Thursday, December 3, 2015

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI NA WAWAKILISHI WA UMOJA WA SEKTA BINAFSI NCHINI – TPSF IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

1
 
MF3MF2
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa  Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IKULU) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa  Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015 PICHA NA IKULUMF4
002 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea Dk Reginand Mengi Mwenyekiti wa  Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) wakati wa mkutano na wafanyabiashara Ikulu leo.
02 
Dk Reginand Mengi Mwenyekiti wa  Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) akisoma hotuba yake katika mkutano huo uliofanyika Ikulu leo.
3
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa salamu zake Kwa Rais Dk John Pombe Magufuli kwa niaba ya wawakilishi wa Mabenki.
4
Baadhi ya watendaji kutoka serikalini wakiwa katika mkutano huo Kulia ni Katubu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole  Gabriel .
05
Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Bw. Farouqh Baghozah katikati akiwa pamoja na wafanyabiashara wenzake katika mkutano huo.
5
Mmoja wa wajumbe akitoa shukurani zake katika mkutano huo. kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka na mfanyabiashara Nicola Angelo wakiwa katika mkutano huo.
7
Bw. Octavian Mshiu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OpenSanit Limited akiwa pamoja na wafanyabiashara wenzake katika mkutano huo.
8
Bw. Issa Hango kutoka kampuni ya madawa ya Shelys pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
9 10
Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akielezea ratiba ya mkutano huo kabla ya kuanza.
12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiingia kwenye mkutano huo huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.
 

Lukaza Blog yaleta Tunzo Nyumbani. Asanteni Wasomaji, watembeleaji na Bloggers wenzangu

Mmiliki wa Lukaza Blog, Josephat Lukaza akiwa ameshikilia Tunzo aliyoshinda katika Kipengele cha Blog Bora ya Siasa katika Shindano la African Blogger Awards 2015 lililofanyika nchini Africa Kusini .Tutembelee kwa kufuata link hii http://www.josephatlukaza.com

Shindano la African Blogger Awards linaloendeshwa na Kampuni ya Webfluential ya Nchini Afrika Kusini lilianzishwa mnamo mwaka 2014 huku Lukaza Blog ikishiriki Kwa Mara ya Kwanza na kuibuka kuwa mshindi wa Pili wa Blog bora ya Kuelimisha kwa mwaka 2014.

Kwa Awamu ya Pili ya Shindano la African Blogger Awards liliofanyika mwaka 2015 Lukaza Blog pia iliweza kushiriki katika Vipengele vitatu huku ikiibuka Mshindi katika Kipengele Kimoja tu cha Blog Bora ya Siasa ambapo ushindi huo ulitangazwa tarehe 5 May 2015 kupitia Kurasa ya Twitter ya African Blogger Awards.

Katika Kinyanganyiro hiko Cha African Blogger Awards nilikua nikichuana na bloggers wengine kutoka Mataifa mbalimbali ya Africa na kuweza kuwagaragaza na hatimaye kuibuka Mshindi wa Kipengele cha Blog bora ya Siasa huku mshindi wa Pili akitokea Afrika Kusini.

Uendeshaji wa Shindano hili ulifanyika kwa kutumia njia ya Kitaalamu zaidi ijulikano kama Impartial Judgement ambapo hakuna kupiga kura wal kutaja jina la blog bali ni mfumo wenyewe wa mtandao ndio unaoweza kutoa majibu.

Ni mara ya Kwanza kabisa nchini Tanzania Mmiliki wa blog ya Lukaza, ndg Josephat Lukaza kuweza kuleta tunzo kutoka Kwenye mashindano yanayohusu blogs ambapo Kwa Tanzania hakuna shindano lililowahi kufanyika Wala kuandaliwa zaidi ya mashindano kama hayo kufanyika Nchi nyingine Duniani.

