Mkurugenzi
Mtendaji Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Bw.Charles Senkondo
akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawapo katika picha) baada ya
kumalizika kwa Mkutano na Sekretarieti za Mkoa kwa njia ya Video jana
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw.Peter Mushi (wa
pili kushoto) akizungumza alipokuwa akiendesha mkutano kwa njia ya
video na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara jana jijini Dar es Salaam (watatu
kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
Umma Bw. Leonard Mchau .
Baadhi
ya watendaji kutoka wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
wakiendelea na Mkutano kwa njia ya Video na Sektertarieti za Mikoa ya
Lindi,Mara,Geita,Singida na Shinyanga jana jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo
Watanzania wametakiwa kutumia
technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano kwa njia ya video
ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo kuokoa fedha na muda.
Rai hiyo imetolea hivi karibuni
na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles Senkondo wakati akiongea na
waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kazi wa video conference kati
ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake,
Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa.
Senkondo alisema kufanya mikutano
kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na hivyo kuepukana na ajali,
kutopoteza muda awapo safarini na na kupata wasaa wa kukaa na familia
yake.
“Kuanzishwa kwa TaGLA kumeongeza
uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia ya kisasa, kwa maamuzi
zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara mahitaji ya wadau na
kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma bora”.
“Kabla ya kukuwa kwa teknolojia
watu walikuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda kushiriki mikutano hivi
sasa wamepunguza safari zisizo na umuhimu. Mtu atasafiri katika
mikutano ya umuhimu tu zamani ilikuwa lazima mtu aje sasa hivi anafuatwa
popote alipo na kuletwa katika video conference”, alisema Senkoro.
SERIKALI KUTUMIA TSH. BILIONI 5 KUHUDUMIA KAMBI ZA MADAKTARI BINGWA WA MOYO
Dar es salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka
2015/16 kwa ajili ya kuhudumia kambi za Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya
Moyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya magonjwa hayo
kwa Watanzania.
Lengo la mkakati huo ni
kuhakikisha Wagonjwa wengi wanahudumiwa katika kipindi kifupi pamoja na
kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, ambao wengi wao
husafiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo, figo na saratani.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando wakati wa ziara yake ya kutembelea
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Dkt. Mbando alisema katika wiki
ya kwanza iliyoanza wiki hii Madaktari hao wanatarajia kutoa huduma kwa
wagonjwa 20 na kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Milioni 500
ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa hao nje ya nchi kwa ajili ya
matibabu.
“Tumeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni
1 zilizopaswa kutumika kuwapeleka nje ya nchi wagonjwa hawa,
tutahakikisha kuwa Wataalamu hawa wanafanya kazi kwa pamoja na Madaktari
wetu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutibu magonjwa haya” alisema
Dkt. Mmando.
Alisema Serikali pia ipo katika
mchakato wa kuzijengea uwezo hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi
ya Kansa ya Ocean Road na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa
kuziwezesha hospitali hizo kuwa na Wataalamu na majengo ya kisasa kwa
ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa Watanzania.
Aidha alisema Serikali imepanga
kufanya mazungumzo na taasisi za kiraia na nyingine ikiwemo taasisi ya
Rotary Club zilizokuwa zikisafarisha watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa
moyo, kuwekeza nguvu nchini kwani Tanzania kwa sasa ina wataalamu wa
kutosha kwa ajili ya kuwatibu wagonja hao.
Kwa mujibu wa Mmbando alisema
magonjwa ya moyo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, hivyo
aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara
na kuacha kunywa pombe na uvutaji wa sigara na kutazama desturi za
ulaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi alisema katika kipindi
cha wiki mbili ambazo madaktari hao watakuwepo hapa nchini wanaweza
kuhudumia jumla ya wagonjwa 55, na hivyo kuifanya Serikali kuokoa kiasi
cha Tsh. Bilioni 1.2
THE 10th SADC DIGITAL BROADCASTING MIGRATION FORUM HELD IN TANZANIA.
By. Aron Msigwa, Dar es salaam.
