Tuesday, February 2, 2016

PSPF “YAVUNA” MAMIA YA WANACHUO WA UDSM NA TUMAINI KAMPASI YA DAR ES SALAAM, WAJIUNGA NA MPANGO WA PSS

Mwanamuziki nyota nchini Vanes Mdee, akiweka dole gumba
tayari kuchapa kwenye fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS),
wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF wakati wa kongamano lililowakusanya wanafunzi wa
kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara na kufanyika chuoni
hapo mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na mpango huo baada ya
kupata elimu ya faida za kujiunga na mpango huo. Wanaoshuhudia, kutoka kulia ni
Balozi wa PSPF, Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anayefanya
kazi zake Ulaya na Marekani, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS wa
Mfuko huo, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Rahma Ngassa.

RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ALAANI

KIGWAGALA 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
…………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohammed Bakar(CCM) lililouliza kuwa bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa maswali na majibu,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kuhakikisha kuwa haki hizi zinapatikana,Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.
Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.
“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto” Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.
Serikali kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

1
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
3
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).
4
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
5
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani).
6
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

Kundi la Mziki la Navy Kenzo latoa Wimbo na Video Mpya-Kamati

THE INDUSTRY MUSIC LABEL
Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaitwa “Kamatia” , Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka, Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya ‘Flash Mob’ Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.
Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava, Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.
Kamatia ni wimbo ambao unaongelea kuhusu wapenzi wawili waliomua kushikana hasa kwenye mapenzi , Midundo ya nyimbo hiyo ina mahadhi ya Dancehall na vionjo vya kipekee kutoka kwa Producer bora Tanzania Nahreel.
Nahreel Ambaye ni mmoja wa Kundi la Navy Kenzo ni Producer wa Muziki bora Mwenye tuzo ya Kilimanjaro Music, Ametengeneza nyimbo mbali mbali zilitamba Kama Nana ya Diamond Ft Flavor,  Joh Makini Ft Aka Don’t Bother and Vanessa Mdee’s Nobody but me, Never ever na Hawajui, pia ndio mpishi wa Nyimbo ya Navykenzo ‘Game’

UNIDO NA CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAENDESHA SEMINA KWA WAMILIKI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO VYA UZALISHAJI (SMEs) NA WAHITIMU WA VYUO TANZANIA

Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro akifungua Semina kwa ajili ya  wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali semina iliyolenga programu ya UNIDO wakishirikiana na Chuo kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Peacock Hotel Dar
Mshauri wa UNIDO Bw. Mike Laizer akichangia jambo katika semina hiyo
Bw. Deosdadit Bernad Msimamizi wa Programu kutoka UNIDO akielezea kwa undani juu ya Programu  hiyo
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiendelea kufuatilia Semina
 Profesa Prosper Ngowi Msimamizi Mkuu wa Programu hiyo akieleza kwa kina nia na malengo ya wao kufanya hivyo kwa kushirikiana na ‘SMEs’ ili kuwapa ujuzi wa kazi wahitimu na wahitimu kutoa ujuzi wao waliokuwa nao ili kuweza kukuwa zaidi
Wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanaendelea kufuatilia semina hiyo kwa makini
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanauliza maswali na kuchangia mawazo katika Semina hiyo
Mmoja wa ‘Mentor’ katika programu hiyo Bw. Kaaya akiwa anatoa maelezo kwa wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali jinsi ambavyo watashirikiana katika kuwafundisha kazi wahitimu hao pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali
Picha ya Pamoja kati ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali, Chuo kikuu cha Mzumbe na wawakilishi kutoka UNIDO
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Ganka akifungua semina fupi na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ambao ni watanzania katika programu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe juu ya Mafunzo ya kazi ‘Internship’ ambayo yataanza hivi karibuni ambapo wahitimu hao watatakiwa kufanya kazi kwa miezi minne katika viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara  na wajasiliamali
Msimamizi Mkuu wa Programu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi akiwaelezea wahitimu juu ya Programu hiyo
Baadhi ya wahitimu wakiwa wanauliza maswali na kutaka ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ambayo walikuwa hawajayaelewa katika semina hiyo iliyofanyika katika Chuo kikuu cha Mzumbe
Dkt. Darleene Mutalemwa akitoa neno la Shukurani kwa wote wahitimu wote waliofika katika semina hiyo kwa niaba ya UNIDO na Chuo kikuu cha Mzumbe
Wahitimu wakiwa katika semina hiyo ya kupata maelekezo juu ya Programu ambayo inalenga kuwapa Mafunzo ya kazi wahitimu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe

Mfuko wa Dharura wa UN watoa Dola Milioni 11 kusaidia wakimbizi wa Burundi na jamii ya Tanzania

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania—ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miaka mingi—imetengewa dola za Marekani milioni 11 (Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24) kutoka katika kiasi hicho kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi.
liu
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa msaada katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara mkoani humo
Zaidi ya raia 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Tanzania hivi sasa ina zaidi ya wakimbizi 193,000. Kutokana na ukweli kwamba takribani wakimbizi 1,500 wanawasili nchini kila wiki, inabashiriwa kwamba huenda idadi jumla ya wakimbizi ikafikia 230,000 hadi mwisho wa mwaka 2016. Hali hii inasababisha changamoto nyingi hasa katika kutoa msaada na kinga ya kutosha kwa wakimbizi.
Mchango huu mkubwa kutoka CERF utakuwa muhimu sana katika kutoa misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, na vilevile kwa jamii za wenyeji ambazo zinahitaji kwa haraka huduma bora za maji safi, usafi wa kutosha, matunzo ya afya, chakula na makazi. Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kushughulikia mlipuko uliopo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeathiri mikoa 19 nchini. Fedha za CERF kwa hiyo zitasaidia kuhakikisha kwamba maeneo muhimu zaidi katika dharura yanafanyiwa kazi na kwamba wakimbizi wanapewa kinga na huduma za msingi.
Picture2
Baadhi ya wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma
“Shirika la Kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) linakaribisha mchango huu wenye ukarimu mkubwa kutoka CERF ambao unakuja katika kipindi mwafaka kabisa. Utoaji msaada kwa wakimbizi ulikuwa ukikabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka 2015, hali iliyoathiri sana uwezo wetu wa juhudi za pamoja katika mwaka 2015. Tuna imani kwamba hii ni ishara ya kwanza kwa upatikanaji wa fedha nyingi zaidi kwa utoaji msaada katika mwaka 2016. Kwa hakika, mchango huu utasaidia kuziba upungufu mkubwa uliojitokeza katika wito wetu wa sasa na hivyo kushughulikia mahitaji makubwa zaidi ya wakimbizi na jamii za wenyeji,” alisema Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Bi. Joyce Mends-Cole.
Kadiri mahitaji ya kiutu yanavyoongezeka, mchango kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa matumaini ya kuendelea kushughulikia dharura ya wakimbizi kutoka Burundi. Tangu mwaka 2006, Nchi 125 Wanachama wa Umoja wa Mataifa na waangalizi, wahisani kutoka sekta binafsi na serikali katika kanda zinazohusika wameendelea kuusaidia Mfuko huo hadi sasa. CERF hadi sasa imetoa jumla ya dola za Marekani bilioni 4.2 (US$ 4.2bn, sawa na shilingi za Tanzania trilioni 9) kwa miradi ya kiutu katika nchi 94. CERF hupokea michango ya hiyari katika mzunguko wa mwaka ili kutoa msaada wa kifedha kwa hatua za kiutu za kuokoa uhai. CERF inapata fedha zake kutoka kwa washirika wengi huku michango mingi zaidi ikitoka: Uingereza, Swideni, Norwei, Uholanzi na Kanada.

