Thursday, December 3, 2015

Dk JOHN MAGUFULI atoa Siku 7 kwa Wakwepa Kodi Nchini

Shock as Tanzanian President Cancels Independence Day Pomp
Download

Tanzania yasaini mkataba wa kuboresha huduma ya afya

images 
Na Jacquiline Mrisho na Nyakongo Manyama -MAELEZO
…………………………………………………………………………………………..
Serikali ya Tanzania imesaini mikataba miwili na Serikali ya Uswisi ili kuendeleza na kuimarisha huduma za kijamii nchini hasa katika Sekta ya Afya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salam Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa kupitia ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, Serikali ya Uswisi inaendelea kusaidia kuboresha Sekta ya Afya nchini hususani kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
“Uswisi imesaidia Sekta ya Afya kwa miaka 15 na mpaka sasa imeshachangia jumla ya shilingi billion 181.7 kuanzia miradi ya afya ianzishwe nchini” alisema Likwelile.
Aidha, Dkt. Likwelile aliongeza kuwa Serikali ya Uswisi imelenga pia kusaidia kuimarisha utoaji wa huduma katika idara ya Afya katika Serikali za Mitaa kwa kuzingatia usawa na ubora wa huduma hizo hasa kwa wanawake,watoto pamoja na makundi yaliyotengwa hasa maeneo ya vijijini.
Zaidi ya hayo, Dkt. Likwelile amesema kuwa Serikali ya Uswisi itarajia kuungana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha sera za malipo kwa wafanyakazi wa Afya ili watoe huduma bora yenye tija kwa jamii.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli amesema kuwa amefurahishwa na utoaji bora wa huduma za Afya Nchini Tanzania ambazo zimekuwa zenye tija kwa wananchi wanapokuwa wanahitaji huduma hizo kwa wakati.
Bi. Florence aliongeza kuwa Serikali ya Uswisi kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya mkoa wa Dodoma umekuwa wa kwanza kunufaika na mfuko huo ambapo mikoa mingine inayotarajiwa kunufaika ni pamoja na Morogoro na Shinyanga ili kuboresha afya ya wanawake, watoto, vijana wazee na watu wasiojiweza.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Donan Mmbando alisema kuwa lengo la fedha hizo ni kuhakikisha huduma za Afya zinawafikia watu wote wenye mahitaji hayo kwa wakati.
“Mchango huo wa fedha umechangia sana katika kutekeleza malengo ya Millenia kwa kupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 4 kwa mwaka 2013 kwa kuboresha utoaji wa chanjo kwa watoto na tiba sahihi ya ugonjwa wa Malaria kwa kiasi kikubwa”. Alisema Dkt. Mmbando
Pia Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Jumanne Sagini amesema kuwa ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa msaada walioupata na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumiwa katika kuboresha zaidi huduma ya Afya katika Mikoa iliyoongezwa kuanzia ngazi za Wilaya.
Mfuko wa pamoja wa Afya ulianzishwa nchini kwa lengo la kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa kushirikiana na Serikali ya Uswisi pamoja na nchi zingine zilizoendelea ikiwemo Canada, Denmaki na washirika wengine wa maendeleo.

Rais Dkt. Magufuli aeleza mikakati ya kuboresha mazingira ya biashara

  husna-TWENDE 
Jacquiline Mrisho
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Tanzania inatekeleza mikakati ya kuweka mazingira bora ili sekta isiyo rasmiiweze kuchangia vizuri katika maendeleo ya Taifa.
Mhe. Magufuli aliyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya Wajasiriamali ya Juakali/Nguvu Kazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akifungua kwa niaba ya Rais, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiki alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweka mpango maalumu wa kurasimisha shughuli za Sekta isiyo rasmi (MKURABITA).
Alisema mpango hu unatoa fursa ya mikopo nafuu kuwawezesha wajasiriamali na kuwapa elimuya namna bora ya kufungasha bidhaa zinazozalishwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiki maonesho hayo yameshirikisha wajasiriamali zaidi ya 700 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pia maonesho hayo wamehudhuriwa na Mabalozi kutoka nchi wanachama, Makatibu Wakuu,Wakurugenzi, Wenyeviti wa Wajasiriamali hao kutoka Nchi wanachama.
Maonesho hayo pia yameshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za Fedha,Taasisi ya Mifuko ya Jamii na Mamlaka ya usajili (BRELA).
Kabla ya kufungua maonesho hayo, Mheshimiwa Said Meck Sadiki alitembelea baadhi ya mabanda ili kuona kazi za wajasiriamali hao.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajasiriamali Wasiorasimishwa Afrika Mashariki, Josephat Rweyemamu alisema madhumuni ya maonesho hayo ikiwemo kuwawezesha wajasiriamali kupanua masoko ya bidhaa zao pamoja na changamoto wanazozipata wajasiriamali hao.
Alieleza baadhi ya changamoto kuwa ni ukubwa wa kodi, pia aliiomba Serikali kufungua kiwanda cha Urafiki ili kuwasaidia wajasiriamali pia kuwatengea maeneo maalum kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Joyce Mapunjo alieleza kufurahishwa na bidhaa za wajasiriamali.
“Nimefurahishwa sana na bidhaa mbalimbali toka kwa wajasiriamali wa Afrika Mashariki na Serikali zetu za Afrika Mashariki zinatambua mchango wa Sekta isiyo rasmi na ndio mana tukawa na maonesho haya”.alisema Mhe. Dkt. Mapunjo.
Hata hivyo, alisema pamoja na mafanikio hayo, Serikali za nchi wanachama zinatambua kwamba Sekta isiyo rasmi inakabiliwa na vikwazo na changamoto nyingi ambazo zinadumaza maendeleo ya Sekta hii isiweze kukuwa na kuwa Sekta rasmi.
Rais John Pombe Magufuli amewahakikishia wajasiriamali wa Tanzania kuwa wameshayajadili na kwasasa wanayafanyia kazi.
“Kuna hatua ambayo Serikali ya Tanzania inatekeleza katika kuweka mazingira bora ili Sekta isiyo rasmi iweze kuchangia vizuri katika maendeleo ya Taifa letu” aliongeza.
Maonesho hayo yalianzishwa tangu mwaka 1999 na hufanyika katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mzunguko.
Kwa Tanzania haya ni maonesho ya Tano kufanyika na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Nunua bidhaa zilizozalishwa na Afrika Mashariki ili kukuza uchumi wa Afrika Mashariki”

No comments :

Post a Comment