Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu
mstaafu, Fredrick Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya
kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther
(kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
(kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya
Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam
leo asubuhi.
Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya, Justine Chiganga (kulia), akizungumza katika mkutano huo
Moja ya kibanda kilichojengwa na wananchi waliovamia eneo la Mhe Sumaye.
Baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wananchi katika eneo la Sumaye.
Askari Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa mchakato wa kutembelea eneo hilo lililovamiwa.
Wananchi wa eneo la Mabwepande wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkazi wa eneo hilo Athuman Mnubi akielezea jinsi walivyovamia eneo la Sumaye.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabwepande Abdalla Omari Kunja akizungumza katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Matinga Ernest akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Ardhi katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada
baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari
33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam.
Serikali
imemuahikikishia Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge
wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki
mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa
wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro
huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali
kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
Alizitaka
pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia
bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea
na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
“Serikali
ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza
Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki
tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna
mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
Alisema
katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika
kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli
hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili
kutafuta suluhu.
Zipo
njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa
kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi
kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema.
Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
Alizitaka
pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo
kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
Awali
katika mkutano huo Sumaye alimueleza Makonda jinsi serikali ilivyo na
kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara
zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu
sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na
nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani
wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha
uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali.
Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa kuwapa wananchi .
Suzan
alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii
kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo
cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo.
Mmoja
wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa
eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo
uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema
wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora
maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa.
WAKATI
huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na
mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan
wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na
alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema
hawana.
Makonda
amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa
maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa
uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na
matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
TIMU ZA ,MAFUNZO NA JKU ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mafunzo Mpira wa Miguu
(Football) Haji Ramadhan Mwambe katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini
Unguja leo,timu hiyo itashiriki mashindano ya
klabu bingwa Afrika kwa kupambana na Timu ya AS Vita ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kwenye Uwanja wa Amaan tarehe 13 Februari,
2016 (katikati) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi.Sharifa Kahamis,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu JKU
Ponsiana Malik Joseph katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja leo,timu
ya JKU ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho itapambana na timu ya
Gaborone United ya Botswana katika uwanja huo huo wa Amaan Studium
tarehe 14 Februari,2016.[Picha na Ikulu.)UMOJA WA WANAWAKE TUGHE TAWI LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA, WAJADILI UMOJA NA USHIRIKIANO JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana
wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia
meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu
ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka
Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana
wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia
meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu
ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka
Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
CCM yaridhishwa na Tume ya Uchaguzi ZEC kwa kutangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi Zanzibar
Na Ally Ndota, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi
Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio
kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.
Kimesema maamuzi ya kufanyika
uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya
wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa
mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,
Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya
kisiasa nchini vilivyobaini kaso
ro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.
ro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.
Waride alisema msimamo wa CCM
katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa
marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoriki katika uchaguzi uliopita
kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika
kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani
wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani
lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na
hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza kwa
wingi wa kura halali.
“ Tunachukua fursa hii kuwaomba
wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na
wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura Machi 20 mwaka
huu.
Tukumbuke kwamba maamuzi hayo
yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya
Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea
katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata
haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na
zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi
huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.
Katibu huyo aliongeza kwamba pia
wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali
kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya
Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili
kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na
malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.
Akizungumzia suala la CUF kususia
Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo
na kususa kwa mipango ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali
katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi,
hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa
Zanzibar.
Alisema kwamba upinzani wa aina
hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo
ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya
baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko
maisha ya wananchi.
“ Kila chama kina sera zake na
misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo
njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao, lakini
sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi
kurudi madarakani ya kidemokrasia.
Aidha alisema chama hicho
kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa
na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa
uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.
Kupitia taarifa hiyo Waride
wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa
mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa
kwa CCM itakayofanyika katika Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31
mwaka huu.
Alisema Mgeni rasmi katika
uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye
pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali
Mohamed Shein.
MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LEO MJINI DODOMA
Baadhi ya wabunge wakiwasili katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Adrew
Chenge akiwakiwasilia tayari kuongoza kikao cha Bunge katika Bunge la 11
linaloendelea mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe
Dkt Philip Mpango akiwasilisha hoja ya Serikali ili Bunge lijadili na
kuidhinisha Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka
mitano
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Suleiman Jafo akitoa ufafnuzi juu ya
maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha
Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene
akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara
hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Sayansi,Teknolojia na
Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako akitoa ufafnuzi juu ya
maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha
Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Naibu wake
Mhe.Annastazia Wambura walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe
Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT) Mhe.