Sisi Kama Lukaza Blog tunajivunia kuibuka na Ushindi huu ambapo Kiukweli umetupa changamoto sana na kutuonyesha kuwa kumbe Blog zetu hata nje ya nchi zinatembelewa na zina wapenzi wengi sana lakini pia imetupa hali ya kujituma zaidi na zaidi na kuhakikisha tunafanya kile tunachoweza kuhakikisha tunaipasha Dunia kuhusiana na kile kitokeacho Duniani, Hususani Tanzania.

Lukaza Blog imeweza kuandika historia kwa kushinda katika shindano hilo la Africa Blogger awards na kufanikiwa kuleta Tunzo Nyumbani.
Tunzo hii iwaendee Wasomaji wangu wote kwa maana bila nyie Lukaza Blog isingeweza Kunyakua tunzo hii katika Shindano la African Blogger Awards lililomalizika Mnamo mwezi May 2015 huko Afrika ya Kusini. Lukaza Blog iliweza Kuibuka Mshindi wa Kwanza katika Kipengele cha Blog Bora ya Siasa na kuwashinda wapinzani wake ambapo Mshindi wa Pili akiwa ni Blogger kutoka Afrika Kusini.

Vilevile Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wafuatiliaji wa Lukaza Blog kwa sapoti yao kwangu na timu nzima kwa maana Mafanikio haya Madogo tu yaliyopatikana wao pia wamehusika.

Shukrani zangu za Dhati kabisa Ziwaendee pia Bloggers Wenzangu Kiukweli Ushirikiano wao Kwangu napo kumeongeza tija na msukumo wa hali ya juu katika Kushinda tunzo hii hatimaye Tunzo hii imekuwa sio ya Lukaza Blog tu bali ni Kwa Tanzania Nzima na Watanzania Wote.

Asanteni sana na hapa sio mwisho tunaendelea kupambana na Changamoto ambapo sisi kama Lukaza Blog kwetu changamoto ni nafasi ya mafanikio.

Asanteni sana Bloggers, Wasomaji, Taasisi za Ndani ya Nchi na Hata Barclays Africa kwa kuona tija na kutuamini Lukaza Blog Kuweza Kufanya kazi na Nyinyi kwa Kipindi chote cha Miezi Sita kuanzia July hadi December yote hii ni njia ya kuelekea Kwenye kilele cha Mafanikio huku Juhudi, Heshima, Busara na ushirikiano vikitawala kichwa kwangu.

Tunzo hii ni heshima pia Kwetu Tanzania kwasababu tumeanza kuonyesha Dunia kuwa na Sisi Tupo tumeanza kwenye Muziki, Filamu na Sasa ni Blogs. Pia unaweza kututembelea kwa Kubofya hapa

MABONDIA THOMASI MASHALI NA FRANSIC CHEKA WATAMBIANA, KUDUNDANA DESEMBA 25 MOROGORO

Mabondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambulisha mpambano wao wa Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransic Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76
Akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro  hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibarua kigumu ambapo atapigana na Cheka mkoani Morogoro
Naye Bondia Cheka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anayetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa nipo vizuri na naendelea na mazoezi
Kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambaratisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro
Naye kocha wa bondia Cheka Bw. Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana
Katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine yaUtangulizi itakayowahusisha  bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ ambaye atapambana na Twaha Kassimu Kg 63 na Vicent Mbilinyi Kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula Kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John  Kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage Kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa

