Maafisa usafirishaji waaswa kuwa wazalendo
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan akifungua kikao cha maafisa usafirishaji wa
Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kilichofanyika leo Jijini
Dar es Salaam Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo
TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe na kulia ni Mhandisi Elirehema
Mmari.
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Matengenezo TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe akizungumza na maafisa
usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika
kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan.
Baadhi ya cha maafisa
usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali
wakifatilia kikao kati yao na Wakala wa Umeme na Ufundi(TEMESA)
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
( Picha zote na Theresia Mwami-TEMESA)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Maafisa usafirishaji kutoka
Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali wameaswa kuwa wazalendo
kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matengenezo na shughuli za kiufundi
Serikalini.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan
alipokuwa akifungua kikao cha maafisa usafirishaji kutoka Wizara, Idara
na Taasisi mbali mbali za Serikali kujadili changamoto zinazowakabili na
kuzipatia ufumbuzi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia
matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali.
Kaimu Mtendaji Mkuu huyo amesema
kwa hali ilivyo sasa imebainika kuwa Sheria na Kanuni za matengenezo ya
magari na mitambo ya Serikali imekuwa ikikiukwa kwa kiasi kikubwa na
hivyo kuilazimu mamlaka husika kutafuta njia mbadala ili kukabiliana na
changamoto hiyo.
“Lengo letu ni kupata namna bora
ya kutoa huduma ya matengenezo ya kiufundi ya vifaa vya Serikali pasipo
kukiuka Sheria na Kanuni zilizowekwa hivyo basi tunaomba ushirikiano
kutoka kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuleta magari na vifaa
kwetu ili tutekeleze wajibu wetu” alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi Manase ameongeza kuwa
pamoja na uchache wa Wizara , Idara na Taasisi za Serikali
zinazotekeleza Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari ya Serikali kwa
kuleta magari TEMESA ila kumekuwa na changamoto katika ulipaji wa
gharama za matengenezo hali inayosababisha Wakala usiweze kufanya kazi
kwa ufanisi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi Sylivester Simfukwe
amesema Wizara , Idara na Taasisi za Serikali zinatakiwa kuzingatia
Sheria na Kanuni zilizopo kwa kupeleka na kulipa gharama za matengenezo
ya magari na vifaa vya Serikali kwani Wakala huu ndio mshauri mkuu wa
Serikali katika masuala ya kiufundi na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo
itasaidia kuongezeka kwa mapato ya Serikali.
Naye Meneja Usafirishaji kutoka
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Jonathan Mhagama ameiomba Serikali
kuiongezea uwezo TEMESA kwa kuwa na karakana za kisasa ili kuendana na
mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo kwa sasa uwezo walionao
wakala huo ni mdogo ukilinganisha na magari yaliyopo Serikalini.
Mkutano kati ya Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) na maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi
mbalimbali za serikali umekuja mara baada ya kauli kutoka kwa Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa ya kuyataka
magari yote ya Serikali kutekeleza Sheria na Kanuni za matengenzo ya
vifaa vya Serikali.
Timu nne zatinga nusu fainali katika Mei Mosi
Kikosi cha Tamisemi kilichoingia nusu fainali katika michezo ya Mei Mosi.
Kikosi cha Uchukuzi SC kilichotinga nusu fainali kwenye michezo ya nusu fainali.
Kiungo wa Ukaguzi, Mansour Juma
(17) akikokota mpira mbele ya Seleman Kaitaba wa Uchukuzi SC katika
mchezo wa soka katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja
wa Jamhuri Dodoma. Uchukuzi SC walishinda 3-1.
Kipa wa GGM Emmanuel Charles
(mwenye jezi nyeusi) akijiandaa kudaka mpira wa kona uliochongwa na Omar
Said ‘Chidi’ wa Uchukuzi (hayupo pichani). Timu hizo zilitoka sare ya
bao 1-1.
