Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Zuma Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob (kushoto) na Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Philipe Nyusi (katikati)
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha SWAPO cha Namibia Rais Hage Gengob, katika
mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa vya Kusini mwa Afrika mjini Maputo, Msumbiji.


Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Makatibu Wakuu wa vyama
vya ANC, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU PF mjini Maputo.
…………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Komredi Abdulrahman Kinana katikati ya wiki iliyopita aliongoza
ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa Kusini
Mwa Afrika.
Mapinduzi (CCM) Komredi Abdulrahman Kinana katikati ya wiki iliyopita aliongoza
ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa Kusini
Mwa Afrika.
Mkutano huo uliohudhuriwa
na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama hivyo, umemalizika mwishoni mwa wiki mjini
Maputo kwa mafanikio makubwa.
na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama hivyo, umemalizika mwishoni mwa wiki mjini
Maputo kwa mafanikio makubwa.
Mkutano huo ulijadili
masuala yaliyolenga kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya
maendeleo kwa ujumla.
masuala yaliyolenga kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya
maendeleo kwa ujumla.
Baadhi ya viongozi wa
vyama hivyo vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika
Kusini Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi,
Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Komredi Kinana na
ujumbe wake.
vyama hivyo vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika
Kusini Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi,
Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Komredi Kinana na
ujumbe wake.
Ujumbe kutoka Tanzania
ulioongozwa na Komredi Kinana umewajumuisha Katibu wa NEC anayeshughulikia
Siasa na Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya
za CCM.
ulioongozwa na Komredi Kinana umewajumuisha Katibu wa NEC anayeshughulikia
Siasa na Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya
za CCM.
UNIDO YAPIGA JEKI VIWANDA VIDOGO VYA MAFUTA YA ALIZETI DODOMA
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga akitoa maelezo jinsi kiwanda hicho
kinavyofanya kazi zake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (kushoto), Mwakilishi
Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (kulia) pamoja na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto kukagua miradi
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. (Picha na Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
Kutoratibiwa
kwa mbegu za alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto
kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika
kuendesha viwanda vyao kwa gharama nafuu.
Hayo
yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus
Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro
Rodriguez.
Mratibu
huyo alikuwa Dodoma kwa shughuli mbalimbali za ukaguzi wa miradi pamoja
na kuhudhuria shughuli za bunge la Tanzania lililomalizika jana.
Timothy
alisema kwamba pamoja kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa mbegu za kutosha
nchini Tanzania,hali halisi inayoelezwa na wasindikaji inaashiria
kwamba sekta hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila
kuwa na mbegu za kusindika.
Aidha
alisema kwamba mbegu za alizeti zinazovunwa kuanzia Aprili hadi Julai
na huwa na bei nafuu kipindi hicho lakini kama wasindikaji wakikosa
mitaji na kununua mbegu chache, msimu unapoisha hawawezi tena kuendelea
kufungua viwanda vyao.
Alisema
kwamba wasindikaji hao wanakumbana na kiwango kikubwa cha riba kuanzia
asilimia 20 kwenda juu , riba ambayo inakwamisha maendeleo ya viwanda
hivyo.
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia), Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa pili
kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum
(katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric
Otto (wa pili kulia) wakipata picha ya ukumbusho katika matanki ya
kuhifadhia mafuta ya alizeti kiwandani hapo.
Hata
hivyo alipoulizwa wanafanya nini katika kusaidia wasindikaji hao
kukabiliana na hali hiyo alisema kwamba kupitia kongano hilo na
Shirikisho la wasindikaji wadogo wa alizeti kanda ya mashariki na kati
(CEZOSOPA). wana mipango ya kuwezesha wasindikaji hao kuwa na nguvu
katika soko na kuwa na uwezo wa kupata mitaji bila gharama kubwa.
Aidha
kupitia kongano hilo chama hicho kitawezeshwa uboreshwaji wa viwanda
vya wanachama wake ili viweze kushindana na kukidhi viwango vya Shirika
la Viwango nchini Tanzania (TBS).
Wakala
huyo alisema hayo katika mahojiano yaliyofanyika kufuatia ziara ya
mradi wa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez
kwenye kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya
Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya
Viwanda na Biashara (TIUMP).