The 10th SADC digital broadcasting migration forum is taking place in Dar es salaam, Tanzania from 2nd to 3rd december 2015
. the main theme is digital broadcasting dynamics: building a sustainable future.
Participants of the forum comes
from sadc countries including Zimbabwe, Tanzania (Host Country)
Seychelles, Malawi, South Africa, Swaziland, Namibia,Lesotho and Zambia.
Speaking at the opening ceremony
of the forum the permanent secretary from the Ministry of Communication,
Cience and Technology from Tanzania Mr. Yamungu Kayandabila said the
SADC digital broadcasting terrestrial television forum is being held at a
time Tanzania has completed migrating from analogue to digital
broadcasting on the day of 30th April, 2015.
Mr. Kayandabila said the
Government of Tanzania has invested heavily on communications
infrastructure deploying the national ict broadband backbone (nictbb)
which runs over 7,500 kilometers in all regional headquarters expect to
bring major leap in the development of ICT in Tanzania.
Issues to be discussed by the
forum member during the two day forum include digital broadcasting
dynamics, building a sustainable future, post digital migration
challenges: Regulatory framework for terrestrial, Satellite,Cable and
online delivery also discussion on digital migration as a platform to
improve consumer choice.
MKUTANO WA WAHARIRI KUHUSU MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE
Mratibu
wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa
Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi
kupambana na magonjwa hayo, ambayo baadhia yake ni Matende, Mabusha,
Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa
vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii leo jijini Dares Salaam.
Mratibu
wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa
Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi
kupambana na magonjwa hayo, ambayo baadhia yake ni Matende, Mabusha,
Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa
vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii leo jijini Dares Salaam.
(Picha na Magreth Kinabo- MAELEZO)
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yapongezwa kwa ushikiano inaotoa kwa wadau wa Vijana
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas
(VSO)Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bibi.
Esther Liwa,Mkurugenzi wa Kanda wa VSO Bibi. Niki Kandirikirika, Afisa
Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service
Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin, Mkurugenzi wa Voluntary Service
Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter na Meneja Mradi wa ICS kutoka VSO
Bibi. Imisa Masinjila
Picha na Frank Shija, WHVUM
Picha na Frank Shija, WHVUM
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika
lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip
Goodwin alipo mtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kufanikisha
majukumu yao.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa shiriki lisilo la Kiserikali la Volountary Service
Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin akifafanua jambo wakati wa kikao baina
ya wajumbe kutoka shirika hilo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) jana
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na
ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO) jana jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la
Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin na
kulia ni Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van
Wetter.
POP UP BONGO ILIVYOFANA, TRINITI BAR OYSTERBAY CHINI YA UDHAMINI WA SMIRNOFF
Co-
founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake
la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake
la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Andrew Mahiga na rafiki ake walikuwapo
Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali mahiri mjini, Aika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden alikuwapo pia
Mbunifu
wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati)
akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika
juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Meneja
chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Wauzaji
wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda
lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster
bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
Tanya akiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Pop Up shop
Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali
zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi
karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi
karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Mratibu wa onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha
Stambuli alisema kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo
viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza wigo wao kibiashara
kwa kukutana na wanunuzi.
kwa kukutana na wanunuzi.
“Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi hao
kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na
wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa
kibiashara” alisema Natasha.
kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na
wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa
kibiashara” alisema Natasha.
Pia ametoa wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho
mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za
bidhaa ziuzwazo nchini.
Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha wa kufahamu
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni
wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni
wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo
hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini
kuongeza pia wigo wa biashara zao.
inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo
hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini
kuongeza pia wigo wa biashara zao.
Kwa upande wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika
kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.
Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika
kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.
“SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up
Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku
wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao katika
Pop Up Bongo” alisema Shomari.
Mhe. Balozi Sefue aendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa
Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi
wa Umma kuivaa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Balozi Sefue
alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana
na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO)
dhidi ya Standard Bank.
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi
Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji
zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi.
Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito
huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni
kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana
tofauti na siku zingine.
Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi
na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na
kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina
yao.
