Saturday, September 19, 2015

BARAZA LA VYUO VIKUU AFRIKA MASHARIK(IUCEA)KUWA NA MAONESHO YA VYUO VIKUU UGANDA

MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU (CCM) YUSUF MANJI AZINDUA KAMPENI ZAKE DAR ES SALAAM

 Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia (kulia), akimtambulisha Yusuf Manji katika uzinduzi huo.
 Mgombea nafasi ya udiwani Kata ya Mbagala Kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Manji (kushoto), akihutubia wananchi na makada wa chama hicho katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika eneo la Kichemuchemu Kaskazini Dar es Salaam leo jioni.
  Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia, akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Mchumi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Urio akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Kada wa CCM, Godbertha Kinyondo akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
 Makada wa CCM wakiserebuka
 Vijana wa hamasa wa CCM wakiwa kazini.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Michango mbalimbali ikitolewa.
 Umati ukimsikiliza Yusuf Manji.
 Mkazi wa eneo hilo, Sharifa Ali akimueleza Manji kuhusu kero ya kutokuwa na soko.
 Dogo akihubia kwenye uzinduzi huo. Dogo huyo alisema wana CCM wanapaswa kumchagua Magufuli kuwa Rais, Mbunge Mangungu na Diwani Manji.
 Chipukizi wakifanya vitu vyao.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Yusuf Manji (kulia) akifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo. 

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WA AFRIKA KUSINI SIPHO MWAKABANE KUSHIRIKI TAMASHA LA KUOMBEA AMANI OKTOBA 4 MWAKA HUU.

 Mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusina na Msanii wa Afrika Kusini,Sipho Mwakabane ambaye atatumbuiza katika tamasha  Oktoba 4 mwaka huu. Pia amesema kuwa msanii huyo wa nyimbo za Injili wa kimataifa. Na kulia ni Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga.
Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salam amesema kuwa watanzania wote bila kujali kabila, rangi na dini zote wajitokeze katika tamasha hilo la kuombea amani ambapo viingilio ni sawa na bure kabisa watu wazima kwa nafasi ya VIP wataingia kwa shilingi elfu tano (5000), kawaida elfu tatu (3000) na watoto ni shilingi elfu moja(1000)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza  Mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama leo jijini Dar es Salaam.
……………
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Afrika kusini, Sipho Mwakabane kuwa atashiriki tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza
na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama.


Msama alisema watoto watachangia shilingi 1000 ambako alitoa wito kwa
Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani
katika nchi yetu.

Msama alisema katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi
hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagia maombi hayo
aidha
Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu,
tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania
kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.


“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo
ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu
ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
Alisema baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo
litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba
11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora),
Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).

Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Nchini -lafana

1
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi katika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi wa Mfuko huo Bi Matilda Nyallu.
Picha na Benjamin Sawe
2
Wafanyakazi wa Mfuko waMfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa katika Banda la Mfuko huo wakatikatika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchinikabla yauzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa kwanza kulia ni Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe.
4
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi akizindua Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini lililofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida Waziri.
5
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi akimlisha keki Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida Waziri katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini mara baada ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania.