Zitto Kabwe walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma
Tanzania kuadhimisha siku ya Ukoma Duniani
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiongea an waandishi wa habari (Hawapo Pichani) leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani Kushoto ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma
Dkt Beatrice Mutayoba akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa ukoma na kwa
Tanzania Elimu zaidi itatolewa ili kupambana na ugonjwa huu.
Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia
,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia picha zikionesha wagonjwa
wa Ukoma kulia ni Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu
maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZOTanzania inaungana na nchi nyingine Duniani kuazimisha siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa tarehe 29 Januari 2016 kwa kutoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na Ukoma Tanzania na kuifanya Tanzania iweze kuondokana na m
aambukizi mapya ya ukoma.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ikiwa ni harakati za serikali kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa elimu kwa umma wa watanzania.
Mhe.Ummy Mwalimu amesema siku hii itawapa fursa ya kutathimini mwelekeo wa jitihada za nchi na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kuduma.
“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014,jumla ya wagonjwa 2,134 wa Ukoma waligunduliwa ambapo wagonjwa 271 kati ya hao ambao ni sawa na asilimia 13walikuwa na ulemavu na pia bado kuna Wilaya 17 za Tanzania bara na 2 za Tanzania Visiwani zilizogunduliwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukoma”
“ Nizitaje wilaya hizi ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukoma kwa Tanzania Bara ni Liwale,Ruangwa,Lindi Mjini,Lindi Vijini,Masasi Vijijini,Newala,Nanyumbu,Namtumbo,Tunduru,na Nkasi. Nyingine ni Mkinga,Muheza,Korogwe,Musoma,Korogwe,Musoma Vijijini ,Chato,Shinyanga Manispaa na Rufiji na kwa Tanzania Visiwani ni Mkoa wa Mjini Magharibi na katika wilaya za kati na kusini. Alisema Mhe Mwalimu.
Aidha amesema kuwa Tanzania katika kuadhimisha siku hii Serikali inayashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa michango yao katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa Tanzania na hivyo kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya ya Ukoma.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 Duniani ambazo bado zina viwango vya juu vya ugonjwa wa Ukoma na kwa zaidi ya miaka 62, siku ya ukoma Duniani imekuwa ikiadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Januari.
PROFESA MBARAWA AKAGUA ATHARI ZA BARABARA MORO – DODOMA
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri
huyo akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu
(kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za
barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Muonekano
wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua
zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko
yanayoelekea katika Mto Mkondoa.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha
uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad
Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri
huduma za usafirishaji.
Gari likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya Gairo-Dodoma.
Magari
yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa
barabara na kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza jumapili.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa – Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
“Hakikisheni Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa mvua za masika zinazokaribia kuanza.
“Chimbeni mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza Waziri Mbarawa.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo kuwezesha kupita maji kwa urahisi.
Profesa Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.

BAWATA waunga mkono tamko la Serikali
Mkurugenzi
wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na
waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria
zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini, kulia
ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.
Picha na Beatrice Lyimo
…………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho-Maelezo
Baraza la Waganga Tanzania
(BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba
asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar
es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed
Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga
wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji
huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi kama Baraza la Waganga
Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari
wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa
mujibu wa sheria”alisema Shaka
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA)
Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila
kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho
hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba
cha utabibu asili.
“kwa niaba ya BAWATA,
tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA
kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio
la shirikisho”. alisema Wiketye.
Ameongeza kuwa,wameafiki tamko
la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na kupendekeza
zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama
hizo.
Tamko hilo lilitolewa baada ya
kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa
tiba za asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali
inayohusu afya ya jamii.
ZIARA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA MAKAO MAKUU YA POLISI
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa
Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa
ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi
jijini Dar es Salaam jana .
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi
Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo
Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao
makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.DIGP ni mmoja wa Viongozi
waliopitia katika chuo hicho.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na
wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC (hawapo pichani) wakati wa
ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi
jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa
Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba na Brigedia Jenerali Minja.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa
ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho katika makao makuu ya
Polisi jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA – Januari 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Ofisini
kwake mjini Dodoma Januari 29, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo
Erasto Mbwilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 29, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TRA yasitisha upokeaji wa maombi ya nafasi za kazi.
