaidia kuanzishwa Kwa
Divisheni ya kushughulikia Mafisadi katika Mahakama Kuu.
Lengo
la Serikali ni Kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale
wanapohitaji huduma mbalimbali ndio sababu tunaendelea kuimarisha vyombo
vyetu kama Taasissi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili
zitekeleze majukumu yake vizuri.
Katika
kuimarisha maadili Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inaangalia
uwezekano wa kuanza kujumuisha masomo ya maadili katika mitaala ya Elimu
hapa nchini ili kuongeza kasi ya kukuza na kujenga maadili miongoni mwa
jamii.
Watanzania Kumiliki hisa Katika Kampuni za Mawasiliano Hapa Nchini.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————-
Serikali
kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki
ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za
Mawasiliano kupitia soko la hisa.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bungeni muswada wa Sheria ya
Fedha ya mwaka 2016.
“Mhe.
Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya
Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta
kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za
mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa
umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati
wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha
Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano
ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na
kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa
kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana
na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya
kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika
kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha
miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
Vile
vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika
kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi
cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe.
Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha
kamati inaishauri Serikali kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha
hisa hizo kuuzwa kwa watanzania pekee na pia kuangalia suala la miezi
sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji
wake.
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA BODI YA MRADI WA MENEJIMEN TI YA MAAFA DAR ES SALAAM.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Bodi ya Mradi ya Menejimenti ya
Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 23,
2016.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu)
Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili
utekelezaji wa mradi huo Juni 23, 2016.
Mkurugenzi
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya
akizungumza jambo katika kikao cha Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa
kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es
Salaam, tarehe 23 Juni, 2016.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
(mwenye suti) akimsikiliza Mtaalam wa Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Kimataifa Bw. Godfrey Mulisa wakati wa kikao cha kujadili
utekelezaji wa mradi huo kilichofanyika katika Ukumbi Ofisi ya Waziri
Mkuu Dar es Salaam, Juni 23, 2016.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
(kulia) akisalimiana na Mchambuzi wa masuala ya mipango wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Kimataifa Bw. Mads Hove wakati wa kikao cha
kujadili utekelezaji wa mradi wa Menejimenti wa Maafa.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa
pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya
Mradi wa Menejimenti ya Maafa mara baada ya kumaliza kikao chao
kilichofanyika Ofisini hapo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QURAAN TUKUFU KUFANYIKA DIAMOND JUBILEE JUMAPILI HII
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo
Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan |
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID MASHINDANO
ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika
Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo
Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo,
Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya
kutekeleza ibadaya funga
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifambalimbali Duniani.
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifambalimbali Duniani.
“
Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko
Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.
Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko
Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.
Katika
mkutano huo na waandishi wa habari, washindani watatu waliwaonyesha
waandishi umahiri wao wa kuhifadhi Quraan, miongoni mwao ni wanafunzi
wawili wenye umri wa miaka kati ya 8 na 10, Abuzar Kholidi kutoka
Tajikistan, na Ahmed Abdallah
kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh
Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia
watumishi wizara ya mambo ya ndani watakiwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi Bi. Lilian Mapfa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo juu ya
masuala mbalimbali ya kiutendaji na uboreshaji mazingira ya kazi kwa
watumishi hao katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Utumishi wa
Umma.
Mtumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Berious Nyasebwa akieleza
changamoto kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria kwa
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano
uliofanyika leo wizarani hapo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma ambayo kilele chake ni leo.
Mtumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Shomari akieleza changamoto
kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria kwa Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo
wizarani hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
ambayo kilele chake ni leo.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Idara na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano
wao uliofanyika wizarani hapo katika kuadhimisha kilele cha Wiki ya
Utumishi wa Umma.
———————————————————————
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi Bi. Lilian Mapfa amewataka watumishi wote wa wizara hiyo kufanya
kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma ili
kuleta ufanisi wa kiutendaji katika kuhudumia wananchi.
Mkurugenzi
Mapfa ameyasema hayo leo wakati akipokea changamoto mbalimbali za
kiutumishi kutoka kwa watumishi wa ngazi tofauti wanaofanya kazi katika
wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
ambayo kilele chake ni leo.
