Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye
ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto)
akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.
Wataalam kutoka Wizara, taasisi na makampuni ya mafuta kutoka Tanzania na Uganda wakifuatilia
kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi kutoka kampuni ya Total
katika mkutano huo.
kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi kutoka kampuni ya Total
katika mkutano huo.
RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI KIKAO KAZI CHA MAKAMANDA WA POLISI, WANASHERIA WA SERIKALI WAFAWIDHI WA MIKOA NA WAKUU WA UPELELEZI WA MIKOA NA VIKOSI.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na
Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi
cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na
Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi
cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi
ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles
Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola,
Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe ,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusuph Masauni na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili
kwenye ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convention Center kwa ajili ya
ufunguzi wa rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi.
Baadhi
ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi wakati Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa
akiwahutubia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya
kufungua kikao kazi hicho.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua
kikao kazi hicho.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya
kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini
Dodoma.
Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na
Tafrija ya mchapalo baada ya Tigo na samaki samaki kuingia Ubia yafana
Vinywaji murua kabisa |
Warembo wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja na wageni waalikwa wote |
Ulinzi ukiimarihwa kwa wageni waalikwa na wateja wote |
Mtaalamu wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar (kulia ) akiwa katika pozi na wafanyakazi wenzake Ummy Mtiro na Natasha |
Mhudumu wa Samaki akitabasamu na kuwakaribisha wageni waalikwa |
Blogger na mdau wa mitandao ya kijamii John Kiandika akiwa katika pozi na mkewe wakati wa hafla usiku wa jana |
Mmoja ya wageni waalikwa akipata maelezo kuhusu huduma ya Tigo 4g kutoka kwa mhudumu |
Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos |
Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout akifurahi jambo na wafanyazi wa tigo wakati wa hafla hii |
Watangazaji maaruf wa kituo cha Clouds tv Hudson Kamoga na Sam sasali wakiwa pamoja kupata maelekezo kuhusa huduma ya intanet ya kasi ya Tigo 4G kwenye hafla hiyo. |
Mhudumu akiandaa chakula |
Wahudumu wa samaki samaki wakiwa katika pozi |
wadau wakiwa katika pozi |
Taswira ukumbini |
Mdau John kiandika na mkewe wakipata maelezo zaidi kuhusu huduma ya Tigo 4g |
wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja |
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania,ikijulikana kama“nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”.
………………………………………………………………………………………………………
Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedhaza kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music ( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na Hivi karibuni Tigo imezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima, na unatarajiwa kuzindualiwa nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya minara mapya 500 yenye mtandao wa Tigo nakufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongezauwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini.
Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 10 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwawateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na Amerika yaKusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani.
Ukiwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokana na mazao ya
baharini na vinywaji nchini Tanzania, Samaki Samaki inamiliki
migahawa mitatu ambayo ipo Mlimani City
(Ubungo/Mwenge),
City Centre (kwenye makutano ya Barabara ya Samora na Mirambo) na
Samaki Samaki kwenye Barabara ya Haile Selassie.
Tangu
kuanzishwa kwa tawi la Mlimani City mwaka 2007 tumeshuhudia kupanuka
kwa Migahawa ya Samaki Samaki hadi matawi miwili zaidi ndani ya jiji
la Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wake,
kuongezeka kwa wateja ambao wanafikia hadi 1,000 kwa siku ndani ya
matawi hayo, kuongezeka kuimarika kwa nembo yetu ya biashara na
kutambuliwa na umma, kupatikana kwa fursa za ajira kwa wazawa, jamii
kutuunga mkono kupitia Mfuko wa Samaki Samaki ( Samaki Samaki
Foundation) ambao unalenga kuwasaidia wahitaji kwa kutoa misaada ya
kuwajibika kwa jamii, jamii imeweza kutufikia kwa kutumia video na
muziki uliorekodiwa katika kukuza nembo yetu kupitia Samaki Samaki
Fleva na kuuza bidhaa zetu nyingine ambazo hazihusiani na chakula
zikiwemo kofia, fulana na CD za muziki.
Dira ya Samaki Samaki ni kushikilia nafasi yake nchini Tanzania kwa kukua hadi mikoa mingine nchini na hata baadaye kusambaa hadi kona nyingine za Afrika na dunia kwa ujumla. Kwa hivi sasa inaangalia Mwanza na Arusha kama vituo vya kuanzia kusambaa hadi mikoa mingine.
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilala Azzan Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini
Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje
kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Ahmed Shabiby wa Gairo
(kushoto) na Suleiman Ahmed Saddiq wa Mvomero, kwenye viwanja vya bunge
mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas
Gama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jovago: to reach our goals in 2016, Setbacks in Tourism sector should not be looked into one perceptive
With the strategies to increase 2 Million number of Tourist arrivals in 2017; JovagoTanzania explains that the gap in Tanzania’s tourism sector should be one of the core factors for development in 2016/2017.
Addressing journalists in Dar Es
Salaam, Lilian Kisasa, Jovago’s Pr and Marketing Manager, exposed the
statistics from Tanzania Tourism board which shows that, the number of
tourist arrivals increased to 1,077,058 in 2012, 1,095,884 in 2013 and
1,140,156 (2014). This progress is a promising signs that Tanzania is
close to reaching its goal of 2M arrivals in 2017.
“We can increase the number
of visitors by not looking at just one category; we really need to focus
on the purpose of visits, how to improve infrastructure and what kind
of hospitality we should provide”. She added
Nevertheless, the statistics from
the Tanzania Tourism Board shows that almost 56% of international
travelers use airport as a mode of transport, only 38% use roads, while
0.5% opt for railway and the remaining travel by Water. This shows there
are still unequal improvements in terms of the transport systems in the
country.