ISO 9001:2008 CERTIFIED
KUSITISHWA KWA MUDA UWASILISHWAJI WA MAOMBI YA KAZI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
kituo cha huduma kwa wateja
08000780078, 0800750075, 0713800333

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKOANI KIBAHA WAPO HATARINI KUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MIUNDOMBINU KUWA MIBOVU
…………………………………………..
SHULE
ya msingi ya mkoani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa
inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa madawati,
madarasa pamoja na miundombinu ya madarasa kuwa mibovu na vyoo kuwa na
nyufa hali ambayo inatishia usalama wa maisha yao kutokana na mazingira
wanayosemea ni hatarishi na sio rafika kwao.
Hali
hiyo imebainika baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikio
kufanya ziara ya kushitukiza katika shule hiyo na kuweza kujionea
ubovu wa majengo hayo wanayoyatumia katika shule hiyo kuwa ni chakavu
kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa kipindi kirefu.
Mkuu
wa shule hiyo Pregua Mseja amekiri kuwepo kwa hali hiyo ambapo alisema
kwamba licha ya shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya ubovu wa
miundombini lakini bado inakabiliwa na uhaba wa madawati pamoja na
nyumba sita vya madarasa vina vuja maji kutokana na mapaa yake kutoboka
hivyo wanafunzi wananyeshewa na mvua.
“Kwa
sasa Mkuu wa Mkoa shule hii ina changamoto nyingi sana kwani licha ya
ubovy wa majengo pamoja na vyoo bado mambo ya msingi yanahitajika kwa
shule hii ili wanafunzi waweze kujisomea katika mazingira mazuri kwa
mfano sasa kuna madasara sita ambayo yanavuja kweli wanafunzi
wananyeshewa na mvua,” alisema Mseja.
Akizungumzia
kuhusiana na fedha ambazo tayari wameshakwisha zipokea katika shule
hiyo kutoka serikalini kwa ajili ya uendeshaji wa elimu bure alisema
kwamba wameshapokea kiasi cha shilingi laki 437 ambazo zitatumika
katika mahitaji mbali mbali ikiwemo suala la utawala michezo pamoja na
mahitaji mengine ya msingi.
Baada
ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kufanya ukaguzi katika maejengo ya utawala,
madarasa ya wanafunzi pamoja na kutembelea vyoo vinavyotumiwa na
wanafunzi hao alitoa agizo kwa halmashauri ya mji wa Kibaha kuhakikisha
wanatafuta fedha haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kukarabati
miundombinu hiyo ili kuwatendea haki ya msingi watoto hao.
Ndikiro
alisema kuwa majengo hayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati wa haraka na
kwamba halmashauri ya mji wa Kibaha ihakikishe inatafuta fedha ambazo
zitaweza kusaidia katika kukarabati miundombinu hiyo ya majengo ili
watoto waweze kujisomea katika mazingira mazuri.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibaha
Mauld Bundala aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa ambapo alisema
anaskitishwa sana na kuona wanafunzi wnasoma katika majengo amabyo yana
nyufa kwani kunaweza kupelekea watoto hao kuangukiwa na majengo.
Naye
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha Grory Diamunye ambao nao
walikuwepo katika ziara hiyo alisema atalivalia njuga suala hilo na
kuahidi kulishughulikia haraka sana ili wanafunzi hao waweze kusoma
katika mazingira ambayo ni rafiki kwao kwani kufanya hivyo kutaweza
kuwafanya waongeze hata kiwango cha ufaulu.
Shule
hiyo ina jumla ya wanafunzi 764 kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto
ya uhaba wa madawati, madarasa, matundu ya vyoo, uchakavu wa
miundombinu ya majengo ahali mbayo inwapa wakati mgumu wanafunzi hao
kusoma katika mazingira ambayo ni hatari kwa masiha yao.
Makamu wa Rais ahudhuria Hafla ya kuwapongeza Vijana wa kuhifadhi Qur’an
Dkt
Abdallah Ghaylaan Mwakilishi wa taasisi ya Kimataifa ya Kuhifadhi
Qur-an wa Saudia akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mh
Samia Suluhu Hassan Tunzo ya kutambua mchango wake katika Malezi wakati
wa Hafla ya kuwapongeza Vijana wa jumuia ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania
waliohitimu katika Vyuo Vikuu mbali mbali jana tarehe 28/01/2016
kwenye hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Cheti mwanafunzi Aziza Juma wakati wa hafla ya kuwapongeza
Vijana wa Jumuia ya kuhifadhi Qur an yalifonyika katika Hotel ya Hyatt
Regency, jijini Da es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Hamza Lusanga wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana
wa jumuia ya Kuhifadhi Qur –an yaliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt
Regency Jijini Dar es salaam jana tarehe 28/01/2016
Baadhi
ya Mabalozi nchini Tanzania wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Tanzania alipokuwa anahutubia kwenye Hafla ya kuwapongeza vijana wa
jumuia kuhifadhi Qur an jana tarehe 28/01/2016
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na mshereheshaji Sheikh Saleh wakati alipowasili kwenye
Hafla ya Kuwapongeza Vijana wajumuia ya kuhifadhi Qur an jana kwenye
Hotel ya Hyatt Regency
Msama aishukuru Basata
…………………………….