Nyalandu kuzindua kampeni zake SINGIDA

unnamedNa mwandishi wetu
…………………………..
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, leo anazindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya kutetea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini.
Nyalandu, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka 15 sasa, anawania tena nafasi hiyo wakati akiwa na rekodi yenye kujivunia kutokana na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Eliah Digha, alisema uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika Kata ya Mtinko jimboni humo.
Alisema Nyalandu alichelewa kuzindua kampeni hizo kutokana na kuwa na majukumu mazito ya kichama na kiserikali na kwamba, wananchi walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa siku hii ya leo.
Digha, ambaye pia ni mgombea udiwani katika Kata ya Msange, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uzinduzi huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni Nyalandu kupanda jukwaani na kuzungumza na wapigakura wake.
“Tunazindua kampeni zetu rasmi leo katika Kata ya Mtinko na baada ya hapo ni nginjanginja mpaka uchaguzi…hatutakuwa na muda wa kusimama hivyo, wapinzani wajiandae kwani hakutakuwa na mapumziko wala mtu kuomba poo. Wametaka kujaribu muziki wa Nyalandu sasa ndio wamewekewa hivyo kama hawajajipanga itakula kwao,” alisema Digha.
Alisema uzinduzi huo utapambwa na vikundi mbalimbali vya burudani kutoka mkoani Singida na kwamba, shughuli nzima itaanza saa nne asubuhi.
Kwa upande wake, Nyalandu alisema atatumia mkutano huo kueleza mafanikio yote yaliyopatikana na mikakati yake mipya ya kuendelea kulivusha jimbo hilo kimaendeleo.
Amesema katika kipindi cha uongozi wake, kwa kushirikiana na wananchi wake wamefanya mambo makubwa kwenye sekta zote muhimu ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii ikiwemo kuwawezesha vijana na akinamama kuanzisha miradi ya ujasiriamali.
Nyalandu, ambaye ni miongoni mwa makada 32 wanaounda timu ya ushindi ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amesema hana shaka na ushindi mwaka huu.
Amesema wagombea wa CCM kuanzia wa urais, wabunge na madiwani wataibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na historia ya utendaji kazi itaendelea kuwainua.
“Dk. Magufuli ana historia ambayo haina utata kuanzia kwenye utendaji kazi hadi uadilifu wake hivyo si wa kufananisha na wagombea wengine kwenye nafasi ya urais. Nyalandu anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge akiwa na historia ya kujivunia mbele ya wapigakura wa Singida Kaskazini…vivyo hivyo kwa madiwani wa CCM ambao wanagombea kwa ajili ya kuwatumia watu na si kwa maslahi binafsi kama walivyo wapinzani,” alisema Nyalandu.
Aidha, ametua fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo na kusikiliza mikakati yake mipya kwa ajili ya maendeleo ya Singida Kaskazini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(IUCEA)Profesa Mayunga Nkunya akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha jana kuhusu hali ya wahitimu katika nchi za Afrika Mashariki na ushirikiano wa Baraza la Wafanyabiashara Afrika Mashariki(EABC) kuwajengea uwezo wahitimu ili kumudu soko la ajira .Taasisi hiyo itakuwa na maonesho ya vyuo katika nchi za EAC  Kampala ,Uganda mwezi Oktoba ,2015.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki(EABC)Lilian Awinja akizungumza katika mkutano huo.

Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini kwaajili kuuhabarisha umma.

CHIKU ; Heri ya Monica Mbega alileta maendeleo jimbo la Iringa mjini kuliko mchungaji Msigwa