Iceland yawezesha TGDC kutafiti Jotoardhi

as1 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson, wakisaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe na Afisa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini Yese Malolela.
as2 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson, (aliyenyoosha mkono), akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini wakisaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya; kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), wanaoshuhudia ni Meneja Mipango wa ICEIDA (kushoto), David Bjarnason, kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya TGDC .
as3 
Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe (wa kwanza kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson. Mkataba huo utawezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Vilevile msaada huo utawezesha pia kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshugulikia Nishati Jadidifu Edward Ishengoma (Wa kwanza kulia) na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na ICEIDA
as4 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Paul Masanja (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Vilevile, Mkataba huo utawezesha kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo.
………………………………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Serikali kupitia Kampuni Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, (TGDC) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), wamesaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi; kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo.
Makubaliano hayo yalifikiwa jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Engilbert Gudmundsson, ambapo tukio hilo lilishuhudiwa na Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Uendelezaji wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma, baadhi ya Maafisa kutoka TGDC na Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, matarajio ya Tanzania ni kuzalisha kiasi cha megawati 200 za umeme unaotokana na nishati ya jotoardhi ifikapo mwaka 2020 ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa, hazina iliyopo kupitia nishati hiyo ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati elfu tano za umeme (5,000), kutokana na nishati ya jotoardhi .
Aidha, Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, utayari na ushirikiano iliyouonesha nchi ya Iceland kupitia ICEIDA itakuwa kichocheo kikubwa kufikia malengo ya serikali ya kuwa na nishati ya kutosha ya umeme kutoka vyanzo mbalimbali.
“Tuna malengo yetu mengi kupitia nishati hii, utafiti ndio njia itakayotufanya kufikia malengo yetu hivyo, ushirikiano huu ni mwanzo mzuri kwa upande wetu. Nafahamu Iceland mlianzia katika hatua za chini kabisa lakini sasa mko mbali. Naamini uzoefu wenu utatuwezesha kuweza kufika mahali tunapotarajia,” aliongeza Mhandisi Masanja.
Aidha, Masanja aliitaka Kampuni ya TGDC, kuhakikisha inashirikiana vizuri na nchi ya Iceland ikiwemo shirika la ICEIDA kuhakikisha linafuata ushauri mzuri wa kitaalamu unaotolewa na shirika hilo ili kuweza kupata uzoefu, jambo ambalo litawezesha sekta ya jotoadhi nchini kupiga hatua na hivyo kuifanya jotoardhi kuwa chanzo kingine cha nishati ya umeme.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, alishukuru utayari wa ICEIDA katika kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia malengo yake ya kuendeleza nishati hiyo, utayari ambao utasaidia kufanyika kwa tafiti katika maeneo yenye viashiria vya jotoardhi ya Luhoi, na Kibiti, Mkoa wa Pwani.
Vilevile, Mhandisi Njombe alieleza kuwa, kutokana na utafiti utakaofanywa, utawezesha upatikanaji wa takwimu sahihi ambazo zitafungua njia ya kupata msaada zaidi kutoka katika taasisi ambazo zimejikita katika masuala ya zenye uhusiano na nishati ya jotoardhi, jambo ambalo pia litawezesha uendelezaji wa nishati hiyo nchini.
Aidha, Mhandisi Njombe alitumia fursa hiyo pia kueleza hatua mbalimbali ambazo tayari zimefanywa na kampuni hiyo katika kuhakikisha kwamba, jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha uzalishaji umeme nchini na kuongeza kuwa, kupitia makubaliano hayo, ICEIDA itawezesha wataalam wa ndani wa TGDC kupata ujuzi na uzoefu utakaowezesha kufanyika kwa tafiti nyingine katika maeneo ya Kiejo/ Mbaka, Mkoa wa Mbeya.
Naye, Mkurugenzi wa ICEIDA, Engilbert Gudmundsson alieleza umuhimu wa nishati hiyo na unafuu wake wa gharama ikilinganishwa na nishati nyingine na kueleza kuwa, asilimia 25 ya umeme unaozalishwa nchini Iceland unatokana na nishati ya jotoardhi.
“Ilituchukua kipindi cha miaka 25 kufikia mafanikio tuliyonayo katika nishati ya jotoardhi. Kutokana na ubobezi huu ni vema kwetu kutoa uzoefu kwa TGDC kuhakikisha inafakia malengo tarajiwa na kwamba jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha umeme kwa Tanzania ambao ni rahisi na nafuu,”aliongeza Engilbert.
Jotoardhi ni mojawapo ya chanzo cha nishati kitokanacho na mvuke unaotoka ardhini, hususan katika maeneo yaliyo katika Bonde la Ufa (Rift Valley). Nchi zilizo katika bonde la Ufa (African Rift Geothemal Facility – ARGeo) ni pamoja na Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Tayari Tanzania imefanya jitihada kadhaa za kuendeleza Jotoardhi ikiwemo uanzishwaji wa Kampuni ya TGDC, ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), iliyoanzishwa mwezi Juni, 2014. TGDC inatajwa kuwa kichocheo muhimu cha uendelezaji wa nishati ya jotoardhi. Aidha, mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi mwanzoni mwa Novemba 2014, Tanzania ilikuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Jotoardhi uliofanyika Jijini Arusha.
Mkutano wa Jotoardhi unatajwa kuinufaisha Tanzania katika kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu ili kuchangia upatikanaji wa nishati hiyo nchini; kubadilishana uzoefu na uelewa na wataalamu kutoka nchi mbalimbali duniani; ikiwemo pia kuharakisha uendelezaji wa jotoardhi

