Kamishna wa Nishati na Maendeleo
ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise akizungumza katika mkutano wa tatu wa
wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao kwa jina la Powering
Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East Africa.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa
kampuni ya Six Telecoms Rashid Shamte akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na mradi wa umeme wa upepo wa Singida kupitia kampuni ya Wind
EA ambao unatarajiwa kuanza uzalishaji rasmi mwishoni mwa mwaka 2017.
Shamte alisema hayo wakati wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa
kuiwezesha Afrika katika utatuzi wa nishati ya umeme umefanyika Dar es
Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi huo, Mark Gammons.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara wa kampuni ya Wind East Africa John Chaggama akifafanua jambo
kuhusiana na uwekezaji wao wa Umeme wa Upepo uliopo mkoani Singida.
Chaggama alisema mradi huo utatatua tatizo la nishati hiyo hapa nchini
mara utakapoanza rasmi uzalishaji mwishoni mwa mwaka 2017.
Wadau na wawekezaji mbali mbali
wa nishati ya umeme wakimsikiliza Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya
Petroli Mhandisi, Hosea Mbise hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao
kwa jina la Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East
Africa.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Wakati Serikali ikibainisha
kuliondoa Shirika la umeme nchini (Tanesco) katika uzalishaji wa umeme,
kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo (Wind East Africa) imesema itaanza
uzalishaji wa nishati hiyo mwishoni mwa mwaka ujao.
Wakizungumza katika mkutano wa
kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya umeme, Kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise na Mwanzilishi na Mkurugenzi
wa wa kampuni ya Wind East Africa, Rashid Shamte walieleza mkakati
uliopo katika kuboresha sekta ya umeme nchini ambapo baada ya muda,
Tanesco itakuwa na kazi ya usafirishaji tu huku kazi ya uzalishaji
ikifanywa na kampuni kama Wind EA.
Mbise alisema kuwa alisema
uzalishaji wa umeme unahitaji uwekezaji wa hali ya juu ikiwamo kutoa
fursa kwa kampuni mbalimbali kuanza kuzalisha umeme kwa manufaa ya
Taifa.
Kwa mujibu wa Mbise, hatua za
awali za kuliondoa Shirika hilo la umeme nchini kuwa mzalishaji wa
nishati hiyo umeanza na ifikapo 2022, Shirika hilo halitajihusisha na
uzalishaji wa umeme zaidi ya kazi ya usafirishaji tu.
“Kwa utaratibu huu, Tanesco sasa
itaondoshwa katika mchakato wa kuzalisha umeme na kubaki kuwa
msambazaji, hatua tayari zimeanza kwa kuangalia madeni yaliyopo Tanesco
na jinsi ya kuyafuta sanjari na kuwachukua watumishi wa Tanesco.
“Ifikapo 2022 hatutakuwa na
Tanesco katika uzalishaji wa umeme bali umeme utazalishwa na kampuni
mbalimbali na mkakati uliopo ni kwamba hadi kufikia 2030, asilimia 70 ya
Watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya umeme,” alisema Mbise.
Kwa upande wake, Shamte alieleza
kuwa mradi wa umeme wa upepo wa Singida kwa sasa upo katika maandalizi
ya kina kuanza na mwaka ujao watakamilisha taratibu mbalimbali kwa
mujibu wa sheria za uwekezaji.
Shamte alisema kuwa mradi huo
ambao utazalisha 100 Mega Watts mbali ya kutatua tatizo la umeme,
utaufanya mkoa wa Singida kubadilika kwa kupata maendeleo makubwa
kiuchumi, biashara na hata kijamii.
Alisema kuwa mkataba mikataba ya kumalizia uwekezaji wamradi huo itasainiwa mwanzoni mwa mwezi ujao (Januari 2017).
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara wa kampuni ya Wind East Africa, John Chagama alisema, mradi wa
umeme wa upepo utakapokamilika utawanufaisha Watanzania hasa wakazi wa
Singida ambako mradi huo unaanzishwa.
“Kwanza utasaidia kutoa ajira
kwa wakazi wa Singida, lakini pia utawanufaisha Watanzania hasa wa
kipato cha chini kwani umeme utakuwa wa gharama nafuu,” alisema.
Chagama alisema kuwa umeme wa
upepo ni mradi wa kudumu na utawafanya watanzania kupunguza gharama za
maisha kwani bei ya umeme itashuka.
MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAFANYIKA SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mwenyekiti
wa Soko la Temeke Sterio Amani Mtemi akiwatambulisha wageni waalikwa
katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
yaliyofanyika katika soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii
Manispaa ya Temeke, John Bwana.
Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe akisoma risala ya Shirika hilo kwa mgeni rasmi.
Mdau Mwajuma Issa akichangia jambo kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia hasa matusi wanayofanyiwa na wanaume katika soko hilo.
Kijana Andrew Kamtu akielezea chanzo cha ukatili wa kijinsia kuwa kinaanzia kwa wazazi wenyewe.
Ofisa wa EfG, Charles akigawa vitabu vya msaada wa kisherea kuhusu ukatili wa kijinsia.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia kutoka Mkoa wa Kipolisi Temeke wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wakina mama wakiserebuka kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wawezeshaji sheria masokoni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea kutoka kwa kundi la Machozi Theatre Group.
Ngoma ya mganda ikichezwa ikiongozwa na chipukizi kutoka kundi la Machozi Theatre Group.
Burudani ya Sarakasi hiyo ikifanyika.
