MORE than 500 magistrates from different levels are to be reprimanded for poor performance in disposal of cases, the Chief Justice (CJ) Mohamed Othman Chande, announced in Dar es Salaam.
The CJ said this at a news conference
held at Mnazi Mmoja grounds in the city, where he disclosed that names
of 508 magistrates would be forwarded to the disciplinary committee for
action.
“We have already directed all judges in
charge of each zone to give seven days to the concerned magistrates to
show why disciplinary action should not be taken against them.
We want this action to be completed
within 21 days,” he insisted. According to him, the Judiciary had set a
target for each resident and district magistrate to determine 250 cases a
year and each magistrate at Primary Court level should determine 260
cases yearly. But, he said, the said 508 magistrate underperformed for
having handled below 100 cases.
“This is not acceptable. We are
operating like a boat which is moving at high speed to ensure early
disposal of cases, but there is an anchor which is preventing us from
moving. The only option we have is to pull it up so that we can stir the
motion,” the CJ said.
The head of the judiciary congratulated
all other magistrates who surpassed the target, saying they deserved to
be praised for the good job. He gave an example of two magistrates in
Dar es Salaam who handled over 900 cases each, another one from Mwanza
who determined 789 cases and another in Arusha who judged 778 cases
within a year.
“Our target is to start with fresh cases
each year. We want all cases that are filed in a year to be determined
within the same year and not otherwise. This move is of paramount
importance as the people want their cases to be determined early,” he
said.
He, therefore, called upon other
stakeholders, notably the prosecution to handle the cases with due
diligence, the police on their part to complete investigations in time
and the advocates to avoid employing technicalities aimed at hindering
timely determination of cases.
The CJ also requested the citizens to
volunteer themselves to come to court to give testimony, while other key
players, like the prison department should ensure inmates are brought
to attend their case without failure wherever required.
Speaking on overview of acceleration of
determination of cases, he said 222,815 cases were determined last year.
At the Primary Court level, the CJ said that 141,025 cases were lodged
in the country and 149,757 (including old cases) were determined.
He pointed out that a total of 1240
magistrates handled the cases at all levels and 74.4 per cent of the
cases determined were at Primary Courts.
Meanwhile, the CJ told the press
conference that the Law Day is expected to be held at national level in
Dar es Salaam on February 4, and President John Magufuli is expected to
be the guest of honour
Mwamuzi wa kwanza mtanzania wa mchezo wa Baseball.
Kijana Innocent Kennedy ni
mtanzania mwenye umri wa miaka 19 tu na kwasasa amekuwa ni gumzo kwa
vyama vya kulipwa vya mchezo huu wa baseball barani Asia hususani nchini
Japan.
Innocent ameonyesha umahiri mkubwa wa kuamua na kwa mara ya kwanza alishiriki katika kuamua mashindano ya Africa ya kutafuta uwakilishi wa kombe la Dunia la mchezo huu, mashindano yaliyofanyika nchini Kenya katika jiji la Meru hapo Disemba, 2014.
Kwasasa kijana Innocent anaendelea na masomo yake ya ICT jijini Dar es Salaam na ametenga muda wake wa kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 13 :30 hadi saa 18:30 jioni kufika viwanjani Azania Sekondari kushiriki mazoezi ya timu ya Taifa ya baseball.
Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball bwana Alpherio Nchimbi alipoulizwa juu ya ndoto ya kumuendeleza kijana huyo, bwana Nchimbi alisema kwa kifupi kuwa lengo kuu ni kuzalisha akina Innocent wengi lakini kwa Innocent anafanyiwa mipango mahususi ya kumpeleka nchini Japan kwa mafunzo zaidi.
Innocent ameonyesha umahiri mkubwa wa kuamua na kwa mara ya kwanza alishiriki katika kuamua mashindano ya Africa ya kutafuta uwakilishi wa kombe la Dunia la mchezo huu, mashindano yaliyofanyika nchini Kenya katika jiji la Meru hapo Disemba, 2014.
Kwasasa kijana Innocent anaendelea na masomo yake ya ICT jijini Dar es Salaam na ametenga muda wake wa kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 13 :30 hadi saa 18:30 jioni kufika viwanjani Azania Sekondari kushiriki mazoezi ya timu ya Taifa ya baseball.
Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball bwana Alpherio Nchimbi alipoulizwa juu ya ndoto ya kumuendeleza kijana huyo, bwana Nchimbi alisema kwa kifupi kuwa lengo kuu ni kuzalisha akina Innocent wengi lakini kwa Innocent anafanyiwa mipango mahususi ya kumpeleka nchini Japan kwa mafunzo zaidi.
WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI
Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,
………………………………………………………………………….
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi la
polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia
halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia
kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza.
Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi
Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi
Kamanda amesema utaratibu huu
huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwaajili ya kuhakiki
silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu
wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa, nawakumbuke
sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia
ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa.
Ameongeza
kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo
tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema
kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti
yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa
umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki
silaha.
Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi .
Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi .
Amehitimisha
kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi
na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na
silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono
ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake,
Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi
septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.
MADEREVA DALADALA JIJINI MWANZA WATISHIA KUGOMA IKIWA MAJIPU YA TAX BUBU HAYATATUMBULIWA.
Ridhione
Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala
wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini
Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua
katika shughuli zao.
Alisema
licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika
eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika
hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu
wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.
Senga
alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika
kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo
amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao
kufanyiwa kazi.
“Sisi
tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao
hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala
licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina
ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala
na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma
yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa”.Alisema Senga.
Ramadhan
Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za
Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo
na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax
bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya
usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.
“Hizi
tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva
wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na
tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku
Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua”.Alisema Athuman
Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko
Jijini Mwanza.
Kaptaini
Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza,
ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri
vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka
husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia
taratibu la utendaji kazi wa tax.
Juhudi
za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha
sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko
yanayowakabiri.
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo
MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WANUFAISHA KAYA MILIONI 1.1 NCHINI
Mpango
wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na
umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya
Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na
umasikini.
Hayo
yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa,
Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo
ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la
Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za
Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
Bi.
Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda
kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi
sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa
alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika
Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na
lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji
ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu
jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo
Tanzania visiwani.
Serikali
ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza
umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa
kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu
ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013
pekee katika wilaya nane nchini.
Mtaalamu
Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis
Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani
Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa
fedha hizo.
Na
mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya
masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya
161 na vijiji 9789 nchini.
Malengo
ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha
kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi
kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa
kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
Asilimia kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo
pichani).
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya
Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
Bi Jabo Omari Othman akiwa kwenye shamba lake alilonunua kutokana na fedha za TASAF visiwani Unguja.
SIMBA SPORT CLUB WAZINDUA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO
Rais
wa Simba Sport Club Evans Aveva Akikata Utepe wakati wa Uzinduzi wa
Duka la Vifaa vya Michezo akiwa Ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuuwa
Eaggroup Ndugu Iman Kajula Pamoja na Wadau wengine wa Club Hiyo.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Rais wa Simba Evans Aveva alisema “kama
mtakumbuka moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani
ulijiwekea ni pamoja na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake
vilivyopo lakini pia kuja na mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na
leo wote tunakuwa mashuhuda katika kuzindua duka letu la vifaa vya
michezo. Duka ambalo litakuwa likiuza kila bidhaa ambayo inachapa Simba
hivyo wanachama na wapenzi wa Simba kuweza kujua ni wapi mahala pa
kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu zaidi”
Duka
hili si tu litasaidia katika kuongeza mapato kwa klabu lakini pia
litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia mema klabu yetu na
kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa sasa mtu
ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende
kuwa sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la
Tanzania kwa ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia
tupende kutumia vitu halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya
kutojali ni kipi halisi na kipi ni feki” aliongeza Rais Aveva
Akizungumza
kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Ltd ambao ni
washauri na watekelezaji wa masuala ya biashara na masko kwa klabu ya
Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa wanasimba tunaweza
kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana na ni
wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo
si pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree
Market. Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote
vitakavyokuwa vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa
vikipatikana kwenye duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza
kuwafikia watu wote popote walipo nchini Tanzania”.
Unapotaka
vifaa vyenye ubora wa hali ya juu hakuna sehemu nyingine zaidi ya Simba
Sports Shop. NUNUA HALISI ICHANGIE TIMU YAKO. Alimalizia Mkurugenzi wa
EAG Group Ltd Imani Kajula
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo msimamizi wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa
kuhamasisha wapenzi wote wa Soka Tanzania kuweza kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza kukuza mapato kwa klabu yetu
lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za chapa ya Simba.
Uzinduzi wa wiki ya Mahakama mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa leo
amezindua wiki ya mahakama kwa maandamano mjini Iringa yaliyoongozwa na
brass band ya Magereza. Akihutubia majaji pamoja na wananchi amesisitiza
uharaka wa kutoa HAKI. kesi nyingi zinachelewa kuisha na wananchi wengi
wamedhrumiwa haki yao na huu ni uvunjwaji katiba.