Kwa
mujibu wa taarifa ya UNIDO, taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inachangia
kuimarika kwa sekta ya viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji mafuta
na kuviweka katika ushindani.
Aidha kupitia UNIDO ni viwanda hivyo vinawekwa katika hali ya kukua kuwa viwanda vikubwa.
Mfanyakazi
wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Alpha Manyanga akiwa kwenye mashine ya kuchujia
mafuta kiwanda hapo.
Katika
ushirika wa aina hiyo ni matarajio ya mradi huo kufanikisha juhudi za
kupunguza umaskini kama moja ya malengo ya maendeleo endelevu
yanayotarajiwa na dunia.
Aidha katika upunguzaji huo wa umaskini mradi utachangia ongezeko la fursa za ajira na ukuaji wa uchumi.
Mkoa
wa Dodoma wenye viwanda vya kusindika mbegu za alizeti vinavyofanyakazi
katika mkaazi wakitumia zana dhaifu na vifungashia visivyokuwa na
ishara yoyote ile na kuuza bidhaa zao kando mwa barabara wanahitaji
mfumo thabiti wa ukuzaji wa shughuli zao na kueleweka.
Kutokana na mazingira hayo wajasirimali hawa hujikuta wakiingia hasara kubwa kwa kupoteza tija na pia soko lenye uhakika.
Kutokana
na madhara hayo na pia kukosa hati ya ubora kwa kukosa mazingira
yanayoruhusu hati hiyo kutolewa, TIUMP imelenga kusaidia wasindikaji
hawa na teknolojia sahihi inayohitajika ili watoke pale walipo na kuwa
na viwanda vidogo au vya kati.
Ingawa
kwa sasa UNIDO inasaidia viwanda vinane vya mbegu za alizeti ili kuweza
kuboresha bidhaa zao na utendaji kuna muonekano wa maendeleo makubwa
siku za usoni hasa kwa wanachama wa CEZOSOPA ambao wameuinganishwa
pamoja kwa ajili ya misaada mbalimbali ya kuwawezesha kuwa washindani
katika soko.
Mtaalamu
wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (aliyeipa mgongo kamera)
akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto
(kulia) walipokua wakikagua mtambo wa kusafisha mafuta (Semi re-finery)
uliofadhiliwa na UNIDO kiwandani hapo.
UNIDO
wanatumia maarifa waliyojifunza Ethiopia kuimarisha wanachama wa
CEZOSOPA ambao tayari wamekubali kuunda kampuni ya pamoja na kuwekeza
katika kitu wanachokifanya kwa pamoja kwa lengo la kuongeza uwezo na
ushindani katika soko.
Halmashauri ya Chamwino tayari imekubali kuipa ardhi CEZOSOPA kwa ajili ya uwekezaji huo mkubwa.
Aidha
UNIDO imewezesha kupatikana kwa teknolojia rahisi kwa ajili ya
usafishaji wa mafuta ya alizeti na teknolojia hiyo inafanyiwa kazi na
VETA.
UNIDO
wamesema teknolojia hiyo hiyo inasaidia kuweka mafuta katika viwango
vinavyotakiwa kitaifa na kimataifa na kwamba teknolojia hiyo tayari
inafanyakazi nchini katika viwanda viwili na vingine saba vimeonesha nia
ya kupata teknolojia hiyo.
Imeelezwa kuwa fedha za mradi huo zinapatikana kutoka UNIDO na wadau wengine kama SIDA na UNDAP.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto akipozi kwa picha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akifurahi jambo alipokuwa
akipewa maelezo na Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid
(kulia) ya mtambo mahususi wa kusafisha mafuta (Semi re-finery)
uliofahdhiliwa na UNIDO.
KANDA YA KASKAZINI WAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.