Mwezeshaji Sheria Kashindye Kapambala akichangia jambo kuhusu ukatili wa jinsia.
Wanawake
wakitembea katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
yaliyofanyika katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Wasanii
wa Kikundi cha Sanaa cha Machozi Theatre Group wakitoa burudani kwenye
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika
katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo
yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa sheria masokoni akichangia jambo kuhusu ukati wa kijinsia masokoni unavyofanyika.
……………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MASHIRIKA
yasiyo ya kiserikali yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha jamii
kuhusu kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo kusaidia kupunguza
vitendo hivyo nchini.
Hayo
yalibainishwa na Ofisa wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Meshack Mpwaga katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili
wa kijinsia yaliyofanyika Soko la Temeke Dar es Salaam leo mchana
yaliyokuwa na kauli mbiu ” Funguka chukua hatua mlinde mtoto apate
elimu”
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo yaliyoa andaliwa na
Shirika la Equality for Growth (EfG), Mpwaga alisema mashirika yasiyo ya
kiserikali kwa kiasi kikubwa yameisaidia nchi katika kutoa elimu na
kuhamasisha jamii juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa
kijinsia ambapo uelewa umekuwa mkubwa.
“Uelewa
kwa jamii kuhusu vitendo hivyo ni mkubwa mno wito wangu jamii iendelee
kutoa taarifa polisi pale inapobaini kuwepo kwa vitendo hivyo nasi
tutachukua hatua stahiki” alisema Mpwaga.
Mkuu
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Temeke, John Bwana, ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ametoa mwito kuwa siku 16 za
kupinga ukatili wa jinsia jamii izitumie kuelimishana na kupambana na
ukatili huo wa kijinsia.
Alisema
ni muhimu sasa jamii kuelimika na kuachana na vitendo vya udhalilishaji
sehemu yoyote ili kupata taifa la watu waliostaraabika.
Alisema
serikali hasa idara ya maendeleo ya jamii imekuwa ikisaidia na taasisi
binafsi katika kupiga vita vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia jambo
linalosaidia jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa uhuru.
Ofisa
Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe alisema utafiti
uliofanywa na shirika juu ya ukatili dhidi ya wanawake masokoni
unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta isiyo rasmi
wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na matusi katika
maeneo yao ya kazi.
Alisema
mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Temeke na Ilala ndani ya masoko
sita ambayo ni Feri, Kisutu, Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na
Temeke Sterio na kuwa umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo
rasmi hususani wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Serikali kuendelea kuimarisha Sekta ya Uvuvi
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya
Mifugo na uvuvi Bi Judith Mhina akifafanua kwa waandishi wa habari
kuhusu mradi wa udhibiti wa uvuvi na maendeleo shirikishi Kusini
Magharibi mwa bahari ya Hindi “SWIOFISH” leo jijini Dar es salaam wakati
wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara
ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi Fatma Sobo.
Afisa
Uvuvi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bw. Silas William
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na
Serikali katika kuwainua wavuvi wadogo hapa nchini ili kushiriki katika
kukuza uchumi wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi Fatma Sobo.mwisho kushoto ni Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na uvuvi Bi Judith Mhina.
Baadhi
ya Maafisa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakifuatalia
mkutano wa Wizara hiyo na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar
es salaam.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano kati
yao na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambao pamoja na mambo
mengine ulibainisha kuwa Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu hapa
nchini hasa kwa kutumia mabomu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Wizara
ya Mali asili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya mambo ya
Ndani na ile ya Katiba na Sheria.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Rais Dkt. Magufuli atoa siku saba kwa wafanyabiashara wakwepa kodi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa Sekta Binafsi na kuwaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika ukuaji wa uchumi na kuwasihi kuwa wazalendo katika suala la utoaji kodi ili kulipeleka taifa katika nchi yenye uchumi wa Kati Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Hassan Silayo Maelezo)
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewapa siku
saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza
mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Hayo
yamesemwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika
mkutano wake na wadau wa sekta binafsi alipoamua kufanya mazungumzo nao
pamoja na kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika
kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni
kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.
Mheshimiwa
Rais aliendelea kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano
amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi
anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.
“Tutaangalia
namna ya kupunguza utitiri wa ushuru katika bidhaa mbalimbali,mfano
katika kipindi cha kampeni niligundua katika Mkoa wa Kagera na
Kilimanjaro wanakolima zao la Kahawa,wamekuwa wakitozwa tozo 26 kwa zao
hilo na hiyo imechangia kusababisha wafanyabiashara wa zao hilo kufanya
biashara haramu ya kupeleka zao hilo kwa magendo kuuza katika nchi
jirani”,alisema Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja
na hayo Mheshimiwa Dkt.Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi
ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na
pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi
ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Mheshimiwa
Rais Dkt.Magufuli ameendelea kusema kuwa kama kutakuwa na mfayabiashara
yeyote atakayetaka kuwekeza na akakwamishwa na mtu aliyechini ya uteuzi
wake basi mtu huyo ataondoka kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta
binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyo toa ajira.
Pamoja
na hayo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara
wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka
kwenye machimbo ya madini,kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa
bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo na mazao ya misitu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw.Regnald
Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa Mheshimiwa Rais
katika kuhakikisha uchumi watanzania unakuwa kwa haraka na pia amemuomba
mheshimiwa rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa pamoja kusaidia
kupunguza utitiri wa kodi.
Displaying TPSF-COUNCIL IKULU.docx.
No comments :
Post a Comment