“Nimeamua kuonyesha mfano kwa
vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji
inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina
langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi
nimeshalivaa”.
“Mtumishi wa umma anapomuhudumia
mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya
kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji
inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote
wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe.
Balozi Sefue.
Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano
na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya
Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard
Bank.
MAJALIWA AAGANA NA BALOZI WA DRC
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo nchini, Mhe. Juma – Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini
kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye
alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015
kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, Mhe. Juma- Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
Akizungumza na balozi Mpango leo
(Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es
Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba
aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea
nyumbani.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea
heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya
uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
Kwa upande wake, Balozi Mpango
ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu
kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa viongozi wa Tanzania kubwa
vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona utawala wa Rais Benjamin
Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa
na hatua mnazochukua hivi sasa katika kupambana na rushwa na ufisadi,”
alisema.
“Mambo niliyojifunza tangu nimekaa
hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona kabisa kwamba mtu anaamini
kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa mtumishi wa umma. Anachotakiwa
kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia wananchi,” alisema kwa Kiswahili
sanifu.
Balozi Mpango aliomba mahusiano ya
nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya
bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za
nje.
“Bandari ya Dar es Salaam ni
muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000,
mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani
tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.
Katibu
Mkuu wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Juma Malik Akili akitoa
maelezo kwa waandishi wa Habari wa ZBC kuhusiana na Ujenzi wa Bandari ya
Maruhubi ambayo inatarajiwa kujengwa kuanzia Januari mwakani mjini
Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdallamwinyi Khamis baada ya kuwasili katika eneo la maruhubi
ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari kuanzia Januari mwakani mjini
Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kushoto akipata maelezo ya
ramani ya ujenzi kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk
Hamadi Mbarouk katika ziara ya kutembelea eneo ambalo linatarajiwa
kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Badari Maruhubi mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo kutoka kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya miundo mbinu na Mawasiliano Juma Malik Akili
wakati alipofanya ziara kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa
Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.
PICHANA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
MAJINA SAHIHI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.
Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa
huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu
akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la
ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.
Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015 na
kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo
hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino,
Dodoma.
TANAPA yaimarisha ulinzi wa tembo kwa kuwafunga vifaa maalum
Wataalam
wa Uhifadhi wakiongozwa na Dk. Alfred Kikoti (wa kwanza kulia)
wakiendelea na zoezi la uwekaji kola maalum kwa tembo zinazosaidia
kudhibiti mienendo ya tembo ndani nan je ya hifadhi ya Mfumo wa Ikolojia
wa Ruaha Rungwa.
Zoezi la uvalishaji wa kola maalum kwa tembo katika hifadhi ya Ruaha likiendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (mwenye kofia) akishuhudia zoezi
la uvalishaji kola maalum kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Daktari
wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI)
akijiandaa kumdunga sindano ya kumzindua tembo baada ya kukamilika kwa
zoezi la kumvalisha kola maalum
Picha
ya pamoja ya wahifadhi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa program maalum
ya uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kulia) akiongea na Mwenyekiti
wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa wakati wa zoezi la
uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
…………………………………………………………………………………..
Na Jovina Bujulu-MAELEZO)
Utalii ni miongoni mwa sekta muhimu zinazoliingizia Taifa pato hasa fedha za kigeni zinazotolewa na watalii wanaofika nchini kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kuangalia wanyama na vivutio vilivyopo katika hifadhi za taifa.
Sekta hii ya utalii inakumbana na tatizo kubwa la ujangili ambalo linaripotiwa kuiingizia taifa hasara kubwa kutokana na idadi kubwa ya wanyama pori hasa tembo kuuawa kila mwaka.
Hivi karibuni Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) limezindua programu maalam ya kuwavalisha tembo kifaa maalumu kijulikanacho kama “kola” au king’amuzi maalum shingoni mwa tembo hao kinachong’amua na kurekodi mienendo yao kwa kutumia mawasiliano ya satelaiti.