Pia amesisitiza wakimama wasimamiwe haki zao. Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika? Wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi. Bila haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo.
Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia kutembelea magereza yote ili kubaini waliocheleweshewa haki zao.
Pia amesisitiza wakimama wasimamiwe haki zao. Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika? Wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi. Bila haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo.
Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia kutembelea magereza yote ili kubaini waliocheleweshewa haki zao.
BONDIA VICENT MBILINYI APIGIA MKWALA MZITO MWINYI MZENGELA KUPIGANA PASAKA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi
anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila ‘Super D’ amemchimbia mkwala mkali bondia Mwinyi Mzengela
watakapokutana siku ya April 26 katika sikukuu ya Pasaka
Mbilinyi amemtangazia kiama
Mzengela baada ya kukubali kupambana nae katika uzito wa KG 63 amesema
nitamsambalatisha mapema mno bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa KG
63 kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC)
Mbilinyi aliongeza kwa kusema
namuheshimu Mzengela kwa kuwa ni bingwa wa Taifa hata hivyo
nitahakikisha nausambaratisha utawala wake na mimi nakuwa juu yake kwa
kuwa nia ninayo uwezo ninao na nitaonesha jinsi ngumi zinavyochezwa
Najuwa katika ngumi za kulipwa
sina muda mrefu sana na nimeshatambulika kwa kuwa najua nini nakifanya
katika mchezo uhu wa masumbwi nchini
Nimeingia katika ngumi za
kulipwa sio kupoteza mda kwa kuwa najua mchezo wa ngumi ila kwangu mimi
ni ajira na ndio ninayo itegemea.
WATUMISHI 508 WA MAHAKAMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU ASEMA JAJI MKUU MHE. MOHAMED OTHMAN CHANDE.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohamed Othman Chande akizungumza wa waandishi wa Habari kuhusu kuanza
kwa Mwaka wa Sheria 2016, Wiki ya Sheria na Utendaji wa Mahakama ya
Tanzania kwa mwaka 2016. Wengine Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.
Omary Othman Makungu (Kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Lila
(kulia).
………………………………………………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohamed Othman Chande amesema kuwa Mahakama ya Tanzania itawachukulia
hatua za kinidhamu na za kisheria Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo,Wilaya
na wale wa Mahakama za Hakimu Mkazi wapato 508 kote nchini waliotekeleza
majukumu yao chini ya kiwango na kushindwa kutimiza wajibu wa Mahakama
wa Utoaji wa Huduma Bora kwa wananchi katika mwaka wa Sheria wa
2015/2016.
Akizungumza na waandishi wa
Habari leo jijini Dar es salaam alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu kuanza
kwa mwaka mpya wa Sheria wa 2016 na Maadhimisho ya Wiki ya Sheria
ambayo kilele chake kitakua Januari 4,2016 Jaji Mkuu amesema kuwa kwa
mujibu wa taratibu za uendeshaji wa Mahakama na upimaji wa viwango vya
utendaji kazi vilivyowekwa, Mahakimu hao wa Mahakama za wilaya na Hakimu
Mkazi 121 na 387 wa Mahakama za Mwanzo watatakiwa kutoa maelezo ndani
ya siku 7 juu ya sababu zilizowafanya washindwe kutimiza lengo
lililowekwa la kushughulikia mashauri 260 kila mmoja.
Amesema watakaothibitika kamati
za nidhamu na maadili za kila wilaya na Mikoa ambazo ni Kamati ndogo za
Tume ya Utumishi wa Mahakama zitawafungulia kesi za kinidhamu ndani ya
siku 21.
“Wale watakaobainika watakumbwa
na adhabu ya kupewa Onyo, kushushwa vyeo na kufukuzwa kazi ili iwe
fundisho kwa wengine, ninajua wapo baadhi ambao waliajiliwa katikati ya
mwaka, wengine kwenda mafunzo ya vitendo vyuoni, wajawazito na baadhi
vituo vyao kuwa na kesi chini ya 260 kwa mwaka” Amesisitiza.
Aidha, katika hatua hiyo
amewapongeza Mahakimu waliofanya vizuri katika utendaji wao wakiwemo 14
walioshughulikia mashauri zaidi ya 700 kila mmoja, Mahakimu 50 walioamua
kesi zaidi ya 500 kila mmoja baadhi wakitokea wilaya ya Mkuranga,
Rufiji na Bukoba mjini na wengine wawili kutoka Dar es salaam walioamua
kesi zaidi ya 900 kila mmoja na kuvuka lengo la utendaji lililowekwa
la kushughulikia mashauri 260 kwa mwaka.