TAZARA yapokea mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya Watu wa China

tz1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka akipanda kwenye moja ya vichwa 4 vya treni ya Tazara vilivyotolewa na Serikali ya China.
tz2 
Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza kabla ya makabidhiano
tz3 
Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga akizungumzia umuhimu wa reli ya TAZARA kwa Tanzania na Zambia.
tz4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka akizungumzia mustakbali wa TAZAMA katika kujenga uchumi wa Tanzania.
tz7 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) Ronald Phiri akibadilishan hati za makabidhiano ya mabehewa 18 na vichwa 4 vya treni na Makamu wa Rais wa CCECC kutoka Serikali ya Watu wa China Lin Zhiyong.
tz8 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka (katikati) akikata utepe pamoja na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa kwa mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya China.
tz9 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga, wakielekea kupanda kwenye treni ya kichwa na mabehewa mapya ya TAZARA.
tz10 
Moja ya mabehewa mapya
tz11 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga (kulia) wakibadilishana mawazo wakiwa ndani ya sehemu ya kulia chakula iliyomo kwenye moja ya behewa jipya.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji TAZARA, Ronald Phiri na Mwakilishi wa Balozi wa China.
tz12 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga, wakiteremka kutoka kwenye moja ya behewa jipya baada ya kusafiri nalo kwa dakika kumi kufanyia majaribio.
tz13 
Moja ya kichwa kipya na mabahewa 18 mapya yaliyokabidhiwa kwa TAZARA.
tz14 
Baadhi ya maafisa kutoka Serikali ya Watu wa China na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), wakishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya Watu wa China.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………

TGDC yatarajia kuzalisha umeme Megawati 200 ifikapo 2020.

tg2
Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
tg3
Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bwana Kato Kabaka akitoa mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
tg4
Mtaalamu wa masuala ya nishati toka Benki Kuu ya Dunia (ESMAP) Bwana Thrainn Fridriksson (aliyesimama mbele) akitoa mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
Mtaalam wa masuala ya nishati ya jotoardhi toka Shirika la Pertamina Geothermal Energy la nchini Indonesia Bwana Hendrik Kurniawan Sinaga (kulia) akitoa mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia. Kuhsoto ni Mtaalam mwenzie wa masuala hayo Bwana Agus Zuhro.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga, Maelezo.
 
TGDC imepewa lengo na Serikali la kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa Megawati 200 na kuuingiza katika gridi ya Taifa kufikia mwaka 2020.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe wakati wa warsha ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambayo iliwakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi.
 
Mhandisi Njombe alisema kuwa warsha hiyo ina lengo la kujadili njia mbalimbali zilizotumiwa na baadhi ya mashirika hayo hadi kufanikiwa kupata nishati hiyo ikiwemo uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC.
 
“Matokeo ya warsha hii tuliyoifanya tumeweza kuwasiliana na wenzetu wa Benki ya Duni (ESMAP) kwa kukusanya wataalam toka taasisi mbalimbali pamoja na Mashirika mbalimbali ambayo yamewahi kufanya kazi hii ya utafutaji wa nishati ya jotoardhi na lengo letu ni kutaka kufahamu njia ambazo wenzetu walizitumia mpaka kufanikiwa ili na sisi tupate kujifunza”, alisema Njombe.
 