President Kikwete Statement


jkk
ADDIS ABABA, Ethiopia, 31 January 2016,
It is my pleasure to announce today that I have accepted the invitation from the Confederation of African Football and from Gavi, the Vaccine Alliance to serve as Champion for Immunization and as Global Ambassador of Africa United. Africa United is a pan-African innovative initiative led by Gavi, the Confederation of African Football, the African Union, the World Bank Group and the CDC Foundation. This initiative leverages sport to catalyze action on critical health issues facing the continent.
Africa United was first deployed during the Ebola crisis, enlisting influencers like Kei Kamara of Sierra Leone to spread Ebola prevention messages and to encourage the population to trust and seek care within the health system. Africa United spokespeople also brought increased attention to the crisis through an African Union-led awareness and fundraising campaign called Africa Against Ebola.
Under my leadership, Africa United will focus on promoting universal health access, beginning with a focus on Universal Immunization. Immunization is crucial to saving the lives of children across Africa – and the world. Immunization will be key to preventing over 1.5 million deaths each year. Universal vaccination will also play a fundamental role in developing a healthy, resilient population and in ensuring that we develop the economies we need to face the challenges of the next century.
Today, as I announce my commitment to the health of the African continent, I call on every Head of State across Africa to prioritize access to vaccination in each and every community.
Africa United will formally launch its universal immunization initiative next week in Kigali at the 4th Edition of the Orange African Nations Championship – Rwanda 2016. In Kigali, my esteemed partner in this fight, CAF, will remind everyone that “Every Shot Counts” as we look achieve our goal of Universal Immunization.
Please join me and Africa United as we fight for a more secure future through universal access to immunization.MAUAJI YA RUBANI WA HELIKOPTA ILIYOTUNGULIWA NA MAJANGILI WA TEMBO
te1

DKT.SHEIN AZINDUA MIAKA 39 YA KUZALIWA CCM.

????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula leo katika mkutano wa hadhara wa   ya shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali Chama cha Mapinduzi CCM mara alipowasili katika viwanja vya Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar, katika Mkutano wa hadhara wa Mikoa minne ya Unguja katika Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwasalimia  Wanachama cha Mapinduzi  katika mkutano wa hadhara wa Mikoa minne  ya Unguja mara alipowasili katika shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu .
????????????????????????????????????Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana alipokuwa akisalimiana na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo aliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,
????????????????????????????????????Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana Taifa wakati alipowasili katika uwanja wa Ofisi ya CCM Kisiwandui katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM
????????????????????????????????????Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akisalimiana na  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar pamoja na Viongozi wengine wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo aliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM,

MHE. NAPE AIPONGEZA BLOG YA VIJIMAMBO KWA KUTIMIZA MIAKA 6

indexNapenda kuipongeza blog ya Vijimambo kwa kutimiza miaka 6.
Blog ya Vijimambo imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa habari za uhakika na kwa wakati.
Pia imekuwa daraja zuri kati ya nchi yetu na Watanzania na wapenda Kiswahili duniani.
Imekuwa na mchango mkubwa  katika kupeleka utamaduni wa kitanzania nje ya nchi yetu!
Nawatakia kila la heri na mafanikio mema .

MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT ASKOFU SHOO MJINI MOSHI 

1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye na mkewe Esther katika Ibada ya kumuingiza   kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo  (kulia) na Mkuu wa Kanisa hilo mstaafu, Askofu Alex Malasusa katika  Ibada ya kumuingiza  kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi januari 31, 2016.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

TANROAD YA BOMOA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKA HIFADHI YA BARABARA MAENEO YA BUZA, LUMO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
 Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
 Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.
 Mkazi wa Buza akiondoa mabaki ya mbao baada ya nyumba yake kubomolewa.
 Moja ya nyumba iliyobomolewa.
 Wananchi wakiangalia moja ya Baa iliyobomolewa.
 Tingatinga likiwa kazini.
 Watoto wakiangalia zoezi la ubomoaji lilivyokuwa likiendelea.
 Ofisa wa Tanroad akisimamia ubomoaji huo.
 Wananchi wakiangalia zoezi la ubomoaji.
 Tingatinga likiisambaratisha moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Buza kwa Lulenge.
 Wananchi wakiangalia  ubomoaji huo.
 Tingatinga likifanya vitu vyake bila huruma.
 Askari wa kutuliza ghasia wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.

