Friday, December 4, 2015

PSPF YATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM, NIA NI KUKUZA USHIRIKIANO



UONGOZI wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Bw. Adam Mayingu, umefanya ziara ya kutembelea vyombo vya habari hapa jijini Dar es Salaam, ili kuimarisha ushirikiano miongozi mwa taasisi hiyo ya umma na waandishi wa habari.
Bw. Mayingu na timu yake walitembelea vyombo vya habari vya kampuni ya Mwananchi Communications Limited, MCL, yenye makao yake makuu, barabara ya Mandela eneo la Tabata reline, na kampuni ya Business Times, wachapishaji wa gazeti la Majira, yenye makao yake makuu eneo la Gerezani.


Pichani Bw. Mayingu (kulia), akimpatia zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw. Francis Nanai, mara baada ya mazungumzo baina ya uongozi wa PSPF, na ule wa MCL. (Picha zote na Abdul Njaidi wa PSPF)



Meneja Mkuu wa Business Times Limited Bw. Aga Mbuguni,(kushoto) akipokea machapisho mbalimbali ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam Mayingu baada kikao cha watendaji wakuu wataasisi hizo kilichofanyika Makao Makuuya Business Timesjijini Dar es Salaam.

 Bw. Mayingu (katikati) akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa MCL

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo (wanne kushoto) akisisitiza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa kuu  wa Mfuko wa  Pensheni wa PSPF na Business Times.

Mtoa huduma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Neema Mashingia akimsaidia mteja kuhama kutoka huduma ya 3G kwenda huduma ya 4G wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya 4G LTE uliofanyika jana mjini Morogoro

 Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe akiongea na Mtaalam wa mitandao ya kijamii wa Tigo bi Samira Baamar wakati akijiandaa kutoa zawadi za washindi wa bahati nasibu, wengine ni binti wa mkuu wa mkoa, Afisa maendeleo ya masoko Shavkat Berdiev (kulia) na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Mashariki Goodluck Charles.

Wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakisikiliza kwa mageni hotuba zilizokuwa zikitolewa.

Mgeni rasmi, mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe akisalimiana na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Mashariki Goodluck Charles, katikati ni Afisa wa maendeleo ya masoko Shavkat Berdiev.

 Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Suleiman Bushagama (Kushoto) Mutalemwa (katikati) na Ben Mponzi (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.

 Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Suleiman Bushagama (Kushoto) Mutalemwa (katikati) na Ben Mponzi (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.