Program hiyo inatekelezwa katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwa ambapo tembo 30 wanaoongoza makundi 30 wamevalishwa kola hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Bwana Allan Kijazi alisema kuwa inalenga kuimarisha ulinzi wa tembo nchini. “Lengo kuu la program hii ni kupata taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwe zitakazosaidia kubainisha maeneo shorobo (njia za wanyama) na mitawanyiko yao kwa ajili ya ulinzi wa tembo” alisema Bwana Kijazi.
Aliendelea kusema kuwa teknolojia hiyo inawawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua walipo, wanapopita, kasi yao, sehemu wanazojificha, wanapokunywa maji, ikiwa wamejeruhiwa, wanapopumzika, maeneo wanayokaa muda mrefu, kama wamekufa, kama wamehama hifadhi moja hadi nyingine na taarifa nyingine nyingi, hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori kufuatilia usalama wa tembo hao.
Akizungumzia uanzishwaji wa program hiyo, Bwana Kijazi alisema kuwa inafadhiliwa na taasisi ya Global Government Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP); ambapo UNDP kwa kushirikiana na TANAPA na SPANET wametoa kandarasi ya kufanya kazi hiyo ya kufunga “kola” kwenye tembo kwa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo “WORLD ELEPHANT CENTRE “ kilichopo mkoani Arusha.
Utalii ni miongoni mwa sekta muhimu zinazoliingizia Taifa pato hasa fedha za kigeni zinazotolewa na watalii wanaofika nchini kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kuangalia wanyama na vivutio vilivyopo katika hifadhi za taifa.
Sekta hii ya utalii inakumbana na tatizo kubwa la ujangili ambalo linaripotiwa kuiingizia taifa hasara kubwa kutokana na idadi kubwa ya wanyama pori hasa tembo kuuawa kila mwaka.
Hivi karibuni Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) limezindua programu maalam ya kuwavalisha tembo kifaa maalumu kijulikanacho kama “kola” au king’amuzi maalum shingoni mwa tembo hao kinachong’amua na kurekodi mienendo yao kwa kutumia mawasiliano ya satelaiti.
Program hiyo inatekelezwa katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwa ambapo tembo 30 wanaoongoza makundi 30 wamevalishwa kola hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Bwana Allan Kijazi alisema kuwa inalenga kuimarisha ulinzi wa tembo nchini. “Lengo kuu la program hii ni kupata taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwe zitakazosaidia kubainisha maeneo shorobo (njia za wanyama) na mitawanyiko yao kwa ajili ya ulinzi wa tembo” alisema Bwana Kijazi.
Aliendelea kusema kuwa teknolojia hiyo inawawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua walipo, wanapopita, kasi yao, sehemu wanazojificha, wanapokunywa maji, ikiwa wamejeruhiwa, wanapopumzika, maeneo wanayokaa muda mrefu, kama wamekufa, kama wamehama hifadhi moja hadi nyingine na taarifa nyingine nyingi, hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori kufuatilia usalama wa tembo hao.
Akizungumzia uanzishwaji wa program hiyo, Bwana Kijazi alisema kuwa inafadhiliwa na taasisi ya Global Government Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP); ambapo UNDP kwa kushirikiana na TANAPA na SPANET wametoa kandarasi ya kufanya kazi hiyo ya kufunga “kola” kwenye tembo kwa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo “WORLD ELEPHANT CENTRE “ kilichopo mkoani Arusha.
Twanga Pepeta kuwapagawisha uzinduzi wa Kibaha Carnival ijumaa
Mwimbaji
Ally Choki kushoto akiwa na Luiza Mbutu katika moja ya shoo zao, bendi
hiyo inatarajiwa kufanya nyoo kabambe katia uzinduzi wa eneo jipya la
burudani la Kibaha Carnival siku ya ijumaa desemba 4 mwaka huu.