…………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU nne za soka zimeingia hatua
ya nusu fainali kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye atika
uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Timu hizo ni Tamisemi na Tanesco zilizotoka kundi A, wakati za kundi B ni Uchukuzi SC na Geita Gold Mine (GGM).
Nusu fainali hiyo itafanyika
keshokutwa kwa kumshindanisha mshindi wa kwanza wa kundi A na mshindi wa
pili wa kundi B kwa mechi ya saa 8:00 mchana na mechi ya saa 10:00
mshindi wa kundi B ataumana na mshindi wa pili wa kundi A.
Timu zilizoishia kwenye hatua ya makundi ni TPDC, CWT na UDOM za kundi A na za kundi B ni Ukaguzi, CDA na Mambo ya Ndani.
Kwa upande wa netiboli
inayochezwa kwa mtindo wa ligi, timu ya Tamisemi inaongoza kwa kuwa na
pointi sita sawa na Uchukuzi SC, lakini wanamagoli mengi ya kufunga
ambayo ni 76 wakati wenzao wanayo 54, wakifuatiwa na CDA yenye pointi
tatu, huku Tanesco na TPDC wakiwa hawana kitu.
Katika michezo ya awali ya kuvuta
kamba timu ya wanawake ya Uchukuzi SC ilipata ushindi wa chee dhidi ya
UDOM, ambao hawakutokea uwanjani, pia Tanesco wanaume walipewa pointi
baada ya CWT kushindwa kuonekana ulingoni, nayo TPDC wanawake waliwavuta
Tamisemi kwa mivuto 2-0.
Katika mchezo wa bao wanawake
Mayasa Kambi wa UDOM alitwaa ubingwa akifuatiwa na Thea Samjela wa
Uchukuzi SC na mshindi wa tatu ni Catherine Likunguwa wa CDA; wakati kwa
wanaume Omari Said wa Uchukuzi SC alitwaa ubingwa baada ya kumfunga
Lameck Mboje wa Tamisemi katika mchezo wa fainali.
Nayo TPDC ilitoshana nguvu na
Tanesco katika soka kwa kufungana bao 1-1. Tanesco ndio walikuwa wa
kwanza kufunga bao katika dakika 25 na TPDC walisawazisha katika dakika
za nyongeza.
Michuano hiyo itaendelea Jumanne
(Aprili 26,2016) katika soka kwa Uchukuzi SC kuwakaribisha CDA Dodoma
asubuhi na jioni Ukaguzi watacheza na Mambo ya Ndani.
Vyeti vya kuzaliwa havitolewi kwa misingi ya kisiasa
Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI ya Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba imekanusha taarifa zilizotolewa na wananchi ya
kwamba vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya hiyo hutolewa kwa misingi ya
kisiasa .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid
Juma Ali aliyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara ambao
baadhi yao waliodai kwamba kuna ubaguzi juu ya utoaji wa vyeti vya
kuzaliwa
Alisema kuwa kwa kipindi cha
miezi mitano tangu ashike wadhifa huo tatizo la upatikanaji wa vyeti
vya kuzaliwa kwa watoto katika wilaya hiyo limeanza kupatiwa ufumbuzi .
Alifahamisha kuwa kwa
kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vizazi na Vifo , ameanza
kulipunguza tatizo hilo , ambapo watoto wengi wameweza kupatiwa vyeti
kwa wakati na bila usumbufu .
“Mtoto hana chama iweje basi
nimbague kwa misingi ya siasa , natambua wajibu na majukumu yangu kwani
mimi ni mtumishi wa umma na ninawatumikia wananchi wote pasi na ubaguzi
”alifahamisha .
Awali mfanyabiashara Ali Salimu
Ali (Baraka) wa Wingwi alisema kwamba kunahitaji kuangaliwa upya Ofisi
inayohusika na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwani imekuwa ikichelewesha
kupatikana kwa vyeti kwa baadhi ya watoto .