However, she added that in order
to improve the direct contribution of the tourism sector in 2016, there
is need to promote domestic tourism; which covers only 40%.
International tourists contribute to the remaining 60%.
In addition, the Country Manager of JovagoTanzania Mr
Andrea Guzzoni noted that 2016 is a year of change and improvements.
According to Andrea, there are trends in visitors’ preferences, with the
bottom line being value for money.
Jovago has planned to promote the
best secured and classic accommodation in Tanzania in 2016. The leading
online booking company noted that Wireless services, swimming pools,
airport pickup services, Ac, free breakfast and the best customer
service are top of the determining factors in the hotel industry.
The statistics shows that 80% of
visitors travel for leisure, recreation and holiday, while only 5%
travel for business and professional purposes and the rest travel to
visit relatives and in transit. There is therefore need to improve
services that suits all of the travelers’ needs
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MNH- YAWEKA MIKAKATI KUHAKIKISHA WATOTO WANAOZALIWA NA MATATIZO YA KUTOSIKIA WANAPATIA MATIBABU.
Mtaalam
wa masikio Fayaz Jaffer akitoa elimu kwa wazazi / walezi , jinsi ya
kutunza kifaa kinachomsaidia mtoto mwenye matatizo ya kusikia kuweza
kusikia na kuwasiliana. Mtaalam huyo ametoa elimu hiyo leo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- alipokuatana na wazazi ambao watoto
wao walifanyiwa upasuaji nchini India na kuwekewa kifaa hicho.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa
Lawrence Museru akielezea mipango ya MNH katika kuhakikisha huduma hiyo
inakuja kutolewa hapa MNH kwa siku zijazo
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza mtaalam wa Masikio Fayaz Jaffer leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH.
Kaimu
Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru pamoja na Mtaala wa masikio
Fayaz Jaffer wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao
walifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum cha kuwasaidia kusikia ili
kuweza kuwasiliana.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Museru ( katikati) akiwa na Mkuu wa
Idara ya Masikio , Pua na Koo Daktari Edwin Liyombo ( kushoto ) na Fayaz
Jaffer .
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Hospitali
ya Taifa Muhimbili-MNH- imeweka mikakati ya kuhakikisha watoto
wanaozaliwa na matatizo ya kutosikia wanapatia matibabu hayo katika
Hospitali hiyo ili kuwawezesha watoto wengi wenye matatizo hayo kupata
huduma hiyo kwa wakati.
Mikakati
hiyo imeelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
MNH Profesa Lawrence Museru wakati akizungumza na wazazi / walezi ambao
walifika MNH kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao ambao wana
matatizo ya kusikia sanjari na kupata maoni mbalimbali kutoka kwa
wazazi hao.
Akifafanua
Profesa Museru amesema kimsingi mahitaji ya matibabu hayo ni makubwa na
upasuaji huo haufanyiki nchini hivyo wagonjwa hutegemea matibabu hayo
nje ya nchi na ambayo ni gharma kubwa .
“
Mpango uliopo sasa ni kuhakikisha huduma hiii inafika hapa MNH ili
wagonjwa wenye matatizo hayo waweze kutibiwa hapa nchini kwasababu tuna
wataalam wa kutosha , pia naamini hatua hiyo itawasaidaia wananchi wengi
kupata matibabu hayo ” amesema Profesa Museru.
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Masikio ,Pua na Koo wa MNH Daktari Edwin
Liyombo amesema tayari dokezo limeandaliwa ili kuiomba serikali
kuanzisha program maalum itakayowasaidia Madaktari kupata mafunzo pamoja
na kupata vifaa tiba ili upasuaji huo uweze kufanyika hapa nchini.
Kwa
mujibu wa Daktari Liyombo mgonjwa mmoja akipelekwa nchini India kwa
ajili ya kufanyiwa upasuaji hugharimu kati ya Shilingi Milioni 85 hadi
Milioni 100 lakini endapo matibabu hayo yatafanyika hapa nchini gharama
itapungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia
kuhusu utaratibu wa kukutana na wazazi ambao watoto wao wana matatizo
ya kusikia, Daktari Liyombo amesema utaratibu huo ni endelevu kwani una
lenga kufuatilia maendeleo ya mtoto na kumuwezesha mzazi kupata ushauri
wa kitaalam , leo zaidi ya wazazi 40 wamejitokeza MNH kwa ajili ya
kukutana na watalaam .
StarTimes yawaletea wateja wake tamthiliya ya ‘Scars’
Meneja
wa Maudhui na Vipindi wa StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
wa tamthiliya ya ‘Scars’ itakayoanza kuonekana siku ya Jumatatu ya Mei
2, 2016 kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. Akimsikiliza kwa makini
katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Uhusiano wa Umma, Bw.
Muddy Kimwery.
- Ni tamthiliya inayohusu simulizi na visa vya kweli katika maisha ya watu.
- · Itaonekana katika chaneli ya StarTimes Swahili, mahususi kwa vipindi vinavyotumia lugha ya Kiswahili inayoonekana pia nchini Kenya.
- · StarTimes yahamasisha watanzania kuchangamkia fursa kwa kutengeneza filamu na tamthiliya ili ziweze kuonekana kupitia chaneli hiyo ili kupanua wigo wa mashabiki wao.
Katika kuboresha maudhui
yanayotumia lugha ya Kiswahili, kampuni ya StarTimes Tanzania kupitia
chaneli yake mahususi kwa vipindi vya Kiswahili ya StarTimes Swahili
imewatangazia wateja wake ujio wa tamthiliya mpya na ya kusisimua ya
‘Scars au Makovu’ itakayoanza kurushwa siku ya Jumatatu ya mwezi Mei 2,
2016 saa 2:30 usiku.
Akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa tamthiliya hiyo Meneja wa Vipindi na
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri amebainisha kuwa
tamthiliya ya ‘Scars’ itakuwa ni ya aina yake na kusisimua zaidi kwani
inagusa zaidi maisha halisi ya kila siku.
“Tamthiliya hii ni tofauti na
zingine kwani ndani yake ina visa na simulizi za kweli kabisa za maisha
ya wahusika waliocheza ndani yake. Masuala kama ya changamoto mbalimbali
wanazopitia watu kwenye familia zao kama vile mateso, udhalilishaji na
unyanyasaji wanaopitia wanawake katika ndoa zao. Haya yote yatakuwa
yakisimuliwa na kuonekana kwa wateja na watazamaji wa chaneli ya
StarTimes Swahili.” Alielezea Bi. Kimweri
Meneja huyo wa Maudhui katika
kampuni hiyo inayotoa huduma ya matangazo ya luninga kwa njia ya
dijitali alifafanua zaidi kuwa, “Lengo kubwa la kuanzishwa na kuwepo kwa
chaneli hii mahususi kwa vipindi vya Kiswahili si tu kuwaburudisha
wateja wetu kwa maudhui mazuri bila pia kukuza lugha ya Kiswahili kwani
chaneli hii inaonekana katika nchi za Tanzania na Kenya. Pia hutoa fursa
kwa watayarishaji na wasanii wa vipindi vya Kiswahili baina ya nchi
hizi. Hivyo basi hii ni fursa kubwa ya kufurahia wasanii wetu na
kuipaisha lugha yetu ya Kiswahili ambayo kwa sasa inazidi kupaa katika
anga za kimataifa.”
“Nina imani kubwa na tamthiliya
hii ya ‘Scars’ kwamba itapendwa sana na wateja wetu kwani inagusa maisha
halisi kwa simulizi zitakazopatikana ndani yake. Katika uchaguzi wa
tamthiliya tunazotaka zionekane kwa wateja wetu huwa tunazingatia sana
suala la ujumbe na mafunzo yanayopatikana ndani yake na si burudani
pekee. Hivyo, basi ningependa kuchukua fursa hii kuwataka wateja wetu na
watanzania wapenda tamthiliya tamthiliya kukaa mkao wa kula na kutega
macho ya mbele ya luninga zao ifikapo siku ya Jumatatu na zinginezo kila
ifikapo saa 2:30 usiku kwenye chaneli ya StarTimes Swahili. Nawaomba
walipie kwani malipo yetu ni nafuu ili kila mtu aweze kufurahia huduma
zetu.” Alihitimisha Bi. Kimweri
Mbali na tamthiliya mpya ya
‘Scars au Makovu’ pia kupitia chaneli ya StarTimes Swahili ambayo
inaonekana kwenye kisimbuzi cha kampuni ya Startimes kwa nchi za Kenya
na Tanzania pia kuna tamthiliya moto moto zinazoonekana kwa sasa kama
vile; Urembo, Fihi, Majaribu, Kijakazi, Majaribu, Kivuli na Sumu la
Penzi.
Chaneli hii imeanzishwa mahususi
kabisa katika kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya lugha ya Kiswahili
ambapo lugha hiyo inazungumzwa katika nchi nyingi za Afrika ya Mashariki
na Kati. Kupitia chaneli hii si tu kukuza lugha ya Kiswahili bali pia
ni fursa kubwa kwa wasanii kuonekana na kujitangaza kupitia kazi zao ili
ziweze kuonekana katika soko la Afrika ya Mashariki. Hivyo basi hii
fursa kubwa kwa wasanii wa nchini Tanzania kuchangamkia faida zinazokuja
na matangazo ya dijitali kwa kupeleka kazi zao katika kampuni ya
StarTimes ili ziweze kuonekana hewani.
Ndugai akabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la
Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda
wake. Alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11)
wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika
Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt
Thomas Kashililah
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Bunge la Seniti la
Burundi Mhe Reverien Ndikuriyo wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na
moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Arusha.
pika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega (katikati) na Spika wa
Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi
na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Arusha.
………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.
Spika
Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11)
wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika
Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.
Mkutano
huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Spika wa
Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge
la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika
Mashariki.
Akiukabidhi
Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano
walimuonesha katika kipindi chote cha Uongozi wake na kumtakia kila la
kheri Mwenyekiti mpya wa jukwaa hilo.
Maspika
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa
Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo
Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.
Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa
hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine
katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.
Pamoja
na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali
yanayohusiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la
Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa
mwaka 2008.
MSAJILI WA HAZINA ATOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UMILIKI WA HISA ZA SERIKALI KATIKA SHIRIKA LA USAFIRISHAJI DAR ES SALAAM (UDA)
Msajili
wa Hazina Bw. Laurence Mafuru akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kuhusu umiliki wa hisa za Serikali katika
Shirika la Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na kubainisha kuwa Serikali
inamiliki hisa 49% katika shirika hilo kinyume na upotoshaji unaofanywa
na baadhi ya watu kuwa Serikali imeuza hisa zote kwa muwekezaji. Kulia
ni Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Gerald Chami.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Msajili wa Hazina leo
jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu faida za Ripoti ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kuongeza
uwajibikaji na tija kwenye utumishi wa umma hasa kwa kuzingatia
mapendekezo ya ripoti ya mwaka 2014/2015.
WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Jiji la Dar es salaa kunufaika na upatikanaji wa maji.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack Kamwela akijibu swali la
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua
ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es
salaam.
Naibu
waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na
walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum)
alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo
Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akifafanua jambo Bungeni leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa Ubungo Saed Kubenea akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma
alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika
Jiji la Dar es salaam.
Silafu
Jumbe Maufi (Mbunge Viti Maalum) akiuliza swali leo Bungeni mjini
Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali iatamaliza tatizo la upungufu wa
vifaa vya kufundishia somo la TEHAMA na walimu wa masomo hayo katika
mkoa wa Rukwa.
Wabunge walio katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
WAZIRI WA NISHATI NA MAENDELEO YA MADINI NCHINI UGANDA MHANDISI IRENE MULONI AWASILI NCHINI TANZANIA
Waziri wa Nishati na
Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, aliwasili
nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake kwa lengo la kushiriki Kikao cha
Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka
Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao hicho
kinafanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Julius Nyerere.Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda,
Mhandisi Irene Muloni, aliwasili nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake
kwa lengo la kushiriki Kikao cha Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa
Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga. Kikao hicho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia)
akisalimiana na Ofisa kutoka Ubalozi wa Uganda Nchini Tanzania
Nyiransanziyera Fredah (kushoto) aliyewasili katika Uwanja wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kumpokea Waziri wa Nishati na
Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk.
Fred Kaliisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda
Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa
Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni,
kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na
ujumbe wake.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia)
akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya
ujenzi wa mabomba kutoka Uganda, Habumugisha Johnbosco (kushoto)
aliyeambatana na ujumbe wa Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini
Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kushoto)
akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy
Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini
Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia )
akizungumza na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini
Uganda, Mhandisi Irene Muloni (kushoto) mara baada ya Waziri huyo
pamoja na ujumbe wake kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere.
TANZANIA COMMENDED FOR ENHANCING GIRLS EDUCATION IN ICT.
The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz(centre) poses for a picture with four student
girls from Tanzania who participated in the Girls in ICT Day
Celebrations in Addis Ababa under the auspices of International
Telecommunication Union ITU held at AU Headquarters yesterday.
From
left, Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school, Dorice Mhanga
from Kleruu Secondary School in Iringa, Khudhaima Bedran Sultan from
Chasasa Secondary school in Pemba and Elician Yohana Kapi from Nyankumbu
Secondary school in Geita .
(photo courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia).
……………………………………………………………………………………………..
Tanzania
has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the
country including rural areas with the aim of achieving gender balance
by availing opportunities for girls to acquire skills in science and
technical subjects including Information and Communication Technology
(ICT).
The
compliments were given yesterday (April,28,2016) by the International
Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew
Rugege when officiating at the opening ceremony of the International
Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in
Addis Ababa, Ethiopia.
“
Your Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to
convey my regards to your government for its efforts in promoting ICT
education for girls as witnessed by four girls who travelled all the
way from Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls,
excelled in ICT competition organized by ITU,” he said praising the
girls for successful creating useful IT applications that could be used
for provision of social services.
The
four girl students from Tanzania who were invited for the occasion in
the Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from
Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from
Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary
school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary
school in Dodoma.
Mr.
Rugege said ITU estimates a skills shortfall of over two million jobs in
the Information and communication technology (ICT) sector within the
next five years adding that, Girls and young women who learn coding,
apps development and computer science will not only be well-placed for a
successful career in the ICT sector, but ICT skills are rapidly
becoming a strong advantage for students in just about any other field
they might choose to pursue.
“
Girls in ICT Day reminds us that ICTs help to improve the lives of
people everywhere and especially in Africa – through better health care,
better environmental management, better communications, and better
educational systems that transform the way children and adults learn,”
he said adding that the technology has been instrumental in creating job
opportunities to African youths.
The
girls participating in the school workshops were invited to the African
Union in Addis Ababa HQ for a half day celebration where they had the
opportunity to present their work and what they learned during the
workshops to the ITU officials, the diplomatic community, AU Staff and
ITU Delegates.
Six
girls from various secondary schools in Tanzania who excelled in ICT
competition coordinated by the ITU were invited for the ADDIS Girls in
ICT Day celebration having emerged winners from zonal and eventually
national ICT contests. Two of them could not travel to Addis Ababa to
join their colleague due to delay in visa application.
The Four Girls are scheduled to return home on Saturday.
ITU’s
Girls in ICT Day, is a global initiative aimed at raising awareness
among girls and young women about the importance of digital skills for a
successful professional career in all sectors and encouraging them to
consider studies and careers in Information and Communication
Technologies (ICT).
.ITU is the United Nations specialized agency for information and communication technologies – ICTs.
An
organization based on public-private partnership since its inception,
ITU currently has a membership of 193 countries and almost 800
private-sector entities and academic institutions. ITU is headquartered
in Geneva, Switzerland, and has twelve regional and area offices around
the world.
ITU membership represents a
cross-section of the global ICT sector, from the world’s largest
manufacturers and telecoms carriers to small, innovative players working
with new and emerging technologies, along with leading R&D
institutions and academia.Founded on the principle of international cooperation between governments (Member States) and the private sector (Sector Members, Associates and Academia), ITU is the premier global forum through which parties work towards consensus on a wide range of issues affecting the future direction of the ICT industry.
From Freddy Maro,
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia
HALMASHAURI ZA MASASI, NANYAMBA KUANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO SEKTA ZA UMMA AWAMU YA KWANZA MKOANI MTWARA
MKUU
wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala akizungumza
wakati wa kuhitisha mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la
Misaada la Marekani (USAID) na kutekelezwa katika Halmashauri 97 katika
mikoa 13 nchini. Uzinduzi wa mradi wa PS3 ngazi ya mkloa wa Mtwara
ilifanyika juzi mjini humo.
