Mkurugenzi wa upelelezi Jeshi
la Polisi Kamishina Diwani Athumani akisisitiza jambo mbele ya waandishi
wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na
malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu
uchumi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Upelelezi Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) Bw. Alex Mufungo
akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa
kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti
wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar es salaam
pembeni yake ni Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP Biswalo Mganga.
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athuman
hayupo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya
Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi
uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha zote na Ally Daud -MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………
NA MAGRETH KINABO NA ALLY DAUD – MAELEZO
Serikali inaendelea kusimamia
urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango
wa kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na
kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu
ana makosa hayo.
Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi
wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo Mganga wakati wa mkutano wake na
waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam, ambapo alisema kuwa hatua hizo
zimechukuliwa mara baada ya upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi
kukamilika na kumbaini mhusika.
Aidha Mganga
aliongeza kwamba mhusika hushtakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana
na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo watumishi wa
umma.
“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa
nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya
kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya
kulipa faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika
na makosa hayo” alisema Mganga.
Alisema kufuatia mkakati huo,
Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa
kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini
(20) ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze
kuziwa au kutaifishwa.
Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu.
Mkoani Kilimanjaro kesi
mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani
kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye uzito wa
kilogram tatu zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo
cha maisha.
Kesi nyingine ni namba 46 ya
mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu,
mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na
dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gram 3191.11 na thamani ya
Sh. Milioni 143, watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa
huru.
Mganga alizitaja baadhi ya kesi
nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa
mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China
waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni
Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa
kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila
mmoja.
Kesi nyingine ya uhujumu
uchumi namba 3 ya mwaka 2016 iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid
Ngaza aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo nane
iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, wilaya ya
Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30 na kullipa faini
ya Sh. bilioni 1.2.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi
Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi
kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf ,
Hiace pamoja na nyumba kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya
kuhujumu uchumi.
Aidha, Mganga alitoa rai kwa
wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi
ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe
kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine
aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo
ni kosa kisheria.
“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshirikikuficha mali ya mtu
mwingine inayohusiana na uhalifukwa njia yoyote ile pia anaweza
kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema kuwa
atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na
mali zake kutaifishwa.
“Mhalifu akibainika na mshataka
ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na
kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha
taslimu” alisema Kamishna Athumani.
Aidha, Kamishna Athumani
aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina
ya wake zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya
watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia
za uhalifu.
“Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza Kamishina Athuman.
Mbali na hayo, Mkurugenzi wa
upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex
Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali
zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.
Tangu mwaka 1990, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali
zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kama kipaumbele katika mfumo wa haki
jinai wa kupigana na uhalifu. Haisadii sana katika jitihada za
kupambana na uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini
au kwenda jela ikiwa ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au
mali iliyopatikana kwa uhalifu huo.
Zaidi, fedha zilizoibwa na
wanasiasa wala rushwa pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa
na kuelekezwa katika maeneo muhimu yenye mahitaji.
Sheria ya Utaifishaji wa Mali
Haramu ilipitishwa na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa
Kimataifa pamoja na mikataba ya Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi
yetu.
VIJANA HAWA WATOKA NA WIMBO “SIKUACHI”
This is Brand new Audio from Tanzanian Artist Called WALEO, Song Called “SIKUACHI” Produced by Fraga Studio:: Uprise Music.Enjoy the Good Music
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUZUNGUMZA NA WABUNGE NJE YA UKUMBI WA BUNGE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Januari 28,
2016. Kutoka kushoto ni Jumanne Kishimba wa Kahama, Edwin Ngonyani wa
Namtumbo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,
Hussein Amar wa Nyangwhale, Prosper Mbene wa Morogoro Kusini na Joseph
Kalanda wa Sikonge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Matukio Bungeni katika picha bungeni Dodoma leo
Waziri Mkuu Mhe.Kassim
Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi
cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia
Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama
kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua
zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa
kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka
ajali hiyo.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim
Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu
maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli
za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia
shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais
picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Elimu ya sheria Dar kuanza Januari 31
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa
kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika
viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi
kupata elimu hiyo.
‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria
maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa
shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau
watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law
School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria
Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru
pamoja na Polisi.
Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao
watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo wananchi wenye mashauri
ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa
utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji,
Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka
katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam
inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.
Serikali kuendelea kujenga barabara zaidi kwa kiwango cha lami
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge
katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma. picha na Raymond
Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha
lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng Godwin Ngonyani
akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali
kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya
ubovu wa barabara nchini.
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa
Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi
wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango
cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika mwaka wa fedha 2014/15
na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili
ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa
kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na
baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za mradi huo, Serikali
itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele
Mwakibete Mbunge wa Busokelo (CCM) aliyehitaji kujua ni lini barabara
ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia
Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi
Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani
amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa
kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10
Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha
lami na ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae
Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa
Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi
Buseji,Wilayani Busokelo.
Serikali kupiti Wakala wa Barabara
(TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika
Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini ili kukabiliana na adha ya
ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya
maeneo.
SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI
Spika
wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini
Yasemin Eralp aliyemtembelea ofisini kwake leo tarehe 28 Januari, 2016,
Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai
akisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin
Eralp aliyemtembelea ofisini kwake. Katikati ni Katibu wa Balozi huyo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai
akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp aliyemtembelea
ofisini kwake Mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Bunge)
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA – KOGA – TABORA
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma
kuwa, Barabara ya Mpanda – Koga – Tabora imefungwa kwa muda kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga
na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na
Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa
hiyo
Kutokana na kukatika kwa
mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha
safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza
kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya
maji kupungua katika eneo hilo.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha
Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za
Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.
Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016
KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA
Mkuu
wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akisisitiza
jambo wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP) lililofanyika katika ukumbi wa NACTE,
jijini Dar es Salaam.
(Picha na Philemon Solomon wa Fullshwangweblog)
……………………………………………………………
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kongamano
lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika jana jijini Dar es Salaam
baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa
Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 –
2021.
Akizungumza
na Mo Dewji Blog, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu,
Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha
vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora
na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema
kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini
kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni
kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi
mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na
kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo
waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha
yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili
tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni
walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate
maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende
shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,”
alisema Tandari.
Aidha
Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya
aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza
kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari
kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza
kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa
utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt.
John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa
shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi
wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akiwaelezea
washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP) ambao utafanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka
mitano kuanzia mwaka 2017 – 2021.
Naye
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na
makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya
Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya
awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa
wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo
utakavyofanyika.
Awali
Zulmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo
linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na
wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi
wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora
katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.
Mkuu
wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akielezea jambo katika kongamano la kujadili vipaumbele vya
Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
Mmoja
wa washiriki wa kongamano hilo akizugumza kuhusu Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP), Katikati ni Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera
na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari.
Mmoja
wa wanakikundi akiwaelezea wanakikundi wenzake kuhusu kipaumbele
ambacho walikuwa wamechaguliwa kukijadili na baadae kuwasilisha mbele ya
washiriki wote jinsi kipaumbele hicho kitakavyotumika pamoja na faida
zake.
Mkuu
wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
kutoka Ufaransa, Anton De Grauwe akimuelekeza jambo mwana kikundi
mwenzake wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vitakavyotumika
katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
Baadhi
ya wanakikundi wakiwa makini kufuatilia kila jambo ambalo linaendelea
katika kongamano hilo la siku mbili ili kupata vipaumbele ambavyo
vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
No comments :
Post a Comment