![]() |
| Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini. |
![]() |
| Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia taarifa juu ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. |
![]() |
| Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya siku 16 zakupinga ukatili na aliyekuwa Mwenyekiti wa dawati la Jinsia,Grace Lyimo akizungumza jambo katika kikao cha kamati hiyo na wanahabari. |
![]() |
| Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
MAZISHI YA MAWAZO BADO KIZUNGUMKUTI. CHADEMA KUTINGA MAHAKAMANI.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesitisha shughuli za mazishi ya
aliekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita marehemu Alphonce
Mawazo, baada ya jeshi la polisi Mkoani Mwanza kuzuia zoezi la kuuaga
mwili wake lililokuwa limepangwa kufanyika juzi jumamosi Jijini Mwanza.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe alibainisha hayo jana wakati
akizungumza na Wanahabari Mkoani Mwanza, ili kutoa msimamo wa Chama
baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina yake na familia ya marehemu
Mawazo.
Alisema
kuwa baada ya mazungumzo hayo, Chadema pamoja na familia ya marehemu
Mawazo wamekubaliana kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kufungua shauri
la kuomba tafsiri ya Kimahakama juu ya zuio hilo la jeshi la polisi
kuzuia mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza kabla ya Kwenda
kuzikwa Kijijini kwake Chikobe katika Wilaya ya Busanda Mkoani Geita.
Nae
Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi wa marehemu Mawazo,
alisema anasikitishwa na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi ya
kuzuia mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza ambapo ameeleza
kuwa na matumaini makubwa ya kwamba mahakama itatenda haki juu ya suala
hilo.
Frederick
Sumaye pamoja na Edward Lowasa ambao ni Viongozi Waandamizi wa Chadema,
walisema hatua ya jeshi la polisi kuzuia mwili wa Mawazo kuagwa Jijini
Mwanza si sawa na kwamba inaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kupitia kwa Kamanda
wake Charles Mkumbo, lilizuia zoezi la mwili wa marehemu Mawazo Kuagwa
Jijini Mwanza, kwa madai kwamba limepokea taarifa za kiitelejensia za
kuwepo baadhi ya vikundi vya watu kutumia mwanya huo kufanya fujo na
hivyo kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Aidha
Kamanda Mkumbo aliitaja sababu nyingine kuwa ni uwepo wa mlipuko wa
Ugonjwa wa Kipindupindu Mkoani Mwanza, ambao umesababisha jeshi hilo
kutoruhusu mikusanyiko ya aina yoyote inayoweza kusababisha ugonjwa huo
kuenea zaidi kwa mjibu wa wataalamu wa afya ambapo lilishauri zoezi la
kuaga mwili huo kufanyika Mkoani Geita ambapo mazishi ya marehemu Mawazo
yatarajiwa kufanyika.
Katika
uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, marehemu Alphone Mawazo alikuwa
mgombea ubunge Jimbo la Busanda Mkoani Geita kupitia Chadema, akiwa pia
ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambapo aliuawa kikatili kwa
kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana jumamosi iliyopita ya
Novemba 14 mchana huku kifo chake kikihusishwa na uhasama wa kisiasa.
WADAU WAJITOKEZA KUISAIDIA TIMU YA KIKAPU MBEYA
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Wachezaji
22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo
kwa ajili ya kushiriki mashindano ya
Taifa CUP, yatakayofanyika Mkoani Dodoma November 22 hadi November
30 mwaka huu.
22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo
kwa ajili ya kushiriki mashindano ya
Taifa CUP, yatakayofanyika Mkoani Dodoma November 22 hadi November
30 mwaka huu.
Wachezaji
hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma
hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma
kushiriki mashindano hayo kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha hali
iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.
iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.
Aidha
kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na kujitokeza kwa Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa
wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha
kilicho fanikisha safari hiyo.
kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na kujitokeza kwa Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa
wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha
kilicho fanikisha safari hiyo.
Akizungumzia
juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni
mwalimu wa timu hiyo , Yusuf Nyirenda, amesema
kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza kwa kuchangia kiasi hicho
cha fedha .
juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni
mwalimu wa timu hiyo , Yusuf Nyirenda, amesema
kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza kwa kuchangia kiasi hicho
cha fedha .
Amesema kampuni ya Coca Cola pekee imechangia kiasi cha shilingi
Mil 1.5 ambapo kwa upande wa Tbl wamechangia kiasi cha shilini laki tano hivyo
watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana ili kushiriki mashindano hayo.