Mkoani
Mtwara mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
itahusisha Halamshauri ya Nanyamba na Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Awamu ya pili ambayo itatekelezwa
mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na
Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji
wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya
yaTandahimba.
mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na
Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji
wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya
yaTandahimba.
Baadhi
ya Maofisa wa Mradi wa PS3 pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya Mkoani Mtwara wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Rasilimali Fedha, Dk Daniel Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mshauri
wa Mradi katika Masuala ya Elimu, Dk Rest Laswai akifafanua jambo juu
ya uimarishaji mifumo ya sekta za Umma katika nyanja ya elimu.
Continue reading →Katibu wa Bunge aongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki.
Mwenyekiti
wa kikao cha Makatibu wa Mabunge wa Afrika Mashariki Dkt. Thomas
Kashilila akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika
Mashariki leo jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa kamati ya maadalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki Dkt.
Thomas Kashilila (kushoto) akiongoza kikao hicho leo jijnii Arusha.
Kulia ni Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Bw. Keneth Madete.
Mkurugenzi
wa Uhusiano wa Kimataifa na Itifaki wa Bunge la Tanzania Jossey
Mwakasyuka (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Katibu wa Bunge la Tanzania
ndugu Emmanuel Mpanda
Makatibu
wa Mabunge ya Afrika Mashariki wakitoka ukumbini baada ya ufunguzi wa
kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki leo
jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa kikao cha Makatibu wa Mabunge wa Afrika Mashariki Dkt. Thomas
Kashilila (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya Makatibu wa Mabunge ya
Afrika Mashariki wakiwa Jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Bw. Keneth Madete na Katibu wa Bunge la
Kenya Bw. Justine Bundi (katikati).
Makatibu
wa Mabunge ya Afrika Mashariki na Baadhi ya Maafisa wakiwa katika picha
ya pamoja baada ya ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya mkutano wa
Maspika wa Afrika Mashariki leo jijini Arusha.
Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
…………………………………………………………………………………………………………Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani Singida ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema ufadhili huo umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na Damankia (Ikungi). Vingine ni Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).“Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia kutatua uhaba mkubwa wa maji katika eneo hili la mkoa wa Singida ambalo kwa kiwango kikubwa limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine iliyopita,” alisema Lugata.Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji miongoni mwa wilaya nyingi za Singida umesababisha wakiazi wake kupoteza muda mwinmgi kutafuta bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo Tigo inaamini kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba sugu wa maji uliolikumba eneo hilo na kuchangia kukua ustawi wa jamii kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12 vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.
TANAPA YAKABIDHI MABATI 2800 KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA NA ZAHANATI WILAYANI SERENGETI
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa
Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa
TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani Serengeti.
Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa
TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani Serengeti.
……………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – Dar es Salaam
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara
15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara
15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Akikabidhi msaada huo Meneja ujirani mwema wa Tanapa, Ahmed Mbugi amesema
TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo ya Elimu na Afya katika wilaya
hiyo.
TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo ya Elimu na Afya katika wilaya
hiyo.
“Mabati haya ni msaada ambao tumeutoa kwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni
muendelezo wa misaada tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za
maendeleo wilayani hapa” alisema Mbugi.
muendelezo wa misaada tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za
maendeleo wilayani hapa” alisema Mbugi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Naomi
Nnko aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma
masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za
sekondari wilayani humo.
Nnko aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma
masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za
sekondari wilayani humo.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Juma Keya alishukuru
kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika mengine ndani na nje ya Wilaya
ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri hiyo kuleta maendeleo katika jamii.
kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika mengine ndani na nje ya Wilaya
ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri hiyo kuleta maendeleo katika jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Maftah
Mohammed aliliomba shirika hilo
kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari zilizopo
wilayani humo.
Mohammed aliliomba shirika hilo
kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari zilizopo
wilayani humo.
Mpaka sasa TANAPA imeisaidia Halmashauri hiyo kwenye ujenzi wa maabara
katika Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule za
Sekondari.
katika Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule za
Sekondari.
UVCCM: SUMAYE ACHA KUMBUGHUDHI RAIS DK. MAGUFULI HUNA VIWANGO
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja wa vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Waziri mstaafu Frederick Sumaye,
hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa
kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala
ya utawala.
Sumaye ametakiwa
amuache Rais Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa
dhamana ya kuwa Waziri Mkuu lakini hakufikia hata thekuthi ya utendaji
unaofanyika sasa.
Hayo yamesemwa jana
na Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na
wanachama wa CCM wa kata mbili za Kwandele na Mbichi jimbo Rombo mkoani
Kilimanjaro.
Shaka alisema
anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflisi wanaojaribu kukosoa
utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao
wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi
wameyasahau.
Alisema kama yupo
waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na usimamizi wa
serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye.
“Amekuwa waziri mkuu
kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye
waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961
“alisema shaka.
Aidha Kaimu huyo
katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk Magufuli
katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua dhidi ya
mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema wakati Rais
Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi iuwatumikia wananchi
kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema kina sumaye na wenzake
wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya
kusaka umaarufu wa kisiasa.
“Sumaye aacha
kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda wakati
ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage na
karanga “alisema
Pia shaka aliwataka
wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa
jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na
hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
“Siku zake za kuitwa
mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui anavhokufanya wala
hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo
apigiwe mwaka 2020 “alisisitiza shaka
Akizungumza katika
mkutano huo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma
aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya
kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa nafasi mbali mbali kwa
ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu alisema ikiwa
wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si
jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au
ujamaa.