Bi.
Mapfa amesema kuwa ni muhimu watumishi wakafanya kazi kwa ushirikiano
kwa kuwa ndio nguzo kubwa inayoleta ufanisi wa kiutendaji mahali pa kazi
na hivyo kufanikisha majukumu ya wizara.
Katika
kikao hicho ambacho ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma, Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo vya wizara hiyo pia
walishiriki na kupokea kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili
watumishi wao.
Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na malipo ya fedha za likizo, malipo ya kazi kwa muda wa ziada pamoja na vitendea kazi.
Akijibu
hoja mbalimbali zilizotolewa na watumishi hao Bibi. Mapfa amesema kuwa
ofisi yake imepokea changamoto na kero mbalimbali zilizotolewa na hivyo
zitafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya Utumishi wa
Umma.
Aidha
Bibi Mafpa amewataka watumishi wote kuimarisha upendo na amani miongoni
mwao kwani ndio nguzo pekee inayochangia kuleta maendeleo ya kweli ya
wizara na ya mtumishi mmoja mmoja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wabunge kushiriki harambee ya Media Car Wash
Mjumbe
wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es
Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi
tarehe 25 Juni mjini Dodoma. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car
Wash Grace Nacksso
\Msanii
wa Bongo Fleva Inspekta Harun akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha
magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini
Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa
habari Bw. Peter Nyanje. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash
Grace Nacksso.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Wajumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija, Maelezo
————————————————————————–
Na: Frank Shija, MAELEZO
Zaidi
ya waandishi wa Habari 1000 kutoka vyombo mbalimbali kunufaika na Mfuko
wa Bima ya Afya kupitia msaada kutoka kwa Kamati ya Okoa Maisha ya
Waandishi wa habari.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mjumbe wa kamati hiyo Peter
Nyanje wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambe ya
maalum ya kuosha magari Media Car Wash for health itakayofanyika tarehe
25 Juni mjini Dodoma.
“Lengo
la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya fedha takribani shilingi milioni
200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi zaidi ya 1000
hapa nchini.”Alisema Nyanje.
Nyanje
amesema kuwa harambe hiyo itakuwa ni yapili ikitanguliwa na ile
iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijni Dar es Salaam na
kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidai
kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa taabani.
Aliongeza
kuwa na harambee hiyo imekusudia kuhakikisha waandishi wengi zaidi
wanakatiwa Bima ya Afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha
pale wanapofikwa na maradhi.
Kwa upande wake Mratibu wa Media Car Wash Grace
Nacksso ametoa rai kwa Wabunge, viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa
Dodoma kujitokeza kwa wingi katika katika viwanja vya Jamhuri ili
kushiriki katika zoezi hilo ambapo watu wataoshewa magari yao na watu
maarufu wakiwemo wasanii wa Bongo fleva ,Bongo Movie na Miss Tanzania
Lilian Kamazima.
Grace
amesema kuwa wao kama waratibu wa harambee hiyo wamejidhatiti
kuhakikisha harambee hiyo inafanyikiwa ili kutimiza azma ya kusaidiana
miongoni mwa wanataaluma ya habari nchini.
Harambe
ya Media Car Wash itakayofanyika mjini Dodoma inatahudhuriwa na watu
mashuhuri wakiwemo wasanii Joh Makini, Inspekta Haroun, Nikki Wa Pili,
G. Nako, Aunt Ezekiel,Kajala Masanja, Ray Kigosi, Jacob Steven (JB)
pamoja na Miss Tanzania Lilian Kamazima
TOVUTI YA WANANCHI INAVYOTATUA KERO ZA WANANCHI
Na. Immaculate Makilika -MAELEZO
Ni ukweli usiopingika kwamba
dunia imeingia katika maendeleo ya teknolojia yanayopelekea matumizi ya
vifaa vya kisasa na vyenye utaalamu wa hali ya juu katika kufanya
shughuli mbalimbali, ambazo hapo awali zilifanywa kwa kutumia nguvu
kubwa na idadi kubwa ya watu na kwa muda mrefu.
