Modewjiblog Operations Manager, Zainul Mzige taking a ‘selfie’ with the Nigerian Artist Mr. Flavour at Sir Seerwoosagur Ramgoolan International Airport upon our arrival in Mauritius.
Head of delegation from Tanzania, Public Relations Manager at MultiChoice Tanzania Ltd, Barbara Kambogi pose for a photo with Tanzanian Journalists who have been invited to Mauritius to experience the biggest week in Africa’s video entertainment, hosted by MultiChoice Africa.
Invited guests from Botswana poses for a group photo.
Comedian from Nigeria, Basket Mouth (left) pose for a photo with award winning singer and songwriter Mr.Flavour
The Guardian Newspaper Senior Reporter Sylivester Domasa with Nigerian Comedian Basket-Mouth (right) and award wining singer and song writer Mr.Flavour
Invited guests mingle at the VIP Lounge upon their arrival.
Dear readers
We are in Mauritius to experience the biggest week in Africa’s video entertainment, hosted by MultiChoice Africa.
We have arrived at Sir Seerwoosagur Ramgoolan International Airport just some hours ago and the fun has already started.
For the next five days, we will be treated to ‘ONLY THE BEST’ in video entertainment on the DStv and GOtv.
We are here, and the only thing we have been encouraged, is to open our mind to experience television like we had never before and also to grab the opportunity to interact with various exciting channels that will engage with us and give an exclusive, in-depth and VIP experience of their content.
I trust that throughout this event, I will have plenty of material to share with you.
I look forward to give you an amazing Africa-inspired content live-in action.
While am here definitely I will touch and rubbed shoulders with the stars of Hollywood, Nollywood, Bollywood and so much more. I am truly looking forward to sharing with you this exciting journey of television content discovery.
Be part of the conversation on social media with the hashtag: #OnlyTheBest. And please follow us on social media via Twitter: @MCAShowcase; Instagram: @MultiChoice_Africa and Facebook Group: #OnlyTheBest
MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MATUNDU NANE YA CHOO BORA KWENYE SHULE YA MSINGI KIBAONI SINGIDA
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike,
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane
chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji
Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3
milioni).
Mwakilishi
wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.
Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa
kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili
kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi
wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel,
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya
shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa
shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi
wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia)
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa
pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi
Kibaoni.
Mwakilishi
wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa
pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye
thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia
shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo
la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris
Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
……………………………………………………..
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI
wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga
utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya
shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito
huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda
Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye
matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule
ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao
wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema
uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya
kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama
yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea
mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua,
alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na
kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation
na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO
Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa
shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake
itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya
kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda
nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji
iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji
Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi
wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie
nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake
wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari
umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali
kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
KAMPENI ZA JIMBO LA MOROGORO MJINI WAZINDULIWA
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma akimnadi Mgombea Ubunge Wa
Jimbo hilo Mh Aziz Abood wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo
hilo.Ikumbukwe Mh aziz Abood anatetea Kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo Mara
baada ya Kuongoza Jimbo hilo kwa Miaka 5 Kwa mafanikio ya Hali ya Juu.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro
Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwahutubia Mafuriko
ya wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa
Kampeni za Ubunge za Jimbo hilo
Wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kmpeni za Ubenge na Madiwani wa Jimbo hilo
Mh.Paul Makonda katika uzinduzi wa Vitabu vya Mwl.Lilian Ndegi
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu |
Mh.Paul Makonda akizindua vitabu |
Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua |
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana |
Mh.Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa |
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji |
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua |
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua |
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua |
Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo |
Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo |
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda |
Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe |
Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi |
Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti wa kanisani hapo. |
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa kanisani hapo. |
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul
Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya
mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika
uzinduzi wa vitabu vitatu “MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI
ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water
Center Kawe.
Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.
Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na
kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu
hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti
huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama
yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.
Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.
Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.
Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.
Rais Kikwete ashiriki Mazishi ya Kimbau Mafia
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka udongo katika kaburi la aliyewahi kuwa Mbunge wa Mafia Kanali
Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau huko Mafia leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe
Mama Salma(aliyeketi na mke wa Marehemu kushoto) wakimfariji mke wa
Marehemu Kanali Mstaafu Nyumbani Kwake Mafia wakati wa mazishi ya Mbunge
huyo wa zamani wa Mafia leo jioni.
Baadhi ya wanajeshi wakiwa
wamebeba jeneza la Marehemu Kanali Mstaafu Ayub Kimbau aliyewahi kuwa
mbunge wa Mafia wakati wa Mazishi yake huko Kilwa leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na watoto wa marehemu
Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau wakiomba dua wakati wa mazishi ya
Mbunge huyo wa Zamani wa Mafia yaliyofanyika huko Mafia leo jioni(picha
na Freddy Maro)
DR. MAGUFULI AITIKISA SONGEA, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa
majimaji mjini Songea leo ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya
wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo
wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa
anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya
chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa
kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Amesema pia serikali yake
itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza
mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi ,
wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Amesema ataongeza zaidi kasi
yake katika utendaji tofauti na alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo
awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa akichaguliwa na watanzania
kuwa rais yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua
asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia
alitembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kada maarufu wa
CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki miezi kadhaa
iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na
kuzikwa nyumba ni kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma(PICHA
NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SONGEA)
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima
katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika
kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya
CCM Ndugu William Lukuvi.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada
la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani
Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akishuka
kutoka katika kivuko cha Mv Lituhi mara baada ya kuvuka mto Luhuhu
akitokea mkoani Njombe wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma
kuendelea na kampeni zake.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipunga mkono
mara baada ya kuvuka mto Luhuhu akielekea Mbinga mkoani Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi.