“Tunachotaka
kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa
Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawahyika ,
tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni
kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii “alisema Raib.
Jumla ya wananchi wapya 103 wa
CCM na jumiya zake walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata
nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na
mahare wilaya Rombo.
JAMII YASHAURIWA KUWAPELEKA WATOTO KWENYE CHANJO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mpoki Ulisubisye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
………………………………………………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo- Maelezo
Jamii imeshauriwa kuwapeleka
watoto wote wanaostahili kupata chanjo walio chini ya umri wa miaka
mitano katika vituo vya afya ili waweze kupatiwa chanjo ili kuweza
kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto.
Kauli hiyo ilitolewa Aprili 27,
mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Mpoki Ulisubisye wakati wa maadhimisho ya wiki ya chanjo nchini
yaliyofanyika kwenye hoteli ya Serena Jijini Dares Salaam.
Alisema utoaji wa chanjo hiyo
umeaanza Aprili 25 hadi 29 mwaka huu na kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘
Kumilisha Chanjo,Epuka Ugonjwa wa Polio’. Hivyo vItuo vya kutolewa
kutolea huduma za afya vinafunguliwa kuanzia saa 2: 00 asubuhi hadi saa
11.00 jioni.
“ Kila mmoja wetu anawajibu wa
kuhakikisha mtoto wake , mtoto wajirani au mlengwa mwingine yeyote
anapewa haki ya chanjo ili kumzuia asipatwe na maradhi ambayo yanakingwa
na chanjo au asiwe na hatari kwa wengine kwa kuwaletea ugonjwa,”
alisema Dkt. Ulisubisye.
Aliongeza kuwa chanjo ni
mikakati muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto,
hivyo hupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na taifa kwa ujumla
lingetumia katika kutibu maradhi yanatokana na magonjwa yanayozuilika
kwa chanjo.
Alisema chanjo huzuia takribani
vifo milioni mbili hadi tatu kwa kila mwaka kutokana na maradhi
yanayokingwa kwa chanjo duniani.
Aliyataja maradhi hayo kuwa ni
Dondakoo, Surua ,Polio,Kifua Kikuu,Kifaduro,PepoPunda,Homa ya ini,homaya
uti wa mgongo,kichomi na kuhara.
SERIKALI YAZIDI KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA NCHINI
27/04/2016
Kufanikiwa kwa juhudi za
Kutokomeza ugonjwa wa Malaria kutaufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri na
salama pa kuishi kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuwawezesha
mamilioni ya watu kufikia malengo yao kimaisha.
Hivi karibuni Tanzania
imeungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Malaria
duniani ambapo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu
wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.
Takwimu kutoka Shirika la Afya
ulimwenguni WHO za mwaka 2002 zinaonyesha kuwa kila mwaka watu kati ya
milioni 300 hadi 500 duniani wanapata ugonjwa wa malaria, kati yao watu
milioni moja na nusu hufariki kutokana na ugonjwa huo.
Kulingana na takwimu hizo
katika bara la Afrika watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano
ndiyo wanaathirika zaidi na ugonjwa wa malaria ambapo kila mwaka watoto
milioni tano wanakufa kwa ugonjwa huo barani Afrika.
Kwa mujibu wa WHO idadi vifo
vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hadi kufikia mwaka 2013 vilipungua
kwa takriban asilimia 20 tu duniani kote katika muongo mmoja uliopita
ambapo theluthi moja ya nchi 108 ambazo malaria ilikuwa imeenea
zilitarajiwa kutokomeza ugonjwa huo katika kipindi cha miaka 10.
Kufuatia ufanisi mkubwa
uliopatikana chini ya malengo ya maendeleo ya milenia, ni muhimu
kuuendeleza ufanisi huu na kuutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria chini
ya malengo ya maendeleo endelevu.
Kauli mbiu hiyo inaenda
sambamba na lengo la kuwa na ulimwengu usio na malaria lilijumuishwa
katika mkakati wa kiufundi wa kimataifa kwa ajili ya malaria 2016 hadi
2030, ulioidhinishwa Mei mwaka uliopita na baraza kuu la Afya duniani.
Mkakati huo unalenga kupunguza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya malaria
ulimwenguni katika kipindi cha miaka 15 ijayo.
Continue reading →Uchukuzi SC yawa ya tatu, kipa adaka penati 3
Kipa
Willium Barton wa Uchukuzi SC akikaa tayari kupangua penati ya kipa
mwenzake wa Tanesco Hashim Yahya. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa
penati 3-2.
Abubakar Mwamachi (9) wa Uchukuzi SC akikokota mpira huku mlinzi wa Tanesco Juma Rajabu akiwa ameshika ardhini.
Wachezaji
wa michezo mbalimbali wa timu ya Uchukuzi SC wakishangilia baada ya
timu ya soka kutwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2 dhidi ya Tanesco.
Omary
Kitambo (4) wa Uchukuzi SC akiwania mpira uliopigwa na Stanley Uhagile
wa Tanesco. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.
…………………………………………………………………………………………………….
- Kamba wanaume watwaa ubingwa
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya soka ya Uchukuzi SC jana
ilitwaa ushindi wa tatu wa mashindano ya Mei Mosi, baada ya kuwashinda
Tanesco magoli 3-2 kwa mikwaju ya penati, katika mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Ushindi wa Uchukuzi SC
ulichagizwa na kipa wao mahiri William Barton aliyeweza kudaka penati
tatu kati ya tano zilizopigwa na Tanesco.