MAGEREZA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI KATIKA MIAKA 54 YA UHURU WA TANGANYIKA

KAZ1 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akiwasilia katiki viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kukabishi bendera kwa watumishi 39 wa Jehi hilo wanaotarajia kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
KAZ2 
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akikabidhi bendera ya Magereza kwa kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy leo tarehe 04/12/2015 wakiwa wanajiandaa kupanda Mlima tarehe 06/12/2015 ili ifikapo tarehe 09 siku ya Uhuru wa Tanganyika wawe kileleni
KAZ3 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akitoa nasaha kwa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani)
KAZ4 
Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini nasaha za Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
KAZ5 
Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba nyimbo za hamasa baada ya kupokea bendera kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
KAZ6 
Wapanda Mlima Kilimanjaro wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja (Katikati),wa tatu kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha SACP Hamis Nkubasi, na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro SACP Venant Kayombo, wa tatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa
KAZ10 
Wadau wa Magereza Utalii Klabu wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kukimbia na kutembea katika viunga vya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika sambamba na kuamasisha utalii wa ndani.
KAZ12 
Picha zote na Mrakibu Msaidizi wa Magereza Deodatus Kazinja na Koplo Mfaume Abdalah wa Jeshi la Magereza
……………………………………………………………………………………………..
Na Deodatus Kazinja
Katika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba watumishi wapatao 39 Jeshi la Magereza wakiwa katika uwiano wa wanaume 30 na wanawake 9 wataadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Washiriki hawa wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia Magereza (KMKGM), Pwani, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Mara, Tabora, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani.
Akiongea na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Casmir Minja katika hafula fupi ya kuwakabidhi bendera watumishi hao katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro amesema amefurahishwa mno na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la Magereza nje ya mipaka yake.
Kamishna Minja alisema pia mbali na kulitangaza Jeshi la Magereza unawaweka timamu watumishi hao katika kufanya kazi zao vizuri ikiwa ni kuunga kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.
Aidha Kamishna huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikijitolea kulisaidia Jeshi la Magereza ambapo alitoa taarifa kuwa tayari mikataba ya kununuliwa magari yapatayo 905 na ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 9500 imesainiwa na magari yataanza kuingia mapema Januari 2016.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Magereza Utalii Klabu ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Ndugu Estomih Hamis mbali na kumshuruku Kamishna Minja akwa namna ambavyo amejitolea katika kufanikisha uanzishwaji wa Klabu hiyo kuelezea dhima nzima ya utalii huo.
“ Tumeamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa mfumo huu kwa sababu kadhaa. Mosi , ni kuunga mkono jitihada za serikali za muda mrefu za kuhamasisha utalii wa ndani ambacho ni chanzo kimojawapo cha kuongeza mapato ya ndani ya serikali”
“Pili, ni kuleta mwamko kwa watumishi wa umma na watanzania kwa ujumla katika kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kuliko ilivyo sasa ambapo sehemu kubwa ya watalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania”
Aidha, ndugu Hamis aliongeza kuwa zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro ni zuri kwa kuimarisha afya za watumishi hivyo kujiepusha na magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na utimamu wa mwili na hasa kwa askari wanaotakiwa kuwa hivyo muda wote.
Tukio la watumishi wa Magereza kupanda mlima Kilimanjaro litakuwa ni la pili kwa mwaka huu ambapo mara ya mwisho walipanda mlima tarehe 6 March, 2015 wakiwa ni jumla ya watumishi 20 ambapo 16 walifanikiwa kufika kileleni na wanne kurudia njiani kwa sababu mbalimbali.
Zoezi la upandaji mlima lililopita lilifanyika kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuibua hoja y wa unndwaji wa chombo cha pamoja kinachoweza kuratibu shughuli za utalii ndani ya Jeshi la Magereza kwa kuwaunganisha watumishi wote.
Hoja hiyo ilifanikiwa kwa kuundwa kwa Klabu ya Utalii ya Magereza, klabu ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili. Tayari Klabu hiyo inao viongozi wakiongozwa na Mwenyikiti ndugu Hamis, katibu wake akiwa ni Mkaguzi wa Magereza Dominick Mshana na Mweka Hazina ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Erasto Kipingu.
Nani analipa gharama za utalii huo?
Akijibu swali hilo katibu wa Klabu hiyo Mkaguzi Mshana alisema kwa hivi sasa watumishi hao wanapanda kwa gharama zao wenyewe kutoka katika mishahara yao ambapo karibu kila mshiriki amechanga wastani wa shilingi 300,000.
Mshana amesema ni matumaini yake kuwa katika siku za mbeleni kama watapatikana wadhamini gharama hizo zinaweza kupungua sana kutoka mifukoni mwa washiri.
Aidha amesema gharama za kupanda mlima na kutembelea vivutio vingine kwa ujumla ni kubwa kwa mtu mmoja mmoja lakini kunakuwa na unafuu mkubwa watu wakipanda kama kikundi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUJITOLEA DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DAR

 
 
GB1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia akiongea na wanahabari katika maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Overseas (VSO) Dkt. Philip Goodwin.
GB2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
GB3 
Bi Ritha Mushi (VSO Volunteer) akiongea na Vijana wenzake juu ya umuhimu wa kujitolea katika kongamano la siku ya kujitolea duniani lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
GB4 
Bw. Ian Tarimo anaejitolea katika Shirika lisilo la Kiserikali la Youth For Change akiongea na Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
GB5 
Dr Ven kutoka DFID akiwaasa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
GB6 
Kijana akipata maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika lisilo la Kiserikali la JICA wakati wa kongamano la siku ya kujitolea lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.

WAISHTAKI MAHAKAMA YA ICTR WAKISTAHIKI ZAO

index 
Mahmoud Ahmad Arusha
WALIOKUWA wafanyakazi wa mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, UN –ICTR, ambayo imemaliza muda wake wakuwepo nchini , wameishitaki mahakama hiyo kwenye mahakama ya kazi wakidai kutolipwa stahiki zao.
Wafanyakazi hao wakizungumza kwenye ofisi ya Idara ya kazi mkoa wa Arusha, wamesema wanaishitaki mahakama hiyo kutokana na kutowalipwa stahiki zao ambazo zinahusisha Likizo na nyongeza ya mishahara kulingana na mikataba yao.
Wafanyakazi hao wanaidai mahakama hiyo jumla ya dola za kimarekani, 800,000, ambazo hawajalipwa hadi leo ambapo mahakama hiyo ya Umoja wa mataifa ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 21 ilifunguliwa mjini Arusha mwaka 1994 nayo imemaliza kazi yake mwezi uliopita.
Wafanyakazi hao ambao waliajiriwa na Mahakama hiyo mwaka 1998 walikuwa wakihudumia wafungwa na mabusu wa mahakama hiyo  iliyopo  kwenye gereza kuu la Arusha .
Wamesema walipoaanza kudai na kufuatilia stahiki zao ndipo walipopewa barua za kuachishwa  waliachishwa kazi Septemba 30 mwaka huu .
Wamesema mara baada ya kupewa barua zao hawakutakiwa tena kufika ofisi za Mahakama hiyo zilizokuwa jengo la mikutano ya kimataifa AICC na ndipo walipofika Idara ya Kazi mkoa kwa ajili ya kufungua shauri la madai yao.
Ofisi hiyo ya Kazi iliandikia mahakama hiyo barua ya kutaka kufahamu stahiki za wafanyakazi hao lakini mahakama hiyo haikujibu mpaka leo.
Wafanyakazi hao wamewasiliana na kituo cha haki za binadamu , LHRC, mjini  Arusha ambapo kimewapatia msaada wa sheria ili kudai stahiki zao.
Akizungumza Wakili wa kituo cha haki za binadamu, Shirinde Ngalule, amesema Umoja wa mataifa una kinga ya kutokushitakiwa katika taasisi yeyote ile ikiwemo mahakamani.
Lakini kwa mjibu wa mkataba wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo hapa nchini Mahakama hiyo inatakiwa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia  sheria za nchi husika zikiwemo sheria ya mahusiano ya kazi.
Amesema kwa msingi huo mahakama hiyo inapaswa kuheshimu sheria na haki za binadamu, badala ya kwanyanyapaa waliokuwa watumishi wake kwa kisingizio cha cha kuwa na kinga ya kutokushitakiwa.
Amesema mahakama hiyo imekiuka taratibu katika kuwaachisha watumishi hao ambao taratibu hazikufuatwa ikiwemo kupewa notisi na badakla yake walipewa barua ya kuachishwa  kazi kitendo ambacho ni kinyume na haki za binadamu.
Ameongeza kuwa chanzo ni pale walipoanza kudai mkataba wa kazi ndipo walipoaanza kufukuzwa mmoja mmoja 

