Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akihutubia
Bunge la Jamhuri kama ishara ya kuzindua Bunge la 11. mjini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na: Immaculate Makilika, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli amezindua Bunge la 11 leo mjini Dodoma na kusema
anakusudia kuunda Mahakama ya rushwa na ufisadi ili kusaidia kutatua
kero hiyo ambayo imeonekana kukera wananchi wengi.
Rais Magufuli amezindua Bunge hilo kwa mujibu wa Ibara ya 97, Ibara ndogo ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Rais Magufuli amesema, “wananchi wamekua wakilalamika sana juu ya rushwa na ufisadi unaondelea nchini kwa kusababisha wananchi kutopata haki zao na kutatuliwa shida zao kwa wakati, kati ya mambo ninayokusudia kuyashughulikia ni pamoja na kuunda Mahakama rushwa na mafisadi.”
Kwa mujibu wa Rais Magufuli maeneo mengine ambayo wananchi wameyalalamikia ni pamoja na matatizo ya upatikanaji wa maji, migogoro ya ardhi, mgogoro ya mipaka kati ya vijiji na hifadhi za taifa, huduma za afya ,madini, kilimo, reli, elimu, ajira, haki za wazee, na maslahi ya wafanyakazi na wasanii.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaondoa urasimu katika uwekezaji na kutowavumilia wale wote watakaokwamisha nia za wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.
Aidha, Dkt Magufuli ameeleza kuwa awamu hii ya Tano, itaweka msisitizo katika ujenzi wa viwanda ambavyo vitazalisha mahitaji ya watu (mass consumption) na kusema kuwa “waliobinafsishiwa viwanda waanzae kazi mara moja ,Serikali yangu haitawavumilia.”
“Tutatatua kero za wananchi, na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuimarisha Muungano. Muungano wetu ndio umoja wetu”.
Kwa mujibu wa Rais huyo wa awamu ya Tano, yatakayoshughulikia ni pamoja na mchakato wa Katiba, Upanuzi wa barabara, reli na masuala ya uchumi.
Rais Magufuli anakua Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 1961 baada kuibuka mshindi kwa zaidi ya asilimia 50 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015.

No comments :
Post a Comment