Baada ya ushindi huo, Barton
alimwaga machozi ya furaha, kwani alidaka penati zilizopigwa na kipa
mwenzake Hashim Yahya, Khalifa Shekuwe na Abdallah Magubile.
Penati za Uchukuzi SC zilifungwa
kwa ufundi stadi na Fidelis Kyangu, Masoud Masoud na Kado Nyoni, wakati
waliokosa ni Omary Said ‘Chidi’ na Seleman Kaitaba.
Hatua ya penati ilifuatiwa baada
ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na kwa mujibu wa
sheria za mashindano hayo hakina nyongeza ya dakika 30 na inapigwa
mikwaju ya penati moja kwa moja.
Kocha wa Uchukuzi SC, Elutery
Muholeli alisema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, na wachezaji
wake walicheza kwa kujituma, na dhamira yao ilikuwa ni kutwaa ubingwa,
lakini bahati haikuwa yao na wamebahatika kutwaa ushindi wa tatu.
Naye kocha wa Tanesco, James
Washokera alikiri wachezaji wake kukosa umakini kutokana na kikosi chake
kukosa wafungaji, na aliamua kuwatumia viungo zaidi, ili kufunga magoli
lakini walishindwa kutokana na kucheza nafasi sio yao.
“Unajua hii timu yetu ilitakiwa
kuwa ni kombaini ya Tanesco Tanzania nzima, lakini haikuwa hivyo na
badala yake wametoka sehemu chache na nilitarajia ningechagua wafungaji
kutoka mikoani, lakini sikupata nafasi hiyo, ila hili tatizo huu ndio
mwisho wake na mwakani tutakuja kamili kwani nitahakikisha ninazunguka
na kupata wachezaji sehemu zote,” alisema Washokera.
Pia Uchukuzi wanaume wameibuka
mabingwa wa mchezo wa kamba baada ya kumaliza ikiwa imejikusanyia pointi
10, na haikuwahi kuvutwa na timu yeyote tangu michuano hiyo ianze.
Nayo CDA ‘Watoto wa nyumbani’
wameshika nafasi ya tatu katika mchezo wa netiboli wakiwa na pointi tatu
sawa na Tanesco iliyoshika nafasi ya nne , lakini wanatofautiana kwa
magoli ya kufunga na kufungwa, huku TPDC ikiburuza mkia ikiwa haijapata
pointi yeyote.
MWANAHABARI MTOTO NA MWANAMAZINGIRA WA UN, GETRUDE CLEMENT ALIVYOPOKELEWA JIJINI MWANZA.
Shujaa Wetu,
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
………………………………………………………………………………………………….
Alihudhuria
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
Kutoka
Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto
na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa
Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.
“Kitu
ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano
ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170
wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia
malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na
viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa
balozi wao”. Alisema Getrude.
“Wazazi
wawaruhusu watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi
ili waweze kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao”. Anasema Mtoto
Mwanahabari Getrude.
Shabani
Njia (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani
Mwanza MYCN akizungumzia mapokezi ya Mwanahabari na Balozi wa Mazingira
wa Umoja wa Mataifa akiwakilisha kundi la Watoto na Vijana Getrude
Clement
Clement Leon ambae ni baba mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza.
Rizik
Athman ambae ni mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika
Uwanja wa ndege Mwanza ambapo anafurahishwa na hamasa aliyonayo mtoto
wake ikiwemo kujiamini katika masuala mbalimbali ikiwemo ya habari.
Getrude (Katikati) akiwa na Wazazi wake, Clement Leon (Kushoto) pamoja na Rizik Athman (Kulia).
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, mapema wakifurahia jambo wakati wakimsubiria Getrude
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN wakiwa pamoja na Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, wakifurahia na Getrude katika picha ya pamoja.
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude, Wengi walimsubiria kwa hamu kubwa.
Shuja, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa UN Getrude Clement baada ya kuwasili Jijini Mwanza.
Tazama HAPA Getrude akihutubia katika Mkutano wa UN
NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE WAWASILI DALLAS, MTANANGE WA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI
Renatusi Njohole akiwa katika picha ya pamoja na kaka yake
Benchi la ufundi la Yanga Bwn.
Gerry Mshana(kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Nico Njohole siku ya
Alhamisi Dallas, Texas. Nico na Renatus wamekuja maalum kuhudhuria
mkutano wa DICOTA na kuchezea Simba kwenye mtanange wa watani wa jadi.
Kutoka kushoto ni Gerry Mshana,
Mary Maswanya (dada mkubwa wa Nico na Renatus), Renatus, Nico na Rais wa
DICOTA, Ndaga Mwakabuka walipopata picha ya kumbukumbu.
Rais wa DICOTA Bwn. Ndaga Mwakabuta akiwa katika picha ya pamoja Nico na Renatus
Kutoka kushoto ni Jerry, Nico, Ndaga Mwakabuta, Renatus, na Gerry Mshana wakiwa kwenye picha ya pamoja
DC KINONDONI AANZA MAPAMBANO DHIDI YA WATUMISHI HEWA
NA BASHIR NKOROMO
Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam, Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.
Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam, Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.
Amesema,
baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita,
amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na
wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331,
734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa
mishahara wakati hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu
mbalimbali.
Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.
Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.
Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.
Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.
Katika
hatua nyingine, Hapi amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa
jina la machinga, kuwa kuanzia kesho ni marufuku kufanya shughuli zao
katika maeneo yasiyo mahsusi kwa biashara katika wilaya ya Kinondoni.
Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.
Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.