Maendeleo hayo ya teknolojia
yamejidhihirisha katika nyanja nyingi mojawapo ni hii ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano
umerahisisha mawasiliano na unatoa fursa kwa jamii kwa ujumla kuwa huru
zaidi katika kutekeleza majukumu yake.
Serikali inatoa fursa kwa
wananchi kutoa hoja na kero zao popote pale walipo kwa kuanzisha tovuti
katika wizara, taasisi na ofisi zake ambazo zinawezesha wananchi kupata
tarifa muhimu na kwa urahisi kuhusu wizara, ofisi ama taasisi husika na
serikali kwa ujumla.
Katika kuzingatia maendeleo hayo
ya teknolojia ya habari na mawasiliano, mwaka 2006 Rais wa awamu ya Nne
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, aliitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati
huo chini ya Idara ya Habari -MAELEZO kuanzisha, kuratibu na kusimamia
Tovuti ya Wananchi.
Dhamira kubwa ya kuanzishwa kwa
tovuti hii ni kutokana na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara ya 18 toleo la mwaka 2005, maagizo ya Sera
ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003; na dhana ya Serikali
inayozingatia Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ilivyoainishwa
katika Ibara ya 19 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Aidha, tovuti hii inatoa fursa
kwa wananchi kuwasiliana moja kwa moja na Serikali yao, kuwawezesha
watanzania popote walipo duniani kuweza kuwasilisha hoja zao, maoni na
malalamiko serikalini kwa kutumia mtandao wa intaneti .
OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUSIKILI KERO NA MAONI TOKA KWA WATUMISHIWA OFISI HIYO
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.
Eva Mbigi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais
(katikati) ili kuongea na Watumishi wa Ofisi hiyo. aliyekaa kushoto ni
Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil akiongea na
kutolea ufafanuzi kero mbalimbali toka kwa Watumishi wa Ofisi ya Makamu
wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu
ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
Ofisi hiyo Bw. Mbarak Abdulwakil alipokua akitoa ufanunuzi wa kero
mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyakazi wa Ofisi .
HARAMBEE YA OKOA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIKA JUMAMOSI JUNI 25 MKOANI DODOMA
Mjumbe
wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa
habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya
kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini
Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani
shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu
kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa
muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR.
Mratibu
wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa
ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari
waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa
kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June
25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya
fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari
takribani 1000 hapa nchini.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta
Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii
watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.
Mkutano ukiendelea kuhusiana na harambe hiyo.
====== ====== ====== ======
Kamati
ya Maandalizi ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee
maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health,
litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi
June 25, 2016.
Lengo
la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya
Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya
Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson
Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge.
Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya
Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-,
zilichangishwa.
Fedha
hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa
mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu
limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa
bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale
wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi
maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge
kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na
wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili.
Pia
tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze
kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni
ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms
Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja
kushiriki zoezi hilo.
Wasanii
hao ni kundi la Weusi ambalo linajumuisha John Simon Makini a.k.a Joh
Makini, Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili na George Sixtus Mdemu a.k.a G
Nako, wenye asili ya Arusha na wanafanya shughuli zao za kimuziki
Jijini Dar es Salaam pamoja na Haruna Kahena a.k.a Inspekta Haruni.
Wasanii wa Bongo Movies ni pamoja na Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Ray
Kigosi na Jacob Stephen a.k.a JB. Na pia kutoka Orijino Komedi tumepewa
mwakilishi Isaya Mwakilasa ambaye zaidi anajulikana kwa jina la
Wakuvanga na maarufu zaidi kama Mama Bele. Asanteni kwa Kunisikiliza
Judicate Shoo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee
Jeshi la Polisi nchini kuzinduzi mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao
Jeshi
la Polisi nchini, linatarajia kufanya uzinduzi wa mpango wa kuboresha
usalama wa jamii na mali zao, ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu
nchini. Mpango huu utaanza kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi wa
Kinondoni kuanzia mwezi wa Julai mwaka huu na baadaye kuufikisha katika
mikoa yote nchini mwanzoni mwa mwaka 2017.