unnamedNa Franci Godwin,Iringa
……………………………..
MGOMBEA  Ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia ACT Wazalendo Bi Chiku Abwao(pichani) amesema heri ya miaka mitano ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mobica Mbega ( CCM) kuliko miaka mitano ya Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)hivyo ametawa mwaka huu wananchi kumchagua yeye
Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni za Ubunge jana  kata ya Kihesa alisema iwapo atakuwa mbunge wao atahakikisha anakuwa mbunge wa mfano wa kuwaletea maendeleo sahihi.
Kwani alisema kuwa historia ya jimbo hilo mwaka 1995 walichagua NCCR mageuzi ambapo Bw Mfalamagoha Kibasa kuwa mbunge ila baada ya kushindwa kutekeleza ahadi zake mwaka 2000 walimchagua Monica Mbega ( CCM) ambae kipindi cha kwanza alifanya Kazi vizuri na mwaka 2005 wananchi walimchagua tena ila hakuweza kufanya Kazi ndipo walipomchagua Mchungaji Peter Msigwa( Chadema) ambae hajafanya Kazi yoyote.
Hivyo  alisema  kwa  sasa imani yake  juu ya  wanaume  kuwa  wabunge  katika   jimbo  hilo haipo  tena kwani hawana nia ya  kweli ya  kuwatumikia  wananchi na  kudai kuwa  iwapo  mbunge  aliyemaliza  muda  wake mchungaji Msigwa angetekeleza ahadi  zake vema  leo asingesimama kugombea  ubunge bali  angemuunga  mkono mbunge   huyo ili  aendelee  kwa  kipindi  cha  pili  ila kwa  kuwa hakuna jipya  alilolifanya hana imani nae na  hivyo ni  wakati wa  wananchi wa  jimbo  hilo  kuwapima wagombea  wengine waliojitokeza nje  ya mbunge  huyo .
Alisema ahadi  za  mbunge  aliyemaliza muda  wake  zilikuwa zaidi ya 14  ikiwemo ya  kuwawezesha wananchi  waliojiunga katika  vikundi  kupatiwa  mitaji ya  kuanzisha  biashara  kwa  wakati  huo  alisema  yeye  si mbunge  wa  kutoa pesa bali atawawezesha  kiuchumi kwa  kuwapa nyavu  (mitaji) ila baada ya  kuwa mbunge alianza  kuwasema  vibaya  wananchi kwa kudai yeye  si mbunge wa  kutoa  pesa (ATM)pia  aliahidi  ujenzi  wa  soko la kisasa  Kihesa  na  kumweka mwanasheria  katika  ofisi  yake  ila hadi  sasa hakuna alichofanya na  akikumbushwa  hukimbilia  kujenga  chuki na  kila mtu .
Bi  Abwao  ambae  amepata  kuwa  mjumbe wa kamati  kuu ya Chadema  Taifa na  mbunge  wa viti maalum  mkoa  wa Iringa  kupitia Chadema  alisema  kuwa hali ya chadema na UKAWA  kwa  sasa  imepoteza mwelekeo na  chadema kugeuka ni  chama  cha kutetea  mafisadi   tofauti na  iliyokuwa awali kuwa chama cha  kupinga  ufisadi .
Hivyo  alisema  sababu ya  kukihama  chama  hicho na  kujiunga na ACT  wazalendo ni kutafuta  chama cha  upinzani makini ambacho atawatumikia wananchi  bila ya kuwajengea maswali kama  ilivyo  hivi  sasa kwa  mgombea  wa Chadema Iringa mjini mhungaji Msigwa ambae alikuwa mbele  kupinga ufisadi na hata  kusema  wanaomuunga mkono aliyekuwa  waziri  mkuu Edward  Lowassa ambae ni mgombea wa Chadema kwa  sasa wakapimwe akili  zao .
Alisema Chadema  kwa  sasa  imekuwa ni  chama  cha kupiga  dili akiwemo  aliyekuwa  mbunge wa  jimbo hilo Mchungaji Msigwa ambae leo kati ya maswali magumu ambayo anahojiwa  na  wapiga  kura  wake ni  juu ya kauli  yake  dhidi ya wale  wanaomuunga mkono  LOwasa  kutakiwa  kupimwa akili  zao.
Akielezea  kuhusu  sera  zake  kwa  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini iwapo  watamchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo atahakikisha anautumia  vema  mfuko  wa  jimbo kwa  kuwasaidia  wazee ,vijana na  wanawake  kuwa na  vikundi  vya kiuchumi tofauti na  ilivyokuwa awali miaka  mitano iliyopita  kwa  mfuko  huo kushindwa  kufanya kazi  yoyote.
Pia  kuhakikisha  anaibana  serikali  ili vijana  kupewa mikopo  nafuu na  kuzuia posho kwa  watumishi  wa umma ambazo  zimekuwa  zikikwamisha maendeleo katika  jimbo  hilo .