Umati wa wananchi ukiwa umefurika
katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika mkutano wa kampeni
uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli.
Mmoja wa wana CCM akifuta vumbi
kwenye picha ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi mjini Mbinga kwenye uwanja wa Taifa kumsikiliza Dr John Pombe Magufuli.
Kada wa CCM Bw. Amon Mpanju akiwahutubia wakazi wa mjini Songea mkoani Ruvuma leo.
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita.
Mabasi Maalum ya Kampeni za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea wa CCM jimbo la Songa Mjini Mh. Leonidas Gama.
Baadhi ya wana CCM wa wilayani
Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa
CCM kwenye uwanja wa Taifa uliofanyika katika mji huo.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
mjini Mbinga.
Baadhi ya wananchi wakiwa
wameshika picha za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza
mgombea ubunge wa jimbo la Mbinga Komredi Sixtus Mapunda wakati
alipokuwa akiwaomba kura wananchi wa mji wa Mbinga.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi Mh.
Jenista Mhagama mgombea ubunge wa jimbo la Peramiho katika mkutano
uliofanyika Peramiho.
Wana Peramiho wakimkaribisha Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Peramiho ikizizima kwa bendra za CCM wakati wa mapokezi hayo.
Umati uliohudhuria katika mkutano huo
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mkutano wake
uliofanyika Peramiho.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi
Ilani ya Uchaguzi Mh.Jenista Mhagama ambaye Mgombea ubunge wa jimbo la
Peramiho
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa na
watoto mara baada ya kumaliza mkutano wake Peramiho.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.
Majimaji ikiwa imetapika
Kundi la TOT likifanya vitu vyake jukwaani.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na viongozi
mbalimbali wakiwa wameketi meza kuu.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Songea mjini Dr. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi na kumpigia
debeMgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk.
John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja
wa Majimaji mjini Songea.
Huyu naye alivaa makufuli
kichwani na shingoni kupeleka ujumbe wa mapenzi yake kwa Mgombea wa
Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli.
Kutoka kulia ni Mwingulu Nchema, Jenista Mhagama na William Lukuvi wakiteta jambo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Songea mjini Mh. Leonidas gama akijinadi kwa wananchi kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji.
GLOBAL PEACE FOUNDATION, TAWI LA TANZANIA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Viongozi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ),
Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana
wakati
wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka
kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la
Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na
kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
Mkurugenzi
wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji
Thomas Goda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi
wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
Ofisa
Utawala wa Shirika hilo, Hilda Ngaja (kushoto) na Balozi wa Amani wa
GPF, Dk.Ulimwengu (kulia), wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha
kushiriki uchaguzi kwa amani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
GLOBAL Peace Foundation Tawi
la Tanzania (GPFTZ), kwa kushirikiana na
Mshirika wake, Baraza la Wadhamini la
Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), wamezindua kampeni ya
kuhamasisha Amani nchini Tanzania katika
kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ,
jina la kampeni ni “Amani Kwanza”.
la Tanzania (GPFTZ), kwa kushirikiana na
Mshirika wake, Baraza la Wadhamini la
Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), wamezindua kampeni ya
kuhamasisha Amani nchini Tanzania katika
kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ,
jina la kampeni ni “Amani Kwanza”.
Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuhamasisha watanzania wote
kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa
Amani ambao unatarajia kufanyika Okotoba 25, 2015
kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa
Amani ambao unatarajia kufanyika Okotoba 25, 2015
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi alisema Walengwa wakuu wa
Kampeni hiyo ni Wanawake na Vijana ambao ni wengi
zaidi ukilinganisha na rika na makundi
mengine, na pia Wanawake wamekuwa
wakihathirika zaidi endapo inapotokea machafuko
hali kadhalika Vijana wamekuwa chanzo cha uchochezi wa
machafuko katika nchi mbalimbali duniani.
Kampeni hiyo ni Wanawake na Vijana ambao ni wengi
zaidi ukilinganisha na rika na makundi
mengine, na pia Wanawake wamekuwa
wakihathirika zaidi endapo inapotokea machafuko
hali kadhalika Vijana wamekuwa chanzo cha uchochezi wa
machafuko katika nchi mbalimbali duniani.
“kampeni hii haina lengo lolote la kuunga mkono ama
kupinga Chama chochote cha Kisiasa au
mgombea wake, na wala haina mahusiano
yoyote ya kisiasa na kauli kauli mbiu yake ni “KURA YANGU UZALENDO
WANGU, AMANI YA NCHI YANGU NI JUKUMU
LANGU” alisema Nghambi.
kupinga Chama chochote cha Kisiasa au
mgombea wake, na wala haina mahusiano
yoyote ya kisiasa na kauli kauli mbiu yake ni “KURA YANGU UZALENDO
WANGU, AMANI YA NCHI YANGU NI JUKUMU
LANGU” alisema Nghambi.
