Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli kulia
akifurahia jambo na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Balozi Seif ali Iddi aliyefika ikulu kwa ajili ya mazungumzo
leo jijini Dar es salaam..
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akizungumza na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi aliyefika ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya
mazungumzo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akiagana na makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufanya nae mazungumzo ikulu jijini
Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akizungumza na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufanya nae mazungumzo ikulu jijini
Dar es salaam.
SERIKALI YATAKA KILA KAYA KUWA NA CHOO BORA
Na Magreth Kinabo- MAELEZO
Serikali imewaagiza maafisa wa
afya nchini kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora ikiwa ni
hatua ya kuhakikisha jamii inaepekana na magonjwa yanayotokana na
uchafu mazingira , sambamba na suala la usafi wa mazingira kuwa
endelevu kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha Serikali imepiga marufuku ulaji wa matunda yaliyomenywa barabarani.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando,
wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Katibu Mkuu huyo ambaye alikuwa
ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na
Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwemo wa wizara yake kwa ajili ya kuzungumzia
mambo matatu ambayo ni suala la usafi wa mazingira katika kuadhimisha
siku ya Uhuru ,Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa kipindupindu na
polio.
“Wakuu wa mikoa na wilaya
wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa kujiwekea utaratibu wa kufanya
usafi maeneo yao,” alisema Dkt. Mmbando.
Dkt. Mmbando alisema ikumbukwe
kuwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayohusiana
na uchafu huenea kwa kasi kutokana na hali duni ya usafi katika maeneo
tunayoishi. Hivyo takwimu zinaonesha kuwa kati ya taka ngumu
zinazozalishwa ni 50% tu huzolewa na kupelekwa dampo. Kiasi cha taka
kinachobaki huzagaa katika maeneo mbalimbali hususani kando kando ya
barabara, katika maeneo ya kukusanyia taka (Collection points), chini ya
madaraja na katika maeneo ya wazi hali inasayobabisha miji yetu
kuonekana michafu.
“Hali kadhalika, takwimu
zinaonesha kuwa ni kaya zipatazo 34% ndizo zina vyoo bora na asilimia
12% hazina vyoo kabisa. Hali hii inahatarisha afya ya jamii na
kusababisha kuenea kwa urahisi kwa magonjwa ya kuambukiza. Kwa mijini
na miji midogo, mifereji ya maji taka na ile ya mvua ni michafu na mingi
imeziba, hivyo hutiririsha maji ovyo na kuhatarisha afya ya jamii,”
alisema .
Aliwataka watendaji hao,
kusimimia suala hilo kwa kuzingatia sheria za afya zilizopo, huku
akizitaka halimashauri na mamlaka kuweka sheria ndogo ndogo ambazo
hazileti unyanyasaji kwa wananchi. Katika kutekeleza kwa vitendo agizo
la Mhe. Rais .
Kubainisha maeneo yote ya umma
ambako shughuli za usafi wa mazingira zitafanyika siku hiyo,kuhamasisha
jamii kwa njia mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli za
usafi katika maeneo yao na sehemu za kazi au biashara, vyombo vya
usafiri wa abiria na vituo vya wasafiri ili vifanyiwe usafi wa
kuridhisha,kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, vyombo
vya ulinzi na usalama, taasisi za elimu, n.k. ili kufanikisha zoezi zima
la ukusanyaji, usafirishaji na utupaji salama wa taka (madampo) kutoka
katika maeneo ya kaya, umma na taasisi kwa siku hiyo.
Aliongeza kwamba wanapaswa
kuhusisha au kushirikisha vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii
katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la usafi,kupanga ratiba na
wajumbe wa kusimamia kazi hiyo katika halmashauri kwa tarehe
9,Desemba,2015 kwenye maeneo ya kaya na ya umma na kupanga ratiba
endelevu baada ya hapo,kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi hizi
kwa mfumo na muda ulioinishwa na Wizara.
Pia kwa kushirikiana na wadau,
halmashauri zina wajibu wa kuandaa vyombo vya usafirishaji taka ngumu na
maji taka kutoka maeneo ya uzalishaji hadi maeneo yaliyoainishwa
kutupwa bila kuathiri mazingira.
Kwa upande wa wananchi
aliwataka wafanye yafuatayo ili kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa
kipindupindu kila mmoja Kuchemsha maji ya kunywa au kutibu kwa dawa
maalumu (waterguard)Kuepuka kula chakula kilichopoa au kuandaliwa katika
mazingira yasiyo safi na salamaKunawa mikono kwa sabuni na maji safi na
salama,kabla ya kula,baada ya kutoka chooni.
Mambo mengine ni baada ya
kumnawisha mtoto aliyejisaidia,baada ya kumhudumia mgonjwa,kuosha
matunda kwa maji safi kabla ya kula,Kukomesha utiririshaji wa maji
kutoka chooni ,Kutoa taarifa katika kituo cha kutolea huduma za afya
endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika,kutoa taarifa kwenye
ofisi za serikali endapo mtu au kikundi cha watu kitafanya shughuli
zenye kuashiria uchafuzi wowote wa mazingira.
Aliongeza kwamba Serikali
itaendeleza juhudi za kuwezesha wananchi kupata maji safi na salama.
Napenda kusisitiza kwa wananchi wote, tuwe makini kutumia maji
yanayotoka katika vyanzo visivyo salama. Hii ni muhimu kwani, kwa sehemu
kubwa, ugonjwa huu huenezwa kupitia maji yasiyo salama.
Tangu kutokea kwa ugonjwa huu
kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti, 2015 katika mkoa wa Dar es Salaam
ugonjwa huu umeendelea kusambaa kwa kasi. Hadi tarehe 2/12/2015 Mikoa
mingine 20 ya Morogoro, Iringa, Pwani, Kilimanjaro, Kigoma, Dodoma,
Geita, Mwanza, Arusha, Mara, Shinyanga, Tabora, Singida, Tanga, Lindi,
Rukwa, Manyara, Kagera, Katavi na Mbeya imeshaathiriwa.
Takwimu zinaonesha kuwa hadi
tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya watu 9,906 walipata ugonjwa huu na
kati yao jumla ya watu 149 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa
huu. Aidha, wagonjwa wengine wamepata matibabu na kuruhusiwa kurudi
nyumbani ambapo hadi tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya wagonjwa 128
waliendelea kupatiwa matibabu katika vituo vya kutolea huduma.
WWF YAIJENGEA UWEZO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira
duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako akizungumza kwenye mkutano wa
Wasaa wa Mazingira(Earth Hour City Challenges)
duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako akizungumza kwenye mkutano wa
Wasaa wa Mazingira(Earth Hour City Challenges)
Watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa zenye lengo la kulifanya Jiji kuwa la mfano barani Afrika.
Watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakifatilia kwa makini mada . |
Afisa Mawasiliano wa WWF,Michael Bwoma(kushoto)akifatilia kwa makini wengine ni waandishi wa habari mkoani Arusha. |
No comments :
Post a Comment