ZAIDI YA MITAMBO 30 YA UMEME JUA YATOLEWA MSAADA KWA JAMII

images 
Na Mahmoud Ahmad Arusha
ZAIDI ya mitambo ya sola 30 imetolewa kwa jamii mbalimbali yenye
 uhitaji zikiwemo Zahanati ,vituo vya afya,ofisi za watendaji kata  na
 shule mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha huduma zao
 wanazotoa kwa jamii.  Hayo yalisemwa jana na Meneja masoko wa kampuni ya Sola ya  Mobisol
 ,Seth Matemu  na  Meneja Mauzo ,Joseph Zikhali wakati wakizungumza na
 waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza ofa mpya ya msimu wa
 sikukuu kwa wateja wake .
Alisema kuwa, kampuni hiyo ya sola imekuwa ikisaidia shughuli
 mbalimbali za kijamii hususani zenye uhitaji ambapo hadi sasa hivi
 wamekwisha tumia kiasi cha shs 15 milioni kwa ajili ya kusaidia
 mitambo hiyo .
 Matemu  alisema kuwa, lengo la kuwasaidia jamii hiyo ni mojawapo ya
 malengo ya kampuni hiyo kuhakikisha kuwa inarudisha sehemu ya faida
 kwa wananchi wake kwa kugawa mitambo ya sola bure kwa wenye mahitaji.
 Alisema kuwa,kampuni hiyo ina zaidi ya wateja 20,000 kwa Tanzania
 nzima ambapo wananchi wengi  kwa sasa wana mahitaji ya umeme wa jua
 kutokana na changamoto kubwa ya umeme unaokatika kila wakati na hivyo
 kuchangia baadhi ya shughuli kusimama .
 Naye Meneja wa huduma kwa wateja kutoka kampuni hiyo, Tery Odiko
 alisema kuwa, kampuni hiyo imejiwekea mikakati zaidi ya kuhakikisha
 inafikisha huduma zake katika maeneo ya vijijini ambapo huduma za
 umeme hazijawafikia wananchi.
 Alisema kuwa,huduma hizo wanazotoa zimekuwa zikisaidia kukuza ajira
 kwa vijana kwani kwa kumiliki mitambo hiyo wana uwezo wa kuanzisha
 shughuli mbalimbali za kuwaingia kipato muda wote kama vile salon
 sehemu ya kuchajia simu  kwa kuwa na umeme wa uhakika.
 Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kununua mitambo ya sola kwa
 msimu huu wa sikukuu kwani wanatoa ofa maalumu kwa wateja wake .