Akitoa tathmini ya utendaji wa
Mahakama kwa mwaka wa sheria uliopita amesema kuwa Mahakama ya Tanzania
ina Mahakama za Hakimu Mkazi kila Mkoa na Mahakama za Wilaya 111 katika
wilaya za Kiserikali 133 pamoja na Mahakama za Mwanzo ambazo hupokea
asilimia 93 ya mashauri yanayofunguliwa kote nchini.
Amesema mwaka 2015 Mahakama zote
nchini zilipokea jumla ya mashauri 206,115, kati ya hayo mashauri
220,815 yaliamuliwa kukiwa na ziada ya mashauri 14700 jambo
linaloonyesha kuwa Mahakama zinapokea mashauri na kuyashughulikia kwa
kasi inayoridhisha huku mashauri yanayosababisha mrundikano ni yale
yaliyo nje ya idadi iliyopangwa.
Ameongeza kuwa katika katika
kipindi cha mwaka huo wa 2015 Mahakama za Mwanzo zilipokea mashauri
141,025 ambapo kati ya hayo Mashauri 149,757 yalishughulikiwa huku idadi
ya Mahakimu walioshughulikia mashauri hayo ni 1240.
“Ukiangalia mwenendo wa ufunguaji
wa mashauri yote kote nchini hasa Tanzania Bara utagundua kuwa Mahakama
za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi zinapokea mashauri mengi kwa
asilimia 93 ,katika kila mashauri 4 yanayofunguliwa nchini 3 yako
mahakama za mwanzo ambako wananchi wengi wanatafuta ufumbuzi wa kesi zao
lazima tuweke mkazo” Amesema Jaji Mkuu.
Kuhusu kuanza kwa mwaka mpya wa
Sheria mwaka 2016 amesema Mahakama inauanza chini ya Kauli Mbiu Isemayo
“Huduma Bora kwa Wananchi ni Wajibu wa Mahakama na Wadau wake” ikiwa na
kesi 20,431 ikilinganishwa na 34,126 ilizoanza nazo mwaka 2015 na
kuongeza kuwa licha ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania
mkakati uliopo ni kupunguza idadi hiyo hadi kufikia 0 kwa kila mwanzo wa
mwaka wa sheria.
Akitoa ufafanuzi kuhusu
upatikanaji wa Nakala za hukumu amesema Serikali inaendelea kuijengea
uwezo wa kifedha Mahakama wa kuajiri wachapaji wa nakala wengi zaidi ili
Nakala za Hukumu za Kesi ziweze kupatikana pindi tu kesi zinapomalizika
katika mahakama zote nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo hupatikana
Mahakama Kuu na Mahakama za Rufani.
Aidha, amesema Mahakama
inaendelea kuboresha miundombinu yake ikiwemo majengo na ujenzi wa
mahakama mpya katika maeneo yasiyo na huduma hiyo katika mwaka 2016. “
Hivi sasa tuna wilaya 23 hazina Majengo ya Mahakama za wilaya, kwenye
baadhi ya maeneo kesi zinasikiliziwa Ofisini kwa Hakimu wakati ilitakiwa
ziwe kwenye jengo lenye ukumbi wa wazi,tumejiandaa kwa michoro ya
majengo kwa mahakama zote ili tuanze kujenga kwa gharama nafuu”
Mhe. Chande ametoa wito kwa
wananchi kutosita kuitumia Mahakama ya Tanzania katika kupata ushauri wa
kisheria kupitia wataalamu wake, kuhudhuria maonesho mbalimbali ya
kisheria yanayofanyika nchini huku akitoa angalizo kwa baadhi ya watu
wanaochangia kuwepo kwa mrundikano wa kesi kwa kufungua kesi za madai au
kupeleka mashauri Mahakamani kama sehemu ya maegesho ya masuala yao.
“Baadhi ya watu wamekuwa
wakipeleka kesi Mahakamani kama sehemu ya maegesho, huzifungua kisha
hushindwa kujitokeza Mahakamani hizi ni tofauti na zile zenye vipengele
vingi ndani ya kesi moja au zile ambazo mashahidi wake wamehama kutoka
eneo moja kwenda linguine, hizi nawahakikishia tutazifuta ili kupunguza
mrundikano wa kesi kwenye Mahakama zetu” Amesisitiza Mhe. Chande.
