Wednesday, December 2, 2015

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mashine za MRI, CT-SCAN Hazitakwama Tena

muh1

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria kufungualiwa kwa  duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  wa MNH, Profesa Lawrence Mseru.
Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
muh2 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akipewa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu kufungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
muh3 muh4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua duka la dawa linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).  Duka hilo limefunguliwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
muh5 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa duka la dawa la MSD.
muh6 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hospitali hiyo baada ya kufunguliwa kwa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) leo jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………
Serikali imewahakikishia Watanzania kwamba mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) pamoja na Computerized  Tomography Scan (CT-SCAN) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  hazitakwama kufanya kazi kwa kuwa imeweka utaratibu mzuri wa kuzitengeneza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando amesema serikali imezungumza na Philips na wamekubaliana kwamba mashine hizo hazitakwama na endapo litatokea tatizo la kiufundi watashughulikia mara moja.
“Mwaka ujao ni mwaka wa bajeti  serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza mashine za CT-SCAN na MRI,  lakini mtambue kwamba si tu mashine hizo zinapaswa kutengenezwa bali na mashine nyingine.”amesema Dk Mmbando.
Pia, Dk Mmbando  amefungua duka la dawa  la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kueleza kwamba kufunguliwa kwa duka hilo kutasaidia wananchi kupata huduma haraka na kununua dawa kwa gharama nafuu  na huduma hiyo itatolewa kwa saa 24.
Akifafanua  kuhusu mashine za MRI na CT-Scan, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Mseru amesema Novemba 25, 2015  alifika fundi kutoka Afrika Kusini ambaye pia ni fundi wa MRI na kuitengeneza na kuanza kufanya kazi tangu Novemba 26 mpaka Disemba 2, mwaka huu. Wagonjwa 152   wamepimwa na kwamba wengi wagonjwa wa dharura.
Amesema hivi sasa mafundi wanafunga mashine ya Digital X-Ray iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo  usimikaji unatarajiwa  kukamilika mwishoni mwa juma hili.
Akielezea utekelezaji wa agizo la wagonjwa wanaolala chini kupatiwa vitanda, Profesa Mseru amesema ili kuondoa wagonjwa wote waliolala chini, serikali kupitia MSD ilileta vitanda 300 pamoja na magodoro yake, vitanda hivyo vyote vilipelekwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na tayari MOI imeanza kuhamisha wagonjwa waliokuwa wamelala chini kutoka wodi za MNH walizokuwa wanazitumia, mpaka sasa wagonjwa 120 wamehamishwa.
Novemba 9, mwaka  huu Rais John Magufuli alifanya ziara MNH na kutoa maagizo kwamba ndani ya wiki mbili mashine ya MRI na CT-SCAN ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi, wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda  na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ifungue duka la dawa ndani ya hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa.

RC Makalla atembelea kiwanda cha sukari TPC

RC Makalla
atembelea kiwanda cha sukari TPC, akerwa na sukari inayoingia kwa wingi kutoka
nje
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla akiwa kwenye ukaguzi wa kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani humo, kama sehemu ya kuangalia hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. Picha na Mpigapicha wetu.
Na Mwandishi
Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa
Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara katika kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo
Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kujionea hali ya uzalishaji wa sukari kwenye
kiwanda hicho.
RC Makalla
alijionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho sasa kinazalisha sukari tani
105,000 baada ya kubinafsishwa, tofauti na uzalishaji wa tani 35,000 tu hapo
zamani.
Ziara inaendelea kiwandani hapo.
Akizungumza katika kiwanda hicho, RC Makalla alisema kwamba amefurahishwa na hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho, huku akiahidi kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje ya nchi. Alisema atashirikiana na serikali ya Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari hiyo ya nje, akiamini kuwa kutasababisha kiwanda hicho kupiga hatua kwa kuuza sukari yao nchini.
Majadiliano yanaendelea kiwandani hapo dhidi ya RC Makalla
“Kilio cha kiwanda hiki ni uingizwaji wa sukari kutoka nje, hivyo Kilimanjaro tutashirikiana kwa karibu na wenzetu wa Tanga ili kuweka ulinzi mkali kwa ajili ya kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje kwa kupitia mkoani Tanga.
“Naamini tukifanya hivyo tutaweza kukiweka kiwanda hiki katika hali nzuri, ukizingatia kuwa viwanda vyetu ili viweze kujiendesha vinapaswa kuuza bidhaa zao vizuri na si kupata changamoto zinazoweza kuwaathiri kama suala hili la sukari nyingi kuingia kutoka nje wakati wao pia ni wazalishaji,” alisema Makalla.
Kwa wiki kadhaa sasa RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani Kilimanjaro pamoja na kufanya vikao muhimu vyenye lengo la kuhakikisha kwamba wanaenda mchaka mchaka ili kwenda sambamba na kauli ya hapa kazi ya Dr John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MELI MPYA YA MV. MAPINDUZI II YAWASILI BANDARI KUU YA ZANZIBAR