TAARIFA KWA WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA ZIKA (ZIKA VIRUS)


  1. logoUtangulizi
Kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Kitaifa na Kimataifa kuhusu Homa ya Zika ambao ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus”. Ugonjwa huu uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Uganda katika miaka ya 1947 kwenye wanyama aina ya sokwe/nyani (rhesus macaque) ndani ya Misitu ya Zika, karibu na Ziwa Victoria. Mnamo mwaka 1952, ugonjwa wa zika uligundulika kwa binadamu nchini Uganda na Tanzania, na mwaka 1968 uligunduliwa nchini Nigeria. Kuanzia mwaka 1951 hadi 1981, ugonjwa huu umeshatolewa taarifa katika nchi takribani sita (6) za Afrika ambazo ni Afrika ya Kati, Egypt, Gabon, Sierra Leone, Tanzania na Uganda. Vile vile, ugonjwa huu umeshatolewa taarifa katika nchi za India, Indonesia, Malaysia, Philipine, Thailand na Vietnam na pia nchi za Amerika na Pacific.
Kuanzia mwezi Mei 2015, ugonjwa huu ulianza kutolewa taarifa ambapo hadi sasa umeathiri zaidi Bara la Amerika ya Kusini. Kuna takribani nchi 22 ambapo Wagonjwa wamethibitishwa kimaabara kuwa na ugonjwa wa Zika. Nchi hizo ni Brazil (Majimbo 14 yameathirika),  Colombia, Suriname, El Salvador, Guatemala, Paraguay, Mexico, Venezuela, Panama, Cape Verde, Honduras, Panama, France (French Guiana na Martinique, United States of America (Puerto Rico), Guyana, Barbados, Ecuador, Bolivia, Haiti, Ujerumani, France (Saint Martin and Guadeloupe na Dominican Republic.  
Ugonjwa huu unaenezwa na mbu aina ya Aedes ambaye (huwa ana tabia ya kuuma asubuhi na pia nyakati za mchana/jioni). Aina hii ya kirusi ipo katika familia ya “Flavirus” ambapo pia wapo virusi vya ugonjwa wa Dengue, Homa ya Manjano (Yellow Fever), Japanese ancephalitis na West Nile Virus.
Kirusi cha homa ya Zika kama kile cha Dengue kinaambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuumwa na mbu wa jamii ya Aedes hasa Aedes aegypti. Mbu huyu anaishi katika mazingira ya makazi ya binadamu, huuma wakati wa mchana ndani ya nyumba au kwenye maeneo yenye viwili, hususani majira ya asubuhi na jioni kabla ya jua halijazama.  Mbu huyu anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, makopo nk.
  1. Dalili za Homa ya Zika
Dalili za ugonjwa huu zinafanana na za homa ya Dengue, ambazo ni homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo, macho kuwa mekundu na vile vile kupata vipele vidogo vidogo kama harara (Skin rashes). Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 2 hadi 7 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya Zika.

Wachina waishio nchini waadhimisha mwaka mpya 2016 “Ngedere”