UMOJA WA WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA HEGONGO,MUHEZA WAANGUSHA PARTY LA NGUVU
Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya
Hegongo, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wakicheza muziki wakati wa
hafla yao ya kukumbukana iliyofanyika kwenye Mgahawa wa City Sports
Lounge, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Martine Jengo (kulia) na Mzee Hassan wakiserebuka
Mmiliki wa TSN Group, Farouq Baghoza (kulia), ambaye pia alisoma katika
shule hiyo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumbukumbu.
Mmiliki TSN Group, Farouq Baghoza (kulia) akiwa na wanafunzi aliosoma
nao katika shule ya Hegongo, Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports
Lounge, Benny Kisaka (kushoto) pamoja na Gerald Yambi ambaye ni
mwanachama maarufu Kundi la Friends of Simba. Baghoza aliwahi pia kuwa
Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars Ishinde.
Sasa ni wakati wa mlo
Mwanafunzi Edwin Pemba (kushoto) akiwa na Mwalimu John Sebo (katikati) aliyewahi fundisha katika Shule ye Sekondari ya Hegongo.
Aliyewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hegongo, John Sebo
akishukuru kualikwa na waliokuwa wanafunzi wake katika hafla hiyo
muhimu.Kulia ni Mwanafunzi Benny Kisaka ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi
wa Mgahawa wa City Sports Lounge.
Hawa walimaliza Kidato cha Nne katika shule hiyo 1985.
Hawa walisoma katika shule hiyo na kumaliza Kidato cha Nne miaka ya tisini
JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana ,
kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za
wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508
watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na
kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa
Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban
Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya
Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi
Msaidizi Ukaguzi na Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng’humbu
(kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati
mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada
wa kisheria katika maonyesho hayo.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akisoma moja ya daftari katika banda
la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness
Ndesamburo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo.
…………………………………………
Na Dotto Mwaibale
JAJI
Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508
watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na
kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.
Jaji
Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Alisema
kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na
Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama
hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
Alibainisha
kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo
mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi
chini ya 100 mwaka jana.
“Ukiondoa
wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za
mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya
mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.
“Majaji
Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa
kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa
mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini
wasichukuliwe hatua,” alisema Jaji Chande
Jaji
Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka
idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane
ni hatua gani wanachukuliwe.
“Mahakama
haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya
hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika
mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini
ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo,” alisema
Jaji
Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya
kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na
kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.
“Mahakimu
wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan
sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko
walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za
Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki,” alisema
Hata
hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango,
ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu
wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Alisema
mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna
baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka
upya.
Jaji
Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi
34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha
kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni
zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji
asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
BALOZI WA SWEDEN AMTEMBELEA SPIKA OFISINI KWAKE
Balozi
wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt akisaini kitabu cha Wageni
alipomtembelea leo ofisini kwake tarehe 01 Febuari, 2016 Mjini Dodoma.
Kulia kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
WANANCHI WAMESHAURIWA KUACHA TABIA YA KULA KATIKA MAZINGIRA SI SALAMA
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
……………………………………………
Wananchi wameshauriwa kuacha tabia
ya kununua matunda yaliyomenywa barabarani au kula chakula
kilichoandaliwa katika mazingira ambayo si safi na salama ili kuweza
kuepuka ugonjwa kipindupindu na kulinda afya zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Michael John wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam kuhusu taarifa za ugonjwa huo kwa nchi nzima.
“Suala la kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu linahitaji ushirikiano wa watu wote.Usiponunua matunda yaliyomenywa na watu wanaouza barabarabani, hata wale wanaouza wataacha kuuza. Pia Serikali itatumia nguvu kidogo kwa ajili ya kuwadhibiti,” alisema John.
Akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanyika za kukabialiana na ugonjwa huo, alisema hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambayo imekwenda Morogoro ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya na nyingine mkoani Dodoma ambayo itakuwa na Waziri wa wizara hiyo,Ummy Mwalimu ili kuweza kushirikiana na mamlaka, watendaji na baadhi ya wadau kuudhibiti ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa ripoti ya ugonjwa huo kwa kipindi cha wiki jumla ya wagonjwa 459 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika mikoa 15 na vifo vitano.
Alisema mkoa wa Simiyu ndio unaongoza kuwa na idadi ya wagonjwa wengi, ukifuatiwa na Mwanza, Mara na Morogoro. Pia mikoa ya Njombe , Ruvuma na Mtwara haijawahi kuripotiwa na ugonjwa huo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Michael John wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam kuhusu taarifa za ugonjwa huo kwa nchi nzima.