Uzinduzi huo utafanyika siku ya
Jumamosi, tarehe 25 Juni, 2016 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar
es Salaam, kuanzia saa tatu asubuhi, ambapo Mgeni Rasmi katika uzinduzi
huo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dr John Joseph Pombe Magufuli.
Sambamba na uzinduzi huo wa mpango, Mhe. Rais ataanza kuzindua kituo cha
Mawasiliano ya simu za dharura za Polisi 111, na 112 (Police Call
Centre) na kituo cha Polisi cha kuhamishika kilichopo maeneo ya Coco
beach mkabala na jengo la Coco Plaza, ambacho ni miongoni mwa vituo 13
vitakavyowekwa kwenye maeneo tete kiuhalifu yaliyoainishwa katika mkoa
wa kipolisi wa Kinondoni.
Lengo la Mpango huu ni kuimarisha
usalama wa wananchi katika jamii na mali zao. Huu ni ubunifu wa Jeshi
la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ambapo Jeshi la Polisi
limeamua kuondokana na utendaji wa kimazoea kwa kuanzisha mikakati
mikuu minne ambayo ni kuongeza ufanisi katika shughuli za kipolisi,
kuongeza ubora katika utoaji wa huduma za kipolisi, kuimarisha
mawasiliano na ushiriki wa wadau pamoja na kubuni vyanzo mbalimbali
katika kutafuta rasilimali fedha.
Kupitia mikakati hiyo, Jeshi la
Polisi litaanzisha mpangilio mpya wa ulinzi na doria katika maeneo
yaliyokithiri kwa uhalifu, litaboresha Vituo vya Polisi kuwa katika
muonekano bora na wa aina moja nchi nzima, litaimarisha ubia na sekta
binafsi za ulinzi, litaongeza uharaka wa kufika kwenye matukio ya
uhalifu yanayoripotiwa, litaimarisha na kudumisha misingi ya maadili,
litaweka mifumo thabiti ya kusimamia rasilimali watu, litaimarisha
mawasiliano ya ndani na nje ya Jeshi, na mwisho litatafuta vyanzo
mbadala vya fedha zinazohitajika ili kuliwezesha Jeshi la Polisi
kutekeleza wajibu wake. Vyanzo mbadala vitaongeza wigo wa kutafuta
rasilimali fedha kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Serikali ambayo Jeshi
la Polisi limekuwa likipata kila mwaka.
Aidha, uzinduzi huo utasindikizwa
na Wasanii mbalimbali wa Muziki wakiwemo, Bendi ya Polisi, ya Moto
Band, Manfongo, Ndolela, Man Prince pamoja na wasanii wengine na
burudani mbalimbali zitakuwepo.
Wananchi wote kwa ujumla
wanakaribishwa ili kupata maelezo ya kina na uelewa juu ya mkakati huu
mpya wa kimageuzi ulioandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya
Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery
Bureau-PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na:
Advera J. Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Watumishi wa Umma watahadharishwa kutosambaza Nyaraka za Serikali katika mitandao ya kijamii
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Eliakim Maswi akizungumza na Watumishi wa
Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni
sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dkt. Joel Bendera akizungumza na Watumishi wa
Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni
sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa
Watumishi wa Umma wa mkoa wa Manyara kuhusu hoja mbalimbali
alizozipokea wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma mkoani Manyara.
Afisa
Muuguzi Msaidizi, Mkoa wa Manyara,Bi. Josephine Mosha akiwasilisha
maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe.
Angellah Kairuki wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma mkoani Manyara.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akikabidhiwa ripoti kuhusu kero na maoni
kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa (CWT)-Manyara Bw. Qambos
Michael Sulle ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2016.
…………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
(Mb) amewataka Watumishi wa Umma kuacha tabia ya kusambaza Nyaraka za
Siri za Serikali katika Mitandao ya Kijamii.
Waziri Kairuki aliyasema hayo katika kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.