WANANCHI WATAKIWA KUFANYA ZOEZI LA USAFI ENDELEVU WILAYANI TEMEKE

TM1 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(katikati)  akitoa mwongozo jana juu ya suala la kufanya usafi kwa wakuu wa idara(hawapo pichani) wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke. Wengine katika picha ni Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kushoto) na Mkurugenzi wa  Utumishi na Raslimali Watu wa TAMISEMI Bw. Mohamed Pawaga(kulia)
TM2 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba akisisitiza juu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  la usafi wa mazingira ,jana wakati alipotembelea Ofisi ya Msimamizi wa soko la Temeke Sterio lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
TM3 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(aliyetangulia) akikagua machinjio ya kuku jana katika soko la Temeke Sterio Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
TM5 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (wa pili kushoto) akimwongoza  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(katikati)  kukagua soko la Temeke Sterio lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.Zoezi hilo lilifanyika jana wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  la usafishaji wa mazingira.
TM6 
Katapila la Halmashauri la Manispaa ya Temeke likizoa uchafu jana katika soko la Temeke Sterio ikiwa ni utekelezaji agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  la usafishaji wa mazingira.
TM7T
akataka zikiwa zimezagaa mitaani baada ya kutupwa na wananchi wa Kiburugwa katika Manispaa ya Temeke.
TM9 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(kulia)  akitoa agizo kwa  Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Manispaa ya Manispaa ya Temeke Bw. Ally Hatibu ya kuondoa mara moja uchafu katika eneo la barabara ya Kiburugwa ambayo wakazi wa huko wamegeuza sehemu ya kutupa takataka.  Agizo hilo alilitoa jana wakati alipofanya ziara ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  la usafishaji wa mazingira.
 Picha zote na Beatrice Lyimo -MAELEZO
………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
 
Dar es salaam
 
Serikali imewataka wananchi wote kuwajibika katika usafishaji wa mazingira na maeneo yanayowazunguka ili kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Zuberi Samataba wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ya ukaguzi na utoaji mwongozo katika kutekeleza agizo la Rais la kutumia siku ya Uhuru kufanya usafi.
Alisema kuwa kila mwanachi anapaswa kuhakikisha mazingira anayoishi na yale yanayomzunguka yanakuwa safi wakati wote ili kupunguza mlipuko wa kipindupindu.
Samataba alisema kuwa mazingira yanayowazunguka wananchi yakiwa safi yatapunguza matumizi ya serikali yanatokana na ununuzi wa dawa za kutibu wagonjwa wa kipindupindu na hivyo fedha hizo kuelekezwa katika matumizi mengine.
“Kila mmoja akiwajibika mahali pa kazi na mazingira yanayomzunguka hali hii itasaidia kuimarishwa usafi na hivyo kila mtu anapaswa awajibike kwa uchafu anaouzalisha nyumbani kwake au sehemu ya kazi yake kwani jukumu la usafi ni la kila mtu” alisisitiza . Samataba.
Alisema kuwa kila Halmashauri nchini inapaswa kujipanga vizuri katika kuhakikisha kuwa inaondoa uchafu mitaani na kusafisha maeneo yake  ili kuondokana na tatizo la kipindupindu.
Samataba aliwaagiza viongozi wa Manispaa ya Temeke na Halmashauri nyingine nchini kusimamia suala la usafi  kuhakikisha linakuwa  endelevu kwani jukumu la usimamizi wa usafi ni la kila mtu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo alisema kuwa wananchi wa Halamashauri hiyo wamelipokea suala la utekelezaji wa agizo la Rais na wanaahidi kuhakikisha kuwa maeneo yote yanakuwa safi siku zote.
 

Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za SADC wahitimishwa jijini Dar es salaam.

MB1 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa  uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo jana. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada  ya  kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
MB2
MB3 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene (katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam. 
MB4 
Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
MB5 
Mada mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa  Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.Picha Aron Msigwa – MAELEZO.

TAARIFA YA MSIBA WA MAREHEMU WILLY CHIWANGO KUTOKA TASWA

SI_20151204_091154 
Nasikitika kuwajulisha kuwa tumepata msiba wa mwanafamilia mwenzetu na mwanataaluma wa siku nyingi katika uandishi wa habari za michezo nchini, Willie ‘Willy’ Chiwango,
Chiwango alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Massana, Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwake Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ambapo mipango ya maziko inafanyika.
Wakati wa uhai wake marehemu Chiwango alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya serikali, Daily News na Sunday News. Pia amepata kufanya kazi This Day na vyombo vingine.
Kwa wanaohitaji taarifa za msiba huu, namba za wahusika ni mtoto wa marehemu 0659-353006, kama ukimkosa hata mjane wa marehemu pia anazungumza 0652-722173.
Naomba tushirikiane na familia katika kipindi hiki kigumu. Mungu amuweke mahali pema peponi marehemu Mzee Willy Chiwango. Amina.
Ahsanteni,
Katibu Mkuu TASWA.

WAVUVI UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KUNUFAIKA NA UVUVI WENYE TIJA.

index
 Jovina Bujulu- MAELEZO.
.Dar es Salaam.
 
Wavuvi waishio ukanda wa maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Tanzania Bara na  Zanzibar  wanatarajia kunufaika na elimu ya ukuzaji viumbe kwenye maji  na teknolojia sahihi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi  kupitia mradi wa Udhibiti wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi  Kusini Magharibi  mwa Bahari  ya Hindi  (SWIOFISH).
 
Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi. Fatma Sobo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa  Udhibiti Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi, ulioanza kutekelezwa  mwezi Juni mwaka huu.
Amesema lengo la mradi huo ni kuwasaidia wavuvi wadogo wa ukanda huo ili waweze kunufaika na shughuli hiyo na kuwa na uvuvi  endelevu wenye kuongeza faida kiuchumi, kijamii na kimazingira.
 