“Suala la kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu linahitaji ushirikiano wa watu wote.Usiponunua matunda yaliyomenywa na watu wanaouza barabarabani, hata wale wanaouza wataacha kuuza. Pia Serikali itatumia nguvu kidogo kwa ajili ya kuwadhibiti,” alisema John.
Akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanyika za kukabialiana na ugonjwa huo, alisema hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambayo imekwenda Morogoro ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya na nyingine mkoani Dodoma ambayo itakuwa na Waziri wa wizara hiyo,Ummy Mwalimu ili kuweza kushirikiana na mamlaka, watendaji na baadhi ya wadau kuudhibiti ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa ripoti ya ugonjwa huo kwa kipindi cha wiki jumla ya wagonjwa 459 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika mikoa 15 na vifo vitano.
Alisema mkoa wa Simiyu ndio unaongoza kuwa na idadi ya wagonjwa wengi, ukifuatiwa na Mwanza, Mara na Morogoro. Pia mikoa ya Njombe , Ruvuma na Mtwara haijawahi kuripotiwa na ugonjwa huo.
MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akisoma Mapendekezo ya Mpango
wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa
kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha, 2016/2017,
bungeni mjini Dodoma Februari 1, 2016.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangallah akijibu Maswali Bungeni Mjini Dodoma Februari 1, 2016.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu Maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 1, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SERIKALI YAPANGA KUFANYA MATUMIZI YENYE TIJA
………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija
kwa kuelekeza bajeti kubwa kwenye mambo muhimu hasa sekta zenye za
kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
Akiwasilisha
mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha
2016/2017 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema
mwongozo wa mpango na bajeti umezingatia mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za
uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla
ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika
kipindi hiki.
“
Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla
ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1
ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa mapato yasisiyo
ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion
1.1.
“
katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya
shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia
13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la asilimia 14
ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3
kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
Mhe
Philip Mpango amesema mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na
Mipango, hivyo basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za
serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za
Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na
kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na
bajeti iliyoidhinishwa.
\
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
\
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
Serikali
itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na
kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania
wote.
SERIKALI IMEWATAKA WANANCHI KUYATUNZA MAENEO YENYE ARDHI OEVU.
Afisa
Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha
akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu
maadhimisho ya siku ya ardhi oevu Duniani inayotarajiwa kufanyika
februari 2,2016 ambapo siku hiyo itatumika kutoa elimu kwa kuwakumbusha
watu kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhi oevu.
Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Lusungu Helela, kushoto ni
Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu Kitaifa wa Uhifadhi Ardhi Oevu Bw.
Pellage Kauzeni.
Afisa
Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw. Pellage
Kauzeni akitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya ardhi
oevu kushirikiana na Serikali katika kuyatunza maeneo hayo kushoto ni
Afisa Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha
na kulia ni Afisa Habari wa wizara hiyo Bw. Lusungu Helela.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatlia mkutano wa Wizara ya Mali Asili na
Utalii uliolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maadhimisho ya siku ya
ardhioevu ambayo huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe unaoweza
kusababishwa na mawimbi ya bahari.
( Picha zote na Frank Mvungi )
( Picha zote na Frank Mvungi )
………………………………………………………………………………..
Na Fatma Salum-Maelezo
Serikali
imewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yenye ardhi oevu kushiriki
katika kuyatunza maeneo hayo ili waweze kunufaika na rasilimali
zinazotokana na uwepo wa maeneo hayo.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Afisa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Sadiki Lotha wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Ardhi oevu husaidia upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mimea na wanyama hivyo vyanzo vyake havina budi kulindwa kwa kuepuka shughuli zinazopelekea kuathiri vyanzo hivyo.” Alisema Bw. Lotha.
Akizitaja baadhi ya shughuli zinazoathiri ardh ioevu Bw. Lotha alisema ni ufugaji holela, ujenzi kwenye vyanzo vya maji, kilimo na ukataji wa miti ovyo.
Naye Mratibu wa Kitaifa wa Uhifadhi wa ardhi oevu Bw. Pellage Kauzeni alisema kuwa uharibifu wa ardhi oevu hupelekea athari katika sekta ya uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji na ufugaji hivyo kuharibu bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia.
Aidha Bw. Kauzeni alisema Tanzania imeridhia makubaliano ya kimataifa ya mkataba wa Ramsar kuwa ndio msingi wa usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi oevu duniani uliosainiwa na nchi wanachama mjini Ramsar nchini Iran mwaka 1971.
