Katika
mipango ya kukuza uchumi, sekta ya utalii chini ya Prof Jumanne
Maghembe ambaye ni Waziri mpya wa maliasili na utalii imeamua kuanza
kuweka mikakati katika kuongeza bajeti ya kutosha kwa mwaka 2016, ili
kuongeza bidhaa na huduma zenye ubora kwa lengo la kuvutia watalii wengi
zaidi nchini.
Sekta
ya utalii imekuwa na mpango wa kuongeza watalii wa kigeni zaidi ya
Million 3 mpaka kufikia 2018, ambapo mkakati huu utaenda sambambana na
ongezeko la pato la taifa kuongezeka mara mbili ya kinachopatikana kwa
sasa.
kwa upande wake mdau wa masuala ya Utalii, Bw. Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania
alifafanua kuwa sekta ya utalii imekuwa mstari wa mbele katika kukuza
uchumi baada ya kilimo, hivyo kama suala hili litatiliwa mkazo basi
tunasubiria Tanzania mpya katika uchumi.
Aliendelea
kwa kufafanua kuwa, “Sekta hii inabidi ikabiliane na matatizo
yanayoikabili katika ukusajji wa kodi, kwa namna moja au nyingine
inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kama hatuta chukua hatua
yeyote”.
“Hata
hivyo,inabidi tuangalie maboresho katika nyanja tofauti tofauti, bado
kuna wahudumu wasio na ujuzi wa kutosha, ukilinganisha na huduma ukiwa
nje ya nchi na hapa ni tofauti, hivyo tujaribu kuweka mafunzo ya ziada
kwa waajiriwa na waajiri ili kuongeza ufanisi katika kazi”.
MAJALIWA ATAKA WATANZANIA WAFUNGUE SPORTS ACADEMY
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wafungue shule za michezo yaani Sports Academy ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo.
Ametoa wito huo jana mchana
(Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza
na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya
mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika mjini Dodoma.
Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.
“Michezo ni sayansi kwa hiyo
tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya michezo na kuwapa mbinu
tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema wapo Watanzania wachache
ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na kuwataja Filbert Bayi
(shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu (shule ya Lord
Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.
Alisema michezo ina nafasi kubwa
ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo maana Serikali imeamua
kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na habari.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye ameamua kutembea kwa
miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Dk. John
Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.
Kijana Joseph (19) ambaye
alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku 13 tangu aanze safari
hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku. “Ninatembea kwa saa 12 kwa
siku na ikifika jioni natafuta mahali penye mji na kupumzika,” alisema.
Joseph ambaye amehitimu kidato
cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya Mtoni iliyoko
Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya mitihani yake
lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo akaamua
kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.
Alipoulizwa anafanyaje anapopita
kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya kutisha, Joseph alisema
hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha isipokuwa kwenye milima ya
Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa Dodoma.
Joseph amesema anatarajia kuanza
safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa (Jumanne, Februari 2, 2016)
kwani anasubiri kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.
MAJALIWA ATAKA WATANZANIA WAFUNGUE SPORTS ACADEMY
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wafungue shule za michezo yaani Sports Academy ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo.
Ametoa
wito huo jana mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa
Jamhuri wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali
walioshiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5)
zilizofanyika mjini Dodoma. Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI
TU HALF MARATHON”.
“Michezo
ni sayansi kwa hiyo tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya
michezo na kuwapa mbinu tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali
ya kitaifa na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema
wapo Watanzania wachache ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na
kuwataja Filbert Bayi (shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi
Kipingu (shule ya Lord Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.
Alisema
michezo ina nafasi kubwa ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo
maana Serikali imeamua kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na
habari.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye
ameamua kutembea kwa miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga
mkono Rais Dk. John Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.
Kijana
Joseph (19) ambaye alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku
13 tangu aanze safari hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku.
“Ninatembea kwa saa 12 kwa siku na ikifika jioni natafuta mahali penye
mji na kupumzika,” alisema.
Joseph
ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya
Mtoni iliyoko Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya
mitihani yake lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo
akaamua kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.
Alipoulizwa
anafanyaje anapopita kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya
kutisha, Joseph alisema hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha
isipokuwa kwenye milima ya Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa
Dodoma.
Joseph
amesema anatarajia kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa
(Jumanne, Februari 2, 2016) kwani anasubiri kukutana na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.
IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.