Dk Shein Aendelea na Kampeni Zake na Kusema Ataendeleza Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Kuleta Maendeleo Zaidi kwa Wazanzibar katika Wananchi Wake na Elimu Bure Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Mpira Konde Kisiwani Pemba kuendelea na Kampeni Kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa Kampeni zake kisiwani Pemba.
Taswira ya wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia CCM katika viwanja vya mpira Konde Pemba kama inavyooneka Mwanachama huyu wa CCM akishangilia akiwa na picha ya Mgombea Urais wa CCM Dk Shein.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo Zanzibar katika kipindi chake Dk Shein cha miaka mitano na kuwataka kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar katika sekta mbalimbali za Jamii

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.
Katibu wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu akiwahutubia Wananchi wa Konde katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika katika uwanja wa mpira Konde Kisiwani Pemba.

HAPPY BIRTHDAY KAMANDA RAS MAKUNJA

v
Siku kama ya leo 19 September ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja aka mkuu wa viumbe wa ajabu “Anunnaki Alien” alizaliwa mjini Dar-es-Salaam,
akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja),
Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja mtunzi na mwimbaji  mahili wa muziki wa dansi leo ndio Happy Birthday !!!!! yake
pia unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni at

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA KONDE KASKAZINI PEMBA

1
Naibu katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali Vuai akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika Mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
Picha zote na Ikulu.
3
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika Mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
4 5
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Naibu katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali Vuai wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
6 7
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
8
Kikundi cha Kwaya kitwacho DK.Salmin cha Konde Wialaya ya Micheweni wakitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwanadi wagombe wa Ubunge,Uwakilishi na Udiwani  kwa wananchi,mkutano uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,[
9
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Bw.Mberwa Hamadi Mberwa wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na kuwanadi wagombea ngazi mbali mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na Udiwani.
10
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwa na Picha la Mgombea Urais wa Ranzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na kuwanadi wagombea ngazi mbali mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na Udiwani,
11
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakionesha picha za Mgombea Urais wa Ranzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na kuwanadi wagombea ngazi mbali mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na Udiwani,
13
Wajumbe wa jumuiya ya wanawake wa Mkoa wa kaskazini Pemba wakiwa katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika uwanja wa Mpira Konde Mjini na kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

TPB YAKADIDHI JENGO LA KITUO CHA AFYA PEMBA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud (Wanne kushoto waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Litice Rutashobya, (watatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanakijiji, mbele ya jengo la Kituo Cha Afya, Ungi, Shehia ya Msuka Mashariki, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya TPB kukabidhi jengo hilo kwenye hafla iliyofanyika Sptemba 17, 2015. Kituo hicho kimekamilishwa ujenzi wake na TPB.
Waziri Abloud, akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa kituo hicho. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Letice Rutashobya, (katikati mwenye miwani) na Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika wa TPB, Noves A. Moses
Waziri Aboud, (wapili kulia), Profesa Letice Rutashibya, (wapili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Suleiman Haji, wakibadilishana mawazo mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo la Kituo cha Afya