Siku ya Ardhi Oevu duniani itafanyika kesho tarehe 2 Februari, 2016 ikiwa na kaulimbiu “MAISHA YA KIPATO ENDELEVU”.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Afisa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Sadiki Lotha wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Ardhi oevu husaidia upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mimea na wanyama hivyo vyanzo vyake havina budi kulindwa kwa kuepuka shughuli zinazopelekea kuathiri vyanzo hivyo.” Alisema Bw. Lotha.
Akizitaja baadhi ya shughuli zinazoathiri ardh ioevu Bw. Lotha alisema ni ufugaji holela, ujenzi kwenye vyanzo vya maji, kilimo na ukataji wa miti ovyo.
Naye Mratibu wa Kitaifa wa Uhifadhi wa ardhi oevu Bw. Pellage Kauzeni alisema kuwa uharibifu wa ardhi oevu hupelekea athari katika sekta ya uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji na ufugaji hivyo kuharibu bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia.
Aidha Bw. Kauzeni alisema Tanzania imeridhia makubaliano ya kimataifa ya mkataba wa Ramsar kuwa ndio msingi wa usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi oevu duniani uliosainiwa na nchi wanachama mjini Ramsar nchini Iran mwaka 1971.
Siku ya Ardhi Oevu duniani itafanyika kesho tarehe 2 Februari, 2016 ikiwa na kaulimbiu “MAISHA YA KIPATO ENDELEVU”.
MKUU WA WILAYA YA WETE RASHID HADID AMEWATAKA WALIMU WAKUU KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA HATI MILIKI YA MAENEO YA SKULI ZAO .
…………………………………………
MKUU
wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid amewataka walimu wakuu katika
wilaya hiyo , kusimamia upatikanaji wa hati miliki ya maeneo ya skuli
zao .
Amesema
kuwa maeneo mengi ya Skuli ndani ya Wilaya ya Wete yanakabiliwa na
migogoro ya ardhi inayosababishwa na kutokuwepo na hati miliki .
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na walimu Wakuu wa Wilaya hiyo kwenye
ukumbi wa mikutano wa zamani wa Chuo cha uwalimu Benjamini Mkapa kwenye
mkutano wa kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo .
‘Kila
mwalimu analojukumu la kusimamia upimaji wa maeneo ya Skuli na kisha
kupatiwa hati miliki , hii itaondoa migogoro inayojitokeza kwa sasa
”alisisitiza
Amesema
kwamba Serikali ya Wilaya iko tayari kushirikiana na Uongozi wa Skuli
katika Wilaya hiyo kuhakikisha maeneo hayo yanapimwa na kupatiwa hati
miliki .
“Serikali
ya Wilaya iko tayari wakati wowote kutoa msaada wa uoatikanaji wa hati
miliki ya maeneo ya Skuli , tunashirikiana kufuatilia katika ngazi
zinazohusika ”aliafahamisha.
Mapema
Afisa Elimu na Mafunz ya Amali Wilaya hiyo Khamis Said Hamad amesema
kwamba yapo baadhi ya maeneo ya Skuli yamepimwa lakini imekuwa ni vigumu
kupatikana kwa hati miliki .
Hivyo
ameiomba Serikali ya Wilaya kusaidia kupatiokana hati miliki katika
Skuli hizo ambazo tayari maeneo yake yamepimwa ikiwa skuli ya Sekondari
ya Pandani .
“Zipo
skuli tayari maeneo yake yamepimwa lakini bado hati miliki
hazijapatikana , ikiwemo Skuli ya Sekondari ya Pandani ambayo eneo lake
limeshapimwa ”alifahamisha.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mchangamdogo Juma Said Hamad
ameiomba Serikali ya Wilaya kulipa kipaumbele suala la kuyapima maeneo
ya skuli .
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba asilimi 60 ya maeneo ya Skuli
za Wilaya ya Wete hayana hati miliki jambo ambalo linasababisha maeneo
hayo kuvamiwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na makaazi
Walemavu: Msama anajitambua
………………………………………….
BAADHI ya walemavu hapa
nchini wametoa wito kwa Watanzania wengine kujitambua kuhusu Mungu na
mikakati mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwa ni kuelekea
Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 jijini Mwanza.
Akizungumza jana kwa niaba ya
Esperance Wetewabo ambaye ni mlemavu wa mikono na mguu, mchungaji wa
Godfrey Rubanzibwa ‘Punda wa Yesu’ alisema jamii inatakiwa kujitambua
kuhusu Mungu kama alivyo Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha
la Pasaka, Alex Msama anavyotekeleza majukumu yake katika muziki huo.