Aidha, aliongeza kuwa warsha hiyo itawezesha rasilimali chache zilizopo ziweze kutumika ipasavyo katika kuleta matokeo ambayo TGDC inatarajia kuyapata ili kuhakikisha kuwa lengo la upatikanaji wa nishati hiyo linafikiwa.
 
Sambamba na warsha hiyo TGDC kupitia Wizara ya Nishati na Madini wametiliana saini Mkataba wa makubaliano na Shirika linaloshughulikia nishati ya Jotoardhi la nchini Iceland (ICEIDA) utakaoisadia Tanzania kupatiwa vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika maeneo ambayo jotoardhi inasadikiwa kupatikana.
 
Utiaji saini wa mkataba huo ulifanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na kwa upande wa nchi ya Iceland ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ICEIDA Bwana Engilbert Gudmundsson ukushuhudiwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe na Wanasheria.
 
Akiongea mara baada ya utiaji saini wa mkataba huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja alilishukuru shirika la ICEIDA la nchini Iceland kwa mchango wao mkubwa wa kukubali kulisadia shirika la TGDC ili kuhakikisha kuwa nishati hiyo inapatikana.
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ICEIDA Bwana Engilbert Gudmundsson ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza nishati hiyo kwa kuendelea kutoa msaada wa kiufundi na vifaa vinavyotumika katika utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo.
 
Warsha hiyo ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo watu wa Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia kwani hawa wote wameweza kufanikiwa kuipata nishati hiyo, hivyo watatoa mchango mkubwa kuliwezesha shirika la TGDC kupata mafanikio na hatimaye nishati hiyo kuweza kupatikana.
 
TGDC NI Shirika Tanzu la Tanesco lililoanzishwa Desemba 2013 na kuanza rasmi kufanya kazi zake mwezi Julai 2014 ili kuharakisha upatikanaji wa nishati ya jotoardhi nchini.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA ZIARA SOKO KUU SHINYANGA,MAZINGIRA YA SOKO YANATISHA

Desemba 02,2015- Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendelea na ziara za kushtukiza kwenye maeneo ambayo ni kero katika wilaya hiyo.Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi,mkuu huyo wa wilaya akaabukia katika soko kuu la manispaa ya Shinyanga lililojengwa kabla ya uhuru wa Tanganyika..Ikawa faraja kwa Wafanyabiashara wa soko hilo waliodai kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiilalamikia halmashauri ya manispaa kutokana na kushindwa kulifanyia ukarabati soko hilo.Akiwa katika soko hilo Josephine Matiro amesikiliza kero nyingi kutoka kwa wafanyabiashara hao ikiwemo ukosefu wa mitaro,kalo la maji,uchafu sokoni.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..Anatusimulia kwa picha 40 kilichojiri mwanzo hado mwisho..Tazama hapa chini