‘Lengo la mradi huu ni kuhakikisha kuwa wavuvi wa ukanda wa Pwani wanakuwa na uvuvi endelevu na wananufaika na rasilimali za bahari kwa  kuimarisha uwezo wa Taasisi za Kikanda na Serikali” Amesema.
Ameeleza  kuwa katika kufuatilia utekelezaji wa mradi huo , Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,imeanzisha mpango  wa uongozi na usimamizi wa uvuvi ambapo wavuvi wanapatiwa elimu kuhusu aina za samaki, aina ya nyavu za kuvulia, muda wa kuvua, mauzo na uhifadhi wa samaki.
 
Ameongeza kuwa mradi huo utaimarisha mfumo wa taarifa za uvuvi  kama vile mavuno, nguvu ya uvuvi inayotumika , mauzo ya ndani na  nje  nchi yatokanayo na shughuli hizo.
 
Bi. Fatma aliongeza kuwa kipaumbele cha mradi huo kimewekwa katika uvuvi wa samaki aina ya pelagiska, Jodari, Kamba miti, samaki mwamba, pweza na ukuzaji  viumbe kwenye maji bahari ambapo eneo la majaribio litakuwa katika wilaya za Mkinga, Pangani, Tanga, Bagamoyo mjini na Lindi Vijijini.
Aidha, amesema mradi huu utatekelezwa kwa miaka 6, kuanzia 2015 hadi 2021 na umefadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo kwa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 36,000 ambapo utazihusisha wilaya 16 kutoka ukanda wa bahari ya Hindi, mkoa wa Tanga  hadi Mtwara.
 
Ameongeza kuwa mradi huo ukizishirikisha Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (Tanzania Bara), Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) na Mamlaka ya Kusimamia Bahari Kuu utakomesha uvuvi haramu wa kutumia Mabomu.
 
Taasisi zitakazotelekeza mradi huo ni Wakala wa Mafunzo ya Elimu ya Uvuvi, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Vikundi vya Ujasiriamali na Jamii za watu wa Pwani.
 

Joshua Mlelwa achomoza Tamasha la Krismasi

580577_464031296996762_1575473247_n 
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili anayeshika kasi ya muziki huo, Joshua Mllelwa ni mmoja wa  waimbaji watakaopanda kwenye jukwaa la Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mlelwa anaungana na wenzake Rose Muhando, Upendo Nkone,Kwaya ya Wakorintho Wapili (Tanzania) na Ephraim Sekeleti  wa Zambia.
Msama alisema Kamati yake inaendelea na mikakati ya maandalizi ya tamasha hilo ambalo litakuwa na dhamira ya kushukuru baada ya Tanzania kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
“Tamasha la Krismasi litakuwa pia na dhamira ya kumshuruku Mungu bada ya kupita kwenye kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kupiga magoti kwa Mungu kwa kuwasaidia katika kipindi hicho,” alisema Msama.
Msama alisema Tamasha la Krismasi litashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa Tanzania  na nchi mbalimbali kwa sababu ya tunu ya amani iliyo nayo iliyoasisiwa na Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
“Tunashukuru Mungu kwa sababu amani aliyotupa, tunaitunza vilivyo, hivyo tunapopita katika sehemu kama uchaguzi Mkuu hasa wa mwaka huu, hatuna budi kumshukuru Mungu,” alisema Msama.
Aidha Msama  alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza katika tamasha hilo ili kufikisha shukrani ya pamoja kwa Mungu.

TANZANIA YAPEWA CHETI CHA KUTOKUWA NA UGONJWA WA POLIO

index
Na Magreth Kinabo
Tanzania imetangazwa rasmi kuwa ni mojwapo ya nchi isiyokuwa na ugonjwa wa polio katika nchi za Afrika katika mkutano wa Tume ya Afrika ya kuthibitishwa kutokomezwa kwa polio(Afrika Regional Certification Commission for Polio Eradication).
Kutangazwa kulifanyika katika mkutano huo uliofanyika nchini Madagascar, Novemba 26, mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
“Hii inamaanisha kuwa kwa sasa hatuna ugonjwa wa polio tena nchini kwa sababu tumeweza kuwafikia watoto wengi zaidi kwa kuwapatia chanjo ya polio na hivyo kuongeza kinga kwenye jamii.Kutokana na mafanikio hayo, tunatakiwa bado kuendelea na kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote stahiki ili kuongeza kinga kwa jamii pamoja kuimarisha mfumo wa ufutiliaji wa mgonjwa yoyote mwenye ulemavu wa ghafla,” alisema Dkt. Mmbando.
Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba mgonjwa wa mwisho wa polio alipatikana Julai mwaka 1996 hapa nchini.
Aliongeza kuwa ufuatiliaji wa magonjwa yanayokingwa na chanjo uliimarishwa na kufikia viwango vinavyo kukubalika kimataifa na kuthibitisha kuwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 waliopata ulemavu wa ghafla wanapatikana na sampuli zao kuchukuliwa mara moja.
Hivyo kuanzia mwaka 1997 mpaka Oktoba 2015 jumla ya sampuli 6,249 za watoto waliopata ulemavu zilipelekwa kwenye maabara za kimataifa na kuthibitishwa kuwa hakuna sampuli iliyoonesha uwepo wa ugonjwa wa polio.