MWENYEKITI
wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama amelishukuru
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa mchango wake wa kufanikisha
maendeleo ya tamasa hilo na sanaa kwa ujumla.
“Tunaishukuru
Basata na tunazingatia maelekezo ya Serikali ambayo ndio muongozo wa
kufanikisha maendeleo ya sanaa na wasanii pia,” alisema Msama.
Msama
alisema yeye na kamati yake wanashukuru kwa kupata kibali kutoka Basata
na wanazingatia maelekezo ya baraza hilo kama ilivyo sheria na taratibu
zinazvyoeleza.
Msama
alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye
tamasha hilo lenye mlengo wa kusaidia jamii yenye uhitaji maalum kama
yatima, walemavu na wajane ambao wanahitaji msaada.
Aidha
Msama alisema mbali ya kuhusika na maendeleo ya jamii pia linafanikisha
kuibua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili ambao unafikisha ujumbe
was neno la Mungu kwa jamii.
“Tamasha
la Pasaka malengo yake ni kusaidia jamii yenye uhitaji maalum pia
linaibua vipaji vya waimbaji wa nyimbo za Injili ambavyo vinatakiwa
kutekelezwa kupitia tamasha letu,” alisema Msama.
Msama
alimalizia kwa kueleza kauli mbiu ya Tamasha la Tamasa la Pasaka mwaka
huu ni Umoja na Upendo, hudumisha amani katika taifa letu.
MGODI WA BULYANHULU WATOA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’WALE KAMA USHURU WA HUDUMA.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akiteta jambo na mkuu wa idara ya Mahusiano ya Jamii wa Mgodi huo Sara Terri wakati wa hafla ya kukabidhi hundi. |
Madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo. |
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyang’wale Venance Ngeleuya akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo. |
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza na baadhi ya viongozi na madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale (hawapo pichani)wakati wa kukabidhi hundi kwa halmashauri hiyo. |
MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAFUTA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI.
Mrimi Zabloni (Katikati) ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini akiongea na wanahabari
Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
…………………………………………………………………………………
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya
kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana,
katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na
aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Christopher Ryoba Kangoye.
Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche
(Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo
ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.
Baada ya Mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua
kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja
za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya
waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.
Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja
aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Nae Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara, ameelezea kuwa na imani na
Mahakama kutokana na maamuzi iliyoyatoa katika kesi hiyo pamoja na kesi
nyingine zilizowahi kuamuliwa Mahakamani hapo na kuongeza kuwa sasa kazi imebaki moja kwa Mhe.Heche ambayo ni kuwatumikia wakazi wa Jimbo la Tarime Vijijini.
Kwa upande wake Mrimi Zabloni ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, ameelezea furaha
kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwasihi kuweka imani na Mahakama hapa nchini
katika kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.
Wananchi wengi Mahakamani hapo kutoka Jimboni Tarime Vijijini walikuwa ni wafuasi wa Chadema
na wameonyesha kuyapokea maamuzi ya mahakama hiyo kwa furaha kubwa na kwamba wao waliamua ushindi wa Heche tangu Novemba 25 mwaka jana kwenye daftari la kupigia kura.
Kesi hiyo ilisikilizwa January 19,2016 mwaka huu na kuahirishwa hadi juzi January 27,2015 kwa ajili
ya kutolewa maamuzi, lakini pia iliahirishwa hadi jana January 28,2016 ambapo maamuzi
yameweza kutolewa.

MTEJA AILALAMIKIA TANESCO CHARAMBE KWA KUCHELEWA KUMUWEKEA UMEME
Mteja Ambwene Kyoga |
Dotto Mwaibale
……………………………..
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Charambe Temeke jijini Dar es Salaam limelalamikiwa na mteja wake mmoja kwa kushindwa kumfungia umeme kwa wakati licha ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo kuagiza wateja wapya kufungiwa umeme katika kipindi kifupi.