Nghambi alisema Kampeni hiyo imeandaliwa
maalumu kwa malengo ya kuwahamasisha Wanawake
na Vijana kuwa mabalozi wazuri wa
kulinda na kuitetea Amani ya nchi
yetu hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
Kujiepusha na vitendo mbalimbali ambavyo
vinaweza kuchochea uharibifu wa Amani
nchini Kuhamasisha
maalumu kwa malengo ya kuwahamasisha Wanawake
na Vijana kuwa mabalozi wazuri wa
kulinda na kuitetea Amani ya nchi
yetu hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
Kujiepusha na vitendo mbalimbali ambavyo
vinaweza kuchochea uharibifu wa Amani
nchini Kuhamasisha
kila mmoja ashiriki
uchaguzi kwa amani Ili kuhakikisha.
uchaguzi kwa amani Ili kuhakikisha.
Alisema kampeni hiyo inafanikiwa kutokana na Shirika la Global Peace kushirikiana kwa
karibu na vyombo vya habari nchini
vikiwemo Radio, Luninga, Magazeti, na
mitandao mbalimbali ya Kijamii ikiwemo Twitter, Face Book,
instagram na YouTube.
karibu na vyombo vya habari nchini
vikiwemo Radio, Luninga, Magazeti, na
mitandao mbalimbali ya Kijamii ikiwemo Twitter, Face Book,
instagram na YouTube.
Alisema shirika hilo ni Tawi la Taasisi ya Kimataifa isiyo ya Kiserikali na
isiyotengeneza faida Global Peace Foundation
(GPF) yenye makao makuu yake
Washington DC, nchini Marekani.
isiyotengeneza faida Global Peace Foundation
(GPF) yenye makao makuu yake
Washington DC, nchini Marekani.
Alisema shirika hilo linahamasisha kutetea na kulinda Amani dunia
, shirika hili linaamini ya kuwa “ Kwa Mungu sisi
wote ni familia moja” GPF inafanya kazi
kwa karibu na mitandao ya kiserikali
na watu binafsi katika kuendeleza jamii,
taifa na katika kujenga na kulinda misingi
na maadili katika jamii husika.
, shirika hili linaamini ya kuwa “ Kwa Mungu sisi
wote ni familia moja” GPF inafanya kazi
kwa karibu na mitandao ya kiserikali
na watu binafsi katika kuendeleza jamii,
taifa na katika kujenga na kulinda misingi
na maadili katika jamii husika.
GPF ina rekodi nzuri ya kufanya kazi kwa karibu na
kwa mafanikio makubwa kuhamasisha na
kulinda Amani katika nchi mbalimbali dunia
katika bara la Afrika, Asia, Ulaya na Amerika.
kwa mafanikio makubwa kuhamasisha na
kulinda Amani katika nchi mbalimbali dunia
katika bara la Afrika, Asia, Ulaya na Amerika.
Kwa upande wa Afrika, shirika hili limekuwa likijihusisha
na maswala mbalimbali ya kijamii katika
nchi za Kenya, Uganda na Nigeria
kudumisha Amani kwenye ukanda wa Afrika.
na maswala mbalimbali ya kijamii katika
nchi za Kenya, Uganda na Nigeria
kudumisha Amani kwenye ukanda wa Afrika.
JESHI LA POLISI TANZANIA LAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WA SHAHADA, STASHAHADA
TANGAZO KWA UMMA.
JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU
WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA
KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI
ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
• FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.
• FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.
• MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA
PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL],
MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY
ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI
UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES
SALAAM.
• MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
• MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
• WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR
BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA
BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.
• KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA
MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU
NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.
• DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO
UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA
BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI,
ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING &
FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK,
PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL,
REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA
KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI
KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• FANI ZA BENDI, BRASS BENDI,
WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA
BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• FANI YA URUBANI,USAILI UTAFANYIKA KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.
MUHIMU:
1. MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2. MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3. AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MUHIMU:
1. MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2. MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3. AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MAMA SAMIA AKUTANA NA WANAWAKE MJINI DODOMA
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi
ya CCM, Mama Damia, akizungumza na wanawake wa mkoa wa Dodoma, leo
katika ukumbu uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma.
(picha na Bashir Nkoromo
Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dodoma,
Adam Kimbisa akifungua kikao cha Mama Samia na wanawake wa mkoa wa
Dodoma, katika ukumbi ulipo jengo la white House Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma leo.
Mama Tunu Pinda akizungumza kwenye kikao hicho, na Mama Samia na wanawake wa mkoani Dodoma leo
Wanawake wakimpokea Mama Samia ukumbini.
Wanawake wakimvisha vazi la heshima, ya wagogo, Mama Samia.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dodoma, Fatuma Mwenda akimk.abidhi Mama Samia zawadi ya kitenge.
AKUTWA AMEUWAWA HOTELINI ARUSHA
…………………………………….
MTU mmoja mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka
30,amekutwa amefariki dunia na wauaji wakatoweka na kichwa, viganja na
viungo vya uzazi na matiti na maiti ikitelekezwa hotelini .
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa
wa Arusha, Liberatus sabas, amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia leo ,ambapo majira ya saa 3 asubuhi wahudumu walipoingia kufanya
usafi walimkuta marehemu amefariki dunia huku ufungoa wa chumba ukiwa
kwa nje .
Amesema marehemu aliyefahamika
kwa jina moja la Mandela, ambae ana duka la kuuza mabegi lililopo
karibu na benki ya NMB, jijini Arusha ,alikutwa kwenye hotel ya kitalii
ya A.M,iliyopo jijini Arusha.