COSATO CHUMI AMALIZA TATIZO LA VITANDA HOSPITAL YA MAFINGA MJINI

   
Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato Chumi akimkabidhi msaada wa vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga Dk Abdul Msuya juzi
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
Baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm walihudhulia tukio hilo 
…………………………………………………………………………………..
 
TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya
akina mama na watoto
katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu
baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya
uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka
kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

Mbunge wa Mafinga Mjini
(CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina
upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko
mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata
vifaa hivyo .
  
Alisema kuwa umefika
wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni
wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya
kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.
 
“Unajua afya ni kila
kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa
wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge
mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau
mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “
alisema
Chumi aliwaomba wananchi
wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo
kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo
pekee yake.
  
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu
mbalimbali umetolewa
na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya
afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa
uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 
Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata
senti
tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa
hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia
garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika

TAHADHARI KUHUSU KUINGILIA MAWASILIANO YA WATU AU KUFUATILIA

images 
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE.
Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi.
Kwa yeyote aliyekuwa na nia hiyo ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu mwingine alihitajika kulipia fedha kiasi cha Tshs 35,000/= kupitia mitandao ya simu ili kupata namba ya siri kwa ajili ya kuwezesha nia hiyo.
Mamlaka ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa programu hiyo na ukweli kuhusu uwezo wake wa kufanya kilichodaiwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia madhara ya program hiyo na sheria inasema nini kuhusu suala hili. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini na imejiridhisha kuwa program (Application) hiyo haina uwezo huo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi kama ilivyodaiwa.
Aidha Mamlaka imebaini kuwa watengenezaji (Developers) wa programu hiyo walikuwa na nia ya kutapeli na kujipatia fedha hiyo kiasi cha Tshs 35,000/= kwa njia ya udanganyifu wakitumia kivutio cha kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu za watu binafsi.
Programu (Application) nyingine ya aina hiyo iliibuka tena ikiitwa SIMNET Tanzania ikiwa na maelezo kama ya awali.
Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Jeshi la Polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi, tunapenda kuuarifu umma wa Watanzania kuepuka kufanya mambo yafuatayo:
1. Kuvutiwa na matendo yaliyo kinyume na sheria na maadili ya matumizi mazuri ya mawasiliano kama hili la kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi. Kitendo hiki ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na kifungu cha 123 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya Mwaka 2010. Sheria katika vifungu hivyo inakataza mtu yeyote kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine. Adhabu kali ya makosa haya ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
2. Mamlaka inawatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kutokuwa wepesi na kudanganyika kufanya malipo yoyote kwa njia ya mitandao kwa huduma wasiyokuwa na uhakika nayo au bila kujiridhisha na uwepo wa huduma hiyo. Ni vizuri kutoa taarifa kwa mtoa huduma wako au kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano kupitia barua pepe malalamiko@tcra.go.tz au kupiga simu namba 0784558270/1.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
04/12/2015

KITUO CHA RADIO CHA HITS FM RADIO CHATIWA MOTO NA WATU WASIO JUULIKANA USIKU WA JUZI

HI1 
Vifaa  vyote vya kutangazia katika Studio ya Hits FM Radio vilivyoteketea kwa moto usiku wa juzi  katika studio hiyo mara baaada ya kuvamiwa na watu wasipjuulikana  huko Migombani Mjini Zanzibar
HI2 
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
HI02 
Mwandishi  wa habari akimuhoji Mkuu wa Utawala wa Afisi kuu ya CCM FM Salum Khatibu Reja alipofika katika kituo cha Radio ya Hits FM na kujionea hali ya kituo hicho.
HI3 
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
HI4 
Mwenyeki ti wa MCT Suleiman Seif katikati akifafanuwa  jambo  kwa waandishi wa habari kuhusiana  na kutiwa moto  Hits FM Radio  usiku wa juzi iliyopo Migombani Mjini Zanzibar.  