……………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
BENDI kongwe ya muziki wa dansi
hapa nchini Twanga Pepeta ‘wazee wa visigino’wanatarajia kutoa burudani
ya aina yake katika uzinduzi rasmi wa eneo jipya linalojulikana kwa
jina la ‘Kibaha Carnival’ siku ya ijumaa Desemba 4 mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi i wa
habari hizi Katibu wa kamati ya maandalizi kwa ajili ya siku hiyo
shauri Yomba Yomba alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya aonyesho hilo
ya aina yake ambalo litakwenda sambamba na huo yamekamilika.
Yomba yomba alisema kwamba
katika uzinduzi huo utakuwa wa aina yake kutokana na maandalizi mazuri
ambayo tayari yamekamilika na baadhi ya vitu vichache vinaendelea
kufanyiwa kazi ili siku hiyo iwe ya kiutofauti zaidi.
“Hapa kikubwa ndugu mwandishi
siku ya ijumaa desemba 4 nadhani itakuwa ni siku ya kipekee zaidi kwani
ndio ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na
mashabiki wa burudani pamoja na kujionea eneo jipya la kisasa la Kibaha
Carnival likizinduliwa rasmi hivyo mambo yanakwenda vizuri mpaka
sasa,”alisema Yomba Yomba.
Pia alibainisha kwamba siku hiyo
ya uzinduzi mbali na bendi ya Twanga pepeta kutakuwepo na burudani
nyingine ambazo zitakuwepo na lengo kuu ni kuhakikisha akila mdau wa
burudani ambaye atafika siku hiyo anapata vionjo vya kila aina ikiwemo
wasanii mbali mbali wa kizazi kipya ambao maskani yao ni Mkoa wa Pwani
na wengine waalikwa kutoka Dar es Salaam.
Kadhalika alisema kwamba
kuanzishwa kwa eneo hilo la Kibaha Carnival ni kutokana na wadau wengi
wa burudani wanakosa sehemu ambayo ni tulivu ya kwenda kutembelea katika
siku za mapumziko hivyo kuzinduliwa sehemu hiyo itakuwa ni mwanzo wa
kuanzisha program mbali mbali za burudani na michezo ili kuweza kukuza
vipaji kwa wasanii wa kibaha na maeneo mengine ya jirani.
Katika hatua nyingine alisema
kwamba kutakuwepo na viongozi wa serikali katika sherehe hiyo ya
uzinduzi rasmi ambapo pia kutakuwepo na mashindano ya kula nyama choma
ambapo washindi watajinyakulia zawadi kutoka kwa uongozi wa Kibaha
Carnival na kuongeza shghuli nzima hiyo itakuwa ikiongozwa na Mc
machachari hapa nchini Mc Jura pamoja na Scope V ‘mtoto wa kasuku.
Dk. Wilbroad Slaa ampa tano Dk. John Pombe Magufuli
Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
“Nadhani sasa unaelewa
niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora
zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji
udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa amelimabia gazeti la Raia Mwema.
Amesema kuwa Bunge linatakiwa
kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini
limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa
amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
MPANGO WA KUBORESHA AFYA NA MAZINGIRA MASHULENI WAZINDULIWA SHULE YA MSINGI WAILESI TEMEKE
Wanafunzi wa Shule ya msingi
Wailesi wilayani Temeke jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wa uzinduzi rasmi mpango wa Fit For School Mpango wa
kuboresha Afya na Mazingira Mashuleni na kuhamasisha watoto mashuleni
wanawe mikono mara kwa mara, Mpango huo unafadhiliwa na Shirika la GIZ
Tanzania kutoka Ujerumani na ulizinduliwa na unatekelezwa na taaisis ya
SAWA.
Mpango huo ukizinduliwa rasmi kwa kukata utepe.
Moja ya mabango yanayoonyesha malengo ya mpango huo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Wailesi wilayani Temeke wakinawa mikono yao mara baada ya uzinduzi.
Bango hili likionyesha hatua tano za unawaji mikono kwa wanafunzi shuleni hapo.
Wanafunzi wakimsikiliza Sekela mmoja wa waratibu wa mpango huo alipokuwa akizungumza nao shuleni hapo wakati wa uzinduzi.
Wanafunzi wakionyesha mikono yao mara baada ya kunawa.
No comments :
Post a Comment