Alieleza kwamba wapo watoto
wamefikia umri wa kwenda skuli lakini hawana vyeti vya kuzaliwa , licha
ya kwamba kumbukumbu zao zipo katika Ofisi ya vizazi na vifo lakini
zimeshindwa kufanyiwa kazi .
“Vyeti vya kuzaliwa bado ni
tatizo , kwani kuna baadhi ya watoto wamefikia umri wa kuanza skuli ,
lakini hawana vyeti , tunaomba hii Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti
uiangalie upya nahisi kama kuna ubaguzi fulani hivi ”alisema .
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na
Madiwani wa Wilaya hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo
kuwataka wafanyabiashara kuwapa ushirikiano wakati wanapokusanya mapato
yatokanayo na biashara zao .
Balozi Amina Salum Ali awataka watendaji Wizarani kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi
WAZIRI
wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali
amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuleta mabadiliko katika utendaji wa
kazi, ili kuifanya Zanzibar iweze kufikia katika uchumi wa kati.
Alisema
kuwa, Wizara imeandaa sera mbali mbali ambazo zinaweza kuifanya
Zanzibar kufikia uchumi wa kati, ikiwa ni pamoja na sera ya biashara,
viwanda na sera ya mpangokazi ambao utekelezaji wake utaanza leo (jana).
Akizuzungumza
na watendaji wa Wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo
tofauti katika ukumbi wa Makonyo Chake Chake, alisema ipo haja kwa
watendaji wake kujibadilisha kwa kuwa na sera madhubuti ya kuwa na
viwanda vikubwa, ambavyo vitaifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati.
Alieleza
suala la kukuza viwanda Zanzibar kuwa, Wizara inataka kukiendeleza
kiwanada cha sukari Mahonda, kujenga kiwanda cha maziwa, kiwanda cha
Zanzibar Milin na kiwanda cha makonyo ambacho hutoa mafuta ya karafuu,
makonyo na mafuta mengine ya mimea.
”Kuna
mambo lazima tuyabadilishe, kwanza utendaji wa kazi wa silka ya kawaida
ambapo wanataraji matokeo yatakayobadilisha maisha ya wananchi,
utendaji utakaotuletea mapato na maendeleo, hii ndio itakayoifanya
Zanzibar kufikia uchumi wa kati”, alisema Balozi huyo.
Balozi
Amina aliwataka watendaji hao kufanya kazi ya ziada katika kubadilisha
Zanzibar na kuwa ya maendeleo zaidi kwa kutumia bidhaa zinazotokana na
kilimo.
Alisema
kuwa, asilimia 85 ya viwanda Zanzibar ni vya wananchi, hivyo ni vyema
juhudi zikatendeka katika kuvibadilisha na kufikia viwanda vikubwa,
kwani Zanzibar inayo nafasi kubwa ya kuzalisha na kuuza bidhaa
zinazotokana na kilimo.
”Tunatakiwa
tufanye kazi ya kuibadilisha Zanzibar kwa kutumia bidhaa zinazotokana
na mimea, kwani uzalishaji unataka bidii kubwa, hivyo ipo haja ya
kuwashirikisha wa Zanzibar na nje yake kwa kutembeleanaili kuona wenzetu
wanafanya nini na sisi tuweze kufuata”, alieleza Waziri huyo.
Waziri
huyo alisema, ipo haja ya kutolewa elimu kwa wajasiriamali na
kuwezeshwa kwa kupitia sehemu za nje zenye maeneo ya kiuchumi ili
kujifunza mambo mbali mbali ambayo wataiga kutoka huko.
”Ili
tufikie huo uchumi wa kati ni lazima Serikali ijipange kuwawezesha
wajasiriamali na wawekeze kupitia sehemu za wenzao ka kuwatembeza,
kupatiwa elimu na soko, jambo ambalo ni changamoto kubwa kwetu”,
alieleza.
Akizungumzia
suala la karafuu alieleza kuwa, Zanzibar imefanya vizuri kwa miaka
mitano iliyopita kwa uzalishali wa zao hilo, ambapo Serikali imenunua
tani elfu 20 kutoka kwa wananchi, ikiwa na thamani ya shilingi billioni
285.89.