Waziri Kairuki alisema serikali
inao utaratibu wake wa kusambaza nyaraka kwa waajiri, na taarifa
kumfikia kila mhusika na sio kupitia mitandao ya kijamii.
“Nawakumbusha kuhusu Kanuni za
maadili katika Utumishi wa Umma ambazo kila mtumishi anapaswa
kuzingatia na kuelewa na endapo kama huelewi uliza ueleweshwe” Waziri
Kairuki alisema na kuongeza Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa
Umma lazima zifuatwe.
Aliongeza, hatua zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kusambaza nyaraka kinyume na taratibu, kupitia namba zao za simu.
Waziri Kairuki, pamoja na mengine
alisisitiza waajiri kuwashirikisha Watumishi katika bajeti kupitia
baraza la wafanyakazi ili wajue mambo ya msingi watakayotekeleza na
kuweza kuhoji pale itakapolazimu kufanya hivyo na kwa Waajiri ambao
hawajaunda mabaraza ya wafanyakazi wameelekezwa kuunda mabaraza hayo.
Pia, Waziri Kairuki alikumbusha
kuwa uhamisho usifanyike kiholela, bali kwa sababu za msingi na pale
kibali cha ajira kinapotolewa utekelezaji ufanyike mapema ili huduma
ziendelee kutolewa.
Aidha, watumishi wanaoteuliwa katika nafasi za madaraka wathibitishwe katika kipindi cha miezi sita.
Pamoja na kupata fursa ya
kuongea, na kushauri, Watumishi wa Umma waliandika kero na maoni ambayo
yalichukuliwa ili kufanyiwa kazi.
Kikao hicho kilikua na lengo la
kupokea maoni na kero za watumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 na kilihudhuriwa na
watumishi wote wa mkoa wa Manyara, kupitia uwakilishi.
Wiki ya Utumishi wa Umma ni moja
ya tukio muhimu katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU), ambayo
huadhimishwa kutambua mchango wa watumishi wa Umma barani Afrika katika
kuleta maendeleo, ikiwamo kutatua changamoto zinazowakabili katika
kutekeleza majukumu. Wiki hii huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa
Afrika kwa wakati mmoja.
UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 7 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI
Mtaalamu
wa kujitolea kutoka nchini Japan, Bi.Yuka ITO, akielezea namna
alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa
hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan
waliomaliza muda wao. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.
Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini katika
hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba ( wa tatu kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka
nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla
fupi ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa
Ofisi ya Rais-Utumishi na wawakilishi kutoka JICA.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia
maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya
Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa
kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi
wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Yuka
ITO aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini katika hafla fupi ya
kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi
mapema leo.
SHIRIKA LA I,H,H INSANI YARDIM VAKFI KWA KUSHIRIANA NA JUMUIYA YA MUZDALIFA ZANZIBAR YATOA MSAADA WA FEDHA KWA MAYATIMA ZANZIBAR
Wafanya
kazi wa Jumuia ya Muzdalifat wakitayarisha malipo ya Msaada kwa ajili
ya Watoto Mayatima wanaosaidiwa na Shirika la Misaada la I,H,H,INSANI
YARDIM VAFKI kutoka Uturuki, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya
Haile selasi mjini Unguja.
Baadhi
ya Watoto mayatima wanaopatiwa Fedha za Msaada na I,H,H,INSANI YARDIM
VAFKI kutoka Uturuki,wakishirikiana na Jumuiya ya Muzdalifat
wakiongozana na walezi wao kuchukua fedha zao.Zaidi ya watoto
800,wamepatiwa fedha hizo katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi mjini
Unguja.
Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk akizungumza machache katika
hafla ya kuwa kabidhi Fedha Watoto Mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika
la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,katika ukumbi wa Skuli ya Haile
Selasi Mjini Unguja.