Honoratha
aliumia fursa hiyo kuwapa usia Watanzania wote wakiwemo walemavu kuiga
mfano wa Msama ambaye anatekeleza majukumu hayo.
MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA
Katika
salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa
na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi
ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha
Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa
hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.
TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING
Malinzi
ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col.
Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka
kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu
Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na
kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika
hilo la B.
Washindi
wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda
Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo
miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.
TFF HAINA VITA NA ZFA
Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi.
Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la
kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji
miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba
alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya
maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa
Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji
miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama
Januari 27.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV
Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya
shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe
aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro
mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
Wasamaria
wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha
MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro,
wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani),
wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji
zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi
ya vitu vikiokolewa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya,
akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya
kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasili
Bungeni katika kuanza kikoa cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza
sala ya kuliombea Bunge kabala ya kuanza kikao cha Tano cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiwasilisha hoja ya
Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo mwa mwaka mmoja katika kikao cha
Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja
toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea
Mjini Dodoma.
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo akijibu hoja toka kwa
wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma.
Naibu
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akijibu
hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa akimsikiliza Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbalawa wakati kikao cha
Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula
akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.nape Moses Nnauye akijadiliana
jambo na Waziri wa NChi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano
Mhe January Makamba wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea
Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatila kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YAWAKOMBOA WANAWAKE WA ZANZIBAR KIUCHUMI
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
Baadaye
mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama
Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch
Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamlai .
Mwisho
wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya
kuanzisha na kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa
mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano
Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo
la ukosefu wa ajira.
WATUMISHI WA AFYA NCHINI WATAKIWA KUACHA KUHUJUMU DAWA ZINAZOPELEKWA KWA AJILI YA WANANCHI
Naibu Waziri maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.hamisi kigwangwala akizungmza na watumishi wa Afya.
Baadhi ya wafanyakazi wa bohari ya
dawa(msd)kanda ya kaskazini wakimsikiliza naibu waziri wa
afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani)
Watumishi wa hospitali ya mkoa ya mount meru wakimsikiliza kwa makini dkt.hamis kigwangwala.
watumishi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya naibu waziri.
(Habari na picha toka wizara ya afya)
…………………………………………………………………………………….
Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuacha kuhujumu dawa zinazopelekwa kwa ajili ya wananchi na si za biashara kama wanavyofanya
Onyo hilo yamesemwa mwishoni mwa
wiki na naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto,dkt.hamisi kigwangwalla wakati akiongea na wafanyakazi wa bohari
ya dawa(msd)pamoja na wale wa hospitali ya mkoa ya mount meru.
Dkt. Kigwangwalla alisema serikali
ya awamu ya tano yenye kaulimbiu ya “hapa kazi tu”haitawavumilia
watumishi wa aina hiyo na kama wapo basi waanze kujipima kabla rungu la
dola halijawafikia
Aidha,alisema suala la upatikanaji
wa.dawa kwa wananchi na kwa bei nafuu ni moja ya mambo yaliyopewa
kipaumbele katika serikali ya awamu ya tano
“Wananchi wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha Malibu”
Hatahivyo aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’
Kwa dawa zote zinazokuwa.zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nemo
Licha ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa.zilizopokelewa kwenye mbao.za matangazo
Aliitaka bohari ya dawa(msd)kukamilisha uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na kukagua kama dawa Za.serikali zimefika.hadi sasa vidonge vipatavyo 65 vimekwishawekewa nembo ya GoT.
“Wananchi wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha Malibu”
Hatahivyo aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’
Kwa dawa zote zinazokuwa.zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nemo
Licha ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa.zilizopokelewa kwenye mbao.za matangazo
Aliitaka bohari ya dawa(msd)kukamilisha uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na kukagua kama dawa Za.serikali zimefika.hadi sasa vidonge vipatavyo 65 vimekwishawekewa nembo ya GoT.
Rais Mstaafu JK akutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma
Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa Dkt.
Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika
(kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa
usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia
uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi
za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma
makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu
alilokabidhiwa.
Mheshimiwa
Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani
kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.
Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye
Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na kuwa
tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika
nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake.
Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha
katika kutekeleza majukumu yake.
Serikali kujenga Vyuo Vya VETA kila Wilaya
Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.
……………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia kujenga Vyuo vya Ufundi
(VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani
vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi yatakayowasaidia kujikwamua
kiuchumi na kujenga taifa.
Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGMZO NA RAIS UHURU KENYATA WA KENYA AU ADDIS ABABA
(Picha na OMR)





No comments :
Post a Comment