”Serikali
imejiandaa vizuri na bei itaendelea kuwa ile ile kama alivyoahidi Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed
Shein, lengo ni kuivusha Zanzibar kwenda katika uchumi wa kati”,
alisema.
Alisema
bei ya ununuzi wa zao la karafuu haijashushwa kama baadhi ya wananchi
wanavyodai, kwani hiyo ni ahadi ya serikali katika kustawisha maisha ya
wakulima wa zao hilo.
Aliwataka
wananchi kuacha kabisa uuzaji wa karafuu kwa njia ya magendo na
waendelee kuuza hapa Zanzibar, kwani fedha zinapoingia serikalini
huwafaa wananchi wenyewe kutokana na huduma za kijamii.
”Pia
tufanye biashara inayokubalika kimataifa, karafuu zetu tusuzichanganye
na makonyo kwa sababu kuna ushindani mkubwa wa soko, hivyo ni vyema
tukazianika sehemu sahihi na kuwa kavu kabisa”, alifahamisha.
Aidha
alisema kuwa, Wizara itakuwa na utaratibu wa kuangalia bei ya vyakula
na kuhakikisha kwamba vyakula vinavyoingia vinakuwa na viwango vya
kimataifa pamoja na usafi.
”Tuko
tayari kuingia katika mapambano, kwa nini tusiwe na viwango vya vyakula
vinavyoingia wakati nchi nyengine wanavyo, tutahakikisha zinaingia
bidha zenye ubora na viwango”, alisisitiza.
Mwandishi
wa habari Salim Ali Mselem kutoka redio Istiqama akiuliza swali,
alisema serikali itapanga sera ipi ambayo itawawezesha wananchi wote
wakati wanapoimarisha upande huu, wananchi hukwama kwa upande wapili.
”Zao
la karafuu limeongezwa bei lakini na kodi inaongezeka kwa
wafanyabiashara siku hadi siku, jambo ambalo wenye kipato cha chini
wanaumia, kwa mfano wafanyabiashara wa sokoni hapa Chake Chake wanatozwa
kodi elfu 60 badala ya elfu 30, kweli wananchi wanawezeshwa hivi”,
alihoji Salim.
Nae
Nasra Mohamedi kutoka ZBC televisheni akitoa hoja yake kuwa, kama
iliyoelezwa wajasiriamali wapo asilimia 85, hivyo serikali itafute njia
mbadala ya kuwawezesha ili kutumia njia ya digital katika kufanya kazi
zao ili kufikia maendeleo zaidi.
Waziri
Amina alikuwa kwenye ziara ya kutembelea vitengo mbali mbali vya
Wizara, ambapo aliona jitihada mbali mbali zinazofanywa na wajsiriamali
na kujionea mambo mbali mbali ambayo hufanywa katika kiwanda cha makonyo
Wawi Chake Chake, ikiwa ni pamoja na mafuta yanayotengenezwa kwa
karafuu na makonyo
Serikali yaipongeza Quality Group kwa kuanzisha Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti
nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo
cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
kituo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHUSM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania
(TCCH) kilichopo katika jengo la Qaulity Center leo jijini Dar es
Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti
nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada
ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)
kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo
hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti
nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada
ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)
kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo
hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo
na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume walipokutaka
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania
(TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi
ya picha kutoka kwa uongozi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania
(TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es
Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group
Limited.Kituo hicho ni duka ambalo linauza bidhaa za sanaa na utamaduni
kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi
ya fimbo maarufu kwa jina la Rungu la Kimasai kutoka kwa Mshauri wa
masuala ya bidhaa za sanaa na utamaduni Bibi. Caroline Kessy wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)
kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Ltd ambao ni wamiliki
wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) Bw. Arif Sheikh
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Shija;WHUSM
Serikali yaipongeza Kampuni ya
Quality Group ltd kwa hatua yake ya kuanzia Kituo cha Uridhi wa
Utamaduni Tanzania (TCCH) ambapo kupitia kituo hicho bidhaa mbalimbali
za Sanaa na Utamaduni zinauzwa ndani na nje ya nchi.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo
hicho kutaiuza nchi, utamaduni wetu, kazi za sanaa na kuongeza ajira
miongoni mwa jamii yetu.