Mil 1.5 ambapo kwa upande wa Tbl wamechangia kiasi cha shilini laki tano hivyo
watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana ili kushiriki mashindano hayo.
Amesema,
tayari timu imekwisha ondoka Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati
yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa wamefanikiwa kupata
shilingi milioni 2 kati ya milioni
4,700,000 zinazohitajika.
tayari timu imekwisha ondoka Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati
yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa wamefanikiwa kupata
shilingi milioni 2 kati ya milioni
4,700,000 zinazohitajika.
“Kiasi
cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na
kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.
cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na
kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.
Amesema
kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee
ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .
kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee
ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .
Amesema
kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia
wenyewe katika eneo la usafiri hivyo, amewaomba wadau na mashabiki wa mpira
huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki
mashindano hayo.
kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia
wenyewe katika eneo la usafiri hivyo, amewaomba wadau na mashabiki wa mpira
huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki
mashindano hayo.
( Imeandaliwa na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com- Mbeya 0759406070)
Tigo Yadhamini Gulio la Annual Charity Baazar
| Mtoa huduma wa Tigo, Khalid Omary akitoa huduma kwa wateja wa Tigo kwenye gulio lililoandaliwa na wake wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania lenye lengo kusaidia jamii |
| Kikundi cha sanaa cha Jumping Village kikitoa burudani kwenye gulio la lililoandaliwa na wake wa mabalozi lililofanyika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki. |
| Kikundi cha sanaa cha Jumping Village kikitoa burudani kwenye gulio la lililoandaliwa na wake wa mabalozi lililofanyika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki. |
WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI DAR
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea shada la maua
kutoka kwa Immaculata Warqaso wa Ofisi ya Waziri baada ya kuwasili
kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Novemba 22,
2015 wakitoka Dodoma.Wapili kulia ni Katibu Mkuuwa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Dkt Florence Turuka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR FUMBA
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kwa
ufupi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa
alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya
kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa
na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar
Nd,Salum Khamis Nassor [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kwa
ufupi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa
alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya
kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa
na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar
Nd,Salum Khamis Nassor [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kwa
ufupi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa
alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujwga kiwanda cha utengezaji wa
Lami katika Kijiji cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara
ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa
zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo
kutoka kwa Bw.Hudhaifa Yussuf Ali Mchoraji wakati alipokuwa akiangalia
zamani za ujenzo wa Nyumba za kisasa zitakazojengwa katika fukwe za
Kijiji cha Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja alipokuwa katika ziara maalum
ya kutembea maeneo hayo jana,ujenzi huo utafanyika kwa ushirikiano wa
Kampuni ya Azam Group na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akifuatana na
Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa (katikati) Mkuu wa
Wilaya ya Magharibi A. Bw.Ayoub Mohammed Mahmoud (kushoto) na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor
wakati alipofanya ziara maalum ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji
mpya wa Nyumba za kisasa zitakazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa
kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum
Khamis Nassor wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Ujenzi wa Nyuma za
Kisasa zitakazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar katika maeneo ya fukwe za Kijiji cha Fumba Mkoa
wa Mjini Magharibi Unguja alipofanya ziara maalum,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa
Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa
Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji
mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa
kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali
mbali wakati alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara
ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa
zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana na Serikali nya
Mapinduzi ya Zanzibar [Picha na Ikulu.]
RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI BAADA YA KUMUAPISHA WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA MJINI DODOMA
Rais Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe
Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu mpya Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa
mara baada ya kumuapisha mwishoni mwa wiki katika Ikulu Ndogo ya
Chamwino mjini Dodoma. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi wa
Serikali ya Mapinduzi Zandibar Dkt Abdulhamid Yahya Mzee, Katibu Mkuu
Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Balozi Ombeni Sefue, Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Mhe. Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman
Mkungu.
Rais Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan na Waziri Mkuu mpya Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya
kumuapisha mwishoni mwa wiki katika Ikulu Ndogo ya Chamwino mjini
Dodoma.