UN, SERIKALI ZATAKA VIJANA KUONGOZA KATIKA KUKABILI MABADILIKO TABIA NCHI SINGIDA

IMG_4985 
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Chigulu Charles akitoa neno la ukaribisho kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Singida.
Na Modewjiblog team, Singida
MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi mkazi wa Shirika la Mipango ya Maendeleola umoja huo (UNDP) Bw.Alvaro Rodriguez, amezuru mradi wa ufugaji nyuki uliopo Ikungi mkoani Singida.
Katika Ziara hiyo kwenye mradi unaofadhiliwa na UNDP, Mratibu huyo aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah Hassan.
Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNDAP).
Mradi huo uliofadhiliwa na UNDP kwa thamani ya Shilingi milioni 224 umewanufaisha wafugaji 2,000 huku wanawake wakiwa ni 1,100.
Mradi huo ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2013 na 2014 umelenga kuendeleza shughuli za ufugaji nyuki wilayani Ikungi.
Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.
Kutokana na mradi huo, fursa za ajira zilitengenezwa, hasa vijana wa kijijini, kuwepo na eneo la kisasa la kutengeneza mizinga ya nyuki na uchomaji moto uliokuwa unafanywa katika misitu ukapungua sana.
Akizungumza katika eneo la mradi Bw. Rodriguez, aliusifu utawala wa mkoa wa Singida kwa kufanyakazi na UNDP kwa lengo la kujenga uwezo kwa wananchi na wakati huo huo kutunza mazingira.
IMG_4998 
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, inayosimamia mradi wa ufugaji nyuki kisasa, Boniface Mathew akitoa maelezo ya mradi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Pamoja na mambo mengine Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limeshiriki katika ufadhili wa utengenezaji wa mizinga bora pamoja na kutoa semina mbalimbali kwa wafugaji nyuki uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 224 hadi sasa.
“Ninafuraha sana kuona matokeo mema ya mradi huu; ni lengo letu kutunza mazingira huku tukifaidika na uhifadhi huo. Mafanikio haya yanastahili kuigwa na wengine,” alisema Rodriguez akiongeza kuwa wanawake walifaidika sana na mradi huu kiasi cha kustahili kufanyiwa kazi katika eneo jingine.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone alisema mradi wa UNDP una matokeo yenye tija kubwa na kuwataka waliofadhiliwa kutumika kufunza jamii nyingine umuhimu wa ufugaji na hifadhi ya misitu.
“leo tunashuhudia ufugaji nyuki wa kisasa ambao umebadilisha sekta ya ufugaji nyuki, tija katika ufugaji huu imeongezeka maradufu. Hiyo imesaidia kaya zaidi ya 1000 kupata kipato cha kukabiliana na umaskini.” Alisema Mkuu wa mkoa.
Aidha alisema kwamba wafugaji nyuki wameweza kuwa pamoja na kujipatia asali na mazao mengine kutokana na shughuli ya ufugaji nyuki kama nta, sumu ya nyuki, uchavuaji na kadhalika.
IMG_5016 
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, Boniface Mathew (kulia) akikabidhi taarifa ya mradi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Kutokana na shughuli hizo za ufugaji zaidi ya fursa 2,500 za ajira zilitengenezwa.nafasi hizo ni kama za mfugaji, wachongaji mizinga, wauza asali, wasafirishaji na wachakati wa asali.
Wilaya ya Ikungi imejaliwa kuwa na misitu ya Miombo na Minanga ambayo ni chanzo kizuri cha chavua.
Mradi wa ufugaji nyuki Ikungi umelenga kufungua njia zote za uzalishaji asali na kupiga vita umaskini kwa kuanzisha fursa za ajira za kujitegemea.
Mwakilishi huyo wa UNDP na Mkuu wa mkoa pia walitembelea hospitali ya rufaa ya mkoa ambayo ipo katika awamu ya mwisho ya ujenzi.
Itakuwa ni moja ya hospitali kubwa itakayohudumia mikoa mitano katika ukanda wa kati.
Katika mazungumzo yake Mratibu wa UN alimpongeza Mkuu wa mkoa kwa juhudi zake za kuhudumia wanawake waume na watoto wa Tanzania.
IMG_5009 
Baadhi ya mizinga ya kisasa iliyofadhiliwa na UNDP ikiwa kwenye karakana ya kutengeneza mizinga ya nyuki tayari kugawiwa kwa vikundi mbalimbali vya wanawake na vijana iliyopo kwenye Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi.
IMG_5022 
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, Boniface Mathew akimwonyesha mizinga ya kisasa ya ufugaji nyuki Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati). Kushoto ni “Programme Assistant- Global Environmental Facility Small Grant”, UNDP, Stella Zaa.