Amesema mtu aliyefika hotelini
hapo kuchukua chumba anaitwa Rejinard Mjema, na marehemu alikutwa chooni
katika hotel hiyo ya kitalii akiwa amekatwa viungo vyote na wauaji
wakiwa wametoweka.
Amesema marehemu anaishi
Mianzini jijini Arusha,na kiwili cha mwili kiko chumba cha kuhifadhi
maiti cha hospital ya mkoa wa Arusha, Mount Meru na upelelezi
unaendelea.
WANANCHI WILAYANI KIHABA WAFUNGA BARABARA BAADA YA MWANAFUNZI KUGONGWA NA KUFARIKI
VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI
……………………………………….
WAKAZI wa eneo la Misugusugu wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, wamefunga
barabara kwa muda wa masaa mawili wakiitaka serikali kuweka matuta
katika eneo hilo ikiwa ni baada ya ajali kuua mwanafunzi wa darasa la
tatu katika shule ya Msingi Misugusugu.
Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijafahamika alipoteza maisha
baada ya kugongwa na gari la Polisi jana akielekea shuleni huku
mwanafunzi mwingine wa darasa la nne katika shule hiyo akijeruhiwa
katika tukio hilo la ajali lililotokea majira ya saa moja alfajiri.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jafari Ibrahim alikiri kutokea kwa
ajali hiyo ambapo alibainisha kuwa, ajali hiyo ilitokea maeneo ya
Misugusugu wakati gari hilo la polisi lilkiwa limebeba Askari
wakielekea kazini na ndipo likasababisha tukio hilo.
Aidha Kamanda Ibrahim alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na
Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini huku wakimshikilia
dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo na mara baada ya taratibu
kukamilika wanamfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria na kanuni..
Aidha Kamanda alisema, baada ya ajali hiyo wananchi walifunga
barabarai wawekewe matuta kwenye eneo hilo lakini askari walifika na
kutumia nguvu za ziada kuwatawanya na kuwezesha magari kuendelea na
safari.
Kamanda amefafanua kuwa ajeruhi wa ajali hiyo, anaendelea na matibabu katika Hospitali Teule
ya Rufaa ya Tumbi, huku maiti ya mwanafunzi huyo ikiwa imehifadhiwa
kusubiri taratibu za mazishi.
barabara kwa muda wa masaa mawili wakiitaka serikali kuweka matuta
katika eneo hilo ikiwa ni baada ya ajali kuua mwanafunzi wa darasa la
tatu katika shule ya Msingi Misugusugu.
Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijafahamika alipoteza maisha
baada ya kugongwa na gari la Polisi jana akielekea shuleni huku
mwanafunzi mwingine wa darasa la nne katika shule hiyo akijeruhiwa
katika tukio hilo la ajali lililotokea majira ya saa moja alfajiri.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jafari Ibrahim alikiri kutokea kwa
ajali hiyo ambapo alibainisha kuwa, ajali hiyo ilitokea maeneo ya
Misugusugu wakati gari hilo la polisi lilkiwa limebeba Askari
wakielekea kazini na ndipo likasababisha tukio hilo.
Aidha Kamanda Ibrahim alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na
Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini huku wakimshikilia
dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo na mara baada ya taratibu
kukamilika wanamfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria na kanuni..
Aidha Kamanda alisema, baada ya ajali hiyo wananchi walifunga
barabarai wawekewe matuta kwenye eneo hilo lakini askari walifika na
kutumia nguvu za ziada kuwatawanya na kuwezesha magari kuendelea na
safari.
Kamanda amefafanua kuwa ajeruhi wa ajali hiyo, anaendelea na matibabu katika Hospitali Teule
ya Rufaa ya Tumbi, huku maiti ya mwanafunzi huyo ikiwa imehifadhiwa
kusubiri taratibu za mazishi.
Watanzania wahimizwa kutumia huduma za Bima.
……………………………………..
Watanzania theluthi mbili hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna Bima inavyofanya kazi nchini hasa Bima ya Maisha na Mali.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa
Bima nchini Bw. Israel Kamuzora alipokuwa akifunga mafunzo ya wiki ya
huduma kifedha na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Kamuzora aliwataka washiriki wa
mafunzo hayo kueneza ujuzi na ufahamu waliopata ili wananchi walio wengi
waweze kunufaika na huduma za bima nchini.
“Ninawaomba muwe mabalozi wazuri
wa kueneza ufahamu juu ya faida za Bima kwa ndugu, jamaa na marafiki
ambayo ni mojawapo ya mbinu za kujilinda kimaisha na kujikwamua katika
umasikini”. Alisema Kamuzora.
Kamuzora alisema kuwa kwa upande
wao kama waratibu wa huduma za Bima nchini wanao wajibu wa kuendelea
kujenga mazingira ambayo ni rafiki na wezeshi kwa watoa huduma ya Bima
ili waendelee kuwa wabunifu katika kufikisha huduma hiyo kwa Watanzania
wenye uwezo mkubwa na mdogo.
Aidha, Bw. Kamuzora alisema kuwa
mpango wa Taifa wa huduma Jumuishi za kifedha nchini unalenga kuwafikia
watu wazima asilimia 50 wanaotumia huduma rasmi za kifedha ifikapo
mwaka 2016.
Ili kufanikisha mpango huo, Bw.