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abaas Mwinyi Atimiza Ahadi Zake kwa Kituo cha Afya Fuoni

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe A bass Ali Hassan Mwinyi, akitembelea Kituo cha Afya cha Fuoni Zanzibar kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani wakati akitimiza ahadi yake kwa kutuo hicha, akipata maelezo kutokwa kwa mdhamini wa kituo hicho Muuguzi wa Afya ya Jamii Bi Mwaka Pandu Makame akitowa maelezo ya eneo lao la kuchomea taka za kituo hicho.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassan Mwinyi akitembelea kituo hicho cha Afya Fuoni Zanzibar akiwa katika ziara yake katika jimbo lake kujiuonea ufanisi wa kituo hicho na kukabidha Madawa na kuvifanyia mategenezo vyoo vya kituo hicho ni moja ya kero za Wananchi wanaofika kituoni hapo. 
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Adass Mwinyi akitembezwa katika kituo hicho na Madaktari wa Kituo hicho, akiwa katika ziara yake ya kukamilisha ahadi yake juu ya kituo hicha kikifanyia mategenezo sehemu. 
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi akimsikiliza daktari wa kitengo cha kungolea meno katika Kituo hicho cha Fuoni Zainab Seif na Khadija Khamis, wakimueleza Mbunge huyo baadhi ya vifaa vinakosekana katika kitengo chao kwa ajili ya huduma ya kungolea meno Wananchi wanaofika kituoni hapo. Kituo hicho kinatowa huduma za Uzalishaji wa Kinamama kupiga Utra saund na huduma nyengine za matibabu 
Mbunge wa Fuoni Mhe Abass Mwinyi akizungumza wa Wafanyakazi wa Kitengo cha Meno katika Kituo cha Afya Fuoni wakati wa ziara yake kutimia ahadi alizotowa kwa Wananchi wa Jimbo hilo katika kituo hicho na kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo wanavohitaji katika kituo hicho kuondoa kero kwa Wananchi wake wanaofika kituoni hapo kupata huduma ya meno na nyeginezo.
Mhe Abass Mwinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya kituo hicho, Kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo lake na Wananchi wa jirani.ili kuboresha ufanisi wa huduma ya Afya kituoni hapo.    
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe. Abass Mwinyi akizungumza na wafanyakazi wa Kituo hicho na Wananchi wa Jimbo lake wakati wa ziara yake ya kwanza katika jimbo hilo na kukabidhi vifaa na Madawa kwa kituo hicho. Mhe Mbunge Abass amesema sasa Hapa Kazi Tu, ili kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo lake na kuondoa kero zote katika jimbo hilo na kuwa Jimbo la mfano katika majimbo yote ya Zanzibar. 
Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya Fuoni Said Fadhili Abass akizungumza wakati wa mkutano huo na Mbunge wa Jimbo la fuoni na kumshukuru kwa msaada wake huo kwa Kituo chao. na kusema dawa hizo zitatumika kwa wananchi wa Jimbo hilo wanaofika kituoni hapa kupata huduma mbalimbali za Afya.  
Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi fedha shilingi milioni moja Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya kutatua makero zinazokikabili kituo hicho cha Afya Fuoni ili kufanya kazi zao kwa kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi vifaa kwa akili ya vyoo vya kituo hicho Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass na kulia Muuguzi wa Afya ya Jamii Kituoni hapo Mwaka Pandu Makame. 
Mzee wa Jimbo la Fuoni Mzee Takrima akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi madawa na vifaa katika Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Fuoni wakimsikiliza Mbunge wao. 
Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Imetayarishwa na othmanmapara.Blogspot 
Zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com.
Mobile 0777424152 or 0715424152.

MRATIBU UN ARIDHISHWA NA MATUMIZI YA UFADHILI TABORA

IMG_5447 
Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora. Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya kuelekea kukagua miradi hiyo.
Na Modewji blog team, Tabora
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.
Miradi hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.
Katika ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga vita umaskini na kutunza mazingira.
Ziara ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni moja ya ziara yake ndefu ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.
Alipotoka Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.
Bwawa hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.
Akizungumzia bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas, akizungumza alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.
IMG_5482 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa pili kushoto) walipowasili kukagua mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja kwa mtindo wa utoaji wa chakula kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya Miyombo. Kushoto ni Ofisa Tawala msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Tija wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Dkt. Phillips Mtiba pamoja na Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (wa pili kulia).
Aidha imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka mzima.
Imeelezwa kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja na urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula na Njegere kilo tatu.
Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.
Awali wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.
Aidha imeelezwa kuwa baadae wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.
Aidha alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.
Kikundi hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30 kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.
Alisema ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara, ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi kwa Karanga na Asali.
Akisoma risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.
IMG_5486
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea kupata maelezo ya mradi huo.
Aidha amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.
Aidha ametaka umoja huo kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.
Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).
Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.
Naye Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk. Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye mikutano na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa huo.
Alisema pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya mazingira.
Pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa chakula na hifadhi ya misitu.
IMG_5494
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.
“ Nashukuru sana kwa msaada tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk. Phillips.
Alisema ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.
IMG_5496 
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
Alisema suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.
Aidha alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa chakula.
Alishukuru UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.
Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.
IMG_5520 
Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.
IMG_5532 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nguvumoja watakaonufaika na mradi wa bwawa hilo.
IMG_5538#
HapaKaziTu; ndio maneno aliyokuwa akiyasema Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akichimbia sehemu ya bwawa hilo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
IMG_5540 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akichimba udongo na sururu huku Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akijaza udongo unaochimbwa kwenye ndoo.
IMG_5553#
HapaKaziTu; Wanakijiji pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishangilia kwa pamoja huku wakiunga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya #HapaKaziTu sambamba na mabango 17 ya malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) walioyowafikia wanakijiji wa Nguvumoja. Kwa matukio zaidi bofya link hii
IMG_5583