Aidha Profesa Gabriel amesema
kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao na kushirikiana na wadau wote
ili kuhakikisha kwamba wanafikia mafanikio na malengo waliyojiwekea
katika uwekezaji huo.
Aliongeza kuwa ni vyema sasa
Kituo hiko kikafikiria kuanzisha vituo vidogo vidogo katika kanda ili
kurahishisha upatikanaji wa bidhaa hizo na kusaidi wasanii walioko
pembezoni wapate soko la bidhaa zao kwa Serikali ingependa kuona zaidi
wasanii wa ndani wakinufaika na uwepo wa Kituo hicho.
Pia ameuomba uongozi wa Kituo
hicho kuangalia namna ya kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwajengea uwezo wasanii hili
kujenga soko la uhakika,ubora na viwango vya hali ya juu.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu wa Quality Group Limited Bw. Arif Sheikh ameishukuru Serikali kwa
kuonyesha ushirikiano kna imekuwa faraja kubwa kwao kwa kiongozi wa
ngazi ya juu Serikalini kukubali kuja kuzindua Kituo chao.
Sheikh amesema kuwa kuanzishwa
kwa Kituo hicho kumelenga kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania kwakuwa
kinahusika na uuzaji wa bidhaa za sanaa na utamaduni tu, hivyo wasanii
wanayo fursa ya kujipatia kipato kwa kukiuzia Kituo kazi zao.
Hata hivyo Sheikh alisema kuwa
kutokana na ushauri uliotolewa Kampuni yao ipo tayari kutoa ushirikiano
zaidi kwa Serikali pindi watakapohitajika kufanya hivyo ikiwemoi sualaua
la kuwajengea uwezo wasanii wa kazi za mikono.
Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzaia ambacho kwa kingereza kinaitwa Tanzania Center for Cutural Heritage (TCCH) kipo katika jengo la Quality Center, kinamilikiwa na Kampuni ya Qaulity Group Limited ya jijini Dar es Salaam.
DC HAPI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe.
Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo
tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally
Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa
ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona
maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally
Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan
Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016
JESHI LA POLISI LAKEMEA JAMII KUHUSU MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO NCHINI
Ndugu
zangu waandishi wa habari, kwanza niwashukuru kwa ushirikiano ambao
mmeendelea kutupatia, pia niwashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa
ushirikiano wao wa kudumisha amani na usalama hapa nchini. Tumewaiteni
hapa leo kuzungumzia matukio ya ubakaji
Katika siku za hivi karibuni,
Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa
kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji
tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi
ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa
matukio 1765 ukilinganisha na matukio 1585 katika kipindi kama hicho
mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la matukio 180.
Katika matukio ya Januari hadi
machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani
ingawa bado kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuficha watuhumiwa wa
ubakaji na kumaliza kesi hizo kirafiki au kifamilia jambo ambalo ni
kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara aliyoyapata mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la
Polisi nchini linakemea vikali wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo
viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi wanaofumbia macho vitendo hivyo
na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa kupeana fedha kama fidia ili
wamalize kesi kiundugu au kifamilia.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa
Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za kiraia, walimu na Wananchi
kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika kushughulikia vitendo
hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi wanaofanya makubaliano ya
kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia ili kukomesha vitendo
hivyo.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
ANDIKO LA JK KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI
NHIF YAPELEKA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWA MKOANI NJOMBE
Mganga Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dokta Samuel Mgema akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za
madaktari bingwa mjini Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu
wagonjwa mbalimbali kwa mikoa husika, kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali
Profesa Mohammed Bakari
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na
Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa mjini
Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu wagonjwa mbalimbali kwa
mikoa husika,kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed
Bakari.