WAZIRI MBARAWA ATAKA MAKANDARASI KUTOA MIKATABA YA AJIRA
Mkandarasi wa SynoHydo
Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya
Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa
barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International
Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi
wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa
mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International
Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi
wanaojenga barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya
Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na
kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi
wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni
Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya
Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia)
ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza
kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa
barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki,
usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa
nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.
Amesema hayo wilayani Chemba
Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao
ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km.
43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha
kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa
mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za
Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu
zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja
makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye
urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa
mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa
madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni
sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia
Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu
cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu
ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya
kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit
Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu,
amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo
ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na
kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea
kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na
hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa
wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia
umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini
kudumu kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane
na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya
Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80
wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika
kwa asilimia 52.2 na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8),
umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote
Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.
WAZIRI MBARAWA ATAKA MAKANDARASI KUTOA MIKATABA YA AJIRA
Mkandarasi
wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa
kiwango cha lami.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza
Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan
International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba
bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kwa
Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan
International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya
kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati)
akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani
Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa
mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8)
Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu
akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa
katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha
lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey
Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS
makao makuu.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.
……………………………………………………………….
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza
Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa
wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama
ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za
ujenzi kukamilika kwa wakati.
Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2 na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2 na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi. |
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu Majaliwa. |
Waziri Mkuu akislimiana na Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya . |
Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara ya kushtukiza. |
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali ya rufaa ya Mawenzi. |
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo wagonjwa wanahudumiwa. |
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa mwako. |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa. |
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi. |
Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini. |
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPILI YA MAWENZI
Akuta uhaba wa dawa, x-ray mbovu, theatre haifanyi kazi ipasavyo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye
hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara
baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini jana jioni (Jumamosi,
Januari 30, 2016) alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza
Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na
kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa
iwasilishwe.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua
kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali
yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,”
alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla.
Mara baada ya kuwasili
hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji
(theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali
hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula.
Katika chumba cha upasuaji
ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu vya kufanyia upasuaji lakini
kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza
wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la
upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete.
Akiwa katika wodi ya utabibu ya
wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya
kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi.
Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD
lakini bado hazijafika.
Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye
wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa,
mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto
wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure,
lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa.
Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu
wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa
baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD
tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa
walizoomba.
“RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza
dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara
ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa
dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya hivyo
ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji
Waziri Mkuu.
“Hii hospitali ni kubwa kuliko
idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao
wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za
kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina
maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini
ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji.
Wakati akitoka wodi ya watoto,
kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye
anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba
dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu.
“Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine Kahitwa
apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine za xray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo
baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali
haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya
vipimo.
Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.”
Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla
ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja
alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS
fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena
ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende
kupata vipimo mtaani,” alisema.
LEO NI HEPI BESDEI YA BLOG YA VIJIMAMBO YATIMIZA MIAKA 6
Vijimambo
ilizaliwa Januari 31, 2010 na kuzinduliwa Oktoba 23, 2010 na aliyekua
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar. Picha ni siku
ya uzinduzi ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
Hapa
Balozi Mwanaidi Maajar akiwa mgeni rasmi miaka 2 ya Vijimambo
iliyofanyika Machi 31, 2012 ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville,
Maryalnd.
Rais
mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya
miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyia Julai 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton
Inn uliopo Capitol Heights. Maryland.
Mwenyekiti wa Vijimambo akiwapokea wasanii Shilole na Masanja waliokuja kunogesha sherehe ya miaka 3 ya vijimambo.
Mhe.
Nyarandu (kulia) akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 4 ya
Vijimambo iliyofanyika Septemba 13, 2016 Hotel ya Growne Plaza iliyopo
Rockville, Maryland.
Wasanii
Aunty Ezekiel na Cassim Mganga wakija kunogesha miaka 4 ya Vijimambo,
kushoto ni NY Ebra akipata ukodak moment na wasanii hao walipotembelea
New York City.
Cassim
Mganga na Aunty Ezekiel wakitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa
kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York siku walipotembelea pande
za New York City, kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa
Mhe. Tuvako Maniongi
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ASIFU MIRADI YA UFUGAJI GEREZA LA UZALISHAJI MIFUGO MTEGO WA SIMBA, KINGOLWIRA MKOANI MOROGORO
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la
Magereza katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba,
Constatus Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza
hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji
zinazofanywa gerezani hapo mkoani Morogoro.
Kundi la ng’ombe wa maziwa
wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba,
Kingolwira mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika
picha.