Kamuzora alitoa wito kwa taasisi za kifedha na za utafiti wa sayansi
kuendelea kushirikiana na mamlaka ya Bima kuona namna ya kuendeleaza
matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kuwapatia wananchi fursa ya
kupata huduma za Bima ili kulinda mali na maisha ya Watanzania
waliowengi.
Hadi sasa nchini, takwimu
zinaonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu za mkononi nchini
wanatumia huduma za fedha za simu ziliongeza ndugu Kamuzora.
Mafunzo ya wiki ya huduma za
kifedha na uwekezaji yalipambwa kwa kauli mbiu inayosema “Maisha ni Duni
Bila Bima” yaliwahusisha wajariamali, benki, na kampuni za Bima
yalidhaminiwa na kampuni ya NUEBRAND na Shirika la PESCODE.
watumiaji wa mitandao vibaya sheria kuwadhibiti kuanza leo saa 6:00 usiku.
………………………………….
Sheria mpya ya Makosa ya
Mtandao ya mwaka 2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka
2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo
watumiaji na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka
mkondo wa sheria.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
“Sheria
hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa
6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi
kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya
Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.
Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.
Profesa
Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania
sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo
,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya
Kusini.
Akizungumzia kuhusu
madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli,
bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai
hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi
ambayo si mazuri.
“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.
Aliyataja
baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za
kompyuta na mifumo kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo
ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.
Makosa dhidi ya kompyuta
ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia
kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni, matumizi ya
vifaa kinyume cha sheria.
Makosa yanayohusiana
kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto
makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni
kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki
na hati miliki.
Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.
Kwa upande wa sheria ya
miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la
wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo
hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.
Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa na zitaanza kutumika wakati wowote.
STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake
ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe –
Kocaeli nchini Uturuki.
Taifa Stars ambayo imeweka kambi
nchini Uturuki kwa takribani wiki moja, inajiwinda na mchezo wake dhidi
ya Nigeria siku ya Jumamosi Septemba 5, 2015 katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika mwaka
2017.
Kocha Mkuu wa Stars Charles Mkwasa akiongea na tovuti rasmi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) www.tff.or.tz amesema anashukuru kambi imekua na mafanikio makubwa kwani vijana wanaonyesha mabadiliko makubwa sana.
“Ukiondoa mchezaji moja tu ambaye
ni majeruhi Abdi Banda, Mkwasa amesema wachezaji wengine wote wapo fit
na kila mmoja atakayepata nafasi katika mchezo wa sikuya jumamosi
atafanya vizuri” amesema Mkwasa.
Mkwasa amesema mazingira ya kambi
yamekua mazuri, na katika mechi ya maozezi dhidi ya Libya iliyochezwa
siku ya ijumaa, vijana wake walicheza vizuri kwa nguvu na kufuata
maelekezo yake, makosa machache yaliyojitokeza katika mchezo huo
wameyafanyia kazi na sasa anaamini wako tayari kuwakabili Nigeria.
Mwisho Mkwasa amewaomba watanzania
kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi kuishangilia
timu ya Taifa, kwani uwepo wa washabiki wengi uwanjani utawaongeza
morali zaidi wachezaji na kujiona wapo nyumbani wanapambana kwa ajili ya
Taifa lao.
Naye nahodha wa Taifa Stars, Nadir
Haroub “Cannavaro” amesema maandalizi waliyopata ni mazuri na
yamewajenga vilivyo kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Nigeria siku ya
jumamosi na kuwaomba watanzania kuja kwa wingi kuwasapoti.
Nadir amesema wao kama wachezaji
kila mmoja yupo fit na anahitaji kucheza mechi hiyo, hivyo yeyote
atakayepata nafasi ya kucheza ana imani atafanya vizuri katika
kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Stars ambayo iliweka kambi ya
takribani siku nane katika milima ya Katrepe – Kocaeli, inatarajiwa
kuodoka kesho jumanne saa 1 jioni nchini Uturuki kurejea nyumbani kwa
usafiri wa shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili
uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 9 kasoro usiku.
Mara baada ya kuwasili Dar es
salaam timu itaendelea na kambi kwa kufanya mazoezi mepesi siku ya
jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas
Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo wa
siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria.
SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA RASMI saa 6:00 usiku.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa
(Mb), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika rasmi
tarehe 1/9/2015 kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na ya Miamala ya
Kielektroniki za Mwaka 2015. Anayeangalia ni Bwana John Mngodo, Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
(Mb), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika rasmi
tarehe 1/9/2015 kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na ya Miamala ya
Kielektroniki za Mwaka 2015. Anayeangalia ni Bwana John Mngodo, Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano huo.
TASWA FC, TASWA QUEENS WAMALIZA ZIARA YAO YA MKOA WA ARUSHA NA TANGA BILA KUFUNGWA, TASWA QUEENS WAIBUKA MABINGWA WA BONANZA LA TASWA ARUSHA.