PICHA NA IKULU
DC MAKONDA AZUNGUMZIA KIFO CHA KATIBU WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI MADEREVA TANZANIA (TADWU)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau
wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
Mjumbe wa Chama
cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia),
akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja
(kushoto), pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa
taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es
Salaam leo.
Msemaji
wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani
kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na
utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem akizungumza katika mkutano na wanahabari
Ndugu
na jamaa wa marehu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili
huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.
Ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha
uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa
mazishi.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MWILI
wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania
(TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze
wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.
Saleh
alifariki jana Novemba 20 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili
kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni
mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana
na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea
haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo
yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.
“Saleh
alifariki jana (Novemba 20) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake
haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu
zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari
wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,”alisema.
Alisema
marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya
mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha
mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo
chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.
“Hatukuona
kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua
nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa
kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo
tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi
kazi,”alisema.
Aliongeza
kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku
akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu
mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza
kuokoa maisha yake.
Mwenyekiti
wa Chama hicho, Shaban Mdem alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana
kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika
kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.
“Tunataka
uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu
ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo
serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo
tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,”alisema.
Alisema
Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia
kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote
kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi
kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.
Mazingira ya Kifo
Akizungumzia
mazingira ya kifo Msemaji wa Familia ya Marehemu Jonas Ernest alisema
kuwa Novemba 9 mwaka huu marehemu alipokea simu kutoka kwa rafiki yake
ma kumtaka waende kwenye kikao, ambapo baada ya hapo mwenzake alidai
kuwa na njaa.
Alidai
baada ya hapo walikwenda kuagiza chakula ambapo mwenzake hakula na
kumuacha marehemu akiwa anakula huku mwenzake akiwa amemuaga kwenda
msalani.”Baada ya kurudi msalani alimkuta marehemu akilalamika tumbo
linamuuma na hivyo kuondoka eneo hilo pasi na huyo rafiki kula
chochote,”alisema.
Alidai
kuwa baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo alianza kuharisha na
kutapika na alikimbizwa hospitali lakini uchunguzi ulibaini hakuwa na
tatizo na kurudishwa nyumbani ambapo siku inayofuata alirudi hospitali
na kuambiwa kuwa ana malaria 4.
“Alianza
kutumia dawa za malaria na baadaye kujiskia vibaya na kumrudisha tena
hospitali ya Kairuki laikini madaktari walidai kuwa anatatizo ndani ya
mwili ambalo ni figo kushindwa kufanya kazi vizuri,”alidai na kuongeza
kuwa hadi marehemu anafariki alikaririwa akidai kuwa”Nyama
inanitenganisha na mwanangu lakini”na kumtaja mmoja wa wafanyakazi
wenzake huku akidai kumuona mtoto wake.
Harakati za kudai haki ya madereva
Saleh
alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika
harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu
alikaririwa akisema wamechoshwa na uozo unaoendelea kufanywa na Mamlaka
ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na
Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji
hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.
Wanafunzi wenye mahitaji maalum vyuo vikuu waaswa kutumia vyema utaalamu walioupata kuendesha maisha yao
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika
jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha
Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga.
Picha na Frank Shija, MAELEZO
Baadhi ya
wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho
yaliyofanyika chuoni hapo jana.
Kaimu Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Balozi Nicholas Kuhanga
akiwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE) (hawapo pichani) alipokuwa mgeni wa Chuo katika Mahafali
ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu.
Muhitimu wa
mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwa kupata GPA ya 4.8 Bi.
Ummul Kheir Mustafa akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu mara baada ya kupokea zawadi
yake ikiwemo kukabidhiwa Cheti chake mbele ya hadhara wakati wa
Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Muhitimu huyo
amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa
fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka
masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo
hapo.
Muhitimu wa
mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwakupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul
Kheir Mustafa akionyesha Cheti chake cmbele ya hadhara mara baada ya
kuwa muhitimu wa kwanza kukabidhiwa cheti wakati wa Mahafali ya nane ya
chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Mbali na kukabidhiwa Cheti chake
cha Shahada papo hapo muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza
kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni
hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya
kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo.