DR. JOHN POMBE MAGUFULI AHANI MSIBA WA MWALIMU WAKE MAREHEMU COLNER PASTOR KIJIJI CHA NYAKATUNTU BIHARAMULO

01
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Colner PaStor mwalimu aliyemfundisha katika shule ya msingi ya Chato,  Dk. Magufuli alionekana mwenye huzuni kutokana na kifo cha mwalimu wake huyo wakati alipohani msiba huo katika kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo mkoani Kagera.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-BIHARAMULO)
1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimfariji mama Paskazia Mufuruki mjane wa Marehemu mwalimu Colner Pastor wakati alipohani msiba huo katika kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo loe
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Father Erasto Nakule mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Colner  Pastor.
3
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Father Anthony mara wakati alipohani msiba wa Marehemu mwalimu wake Colner Pastor.
5
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akishiriki katika sara ya kumuombea marehemu.
6
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ndugu Abdallah Bulembo akishiriki kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu mwalimu Colner Pastor.
7
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake katika kaburi la aliyekuwa  mwalimu wake marehemu Colner Pastor.
8
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa  CCM Biharamulo.
10
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli wakati akihutubia mjini Biharamulo.
11
Amona Mpanju kwa mbali akihutubia katika mkutano huo
12
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika mjini Biharamulo.
13 14 15 16
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo mjini Biharamulo.
17
Wananchi wakipunga mikono yao juu kutokana na kufurahishwa na hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
18
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Biharamlo Ndugu Oscar Mkasawakati.
19
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Biharamulo na wahgembea wa viti maalum mkoa wa Kagera.
20\
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wana
21 22 23 24 25 26 27 28
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi katika kijiji cha

WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.

indexaNa. Jovina Bujulu –MAELEZO.Dar es salaam.
………………………………….
Wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi kote nchini wameshauriwa  kuongeza bidii katika kujifunza masomo hayo ili kuendana na  juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwawezesha wanafunzi hao  kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli Manyele kwenye sherehe ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia  kwa mwaka 2013 na 2014.
“Kama wachunguzi wa Serikali ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na Biolojia tumeona ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo ya Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.
Amesema Zoezi la kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na Biolojia limeanzishwa  kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.
Aidha, amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha vipaji vyao vya masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua kuwa Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule mbalimbali za Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo Fedha, Vyeti na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa upande wa wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.
Kwa upande wa Wanafunzi waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza, Marian, Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko jijini Mwanza.
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007  chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Bioloji.

WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU KUFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)

indexNa Beatrice Lyimo Maelezo Dar Es Salaam.
………………………………….
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe  za hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na  matumizi ya madawa ya kulevya.
Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya kemia na biolojia kwa mwaka 2013-2014 iliyofanyika leo Ijumaa (Septemba 18, 2015), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Dkt Donan Mmbando alisema hatua hiyo ni mkakati wa serikali wa kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Dkt Mmbando alisema  Wizara kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa mchango mkubwa wa uchunguzi wa kimaabara kuweza kutambua dawa za kulevya na pia kuwatambua waathirika wa dawa hizo.
“Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa kazi zinazofanywa na wakala wa maabara na mkemia mkuu wa serikali katika kulinda afya na usalama wa watu na mazingira pamoja na kuleta uelewano katika jamii” alisema Dkt Mmbando.
Aidha alisema serikali itaendelea kuitegemea Taasisi hususani katika utaalamu kwa utatuzi wa masuala yanayohusiana na kulinda afya na usalama wa jamii, hivyo itahakikisha inaiwezesha taasisi hiyo katika mahitaji ya rasilimalli watu na fedha.
Aidha Dkt Mmbando aliwapongeza walimu na wanafunzi wote waliofanya vyema katika mitihani yao na kuwakumbusha juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanaweza kufuta ndoto ya kuwa nguvu kazi ya taifa.

Watakao Hujumu Miundombinu ya DART Kulipa faini ya laki tatu.

x1
Mkurugenzi wa Mifumo Junn Mlingi kutoka Taasisi ya Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport) akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo katika kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
x2
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda gari la Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jana jijini Dar es Salaam katika ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi wa DART kabla ya kuanza kutumika .
x3
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
x4
Mmoja wa Afisa wa Tanroads akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
x5
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
………………………………………
Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam (DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.
Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.
“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.
Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.
Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden Dragon kutoka Japan.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA KUPOKEA MISAADA YA VIFAA MBALIMBALI KUSAIDIA SHULE MPYA YA MSINGI KAKUNI MKOANI KATAVI.

1
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta mpakato zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo jijini Dar es salaam. Shule hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia  wazo la Wazo la Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya kisasa katika kijiji hicho na inajengwa kupitia michango na misaada ya wadau mbalimbali.
2
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
3
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezi vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
4
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho  kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi .
5
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya msingi Kakuni mkoani Katavi, ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
6
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.

WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. MILIONI 330 KWA SHULE ALIYOSOMA

imagesWAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea misaada ya zaidi ya sh. milioni 330 kwa ajili ya shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.
HUAWEI na NMB zimetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya msaada huo yaliyofanyika leo mchana (Ijumaa, Septemba 18, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meneja Uhusiano wa kampuni ya HUAWEI, Bw. Jin Liguo alisema kampuni yake inaamini msaada huo utasaidia kupunguza tofauti za kiteknolojia zilizopo kwenye sekta ya elimu.
“Kampuni ya HUAWEI iko Tanzania tangu 2001 na imedhamiria kufanya kazi na wanajamii kila inapoona imepata fursa ya kufanya hivyo, na hasa katika elimu ambako pia tumelenga kupunguza tofauti za kiteknolojia zinazojitokeza kwenye sekta hiyo,” alisema Bw. Liguo.
Kampuni hiyo imetoa kompyuta za mezani 50, HUAWEI Tablets 100, Laptop tano, Printers mbili, Scanner mbili, Projector mbili, Projector Screens mbili, Power System seti moja na Audio System seti moja vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 150,000 (sawa na sh. milioni 300).
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Bw. Waziri Barnabas alisema benki hiyo imelenga kukuza michezo shuleni na ndiyo maana imeamua kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa shule hiyo ya Kakuni.
Benki ya NMB imetoa kompyuta nne; jezi za michezo jozi 192 (soka 72, wavu 40, kikapu 40 na pete 40); mipira 40 (soka 10, wavu 10, kikapu 10 na pete 10). Pia imepanga kuchangia ununuzi wa madawati yenye thamani ya sh. milioni 10 ambayo alisema yapo tayari ila yanasubiri ujenzi wa kituo cha walimu ukamilike. Vifaa hivyo vina thamani ya sh. Milioni 30.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliwashukuru wawaklishi wa HUAWEI na Benki ya NMB kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.
“Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha leo mbele ya waandishi wa habari.
“Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani wanafunzi waliopo ni wengi kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 800. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” aliongeza.
Waziri Mkuu alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto aliyokuwa nayo.
Alisema aliishirikisha Halmashauri kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh. bilioni 1.3/-.
Alisema alipeleka barua kuomba michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 785 na dola za Marekani 267,834 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi amebakiza kiasi cha sh. milioni 40 na dola za Marekani 117,495.
“Katika kuanza zoezi la kukusanya fedha Aprili 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh. milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi – Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza gharama,” alisema.
Hadi sasa majengo yaliyokamilika ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na majengo mawili ya vyoo yenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua za mwisho. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba 18 za walimu, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi, kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.
Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali. Vyote hivi alisema vitagharimu sh. bilioni 2.18.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, SEPTEMBA 18, 2015

FDL KUTIMUA VUMBI KESHO

FDLLigi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na  Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

kumaizikaLigi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

MAJAMBAZI WANNE WAUAWA KWA RISASI ARUSHA-Wakutwa na AK 47 mbili, SMG moja, bastola tatu na Radio “call” mbili za Polisi