np1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
np2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
np4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
np5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
np7
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np8
np9 np11
Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np12 np14
Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np15 np16
Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np17
Vimulimuli vy fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Jumuiya ya Wachina wanaoishi nchini wamezindua na kuukaribisha kwa shamrashamra mwaka Mpya wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Akizindua shamrashamra hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alisema kuwa Wachina na Watanzania ni ndugu ambao uhusiano wao ni wa kudumishwa milele na milele.
“Uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria ambao ni wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwamo kijamii, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni Utamaduni na kimawasiliano kati ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Nape.
Kihistoria, uhusiano wa China na Tanzania ni wa kidugu na kirafiki wakati wote iwe wa dhiki au faraja katika maisha ya kila siku kati ya Watanzania na Wachina.
Ni wakati muafaka kuongeza jitihada za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wan chi hizo mbili ili kuwaenzi waasisi wa ushirikiano huo ambao ni Rais Mwalimu Julius Nyerere  na Mao Tse Tung.
Kwa upande wake Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei alisema kuwa wanajisikia faraja wakati wote wanapofanya kazi na Watanzania kwa kuwa wanamengi ya kujivunia katika historia ya nchi hizo.
Aidha, shamrashamra za mwaka mpya wa Kichina zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu Salum Ahmed Salum, Mizengo Pinda, viongozi mbalimbali na wenyeji wa sherehe hizo ambao ni raia wa Kichina wanaoishi nchini wakiongozwa na viongozi kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Mwaka huu unajulikana kama “Ngedere” wakati mwaka 2015 ulijuklikana kama “Kondoo” ambapo maadhimisho ya Mwaka Mpya wa “Ngedere” yalipambwa na michezo mblimbali ikiwemo bahatinasibu, sarakasi, nyimbo, muziki wa ala, mazingaombwe na ngoma.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA AISHUKURU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, WANANCHI WA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

DC. Paul Makonda
Mnamo tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili kubaini watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu kuchukua hatua za awali za kuwasaidia wale ambao tayari wameshashambuliwa na magonjwa hayo na mwisho kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo. 
Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa huku ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza kujikuta unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama figo aukisukari na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo kumbe tatizo la msingi ni moyo. 
Kimsingi ni kwasababu hizo nilizozianisha nilichukua hatua ya kukiomba taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kinachosimamiwa na Profesa Janabikinisaidie kutoa huduma hiyo bure ndani ya wilaya yangu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana madaktari kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na mwananyamala kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu kulifanya zoezi hilo. zoezi ambalo lilikuwa kubwa na zito kwani kwa makadirio ya awali tulitegemea kupata watu wasiozidi 2000 ila badala yake walijitokeza wananchi zaidi ya 7000 ila kutokana na umahiri wa madaktari hao tuliweza kuhudumia zaidi ya wananchi 5900 ingawa tulilazimika kulifanya zoezi hilo kwa siku ya pili yake ambayo ilikuwa ni tarehe 24. 
Na kwa watu wengine zaidi ya 1200 waliokuwa wamebaki, zoezi lao tulilipanga na kulifanya tarehe 30 ya mwezi huu huu wa kwanza. Ukweli ni kwamba, mambo mengi yalijitokeza kwa siku hizi tatu za upimaji; wapo waliolazimika kukimbizwa kwa ambulance kuelekea hospitali za mwananyamala na muhimbili, wapo waliolazimika kupewa appointments za kuwaona madaktari, wapo waliopewa ushauri wa matumizi ya dawa na wengine kubadilishiwa dawa sambamba na maelekezo ya utumiaji wa chakula na ufanyaji wa mazoeziili kupunguza uzito. 
Nichukue tu fursa hii kuwapongeza wanakinondoni kwa kuitikia wito na kuniamini mkuu wao wa wilaya na serikali yangu kwa ujumla kwamba tuna nia njema na tunawapenda wananchi wetu kwa kuwahakikishia afya zao zinastawi na kuendelea kuwa bora siku zote. 
Kutokama na maelezo niliyoyatoa hapo juu sambamba na sababu zilizonisukuma kufanya zoezi hilo na kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi bila kusahau matokeo ya vipimo vilivyofanyika na kupata majibu ya kwamba watu wengi wanahitaji matibabu, kubadilishiwa dawa, maelekezo ya matumizi sahihi ya vyakula pamoja na mazoezi nimefanya uamuzi wa kulifanya zoezi hili la kudumu na tayari nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na nimetafuta njia na utaratibu bora zaidi wa kulifanya zoezi hili kuwa ni zoezi la kudumu.
Sasa basi, natamka rasmi kuwa serikali ya wilaya ya kinondoni inaanza utaratibu wa kupima bure mara tatu kwa mwaka, utaratibu ambao utaanza katikati ya mwezi wa nne. Zoezi hili litafanyika kwa kupima zaidi ya magonjwa kumi ikiwemo yafuatayo: moyo, kisukari, kansa, macho, figo, meno, kifua kikuu (TB), typhoid, magonjwa ya ngozi, presha, animonia, kansa ya kizazi, kansa ya matiti, mabusha na matende. 

Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa moja kwenye banda husika. 
Ama unaingia kwenye banda limeandikwa Ocean Road hospital kwahiyo yeyote anayetaka kupima kansa ataingia humo…hivyo hivyo kwa magonjwa mengine yote: kutakuwa na mabanda tofauti yaliyoandikwa ni hospitali gani na wanapima magonjwa gani, lengo ikiwa ni kumpa urahisi mpimaji atakayejitokeza. 
Mwisho ila si kwa umuhimu niwashukuru sana wananchi wote wa wilaya nyingine na wale waliotoka mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi na Dodomakwa imani yao kubwa juu ya tukio hili iliyowafanya kutoka mbali na kujisogeza mpaka viwanja vya leaders wakiwa na imani ya kupatiwa huduma hata kama zoezi hili lilikuwa limewalenga wakazi wa wilaya ya Kinondoni. 
Sambamba na kuwashukuru wananchi niwashukuru pia waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari mbele kulitangaza tukio na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati. 
Imetolewa na:- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
 

MTAA WA GONGO LA MBOTO MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDELEA KUUNGA MKONO KAULI YA RAIS DK.MAGUFULI YA KUFANYA USAFI

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Kazi ya usafi ikiendelea.
 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
 Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
 Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
 Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.
…………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
 
Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.
 
Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo  na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
 
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu  Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.
 
 
Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.

Dar Swim Club mabingwa washinda mashinano ya kuogelea ya Taliss

sw1
wachezaji na makocha wa timu ya Dar Swim Club wakishangilia baada ya kutwa ushindi wa jumla katika mashindani ya Taliss yaliyofanyika jana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa.
sw2
 Celina Itatiro wa Dar Swim Club na Ema Imhoff wa Mwanza wakichuana katika mashindamo ya Taliss kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa.
sw3
waogeleaji waki-dive kwenye maji katika mashindano hayo.
sw4
waogeaji wakichuana katika mashindano hayo
 …………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Timu ya Dar Swim Club (DSC) imeshinda mashindano ya kuogelea ya Taliss baada ya kuzipiku klabu nyimgine nane zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule yaKimataifa ya Upanga.
Dar Swim Club  ilijikusanyia pointi 2,421 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za wanawake na wanaume. Katika mashindano hayo, wanawake wa DSC walikusanya jumla ya pointi 1,526 huku wanaume wakijikusanyia pointu 895 kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa.
Waogelaji wa kike Smriti Gokarn, Celina Itatiro na Maia Tumiotto walichangia zaidi ushindi wa timu hiyo kwa kukusanya pointi nyingi na akwa upande wa wavulanai walikuwa Matt Golembeski, Marin De Villard na Carter Golembeski.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na wenyeji Taliss kwa kupata jumla ya pointi 2,298 huu waogelaji wao wa kiume, Adil Dharmal na  Oliver Mclntosh wakiongoza kwa kuchangia pointi nyingi katika ushindi huo.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Shule ya Kimataifa ya Moshi ambayo ilichanganyika nay a Arusha kwa kupata pointi 1,111 huku waogeleaji wake, Josephine Oosterhuis na Pieter De Raadt wakichangia pointi nyingi.
Timu ya kuoglea ya Mwanza ilimaliza katika nafasi ya nne chini ya waogeleaji nyota Elia Imhoff na Emma Imhoff  na kufuatiwa ma shule ya kimataifa ya Morogoro chini ya nyota wake, Dennis Mhini na Charlotte Sanford.
Timu ya Bluefins ilishika nafasi ya sita kwa pointi  553 ambapo waogelaji wake Sahal Harunani alishinda medali ya shaba. Nafasi ya saba ilikwenda kwa timu ya Wahoo iliyokuwa chini ya Ellis Underson na Rania Karume kwa kupata pointi 303 na  huku Champions Rise na Kennedy House wakimaliza katika nafasi mbili za mwisho.
Mhasisi wa Dar Swim Club Ferick Kalengela alisema kuwa siri kubwa ya ushindi wao ni kujituma na kufanya mazoezi ya kisasa huku Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro akiwapongeza wachezaji wake na kusema huo ni mwanzo tu na makubwa yatafuatia katika kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.