Mgeni rasmi
wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama
(DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo
yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu
1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu.
………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanafunzi wenye mahitaji maalum
wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata
kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa
ujumla.
Hayo yamesemwa na Prof.
Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha Studi za Mawasiliano
Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati wa Mahafali ya nane
ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.
Prof. Qorro alisema kuwa mwamko
wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni
mzuri licha ya changamoto zinazowakumba wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.
“Hawa ni wanafunzi wenye uelewa
mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo fimbo nyeupe, vifaa vya
kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za miguu mitatu, viti maalu
na mahitaji mengine ya kijamii” alisema Prof.Qorro.
Prof.Qorro aliongeza kuwa ni
wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar
es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi wanapojaza fomu za
kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili waandaliwe mahitaji hayo
ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili kuwawezesha kuwahi vipindi
vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye
alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mahafali
hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake
ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya 8000 na jumla ya wahitimu
1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu katika mahafali hiyo ya
nane.
Naye muhitim wa mwaka wa tatu
katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo ya sanaa Andrea Sanga
ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum (mlemavu asiyeona)
alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana na kuheshimu ratiba
kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake binafsi ya kujisomea.
Zaidi ya hayo, Sanga alisema
kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na wanafunzi wenzake
na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa wakati na
kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira yake kuu ya
mafanikio.
MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 251 ZILIZOKUWA ZITUMIKE KUJIPONGEZA WABUNGE
Magari
ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia
agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa
ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro.
Na Dotto Mwaibale
…………………………………………………………………………
BOHARI
ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya
Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo
alilotoa Rais Dk. John Magufuli.
Vifaa
hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na
uhaba alioubaini Rais Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza
katika mapema mwezi huu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu
vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema
hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300,
magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea
wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.
Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.
Fedha
hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais
Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa
ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa
hivyo
MKUTANO WA WANASHERIA MAWAKILI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA ZANZIBAR
Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Chama cha Wanasheria Mawakili
Zanzibar kimepata heshma ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa siku mbili wa
mwaka wa Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki utakaoanza
tarehe 27 Mwezi huu katika Hoteli ya Sea Cliff Resort.
Akizungumza na waandishi wa
Habari Ofisini kwake Bwawani, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria
Mawakili Zanzibar Omar Said Shaaban amesema mkutano huo utawashirikisha
zaidi ya Wanasheria 400 kutoaka Nchi zote wananchama wa Afrika Mashariki
na Mataifa mengine Duniani.
Amesema kwa kawaida Jumuiya ya
Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki inawachama wa aina mbili
ambao ni wanasheria wenyewe binafsi na Jumuiya za kila Nchi nazo huwa
ni mwanachama wa pili.
Katibu Mkuu wa Wanasheria
Mawakili Zanzibar amesema Mkutano huo utakuwa na malengo ya kubainisha
kuwa Taaluma ya sheria kama kichocheo cha Biashara na Uwekezaji ambapo
mada mbali mbali zitawasilishwa.
Amezitaja baadhi ya mada
zitakazowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na Kada ya Sheria kama
biashara, muundo mzima wa Biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika
Mashariki na mada nyengine ni masuala ya rushwa na vipato visivyohalali.
Ametoa wito kwa wananchi wa
Zanzibar kuupokea ugeni huo mkubwa wa wanasheria na kuonyesha ukarimu
uliozoeleka kwa wageni na kutumia fursa ambazo zitapatikana kutokana na
kuwepo kwao hapa nchini.
Amesema chama kwa upande wake
tayari kimeliarifu Jeshi la Polisi kuhusu ugeni huo kwa lengo la
kuimarisha hali ya usalama wakati wote wa mkutano.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Wanasheria Zanzibar amesema Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu
atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo.
WAZIRI MKUU MAJLIWA AKISALIMIANA NA VIONGOZI WA MOROGORO
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na viongozi
wa mkoa wa Morogoro wakati waliposimama kwa muda mjini Morogoro wakiwa
njiani kuelekea Dar es salaam wakitoka Dodoma Novemba 22, 2015. Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)










No comments :
Post a Comment