me01 
Meli mpya ya  MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
me1 
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizaza ya Miundombinu waliofika Bandari Kuu ya Zanzibar kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikitokea Korea kusini.
me3 
Sehemu ya ndani ya Meli ya MV. MAPINDUZI II itakayotumika kwa ajili ya mapumziko kwa   abiria  watakao safari.
me4 
Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya matumizi ya gharama zilizotumika mara baada  ya kuwasili kwa Meli ya MV. MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.
me5 
Meli ya MV MAPINDUZI II yatia nanga Bandari kuu ya Zanzibar ikitokea Korea Kusini. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………..
Na Maryam Kidiko Maelezo Zanzibar
Meli mpya ya mv.mapinduzi ( ii) imewasili bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuanza safari zake baada ya kukamilika ujenzi wake huko Korea ya kusini.
Hafla ya kuwasili kwa meli hiyo imeongozwa na waziri wa fedha Omar Yussuf Mzee ambapo amesema ujenzi wa meli hiyo ni agizo la raisi wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali mohamed  shein.
Amesema meli hiyo bado iko katika mikono ya wajenzi hadi sasa na inatarajiwa kuzinduliwa rasmin wiki ijayo na rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Waziri mzee amesema meli hiyo inavifaa vya kutosha kama vile life jacket, pamoja na boti ndogo ili kuweka usalama kwa abiria wataosafiri katika meli hiyo.
Hata hivyo amesema meli hiyo itasafiri Pemba pamoja na Dar es-salaam hivyo amewataka wananchi kuitunza meli hiyo kwani ni matunda yao.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Miundo mbinu na mawasiliano zanizar Dk. Juma Malik amesema lengo kulifanya shirika la meli lifanye kazi kibiashara ili kuongeza pato la taifa.
Amewaomba wananchi kuitunza na kuitumia vizuri meli hiyo kwani wamefanya kazi kubwa na kutumia gharama hadi kufikia kukamilika kwa meli hiyo.
Sambamba na hayo amesema meli hiyo ina uwezo wa kupakia abiria wasiopunguwa 1,200 pamoja na tani za mizigo 200.
Meli hiyo mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola Mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18.

NHIF YAZINDUA KITUO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA SIMU ZA MKONONI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz na mawasiliano kwa njia ya mtandao (Mitandao ya kijamii na simu za mkononi), uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.Picha na Michuzi Blog
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ya NHIF, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akionyesha kipeperushi chenye namba ya mawasiliano ya moja kwa moja na kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SoftNet Tech, Nuru Yakub Othman wakishirikiana kuzindua rasmi Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kushoto) akimuangalia Ofisa Uanachama wa Kituo cha Mawasiliani ya Huduma kwa wateja, Eva Mkwizu wakati akiwasiliana na wateja wa njia ya simu. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba
Baadhi ya Maofisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiendelea kutoa huduma katika kituo hicho.
sab1 
Mmoja wa Maofisa wa mfuko huo Sabina akiendelea na kazi yake.

MASTAA KIBAO NDANI YA FILAMU YA HOMECOMING, KUTINGA CINEMA KISHA SOKONI MWEZI HUU

Mwongozaji mahiri wa filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, Seko Shamte. Filamu
hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa
kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi
na jamii kwa ujumla.
Crew nzima pamoja na baadhi ya waigizaji
 Moja kati ya kamera kali zilizotumika
Kazi ikiendelea location
Na Mwandishi Wetu
WASANII mahiri wameshiriki kwenye filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni akiwamo Daniel Kijo, Mzee Chilo pamoja na mastaa wengine.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.

Kijo ambae anafahamika zaidi katika tasnia ya habari aliwahi kutangaza kwenye kipindi cha Daladala kinachorushwa na Star Tv, katika filamu hii ameigiza kama mhusika mkuu akitumia jina la Abel Mshindi.
Mzee Chilo ambae jina lake halisi ni Ahmed Olotu ameigiza kama mzazi wa Kijo ambae amekuwa akiishi kijijini miaka yote huku Mzee mwigizaji mwengine mahiri nchini Hashim Kambi ameigiza kama Mjomba wa Kijo.

Filamu inaanza kwa kumuonesha Kijo akitokea Marekani ambapo alisomea masuala ya fedha na kisha kurejea nchini na kuajiliwa katika kazi ya benki, kwa muda wote akiwa nchini amekuwa akiishi na mjomba wake ambae ni Kambi huku baba yake (mzee chilo) akiwa anaishi kijijini.