Mchezaji
wa Taswa Fc, Julius Kihampa (kushoto) akikokota mpira wakati wa mchezo
wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha dhidi ya timu ya IMS Maji ya Chai,
kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mchezaji
wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimdhibiti mchezaji wa timu ya Chuo
cha waandishi wa Habari cha AJTC wakati wa mchezo wao. Katika mchezo
huo Taswa
Queens, ilishinda mabao 37 – 3
Queens, ilishinda mabao 37 – 3
Nahodha wa timu ya Taswa Queens, Zuhura Abdulnoor, akipokea Kikombe cha ushindi kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa
Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa
Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
wanaounda timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania, Taswa Fc na Taswa
Queens, wakimsikiliza Afisa wa Hifadhi ya Michael Ngatolu, wakati walipotembelea kwenye hiyo,
walipokuwa katika ziara ya kuhitimisha Bonanza la 10 la Taswa Arusha
lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
Queens, wakimsikiliza Afisa wa Hifadhi ya Michael Ngatolu, wakati walipotembelea kwenye hiyo,
walipokuwa katika ziara ya kuhitimisha Bonanza la 10 la Taswa Arusha
lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
**********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Arusha
TIMU ya
Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo
kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya
siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.
Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo
kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya
siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.
Aidha timu
hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka
kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha
yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha
Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Continue reading →hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka
kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha
yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha
Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
SERIKALI kuimarisha miundombinu ya reli
………………………………………..
Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejidhatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu Tsh. Trilioni 16 katka luleta maendeleo endelevu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dare s salaam waziri wa uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa mkakati ni kuinarisha reli katika maeneo mbalimbali nchini.
Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songeaa hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
“Lengo la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.
Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.
Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.
Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejidhatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu Tsh. Trilioni 16 katka luleta maendeleo endelevu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dare s salaam waziri wa uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa mkakati ni kuinarisha reli katika maeneo mbalimbali nchini.
Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songeaa hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
“Lengo la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.
Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.
Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.
MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA QATAR NA BURUNDI LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al
Maadadi wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu
Dar es salaam leo Agost 31,2015 kwa lengo la kujitambulisha rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi wakati
Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es
salaam leo Agosti 31, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha
ya pamoja na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al
Maadadi wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake
Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati
Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam
leo Agosti 31,2015 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa
kazi hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Balozi huyo
alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo
Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha
ya pamoja na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka
wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu
Dar es salaam leo Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza
muda wake wa kazi hapa Nchini.
(Picha na OMR)
Rais Kikwete Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa National Defence Headquarters
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi muda mfupi baada
ya kuwasili eneo la Lugalo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa National
Defence Headquarters.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali
Davis Mwamunyange akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika
hafla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa National Defence
Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Makamanda wa Jeshi la Ulinzi wakati
wa uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la
Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam
leo.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange,Watatu Kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt.Huessein Ali Mwinyi
na kulia ni Bwana Hu mwakiklkishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiteta jambo na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange
wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa National Defence
Headquarters Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa
majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini
Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
(Picha na Freddy Maro)
WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI WAIOMBA SERIKALI IPUNGUZE ADA YA LESSENI.
…………………………………..
Wanawake Wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Tanga,Singida
,Manyara na Morogoro wameiomba serikali ipunguze ada ya leseni ya
uchimbaji madini ili kuwawezesha kinamama wanaoanza kazi hiyo
wasikwame kiuchumi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya bei kubwa ya
vifaa vya uchimbaji pamoja na ukosefu wa mitaji.
Kinamama hao ambao wameamua kujikita kwenye shughuli za
uchimbaji wa madini wameiomba serikali isikie kilio chao cha muda mrefu
licha ya sekta hiyo ngumu bado inawasaidia kinamama kujikwamua kiuchumi
na kuondokana na umasikini.
Pili Hussein ni mwanamama wa kwanza kuzama katika migodi ya
Mirerani na kuchimba madini ambaye kwa sasa ni mmiliki wa kitalu cha
madini amesema kuwa gharama kubwa za uendeshaji wa migodi zimekua
zikirudisha nyuma juhudi za kinamama hivyo ameiomba serikali na
mashirika binafsi kujitokeza kuwasaidia kinamama kupata mikopo
itakayoiwasaidia kuendesha shughuli za uchimbaji
Wakizungumza katika jukwaa la kinamama wachimbaji wa madini
linaloendelea mkoani Kilimanjaro lilioandaliwa na shirika lisilokuwa
la kiserikali la Hakimadini ,jukwaa lenye lengo la kuunganisha sauti na
nguvu ya kinamama katika kutetea haki zao hususan katika sekta ya
madini na kunufaika ipasavyo,Mwansy Shomari ni Mchimbaji wa Madini aina
ya Ruby kutoka eneo la Kalalani mkoani Tanga amesema kuwa licha ya
changamoto wanazozipitia mfumo dume umekua ukiwakwamisha kinamama kupiga
hatua kiuchumi hususani katika sekta ya madini iliyotawaliwa na mfumo
dume kwa kipindi kirefu
Kwa upande wake Meneja Programu wa Shirika la Hakimadini
,David Ntiruka amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kukusanya
sauti ya kinamama wachimbaji pamoja na changamoto zao ili kuzifikisha
kwenye vyombo husika viweze kufanyiwa kazi
Mwamko wa wanawake kujihusisha na shughuli za uchimbaji
madini bado unakua na kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo
wanawake wachache walithubutu kujihusisha na uchimbaji ,kutokana na
kuongezeka kwa uelewa juu ya haki ya kunufaika na madini kwa jinsia zote
wanawake wengi wanashiriki katika uchimbaji madini.
CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. |
Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo. |
UVCCM WASHAURIWA KUSHAWISHI WENZAO KUKIPA USHINDI CCM
Katibu wa UVCCM Wilaya ya
Mfenesini Haji Machano Juma akisisitiza jambo katika Semina elekezi kwa
Vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja. Kulia
kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Khamis Ali, Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya hiyo Mbarouk Mrakib, na Mlezi wa kundi maalum na Mbunge
wa Vijana Tauhida Galos.
Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Baadhi ya Vijana wa UVCCM kutoka
Wilaya ya Mfenesini wakifuatilia Mada kutoka kwa Viongozi wao hawapo
pichani katika Semina elekezi kwa Vijana hao kuelekea Uchaguzi Mkuu
iliyofanyika Uroa Kusini Unguja.
………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Vijana wa Chama cha Mapinduzi
UVCCM wamehimizwa kuendelea kuwashawishi WanaCCM wenzao na wale wa Vyama
vya upinzani kuipigia kura CCM ili Chama hicho kiendelee kutawala Bara
na Visiwani.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa
Umoja huo wa Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib wakati akitoa mada
katika Semina elekezi kwa Vijana iliyofanyika Uroa kusini Uguja.
Amesema Vijana ndio watetezi
wakubwa wa Chama nakwamba juhudi zao zinahitajika zaidi kipindi hiki cha
kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho
kuliko miaka ya nyuma.
“Tusisahau wajibu wetu ambao ni
kumshawishi kila Mpiga kura bila kujalisha chama chake aipigie kura ya
Ndio CCM kwani ni Chama pekee chenye Nia thabiti ya kuleta mabadiliko ya
Kiuchumi” Alisema Mrakib.
Kwa upande wake Mlezi wa kundi
maalum ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Tauhida Galos Cassian
amewaomba Vijana wa CCM kuwa na msimamo bila ya kuyumbishwa na Vyama vya
upinzani.
Amesema vyama vyote vinakimbilia
kundi la Vijana kwa vile ndio kundi kubwa na jepesi kushawishika hivyo
kuwasisitiza Vijana hao kuendelea kuiamini CCM ambayo ndio Mkombozi wa
Uchumi.
“CCM imefanya mengi katika Nyanja
mbalimbali ikiwemo Elimu, Uchumi, Miundombinu na Michezo hivyo Wananchi
wanakila sababu ya kuendelea kuiamini ili izidi kuleta maendeleo”Alisema
Tauhida.
Akifungua Mafunzo hayo Mgeni Rasmi
wa Semina hiyo Khamis Ali ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa NEC amewataka Vijana hao kushirikiana na kuyatekeleza yale
wanayoambiwa na Viongozi wao.
Naye Katibu wa UVCCM Wilaya ya
Mfenesini Haji Machano Juma amewaomba Vijana walioshiriki Semina elekezi
kuhakikisha Wanatoa elimu kwa Vijana wengine ambao hawakushiriki Semina
hiyo.
Semina hiyo ya kuwajengea uwezo
Vijana hao juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi na wajibu wao ili
kufanikisha Ushindi kwa Chama cha Mapinduzi ilifanyika Mwisho wa Wiki
katika Hoteli ya Coconut Uroa Kusini Unguja.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
KANYAGA-TWENDE YA MAMA SAMIA YAMALIZIKA SINGIDA NA KUANZA DODOMA
Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais ka tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu
Hassan, akitoka Singida mjini kwenda Dodoma, kupitia Ikungi na Manyoni
kufanya mikutano ya kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi, Gishuli Charles, alipowasili
eneo la Makyungu, kufanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida
Kaskazini lililopo katika wilaya hiyo ya Ikungi. Kushoto ni Katibu wa
CCM, Ikungi, Aluu Sagamba.
Wananchi wakimshangilia Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama
Samia Suluhu Hassan alipowasili eneo la Makyungu kuhutubia mkutano wa
kampeni katika jimbo la Singida Kaskazini, wilayani Ikungi.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Makyungu jimbo la Singida Kaskazini
Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Kone akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi.
Kada
wa CCM aliyeko katika kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya
CCM akionyesha furaha kutokana na mambo kwenda vizuri katika mkutano wa
kampeni wa Makyungu,jimbo la Singida Kaskazini. Continue reading →
PSPF WATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI YA MADEREVA WA BODABODA WA KIPUNGUNI
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G
Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha
Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar.
Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya
Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya
Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda
wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akitoa somo kwa madereva bodaboda kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari(PSS) waliofika katika mchezo wa fainali katika uwanja wa Kipunguni B
Mmoja wa Madereva Bodaboda akiendelea kupewa faida za mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto)
Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijisajili kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) kwa ajili ya kuendelea kupata huduma zilizobora na zenye uhakika kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy .
Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijiunga kwenye mfuko
wa (PSPF) kupitia (PSS) ambapo kila mtu anaweza kujiwekea akiba kupitia
kwenye mfuko huo wa hiari wakati wa mchezo wa fainali.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akiwasajili madereva wa Bodaboda kwenye mfiko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) wakati wa mchezo wa fainali wa Madereva bodaboda ambapo G Unity aliibuka mshindi kwa kumchapa Sukuma Land bao 5-2
Continue reading →MKUTANO MAALUM WA ELIMU SACCOS WAFANYIKA ZANZIBAR.
Mwenyekiti wa Elimu Saccos Ahmedi
mohd akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika Mkutano maalum
wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanzibar.
Mgeni Rasmi Mrajisi wa vyama vya
Ushirika Hamis Daudi Simba akitoa hotuba ya ufunguzi katika mkutano wa
maalum wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanziobar,kulia yake ni
Mwenyekiti wa Elimu Saccos Ahmed Mohd na kushoto yake ni Katibu wa Elimu
Saccos Salma Simai.