IMG_5102 
Mwanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa, Juma Simbu akikabidhi taarifa ya kikundi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_5109
Sehemu ya eneo la shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5114 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaidiana na wanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa kupandisha moja kati ya mizinga iliyofadhiliwa na UNDP katika shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5123 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone wakipandisha moja kati ya mizinga iliyofadhiliwa na UNDP kwenye shamba hilo.Kwa matukio zaidi bofya hapa

Tanzania yawa mwenyeji wa mkutano wa kumi wa SADC

index3 
Na Immaculate Makilika -MAELEZO
Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa kumi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wa  uhamaji kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali, imepata heshima hiyo baada  ya  kuonekana  ni kati ya nchi zilizofanya vizuri katika uhamaji wa analogia kwenda digitali.
Mkutano huo wenye kauli mbiu inayosema ‘Digital Broadcasting Dynamics: Building a suistainable Future’ unaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 3 Desemba, 2015 jijini Dar es salaam, una lengo la kubadilishana uzoefu kwa nchi wananchama wa SADC ambazo zimepiga hatua katika uhamaji wa mfumo wa analogia kwenda digitali .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Yamungu Kayandabila alitoa shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa heshima iliyopewa na sekretarieti ya SADC kwa kuifanya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu muhimu.
‘Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na imetumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano (National ICT Broadband Backbone – NICTBB) uliopo zaidi ya kilomita 7,560 ambao umeenea katika makao makuu ya miji yote nchi nzima, ikiwa ni pamoja na mikongo 4 ya kimataifa inayopita  baharini  na hivyo tuna kila sababu  ya kutarajia mafanikio makubwa ya TEHAMA katika kipindi cha miaka mitano ijayo’ alisema Bwana. Kayandabila
Tanzania ilifanikiwa kumaliza uhamaji wa mfumo wa analogia kwenda digitali katika miji 20, tarehe 30 mwezi aprili, 2015, ikiwa ni kabla ya muda wa makubaliano ya  ‘International Telecommunications Union’( ITU) , yaliyozitaka nchi kuhama kabla ya kufikia tarehe 17 Juni,2015.
Naye,  Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Y. Simba alisema pamoja  na changamoto mbalimbali kama gharama kubwa za huduma hizi,  zinazozikuimba nchi katika uhamaji wa mfumo wa analogia kwenda digitali, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara Tanzania imekuwa kati kati ya nchi 3 zilizofanya vizuri ikitanguliwa na Rwanda pamoja na Visiwa vya Shelisheli.
Alitaja baadhi ya sababu zilizosadia Tanzania kufikia hatua hiyo ambazo ni utayari wa viongozi  na ushirikishwaji wa wadau katika kila hatua ya mchakato.
Aidha, faida za kuhamia  katika mfumo wa digitali ni pamoja na fursa za uandaji wa maudhui, namna ya kuwasilisha maudhuui hayo kwa hadhira, vile vile mfumo huo umesaidia kufikisha maudhui kwa hadhira kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ambazo zinaweza kuleta mchango  katika sekta za kijamii na uchumi.
Nchi wanachama wa SADC walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Zimbabwe, Tanzania, Botswana, Namibia, Afrika ya Kusini, Malawi, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Lesotho na Swaziland. Ambapo washiriki walipata fursa ya kujadiliana  na kuuliza maswali  juu ya mada zilizowasilishwa katika mkutano huo uliojumuisha pia wadau wa sekta ya utangazaji nchini. Aidha, mkutano huu ni matokeo ya mkutano wa 9 wa ‘SADC Digital Terrestrial Television Forum ’uliofanyika  mwezi Juni, 2015 nchini Namibia.

UGONJWA WA MTUHUMIWA WAKWAMISHA KUENDELEA KWA KESI

law
Mahmoud Ahmad,Arusha
Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita ililazimika kuhairisha  kesi ya kuidhinisha jumla ya kiasi cha sh,24 milioni kinyume na sheria inayomkabili  mkurugenzi  mkuu wa kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini(Carmatec),Elfariji Makongoro na wenzake wawili hadi  Januari 18 mwakani baada ya upande mshtakiwa kudai Makongoro ni mgonjwa.
 