Uzinduzi wa mtandao wa intaneti ya kasi zaidi wa Tigo 4g LTE mkoani Morogoro wafana

 
Mtoa huduma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Neema Mashingia akimsaidia mteja kuhama kutoka huduma ya 3G kwenda huduma ya 4G wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya 4G LTE uliofanyika jana mjini Morogoro

 Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe akiongea na Mtaalam wa mitandao ya kijamii wa Tigo bi Samira Baamar wakati akijiandaa kutoa zawadi za washindi wa bahati nasibu, wengine ni binti wa mkuu wa mkoa, Afisa maendeleo ya masoko Shavkat Berdiev (kulia) na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Mashariki Goodluck Charles.

Wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakisikiliza kwa mageni hotuba zilizokuwa zikitolewa.

Mgeni rasmi, mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe akisalimiana na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Mashariki Goodluck Charles, katikati ni Afisa wa maendeleo ya masoko Shavkat Berdiev.

 Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Suleiman Bushagama (Kushoto) Mutalemwa (katikati) na Ben Mponzi (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.

 Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Suleiman Bushagama (Kushoto) Mutalemwa (katikati) na Ben Mponzi (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.


MANISPAA YA KIONONDONI NA USAFI WA MAZINGIRA

ki1 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Injinia, Musa Natty akieleza jambo wakati wa mkutano na wadau wa usafi wa mazingira kuhusu mkakati wa kufanya usafi katika Manispaa hiyo kufuatia agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo siku ya sikuu ya Uhuru, inayoadhimishwa kila Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani .
ki2 
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano wa mkakati wa usafi (hawapo katika picha) namna ya kushirikiana katika kuhakikisha mazingira ya jiji la Dar es Salaam yanakuwa safi na salama ili kuepukana na magonjwa ambukizi ikiwemo kipindupindu katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi , kulia kwake ni Katibu Tawala Afya Daktari.Grace Magembe.
ki3 
Wajumbe wa mkutano wa usafi ambao pia ni wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za kifedha, Mazingira,Jeshi la Magereza,Wanamazingira,Vikundi vya Usafi na Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 mwaka huu kuwa siku ya kufanya usafi .
Wajumbe wa mkutano wa usafi ambao pia ni wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za kifedha, Mazingira,Jeshi la Magereza,Wanamazingira,Vikundi vya Usafi na Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 mwaka huu kuwa siku ya kufanya usafi .
ki5 
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akikagua Soko la Magomeni lilipo Manispaa ya Kinondoni wakati ziara ya kuangalia hali ya usafi ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty.
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiongea na wachuuzi wa Soko la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi katika soko hilo.
ki7 
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali kutoka Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi ya soko la magomeni kandokando ni sehemu ya kukusanyia taka za soko hilo na baadaye huchukuliwa na gari maalum la kubebea taka kwa ajili ya kupelekwa dampo kuu.
ki8 
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali kutoka Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi ya soko la magomeni kandokando ni sehemu ya kukusanyia taka za soko hilo na baadaye huchukuliwa na gari maalum la kubebea taka kwa ajili ya kupelekwa dampo kuu.
ki9 
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani(Kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Soko la Tandale Mohamed Mwikya(Kushoto) wakati wa ziara ya kukagua hali ya usafi wa soko hilo
ki10 
Gari la Kuzoa taka kutoka katika Manispaa ya Kinondoni likiwa limebeba taka kutoka Soko la Tandale tayari kwenda kuzihifadhi katika dampo kuu, Manispaa hiyo imekuwa ikihakikisha hali ya usafi katika masoko yake kwa kupeleka magari ya kuzoa taka kila siku ili kuepukana na magonjwa ambukizi ikiwemo kipindupindu.
ki12 
Sehemu ya Soko lilipo kwenye kituo cha Daladala cha Simu 2000 eneo la Sinza kikiwa katika hali nzuri ya usafi huku uongozi wa eneo hilo wakiendelea kuisimamia hali hiyo kama ambavyo ilivyoagizwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuwa siku ya sherehe ya Uhuru ambayo huadhimishwa kila Desemba 9, mwezi wa 12 kuwa ni siku ya usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa amukizi kikiwemo kipindupindu.
ki13 
Sehemu ya Daraja la Tegeta Manispaa ya Kinondoni ikiwa imegeuzwa Dampo na wakazi wa eneo hilo kwa ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani aliagiza uchafu huo kutolewa haraka kwa kuwa inahatarisha hali ya afya kwa wakazi wa maeneo hayo .
(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

No comments :

Post a Comment