Baadhi ya Wanachama wa Elimu Saccos waliohudhuria katika Mkutano maalum wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
UN YAFANYA USAFI SOKO LA TEMEKE STEREO KUADHIMISHA MIAKA 70
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema
(katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto
ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
KATIKA
kuadhimisho miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN)
wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa walijumuika na wakazi wa
Temeke katika kufanya usafi kwenye soko la Temeke Stereo.
Shughuli
hiyo wameifanya baada ya wiki iliyopita kufanya shughuli za upandaji
miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro. Wakiwa katika miteremko ya
milima Kilimanjaro walipanda miti 2,000.
Shughuli hizo za kufanya usafi ambazo ziliongozwa na Mratibu wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, zilifanyika
katika juhudi za kuleta uhalisia wa utunzaji wa mazingira kama umoja huo
unavyofanya.
Akizungumza katika shughuli hizo Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,
ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa
kusherehekea miaka 70.
“Nachukua nafasi hii kupongeza watu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania
kwa kufanya shughuli mbalimbali kuelekea maadhimisho ya miaka 70 kwa
kupanda miti 2,070 kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na hili tendo
la leo la usafi kama mwendelezo wa kaulimbiu inayohimiza utunzaji wa
mazingira ya“ Sayari moja, watu bilioni 7: Ulinzi wa mazingira ni wajibu
wetu,” alisema.
Akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na usafi, Mkuu huyo wa wilaya alisema wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ikiwemo
kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi na wafanyabiashara
wa soko la Temeke Stereo mwishoni mwa juma. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi
Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto. Wa tatu kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa
Wilaya Temeke, Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Celestine Mushy (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Usafi na
Mazingira manispaa ya Temeke, Ally Hatibu. Continue reading →
MGOMBEA MWENZA WA UKAWA JUMA DUNI HAJI AHUTUBIA WAKAZI WA MTWARA
Mgombea
urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Juma Duni Haji
akisalimiana na wakazi wa wilaya ya Newala baada ya kuhutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Diesel mkoani Mtwara.
Umati wa wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Ukawa uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara.
Mgombea
Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya
wakazi wa kakazi wa mjini Mtwara katika mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara.
Mamia
ya wakazi wa Mtwara wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Ukawa
uliohutubiwa na mgombea Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji
katika uwanja wa Mashujaa Mtwara.
Mgombea
Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya
wakazi wa kakazi wa mjini Mtwara katika mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara.
Wananchi wakiwafuatilia hotuba ya Mgombea Mwenza wa Ukawa Juma Duni Haji.
Mgombea Mwenza wa Ukawa, Juma Duni Haji akimtambulisha na kumuombea kura mgombea wa ubunge wa Newala mjini.
LOWASSA AUNGURUMA MKOANI IRINGA
Sehemu
ya Wafuachi wa CHADEMA na Vyama vinge vinavyounda UKAWA wakiupokea
msafara wa Mgombe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania
katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ulipokuwa ukiwasili Mafinga Mjini,
kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 30, 2015.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
akiwapumbia maelfu ya wananchi wa Mji wa Mafinga, Wilayani Mufindi
Mkoani Iringa, waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Wambi,
Mafinga Mjini, Mkoani Iringa Agosti 30, 2015.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai, wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa Agosti
30, 2015, kuliofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Waziri wa zamani wa
Elimu, Mh. Joseph Mungai, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Wambi,
Mafinga Mjini, Mkoani Iringa Agosti 30, 2015, kuliofanyika Mkutano wa
Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika
mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa.
Sehemu
ya Umati wa wananchi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi, wakionyesha
fuaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika
mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 30,
2015.
Waziri
wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mh. Lawrence Masha akihutubia
kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa Agosti 30, 2015.
Continue reading →MWIGULU AWAHAKIKISHIA WANABUKOMBE KUWA CCM ITASHINDA KWA KISHINDO 2015
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg.Msukuma “KING”
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Bi.Vick Kamata akiwashukuru na kuomba kura kwa Wananchi wa Bukombe wampigie J.P.Magufuli ifikapo tar.25.10.2015
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg.Joseph Msukuma akizungumza na Wananchi wa Bukombe kuwa yupo tayari kuzunguka Nchi nzima kuinadi Ilani ya CCM,Pia kumnadi Mgombea Urais wa CCM Dk.J.P.Magufuli kwasababu ndiye Mgombea pekee mwenye dhamira ya dhati yakuwatumikia watanzania tangu akiwa Naibu Waziri.
“Tunahitaji Rais Mchapa kazi,sio Rais aliyezungukwa na Genge la wapiga Dili”Mwigulu.
Sehemu ya Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Bukombe.
Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Bukombe Mkoa wa Singida wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi.
“CCM ni Ile Ile”
Wanabukombe wakifurahia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi,Wameahidi kuwa Miaka 5 walioyokuwa na Prof.Kahidi wa CHADEMA imekuwa yauchungu sana kwao,Hivyo kwa Uchaguzi huu kura zote kwa Dotto wa CCM.
Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mwaka2015 ambayo Madiwani,Wabunge na Mgombea Urais wa CCM ataitumia kutekeleza Shughuli za Maendeleo Nchini Tanzania.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe Ndg.Dotto Mashaka.
Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano huo.
Picha na Sanga Jr.
No comments :
Post a Comment