93
NA RAISA SAID,BUMBULI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na
Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi
ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.
Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo  Kanisa  na Msikiti zimeezuliwa mapaa
katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo imesabisha  kaya  hizo  kukosa  mahali pa kuishi , huku
wengi wa  waathirika  wakipewa hifadhi  kwenye  nyumba  za majirani
zao.
Akizungumza  na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji
cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo
January 27 mwaka huku saa kumi jioni.
Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi  kuwa  ni Vitongoji vya Kwemchaa,
Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio
vimeweza kuathirika na maafa hayo.
Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa
wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa
kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo
anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada
zaidi.
“Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji
Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu  mwingine” alisema Makamba
Makamba   aliwataka  wananchi  wote  kupanda  miti ili kuepuka  upepo
mkali  unaosababishwa  na  mvua  zinazoendelea kunyesha  katika
maeneo tofauti

SUALA LA ADA ELEKEZI KUHUSISHA WADAU WOTE – WAZIRI MKUU

3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.
Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.
“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.
Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.
“Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.
Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.
“Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.
Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.
“Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Askofu ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.
“Si kwa akili na uwezo wangu bali ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo. Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.
Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo. “Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,” alisema.
Waziri Mkuu anarejea Dodoma jioni hii kuendelea na vikao vya Bunge.
IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Mkapa

2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. Rais Dkt. Magufuli alikwenda kumsalimia Rais mstaafu Mkapa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Picha na IKULU

MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT TANZANIA ASKOFU SHOO MJINI MOSHI

1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu  Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
2Baadhi ya waalikwa  walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
4
Waziri MkuuKassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MUU)

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. KIGWANGALA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA

2
Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.
3
NaibuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Dawa la MSD jijini Arusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru.
1
Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Arusha.
NaibuWaziriwaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe. Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo.
Naibu Waziri huyo pia amewahimiza watendaji wa MSD kuwa waadilifu, kuwajali na kuwasilikiza wateja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja, huku akitoaangalizo kwa wale wanao kiuka taratibuza ajira kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhaminiya MSD Prof. IdrisMtulia ameeleza kuwa MSD inaweza kufanya vizuri zaidi endapo changamoto za sheria ya manunuzi, mgawo mdogo wafedha kwa vituo vya Afya, hospitali na zahanati, na mgawo wafedha kuja kwa mafungu zitafanyiwa kazi.
Naye Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa MSD itakuwa na maduka manne tu mkoani Dares Salaam, Mwanza, A Arusha na Mbeya ambapo kwa mikoa mingine MSD wanaafanyama wasiliano na hospitali za mikoa ziwe na maduka ya hospitali wanayoendesha wenyewe na kisha MSD iwauzia dawa na kuwawezesha utaalamu wakuendesha maduka hayo.