Malalamiko hayo yametolewa na mteja wa shirika hilo Ambwene Kyoga ambaye amelipa sh. 320,960 kwa ajili ya kuwekewa umeme na kupatiwa lisiti namba TDB 16841 kwa ajili ya nyumba yake iliyopo Mbagala Kuu Bucha.
Ambwene alisema sasa anaingia mwaka wa pili bado haja fungiwa umeme kwani mwaka jana mwanzoni alipeleka maombi yake ofisi za shirika hilo za Kurasini lakini alipofuatilia aliambiwa faili lake limepotea hivyo aende ofisi za Charambe ambapo alilipa fedha hizo Desemba 28 mwaka jana tangu hapo licha ya kupelekewa nyaya amekuwa akizungushwa kwa kuambiwa nguzo inayotakiwa achukulie umeme imeoza ingawa inaendelea kutumika.
“Watu wa dharura wamekwisha toa taarifa kuhusu nguzo hiyo lakini bado haijabadilishwa jambo linaloweza kuleta maafa iwapo ikianguka na kibaya zaidi wamekuwa na maneno mengi badala ya kazi sijui wanataka kujenga mazingira ya rushwa” alilalamika Kyoga.
Kyoga alisema waziri wao Mhongo anafanya kazi kwa kujituma na alimsikia katika vyombo vya habari akiagiza kuwa ndani ya wiki moja mwombaji wa umeme awe amefungiwa lakini anashangaa Tanesco Charambe jinsi wanavyofanya kazi kwa kusuasua.
Msemaji wa Tanesco ofisi za Charambe ambaye alifahamika kwa jina moja la Mugaya alipopigiwa simu jana ili kuzungumzia suala hilo simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila ya kupokewa hata hivyo gazeti ili linaendelea kumtafuta.

KAMANDA WA MATUKIO BLOG YAPONGEZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA COVERAGE NZURI YA UCHAGUZI MKUU 2015
Mpiga
Picha Mkuu wa gazeti hili, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa
Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa
Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu
cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha
matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha
wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya
vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.
Mwaikenda, alishiriki kikamilifu katika coverage ya kampeni za miezi miwili za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika mikoa mbalimbali nchini.Kazi zake zilikuwa zinatumika kwenye gazeti la Jambo Leo analofanyia kazi na kusambazwa pia kwenye blogu mbalimbali nchini.
Pia alikuwa miongoni mwa wapigapicha waliofanya coverage wakati wa kutangazwa kwa matokeo,mshindi wa urais na kuapishwa Rais Dk John Magufuli Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

(PICHA NA MARGARET CHAMBIRI-NEC)
Mwaikenda akifurahia kupata cheti hicho
ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Vijana
wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya
Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
Kituo
cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa
maji hivyo kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.
Dimbwi la maji likiwa mbele ya jengo la Yanga.
Daraja la Jangwani na Kituo cha mabasi ya mwendokasi kikiwa kizingirwa na maji.
Magari yakipita kwenye dimbwi la maji barabara ya mtaa wa Lindi Ilala.
Moja
ya vibanda wanavyoishi wananchi waliobomolewa eneo la Kinondoni
Mkwajuni maji yakipita katikati yake jambo ambalo ni hatari kwa watu
wanaoishi ndani humo.
Nyumba ikiwa imezingirwa na maji eneo la Mchikichini Ilala kufuatia mvua hiyo iliyonyesha leo
Vijana wakiuangalia Uwanja wa Klabu ya Yanga ulivyojaa maji.
MCHEKESHAJI KUTOKA KENYA, ERIC OMONDI AWASIJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
MWIGIZAJI
na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili mchana huu jijini
Dar leo akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa ‘LIVE SHOW’ kesho
katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es
Salaam.
Mchekeshaji
kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili
katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam leo.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya,
Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media leo alipo wasili
jijini Dar es Salaam kwaajili ya ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika kesho katika
hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka
nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo
Ndembeji (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha
GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiteta jambo na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji leo jijini Dar es Salaam.
Kikosi kazi cha Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji akiwakaribisha wanakikosi kazi wa Mchekeshaji
kutoka nchini Kenya, Eric Omondi leo mara baada ya kuwasili katika
ofisi za GSM Media zilizopo jengo la Alosco Tower Lumumba jijini Dar es
Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji na Mchekeshaji
kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha
mchekeshaji huyo ambapo ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika kesho jijini Dar es
Salaam.(Picha na michuziblog)
No comments :
Post a Comment