Baadhi ya watumishi na madaktari pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Mh.
Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali mara
baada ya uzunduzi huo uliofanyika mjini Njombe leo.
………………………………………………………………………………………………..
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirkiana na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya, wiki hii inaendesha zoezi la huduma za madaktari bingwa katika
mikoa ya Njombe na Iringa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa zoezi hilo mkoani Njombe Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed
Bakari amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapelekwa katika maeneo
mengi ambako wananchi wanahitaji huduma za madaktari bingwa ili
kukabiliana na upungufu uliopo.
Amesema pamoja na kuendelea
kutumia huduma hizo za muda za madaktari Bingwa, Serikali kupitia Wizara
ya Afya, itajitahidi kujenga miundo mbinu bora ya sekta ya afya na
kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi walio wengi.
Akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mganga Mkuu wa Serikali, Mganga Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dokta Samuel Mgema, amesema hospitali yake inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo na ufinyu wa nafasi
ikilingwanishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa katika
hospitali hiyo.
Ameomba Serikali iharakishe
mchakato wa kujenga Hospitali mpya ya mkoa ili kukidhi mahitaji ya
wananchi wa mkoa wa Njomba, kwani hospitali inayotumika hivi sasa ya
Kibena ilikuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya na kupandishwa hadi baada
ya kutangazwa kwa mkoa mpya wa Njombe, miaka minne iliyipita.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey
amesema huduma hizo za madaktari bingwa zimekuwa zikitolewa na Mfuko
wake kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupeleka huduma
bora za matibabu kwa wanachama wa NHIF na kwa wananchi kwa ujumla.
Asema hadi sasa huduma hizo
zimeshatolewa katika mikoa 14, ambazo zaidi ya wagonjwa 11,400
wamepatiwa huduma, miongoni mwao zaidi ya wagonjwa 340 walifanyiwa
upasuaji wa kitaalamu.
Amesisitiza kuwa huduma hizo
zinatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi kwa kufuata taratibu za
kawaida za malipo za hospitali husika.
WAKANDARASI WAPIGA MARUFUKU MAGARI YENYE UZITO MKUBWA KUPITA DARAJA LA NYERERE,WAWATAKA WATANZANIA KULITUNZA DARAJA HILO.
Hivi
ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo
kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya
Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi
wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group
and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) Jamal Mruma akitoa ufafanuzi
kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja hilo.Mhandisi Mruma alisema
kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora mkubwa na lina uwezo wa kuhimili
uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa magari yanayoruhusiwa ni yale
yenye tani kumi kushuka chini,”kwa sasa tunadhibiti uzito mkubwa kwa
sababu kuna baadhi ya maeneo bado hayajakamilika ikiwemo na barabara ya
kuingilia Kigamboni,ambako hakuwezi kumudu kupitishwa uzito
mkubwa”,alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja
Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka akizungumzia namna baadhi ya
Madereva ambao wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa
katika daraja hilo kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa
zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.Mhandisi Karimu
amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya
tani 10,kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara
hazijakamili,hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
Daraja
hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi
Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo
kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa
aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji
matunzo.
Mhandisi
alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na
kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF),
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
Muonekano
wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa mbaali kidogo
unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa Kigamboni.Daraja
hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka kati kati ya jiji
la Dar.
SERIKALI YAUNDA KAMATI YA KUANZISHA TUME YA TEHAMA
Waziri
waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ameunda
Kamati ya mpito ya kusimamia uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo ameipa miezi sita kufanya kazi kuanzia
mwezi Aprili, 2016 ya kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi
rasmi.
Katika kuhakikisha kuwa Tume ya
TEHAMA inaanza kazi mara moja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Prof. Faustin
Kamuzora, amewakabidhi wajumbe wa Kamati hiyo Amri ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Na.532 iliyotolewa kupitia gazeti la Serikali Na.