Hapi
amesema, machinga wote kama wahanitaji kufanya biashara zao ni lazima
waende katika maeneo yaliyopangwa, ambayo alisema, hapo mengi na bado
yana nafasi za kutosha kwa ajili ya kutumika kufanyia biashara.
Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar
Picha ya pamoja kati ya meza kuu, mgeni rasmi na viongozi na kamati ya mkutano huo. |
UONGOZI WA WANAFUNZI WA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR (ZIFASO) WACHAGUA VIONGOZI WAPYA.
Wagombea
wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena
Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha
Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa
ajili ya kupiga kura.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar
Sabrina Yussuf Shaaban akielezea juu ya utaratibu mzima wa kupiga kura
ili kupata viongozi wapya wa ZIFASO .
Mlezi
wa wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Maalim Wazir Hamad
akitoa nasaha zake kwa wapiga kura ambao ni wanafunzi wote wa chuo
hicho.
Mgeni
rasmi katika uchaguzi huo ambae ni Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) Mohd Ali Abdalla akiwanasihi wasimamizi na wapiga kura
kuendesha uchaguzi katika misingi ya haki.
Mgombea
pekee wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan akipiga kura
yake katika uchaguzi huo uliofanyika chuoni Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
Wasimamizi wa uchaguzi wakiwa pamoja na mawakala wa wagombea wakihesabu kura mara baada ya kukamilika zoezi la upigaji kura.
Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakijumuisha kura ili kujua mshindi katika uchaguzi huo.
Rais
mpya wa ZIFASO na Makamu wake Juma Shirazi Hassan na Makamu wake Zuwena
Jaku Hassan wakitoa shukrani na nasaha zao baada ya kuchaguliwa
kuongoza Jumuia hiyo kwa mwaka 2016/2017. Picha zote na Makame
Mshenga-Maelezo.
Supastaa wa Malawi Tay Grin awapania Diamond na Vanessa
Rapper na supastaa wa Malawi, Tay Grin, amedai kuwa ana mpango wa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. Tay ambaye hivi karibuni aliachia video ya wimbo ‘Chipapapa’aliomshirikisha msanii wa Nigeria, 2 Face Idibia, amesema kuwa hao ni wasanii wa Tanzania anaowakubali zaidi.
“Ningependa sana kufanya kazi na wasanii wa Tanzania,” anasema Tay.
“Napenda jinsi wasanii wa
Tanzania wanavyoimba. wako kimuziki sana hata kama sizungumzii
Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii
kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa Bongo
Flava. Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa
wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani
ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo,” ameongeza.
Tay amesema anawakubali wawili hao kutokana na jinsi wanavyojituma na mapenzi yao makubwa kwenye muziki.
“Nimekuwa nikifuatilia kazi zao kwa muda sasa na naweza kusema kuwa wamenishika.”
Tay ni msanii anayeheshimika
zaidi nchini Malawi na amewahi kutumbuiza mara mbili kwenye shindano la
Big Brother Africa na amewahi kutajwa zaidi ya mara tano kuwania tuzo za
Channel 0.
Amewahi kushirikisha wasanii kama
Sway (UK), Brick & Lace (Jamaica), Naeto C, Ice Prince, na 2face
wa Nigeria), Wahu na Nameless wa Kenya, Double HP, Da Les na Lira wa
Afrika Kusini na wengine.
WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA – SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa
mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya
uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu
mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma
ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango.
Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa
mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya
uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.
—
Na Cathbert Kajuna – Itirima, Simiyu.
—
Na Cathbert Kajuna – Itirima, Simiyu.
Wananchi wa Kijiji cha Itobo,
Itirima – Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na
idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi.
Akizungumza katika mafunzo ya
Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya
uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema
kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa
ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa
maskini.
“Nawaasa wananchi wa Kijiji cha
Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto
maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 – 15 jambo
linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia,” alisema
Meena.
Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango.
Akiongea mara baada ya kumaliza
mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika
kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja
kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.
Kongamano la Uwekezaji Tanzania na Urusi
Makamu
wapiliwa Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif
AliIddiakifunguakongamano la kujadili FursazaUwekezajikati ya Tanzania
na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam
ambalolimewakutanishawafanyabiasharambalimbaliwaMataifahayomawili
Waziri
waViwandaBiashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijageakifafanuakwawaandishiwahabari janaJijini Dar es salaam
kuhusufaidazaushirikianowakibiasharakati ya Tanzania na
Urusiutakaochangiamaendeleo katika sektazaKilimo,Usafirishaji na
Nishatihapanchini.
WaziriwaViwanda
na BiasharawaUrusi Mhe. Denis Manturovakizungumzakwenyekongamano la
kujadilifursazaUwekezajikati ya Tanzania naUrusilililofanyikaleoJijini
Dar es salaam.
Baadhi
ya washirikiwakongamano la kujadilifursazaUwekezajikati ya Tanzania na
urusiwakifuatiliamadawakatiwakongamanohiloleoJijini Dar es salaa.
MakamuwaPiliwa
Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif AliIddi(kushoto)
akizungumzajambo na MwenyekitiwaTaasisi ya SektaBinafsi Tanzania Bw.
Reginald MengileoJijini Dar es salaam marabaada ya kufunguakongamano la
Uwekezajikati ya Tanzania na Urusi.
MakamuwaPiliwa
Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif
AliIddi(wannekutokakushoto)akiwa na WawakilishiwaSerikali ya
Urusi,anayefuatani Waziri waViwanda na Biashara Mhe. Charles
Mwijageakifuatiwana WaziriwaViwandaBiashara na MasokowaSerikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.
Pichazote na (Fatma Salum- MAELEZO)
No comments :
Post a Comment