Baadhi ya wanachama na wadau wengine
wa sekta ya hifadhi ya jamii walioshiriki mkutano wa mkutano mkuu wa mwaka wa
wanachama na wadau
Mojawapo ya wajibu wa mifuko
ya pensheni ya hifadhi ya jamii ni kuhakikisha ya kuwa inawashirikisha wadau
wake wote wakuu hasa waajiri, wanachama na familia zao pamoja na serikali
ambaye ndiye mdhamini wa mifuko ambapo makundi haya matatu ndiyo yanaunda kitu
kinachoitwa utatu.
Wananchi lazima wajue na watambue
kuwa wawekezaji wa mifuko hii ni waajiri na wafanyakazi hasa pale
wanapojiandikisha na kuwa wanachama wachangiaji kwa kukatwa asilimia fulani
kutoka katika mishahara yao na mwajiri na yeye kuchangia kiasi hicho hicho au
zaidi kwa ajili ya mfanyakazi wake kwa makubaliano ya mkataba wa kupata huduma
mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii.
Hivyo uwakilishi wao lazima
uwemo ndani ya utawala wa mifuko hii mara kwa mara kwa vitendo. Vile vile
inatambulika ya kuwa hata serikali ina kazi kubwa juu ya mifuko hii ya hifadhi
ya jamii hasa zaidi kwa kuangalia na
kusimamia kiwango cha kinga juu ya majanga wanayokumbana nayo jamii yetu hapa
nchini pamoja na kuangalia mchango wa mifuko hii kwa upande wa uchumi wa nchi
yetu na serikali kama mdhamini mkuu wa
mifuko hii. Serikali kuwa mdhamini hii ina maana ya kuwa mfuko wowote
ukifirisika serikali ndiyo itayowajibika kuwalipa wanachama wa mfuko huo
michango na pensheni zao na madeni mengineyo bila kuteteleka.
Hapa mara nyingi kinachoshindikana
ni utekelezaji kwa vitendo ingawa utaratibu na kanuni zote za uhusiano wa utatu
uliopo kati ya mwajiri, mfanyakazi na serikali na jinsi ya kuwashirikisha
umewekwa. Huenda ugumu unaokuja ni jinsi ya kupata taasisi na au mtu sahihi
ambaye anaweza kuwa mwakilishi wa kutosha wa wachangiaji, wategemezi pamoja na
wadau wengine wa mifuko.
Mfuko wa hifadhi ya jamii
unaweza kuwa na wanachama wengi na kukawa na taasisi nyingi zinazowakilisha
waajiri na wafanyakazi wakati baadhi ya wanachama wengine wakawa hawana mtu
yeyote wa kuwakilisha mambo yao. Lakini kwa upande mwingine mfuko unaweza kuwa
na wigo mdogo wa wanachama na idadi kubwa ya wanachama hao hao wakawa na uelewo
mdogo wa dhana ya hifadhi ya jamii pamoja na kutojua hata utawala wa vitendo wa
mfuko na wakawa hata umoja wao wa wafanyakazi kuwa mdogo kiasi cha kwamba ukawa
hata uwakilishi wao kutokuwa na nguvu yeyote .
Hivyo kuna haja ya kuangalia
hata mgawanyo wa majukumu kati ya serikali na bodi, mgawanyo wa majukumu kati
ya bodi na wawakilishi na mwisho mgawayo
wa majukumu kati ya bodi na mkurugenzi mkuu. Hii mara nyingi mambo mengi
yanakuja kuingiliwa na hali ya kiasi iliyopo nchini. Kwa sababu unakuta
mkurungezi mkuu wa mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii anateuliwa na rais wa
nchi.
Na kwa upande mwingine
wajumbe wa bodi kuchanguliwa wa wizara mama, mfano mfuko wa pensheni wa (PSPF),
mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) na mfuko wa pensheni wa (PPF) yote ipo chini
ya wizara ya fedha, Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) wenyewe upo chini
ya wizara ya kazi na ajira, wakati Mfuko wa pensheni wa (LAPF) wizara ya
serikali za mitaa, wakati mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) wenyewe upo
chini ya wizara ya afya. wizara, ingawa kwa sasa mifuko yote inasimamiwa na
mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA).
Mamlaka ya usimamizi na
udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii iliundwa kwa sheria Na 8 ya hifadhi ya
jamii ya mwaka 2008 kwa lengo la kusimamia na kudhibiti sekta ya hifadhi ya
jamii kwa manufaa ya wanachama na kwa taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi
rasmi mwaka 2010.
Kwa hiyo wawakilishi wote wa
bodi mara nyingi idadi yao kubwa ya
wawakilishi wanatoka serikalini, na mara nyingi katiba za mifuko zinaeleza wazi
sifa za hao wajumbe wa bodi au bodi ya wadhamini ambazo hata kidogo hazifuatwi
badala yake kuchaguliwa kwa kujuana na matokeo yake anaishia kumsikiliza
mkurugenzi mkuu bila kuhoji chochote kwa muda wote wa miaka mitatu na mwaka wa
mwisho wa mkataba huenda ndipo anapoweza kuanza kuelewa baadhi za taarifa za mahesabu
lakini mwanzoni anaishia kuitikia kwa sababu ya kutokuwa na upewa wa kutosha
juu ya mambo ya hifadhi ya jamii.
Kwa hiyo mzigo wote wa
mifuko ya hifadhi ya jamii unabaki kuwa chini ya serikali yenyewe kwa sababu
utawala na usimamizi wote wa mifuko hii upo chini ya usimamizi na uthibiti wa
chombo cha serikali hivyo hata kesho mfuko wowote ukafilisika atayebeba mzigo
wa kulipa mafao au pensheni na na madeni
itakuwa serikali yenyewe kama mdhamini wa mifuko yote hapa nchini lakini
unaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa kwa sababu bajeti yote ya maendeleo ya
kuboresha elimu, afya, maji na mikakati yote ya kupunguza umasikini itakuwa
imeingiliwa kwa kupunguza huduma hizo kwa sababu ya kutofuata utaratibu wa
uendeshaji wa mifuko.
No comments :
Post a Comment