47 la tarehe 20 Novemba, mwaka 2015 iliyoanzisha Tume na Hadidu za Rejea
zinazoainisha majukumu yao. Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia
uanzishwaji wa Tume, kuandaa sheria ya kuanzisha Tume, na kutengeneza
Mpango Mkakati wa Tume. Prof. Kamuzora amewataka wajumbe wa Tume hiyo
kuepuka kuweka mitazamo au maslahi binafsi ya wao wenyewe au ya taasisi
zao katika kipindi cha kuanzisha Tume, bali waishauri Serikali namna
nzuri ya kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaanza kazi ya kusimamia na
kuratibu masuala ya TEHAMA nchini. Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na
Mwenyekiti wao na Katibu wa Kamati ya Kuanzisha Tume ya TEHAMA nchini
ni kama ifuatavyo:
- James Kilaba (Mwenyekiti), Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
- Samson Mwela (Katibu), Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
- Idris Rai (Mjumbe), Makamu Mkuu wa Chuo, SUZA,
- Joan Mbuya (Mjumbe), Mkurugenzi wa Sera na Mipango-Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
- George Mulamula (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-DTBi,
- Juma Rajabu, (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-Maxcom Africa,
- Maharage Chande, (Mjumbe), Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Ofisi ya Rais-President’s Delivery Bureau, na
- Nicolaus Mhonyiwa (Mjumbe), Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA-Ofisi ya Msajili wa HAZINA.
Aidha, Tume ya TEHAMA inatarajiwa
kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo: Kushiriki
katika kushauri juu ya uwekezaji wa TEHAMA nchini kwa ubia na sekta
binafsi; kuwatambua, kujenga uwezo na kuwaendeleza wataalam wa TEHAMA;
kushauri na kushiriki pamoja na wadau katika tafiti za TEHAMA, uwekaji
viwango na ubunifu katika sekta ya TEHAMA; na kushiriki katika kusimamia
miundombinu na programu za kitaifa za TEHAMA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Dkt. Eng.
Maria Sasabo, alisisitiza kuwa Kamati ina kazi kubwa ya kuona namna bora
zaidi ya kuhakikisha kuwa Tume itatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa
ni pamoja na masuala ya uwekezaji; na kusimamia vema viwango vya
wataalamu wa Sekta. Naye Mwenyekiti, Inj. James Kilaba, kwa niaba ya
Kamati alishukuru kwa kuaminiwa na Serikali na pia aliahidi kuwa
watatekeleza majukumu yao kikamilifu. Pia alimalizia kwa kusema,
“hatutawaangusha”.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali
CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa
viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama
chama ambao ni Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa
Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na
Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa
Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa
katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi
mbele ya waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam,
Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum
Makunganya aliyehamia chama hicho.
…………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa
Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa
mikoa ya Mtwara na Dar es
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
Viongozi waliokihama chama hicho ni Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na
Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu,
Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga
CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa
habari.
Wenyeviti
hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa
CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza
rasmi kuwa wanachama wa chama hicho.
Makunganya
alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba
1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi
ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
Wakizungumzia
sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho
kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita
viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri
Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Walisema
sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama
hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali
ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
“Nyie
waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa
Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es
Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama
vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa
uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
Muabhi
akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK
inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya
chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea
misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Muabhi
aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa
kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki
wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea
Bungeni.
“Serikali
ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja
gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni,
wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao
serikalini,”alisema.
Mwenyekiti
wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya
ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi
kutoka kwao.
CHAPTELE WA UCHUKUZI SC AIBUKA BINGWA MARA SABA
Thea Samjela wa Uchukuzi SC (kuilia) akichuana na Regina Mutimangi wa TPDC katika mchezo wa bao.
Omar Said wa Uchukuzi SC (kushoto) akicheza bao dhidi Hamisi Rahis wa Tanesco.