Kesi hiyo ilihairishwa mbele ya  hakimu mkazi wa mahakama hiyo mkoani Arusha,Patricia Kisinda baada ya wakili wa mshtakiwa Arnold Laiser  kuiambia mahakama hiyo kwamba Makongoro bado ni mgonjwa na anaendelea kupata  matibabu.
 
Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo kuhairisha kesi hiyo nambari 1195 ya mwaka 2015 kwasababu mteja wake bado ni mgonjwa na anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Regency iliyopo jijini Dar es salaam.
 
Kutokana na hali hiyo kesi hiyo ilikuwa isikilizwe Oktoba 12 na 20 mwaka huu mfululizo lakini kutokana na sababu hiyo hakimu alilazimika kuiharisha hadi Januari 18 mwaka ujao.
 
Hatahivyo,kabla ya kuiharisha kesi hiyo hakimu  Kisinda alimtaka  wakili wa mtuhumiwa  huyo kuwasilisha  vyeti  vya ugonjwa wa mtuhumiwa mahakamani hapo ifikapo Januari 18 mwakani wakati kesi hiyo itakapoletwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
 
Awali,mwendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) mkoani Arusha ,Rehema Mteta aliiambia mahakama hiyo kwamba Makongoro akiwa kama mkurugenzi wa kituo hicho na wenzake wawili mnamo Juni 26 mwaka 2012 waliipatia zabuni karakana ya Mbilinyi Auto ya jijini Arusha bila kufuata sheria za zabuni.
 
Mteta,alisema kwamba Makongoro ambaye ni mkurugenzi wa kituo hicho,Absolom Nko ambaye ni afisa manunuzi sanjari na Pythias Ntella ambaye ni kaimu ofisa usafirishaji wa kituo hicho walitumia madaraka ya kinyume na sheria kwa kuipatia zabuni karakana hiyo kukarabati gari aina ya Toyota Landcruiser Hardtop mali ya serikali kwa kiasi cha sh,24 milioni.
 

MKOA WA MBEYA WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA TIBA KWA FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UKIMWI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kuhusu   Ununuzi wa Vifaa tiba pamoja na Dawa za ARV kutoka katika fedha zilizochangishwa na wadau kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stella Kategile akitoa taarifa ya UKIMWI kwa mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake.

Dawa pamoja na vifaa tiba vilivyo nunuliwa kutoka katika fedha zilizo changishwa na wadau kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kushoto akimkabidhi Mganga Mkuu mkoa wa Mbeya Dkt Sefu Mhina  moja ya  vifaa tiba vilivyonunuliwa na  kutoka katika fedha zilizo changishwa  na wadau kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.Picha Keneth Ngelesi.
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Siku
chache mara baada ya
Serikali kutangaza kuahirisha shughuli za
maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yalipangwa kufanyika Kitaifa
mkoani Singida mwaka huu na badala yake pesa hizo zikatumike kununua Vifaa tiba
pamoja na Dawa za ARV hatimaye agizo hilo limetekelezwa na uongozi wa Mkoa wa
Mbeya . 
 
Akizungumza na waandishi wa habari  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbasi kandoro, amesema
pesa zilizokusanywa na kamati ya inayoratibu maadhimisho hayo kwa mkoa wa mbeya
ni  kiasi cha shilingi milioni 3.5 ambazo
zimetumika kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo la rais Magufuli kwa ununuzi wa
ununuzi wa vifaa tiba pamoja na dawa hizo za ARV.
 
Amesema, kiasi hicho cha fedha kilipatikana
baada ya wahisani mbalimbali kuchangia na kwamba kiongozi huyo amewataka wadau
ambao hawakupata fursa ya kuchangia waendelee kwani mahitaji bado ni makubwa
hususani katika suala nzima la chakula.
 
Aidha, Mkuu huyo alitoa shukrani za pekee kwa
kanisa la Anglikan mkoa wa Mbeya kwa kuchangia boksi saba za kondomu na
kuwataka wananchi kuendelea kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa
wa ukimwi kwani hali ya takwimu bado si nzuri kwa Mkoa wa Mbeya.

No comments :

Post a Comment