Kijo alijikuta akiingia katika janga la rushwa kutokana na kushawishiwa na shida za baba yake huyo aliekuwa akimtegemea kwa kila kitu huku pia kukiwa na mwanamke ambae nae alikuwa akitaka mahitaji.
Kutokana na changamoto za kimaisha Kijo alijiingiza katika janga la rushjwa na kujikuta akikamatwa na kufungwa.
Wengine katika filamu hiyo ni Susan Lewis maarufu kama Natasha, Uncle Mshindi, maarufu kama Hashim Kambi pamoja na Abby Plaatjes aliewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Afrika.

Pia wapo akina Alpha Mbwana, Magdalena Munisi, Godliver Gordian, Michael Kauffmann na itaanza kuoneshwa kwenye kumbi ya cinema kabla ya kuingia rasmi sokoni. zaidi tembelea www.homecomingtz.com

NAPE ATEMBELEA GAZETI LA RAIA TANZANIA

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa gazeti la Raia Tanzania na Raia Mwema katia ofisi za magazeti hayo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa kikao na wahariri wa magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza huku Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akimsikiliza kwa makini.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni ya Magazeti ya Raia Mwema.
…………………………………………………………………………..
KATIBU wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ametembelea ofisi za kampuni ya Raia Mwema inayotengeneza magazeti ya Raia Mwema
na Raia Tanzania, kwa lengo la kushukuru na kueleza mikakati ya chama chake
.
Itakumbukwa miezi kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu
Nape, alitembelea vyumba vya habari akianzia na Raia Mwema kueleza pamoja na
mambo mengine namna walivyojipanga na uchaguzi ikiwemo kupata mgombea urais. Akizungumza jana katika ofisi hizo alipokutana na wahariri
pamoja na viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo alisema, wanafurahishwa na kasi
ya Rais John Magufuli, kwa sababu kinachotendeka sasa walikipanga hata kabla ya
uchaguzi.
“Tulitaka mtu wa aina hii, haya mabadiliko tuliyarataji
hivyo hatushituki kuyaona, tunachotaka kuwaambia wananchi tu ni kuwa baada ya
kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama,” alisema Nape.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MODEWJI FOUNDATION YASAIDIA UJENZI WA MADARASA KITUO CHA MAFUNZO CHA FURAHINI.

Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo cha Furahini kilichopo Kisangara wilayani Mwanga,Isack Msuya akimuongoza Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation iliyoanzishwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji,Francesca Tettamanzi kutembelea eneo kilipojengwa kituo hicho.
Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akiwa ameambata na wafanyakazo wa kampuni ya METL  walipotembelea kituo cha mafunzo cha Furahini cha wilayani Mwanga.
Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akitembelea majengo hayo yaliyojengwa kwa msaada wa Modewji Foundation.
Majengo ya Madarasa katika kituo cha elimu cha Furahini cha wilayani Mwanga yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Mohamed Enterprises .

WACHINA WAONYESHA UTAMADUNI WAO TANZANIA

ci1 
Kikundi cha wanamuziki kutoka China kikitumbuhiza wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa China hapa nchini.
ci2 
Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Di Yang akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci3 
Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Yang Jing akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci4 
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China. Kundi hilo linaundwa na wanazuoni na watafiti wa muziki wa asili nchini China.
Picha na Frank Shija, WHVUM
…………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho
Maonesho ya utamaduni wa watu wa China yalifanyika jana usiku maeneo ya Makumbusho ya TaifaJijini Dar es salaam baada ya ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China uliofanyika mchana.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa kituo hicho cha Utamaduni wa watu wa ChinaTanzania Bwana GAO Wei ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni waalikwakuangalia utamaduni wa wachina kupitia muziki wao.
Hafla hiyo ilipambwa na wanamuziki mahiri wa kundi la watafiti wa muziki wa asili linaloitwa Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China kilichopo Beijing.
Wanamuziki hao walianza kwa kupiga vyombo vyao vya muziki kwa pamoja bila kuimbachochote na baadae kila mmoja wa wanamuziki hao alipiga chombo kimoja cha muziki ilikuwaonyesha wageni waalikwa sauti na mdundo wa kila chombo cha muziki.
Mwishoni walipiga vyombo vyao kwa pamoja kwa kupiga mapigo ya wimbo wenye asili yakitanzania unaoitwa ‘Malaika Nakupenda’.
Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania ndio kituo cha kwanza kufunguliwa kwa Afrika Mashariki. Kimefunguliwa rasmi jana saa nne kamili asubuhi.Kituo hicho kipo Barabara ya Hassan Mwinyi maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ndugai akutana na Mkurugenzi mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute).

ga1 
Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembea Ofisini kwake Dar es Salaam leo kuelezea mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
ga2 
Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake. Bi. Namusisi alimtembea Mhe. Ndugai Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
ga3 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
ga4 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi (kulia kwake)alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.  Wengine katika picha ni maafisa kutoka taasisi hiyo.
Picha na Hassan Silayo, Idara ya Habari Maelezo.

No comments :

Post a Comment