Mfanyakazi
wa Jumuiya ya Muzdalifat akiwakabidhi Watoto mayatima Wanao fadhiliwa
na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,Fedha taslim za
msaada katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
MBUNGE WA JIMBON LA KIKWAJUNI MHANDISI HAMAD MASAUNIN AKABIDHI JEZI ZA MASHINDANO
Muonekane
wa nyuma wa moja ya jezi zitakazotumiwa katika mashindano ya kombe la
Masauni/Jazeera , kutoka maeneo mbalimbali katika Jimbo la Kikwajuni
kama inavyoonekana.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi nahodha wa
timu ya Mkunazini, Ahmed Omari Haji , jezi zitakazotumiwa na timu yake
wakati wa Kombe la Masauni -Jazeera, linaloanza kutimua vumbi leo katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja,Zanzibar. Wapili kulia ni Diwani wa kata ya
Miembeni, Mbaruku Abdallah Hanga.
Nahodha
wa timu ya Kikwajuni Bondeni, Salum Said (kushoto), akipokea jezi
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).
Nahodha
wa timu ya Kikwajuni Bondeni, Salum Said (kushoto), akipokea jezi
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto), akiwa na baadhi
ya viongozi na makocha wa timu zinazotarajiwa kuanza kumenyana katika
mashindano ya Kombe la Masauni-Jazeera, muda mfupi baada ya kukagua
Uwanja wa Mnazi Mmoja utakaotumika kwa mashindano hayo.(Picha na Mpiga Picha Wetu)
NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AZUNGUMZIA MATUKIO YA KIHALIFU YALIYOTOKEA MKOA WA KUSINI PEMBA
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba,
mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi
kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary
Makame.
Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame, akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya
kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao
yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi
Zanzibar.
Makamanda
wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni katika
mkutano kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba,
mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
MWINYIMVUA: Awataka Watumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
akisoma maelekezo kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili ya Utumishi wa
Umma kwa wafanyakazi wa Ofisi yake jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni,
2016 (hawapo pichani) wakati wa maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoadhimishi kila mwaka Barani Afrika Juni 16-23.
Baadhi
ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo.
Baadhi
ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa
Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………………………………………………………………………………………..
Na. wandishi Wetu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua amewataka Wafanyakazi Ofisi ya
Waziri Mkuu kuzingatia maadili na kanuni za Utumishi wa Umma wakati wa
Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Dkt. Mwinyimvua amesema hayo
tarehe 22 Juni, 2016 Ofisini kwake Jiji Dar es salaam, wakati ofisi
yake ikiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kila mwaka
huadhimishwa Juni 16 – 23, 2016 Barani Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi: Kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.
“Kila mtumishi wa umma anapaswa
kuzingatia maadili na sheria za utumishi wa umma ambazo ndio nguzo ya
kuimarisha utendaji kazi na kuimarisha misingi na maadili ya Umma”
alisema Dkt. Mwinyimvua”.
Kuna sheria ya Utumishi wa Umma
ya mwaka 2002, maboresho ya Kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2009 na
miongozo mbalimbali inayoelekeza namna na jinsi mtumishi wa umma
anapaswa kuifuata.
“Nafahamu zipo changamoto nyingi
ambazo zinawapata watumishi wa umma nataka niwahakikishie kwamba,
serikali inazitambua na inazifanyia kazi hivyo nawasii tufanye kazi kwa
bidii kwani tunatambua kauli mbiu ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe
Magufuli ya Hapa Kazi tu inabidi kuitekeleza kwa kufanya kazi na tuache kufanya kazi kwa mazoea”, alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.
Tumie mda wenu kujisomea vitabu,
Magazeti, Vijarida, vitawasaidia kujifunza na kupata maarifa tofauti
ambayo yataweza kuwasaidia kuwa wabunifu katika sehemu zenu za kazi,
elimu na maarifa inapatikana kwa kujisomea tujijengee mazingira hayo
yatawasaidia kuwaongezea ufanisi wa kazi, alisema Dkt. Mwinyimvua.
Kwa mwaka huu maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma yanaadhimishwa na Wizara na Taasisi za Serikali kwa
kukutana na watumishi wa umma na wadau mbalimbali kwa lengo la kupokea
changamoto, maoni, ushauri ikiwa ni lengo la Serikali la kutaka
kuboresha huduma kwa wananchi
No comments :
Post a Comment