Mtaalamu wa mifugo katika mradi
wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la Wanawake
Tanzania, lililopo Kingolwira mkoani Morogoro, Sajenti Sarah Kabunda
(wapili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza
hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji
zinazofanywa gerezani hapo.
Simba yaitandika timu ya African Sports ya Tanga uwanja wa Taifa
(Kwa hisani ya Saleh Jembe Blog)MPIRA UMEKWISHAAA
Dk 90+2, Simba sasa wanatoa shoo tu, ni pasi fupifupi
DAKIKA 3 ZA NYONGEZADk 89, Mgosi anafunga bao zuri kabisa, lakini mwamuzi anasema aliotea. Inaonekana mwamuzi wa akiba hakuwa makini
DK 87, Mgosi aliyeingia punde, anakanyagwa na beki Gereza wa African Sports, lakini mwamuzi anashindwa kutoa adhabu katika tukio hilo
Dk 84, Majegwa na Kessy wanagongeana vizuri lakini shuti la ajib linapanguliwa na kipa wa Sports
KADI Dk 80 Ally Ramadhani wa Sports analambwa kadi ya njano kutokana kucheza kindava
SUB Dk 77 Simba inamtoa Ugando na nafasi yake anachukua Said Ndemla
GOOOOOO Dk 75 Ugando anaifungia Simba bao safi kabisa baada ya Simba kufanya shambulizi la kushitukiza
Dk 73, Ally Ramadhani anapiga shuti, mpira taratibu unagonga mwamba lakini unaokolewa
Dk 70, Uganda anajaribu kuwatoka mabeki wawili wa Sports lakini mpira unashindwa kufika alivyotarajia
Dk 63, Simba wanafanya shambulizi tena lakini Sports wanakuwa makini na kuokoa
Dk 57, krosi nzuri ya Ramadhani inaokolewa na Isihaka na Simba wanaondosha hatari.
Dk 56, Bado Simba wanaonekana kuwa vizuri zaidi wakitawala mchezo katika kiungo
Dk 51, Ajibu anamlamba chenga beki mmoja ana kuachia shuti kali, kipa Zacharia Maarufu anadaka, anautema lakini anauwahi
Dk 46, Simba wanaanza kwa kasi utafikiri wanatakiwa kusawazisha lakini Sports wanaonekana pia bado wako vizuri
MAPUMZIKO
Inaonekana Simba wametawala mpira kwa 58% dhidi ya 42% ya Sports. Hivyo ni kipindi bora zaidi kwa upande wa Simba
Dk 44 hadi 45, Simba ndiyo wanaonekana kumiliki mpira zaidi na presha kubwa kwa African Sports
GOOOOOO Dk 43, Kiiza anawachambua mabeki wa African Sports na kufunga bao safi kabisa
Dk 35 hadi 40, Simba wanendelea kumiliki mpira kwa kupiga pasi fupifupi
Dk 34, Ajib anawatoka mabeki wa Sports lakini anachelewa na mpira wake unaishia mikononi mwa kipa wa Sports
GOOOOOOO Dk 31, Kessy anafanya kazi nzuri na kufunga bao zuri kabisa la pili kwa mchezo wa leo
Dk 28 hadi 30, Simba wanaendelea kuumiliki mpira kwa pasi fupifupi huku wakipiga krosi ndefu na fupi na African Sports wanaendelea kucheza pasi ndefu
Dk 27, Simba wanagongena vizuri, Ajib anatoa pasi nzuri ya Kisigino kwa Kiiza, lakini shuti lake linapita nje ya lango
Dk 24, Kessy anawachambua walinzi wawili wa African Sports, hata hivyo mwamuzi anasema Kiiza alikuwa ameishaotea
Dk 16 hadi 19, Simba wanaonekana kuongeza mashambulizi na kuwapa presha kubwa Sports huku Kazimoto anaonekana kuwa mwiba zaidi kwa viungo wa Sports
GOOOO Dk 14, krosi nzuri kabisa ya Kessy inatua kwa Kiiza anamalizia vizuri na kuandika bao kwa Simba
Dk Dk 5 hadi 8, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna timu iliyofanya shambulizi kali
Dk 2 hadi 4, Simba wanaendelea kutawala katika, KAzimoto, Mkude wakiendelea kugongeana vizuri na kuwapa wapinzani wao wakati mgumu
Dk 1, mpira unaanza taratibu, Simba wanaonekana kupiga pasi nyingi katikati, lakini African Sports pia wanaonyesha utulivu
No comments :
Post a Comment