Neema Makassy wa Uchukuzi SC (kulia) akitafakari katika mchezo wa bao dhidi ya Joyce Kimondi wa Ujenzi.
Ally Sule wa Uchukuzi SC(kushoto) akicheza mchezo wa fainali dhidi ya Salum Simba wa Tamisemi. Simba aliibuka bingwa.
Timu ya wanawake ya kamba ya Uchukuzi SC wakiwavuta wenzao wa Ukaguzi kwa mivuto 2-0.
Timu ya wanaume ya Uchukuzi SC wakiwavuta wenzao wa Tamisemi kwa mivuto 2-0.
MARIA STOPES YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA JIJI LA MWANZA NA DAR JUU YA UZAZI WA MPANGO
Mchambuzi
wa Sera na bajeti wa asasi ya Health Promotion Tanzania (HPT), Bw.
James Mlali akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na
Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes
Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango.
Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali
mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi
wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja
jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya
watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo
kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi
ya watu.
Waandishi
wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini
mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia
ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2
yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini
kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Mwandishi
wa wandishi na Muandaaji wa vipindi wa habari wa Redio Free Afrika ya
Mwanza, Migongo akiuliza swali kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Wasimamizi wa Mafunzo hayo kutoka Maria Stopes Tanzania.
Mtaalamu
wa uzazi wa mpango, Bi. Shida Masumbi akiwaonyesha waandishi wa habari
wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam moja ya njia mojawapo inayotumika
katika uzazi wa mpango.
Mhadhiri
wa SJMC- UDSM, Bw. Abdallah Katunzi akitoa mwongozo kwa waandishi wa
habari juu ya mafunzo waliyoyapata waweze kuyafanyia kazi ipasavyo.
Mwandishi
wa habari wa Gazeti la Citizen, Bernard Lugongo akiuliza maswali. Picha
zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – Mwanza.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Cathbert Angelo Kajuna, Mwanza.
ASASI
ya Health Promotion Tanzania (HPT) inayojishuhulisha na ongezeko la
idadi ya watu na uzazi wa mpango imeiomba Serikali kuongeza bajeti ya
uzazi wa mpango ifikie Sh. bilioni sita.
Kauli
hiyo imetolewa na Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi hiyo, James
Mlali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar
es Salaam yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuhusu ongezeko la
idadi ya watu na uzazi wa mpango.
Alisema
asilimia 27 ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na asilimia 25 wanakosa
huduma hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa na Serikali.
Mlali alisema bajeti ikiwa ndogo hata elimu inakuwa ndogo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.
“Bajeti
inayotengwa inatakiwa iendane na ongezeko la idadi ya watu kwa
kuzingatia upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni elimu,afya, na
ajira.
“Pia
ongezeko hili alizingatie hali ya uchumi kwasababu asilimia 42 ya
watoto wamedumaa akili kutokana na ukosefu wa lishe bora,” alisema
Mlali.
Mtaalamu
wa uzazi wa mpango, Shida Masumbi alisema kuna njia tatu za uzazi wa
mpango ambazo ni njia ya muda mfupi, muda mrefu na njia ya kudumu.
Alisema njia za muda mrefu ni kitanzi, kipandikizi na njiti, njia za muda mfupi ni sindano, vidonge na kondomu.
“Pia ipo njia ya kudumu ya uzazi wa mpango ambayo ni mume na mke kufunga kizazi.
“Baadhi
ya njia za kisasa za uzazi wa mpango husababisha maudhi kwa kukosa
hedhi, kuongezeka siku za hedhi au kuona matone madogomadogo ya
damu,”alisema Masumbi.
Alisema
pamoja na maudhi hayo lakini kuna faida ambazo ni kuzuia vifo kwa mama
na mtoto, mama kupumnzika kwa muda mrefu na kujishughulisha na kazi
nyingine za kimaendeleo.
Masumbi alisema mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa na wanaume 300 walijitokeza kufunga kizazi kwa mwaka jana.
No comments :
Post a Comment