Wananchi watahadharishwa juu ya homa ya Zika

indexWaziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma (Hawapo Pichani) akitoa tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya Zika kushoto ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula. Picha Na Raymond Mushumbusi Maelezo
……………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya ugojwa wa homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya kusini hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mijini Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini.
Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanznia kuwa na tabia ya kwenda hospitali kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za ugonjwa wa homa ya Zika.
“ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie usafi ili kuzuia mazalia ya mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi vinavyoenezwa na mbu na hao mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na jioni hivyo nawasihi kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”
“Napenda kutoa tamko kuwa ugonjwa huu wa homa ya Zika haujaingia Tanzania na tunawaomba watanzania kuwa makini sana na waripoti dalili zozote ambazo sio za kawaida zitakazojitokeza na mpaka jana kwa taarifa tulizonazo hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na homa ya Zika” Alisema Mhe.Mwalimu.
Aidha naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula amesema wamejiandaa kukabiliana na kesi zozote zinatazojitokeza za homa ya Zika na wana mfumo mzuri wa kubaini magonjwa ya mlipuko na pia kuna maabara ya NIMR ambayo inafanya uchunguzi juu ya magonjwa mbalimbali.
“ Nawaomba watanzania kutopuuzia dalili zozote za homa na kuamua kujitibia manyumbani au kunywa dawa bila kupima na kujua hiyo homa ni ugonjwa gani kwani yaweza kuwa homa ya Zika” Alisema Dkt Chaula.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee wa kushirikiana na Shirika la Afya Dunianoi (WHO) wanafatilia kuhusu ugonjwa huu na watatoa maelekezo ya kuzingatia ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ila mpaka sasa ugomjwa huu haujaingia Tanzania.

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE.OTHMAN CHANDE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI.

1
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
2
Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.
3
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.
4
Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.
5
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.
6
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
7
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).
8
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
9
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
10
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza leo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA masuala ya Usalama Barani Afrika.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
(Picha na OMR)

Tamasha la Pasaka kufanyika Mwanza

indexNa Mwandishi Wetu
……………………………….
TAMASHA la Pasaka 2016 linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions jijini Dar es Salaam linatarajia kufanyika Machi 27 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama mkoa wa Mwanza umepata bahati hiyo baada ya wakazi wake kuomba kwa kipindi kirefu kufikiwa na tamasha hilo.
“Kamati yangu huwa inasikia matakwa ya mashabiki wa muziki wa Injili kwa sababu tamasha hilo ni lao ni vizuri kuwasikiliza,” alisema Msama.
Msama alisema, Kamati yake imekaa na imechunguza Tamasha la mwaka huu lifanyikie jijini humo, hivyo anatoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kujiandaa vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo.
“Tamasha letu linawahusu wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, wajane na yatima ambao misaada yao inatokana na tamasha hilo, hivyo wajipange na kujitokeza kwa wingi,” alisema Msama.
Msama alisema wamesikia kilio cha Wananchi Mwanza baada ya maombi yao ya muda mrefu, tamasha litafanyikia jijini humo ikiwa ni heshima yao.
“Wakazi wa Mwanza walipokee, waimbaji mbalimbali wa mataifa mbalimbali, ni sherehje, raha, vifijo,” alisema Msama.

ONGEZEKO LA BAJETI KATIKA SEKTA YA UTALII

Katika mipango ya kukuza uchumi,  sekta ya utalii chini ya Prof Jumanne Maghembe ambaye ni Waziri mpya wa maliasili na utalii imeamua kuanza kuweka mikakati katika kuongeza bajeti ya kutosha kwa mwaka 2016,  ili kuongeza bidhaa na huduma zenye ubora kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi nchini.
Sekta ya utalii imekuwa na mpango wa kuongeza watalii wa kigeni zaidi ya Million 3 mpaka kufikia 2018, ambapo mkakati huu utaenda sambambana na ongezeko la pato la taifa kuongezeka mara mbili ya kinachopatikana kwa sasa.
kwa upande wake mdau wa masuala ya Utalii, Bw. Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania alifafanua kuwa sekta ya utalii imekuwa mstari wa mbele katika kukuza uchumi baada ya kilimo, hivyo kama suala hili litatiliwa mkazo basi tunasubiria Tanzania mpya katika uchumi.
Aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Sekta hii inabidi ikabiliane na matatizo yanayoikabili katika ukusajji wa kodi, kwa namna moja au nyingine inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kama hatuta chukua hatua yeyote”.
“Hata hivyo,inabidi tuangalie maboresho katika nyanja tofauti tofauti, bado kuna wahudumu wasio na ujuzi wa kutosha, ukilinganisha na huduma ukiwa nje ya nchi na hapa ni tofauti, hivyo tujaribu kuweka mafunzo ya ziada kwa waajiriwa na waajiri ili kuongeza ufanisi katika kazi”

No comments :

Post a Comment