6
Wakutwa na AK 47 mbili, SMG moja, bastola tatu na Radio “call” mbili za Polisi.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
…………………………………..
Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa na askari Polisi wakati wa mapambano ya majibizano ya risasi usiku wa tarehe 17.09.2015 saa 3:30 maeneo ya Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na halmashauri ya Jiji la Arusha.
1
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi. Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Sabas alisema Jeshi hilo lilipokea taarifa za Kiintelejensia juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi lililotaka kufanya uvamizi na uporaji ndani ya jiji la Arusha.
“Tulipata taarifa toka tarehe 19.08.2015 mwezi mmoja nyuma juu ya uwepo wa kundi la majambazi toka nchini Kenya ambao wangeshirikiana na wengine wa hapa nchini kwa nia ya kufanya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo taasisi za fedha”. Alisema Kamanda sabas.
2
“Baada ya taarifa hizo tukaendelea na ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtu aitwaye Sixtus Alfredy Ngowi (51) Mtanzania, Mkazi wa Ngulelo jijini hapa ambapo baada ya mahojiano alikiri kwamba huwa anashirikiana na majambazi wenzake toka nchini Kenya katika kufanya matukio mbalimbali ya kiuhalifu hapa nchini”. Alifafanua Kamanda Sabas.
3
Baadhi ya matukio ambayo ameyafanya ni pamoja na tukio la uporaji wa fedha zaidi ya dola 2,000,000 lilitokea jijini Dar es salaam mwaka 2005 kwenye Kampuni ya Security Group 4 na kisha kufikishwa Mahakamani.
Mbali na tukio hilo pia mwaka 2002 alihusika na tukio la uvamizi wa Benki ya NBC tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro. Mwaka 2014 jambazi huyo amewahi kushtakiwa nchini Kenya kwa matukio ya uhalifu katika Mahakama ya Mlimani Law Court iliyopo jijini Nairobi lakini baadae aliachiwa huru.
4
Alizidi kukiri kuhusika katika matukio ya ujambazi huku akishirikiana na wenzake katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika jiji la Arusha ambalo lilikuwa linawalenga wafanyabiashara wakubwa wa Madini ya Tanzanite na Hoteli za Kitalii. Miongoni mwa tukio walilolifanya ni kumjeruhi mfanyabiashara wa madini aitwaye Mathius Manga ambaye alipigwa kwa risasi kwenye ubavu wa kulia.
Kamanda Sabas alisema kwamba mara baada ya kuridhishwa na mahojiano baadae jambazi huyo alikubali kushirikiana na Polisi ili aweze kufanikisha juu ya upatikanaji wa wenzake ambao siku ya jana walipanga kuvamia katika duka la kubadilishia fedha liitwalo Sanya lililopo jijini Arusha.
Walipokuwa wanaelekea kwenye eneo la tukio akiwa anaongozana na askari Polisi kwa nia ya kufanikisha kuwapata majamabzi wengine, mara tu baada ya kufika kabla hawajawakamata majambazi hao ambao walikuwa kwenye gari aina ya Noah rangi ya silver yenye namba za usajili T. 981 AVK walishtuka na kuanza kulishambulia gari lililokuwa na askari Polisi na kumjeruhi mwenzao Sixtus Alfedy Ngowi ambaye alifariki muda mfupi wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali.
5
Mara baada ya kuona hivyo, Polisi nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi watatu huku wengine wakifanikiwa kukimbia. Katika upekuzi kila mmoja alikutwa na bastola pamoja na risasi. Pia walikuta mabegi matatu meusi ambapo ndani yake kulikuwa na bunduki mbili aina ya AK 47 zenye namba 83 LG 3953 56-1 na nyingine yenye maandishi ya kirusi pamoja na SMG moja yenye namba 56-1 28038394.
Bastola ambazo zilikutwa toka kwa majambazi hao zilikuwa na namba CZ 75 Compact Luger-9mm namba A. 269206, CZ 85 B Luger 9mm namba 051967 na Chines Pistol namba 967741. Pia zilipatikana magazine nne tupu za SMG, risasi 85 za SMG/AK 47 na risasi 28 za bastola.
Mbali na silaha hizo pia walikutwa na Radio “Call” mbili aina ya Kenwood zilizokuwa hewani na wimbi la Polisi Arusha, bullet proof moja, vifaa vya kusafishia bunduki, mifuko mitatu ya kubebea pesa na vifaa vingine.
Majambazi hao ambao kwa sasa miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Mount Meru walikutwa pia na vitambulisho mbalimbali vya Jamhuri ya Kenya pamoja na simu tano aina ya Nokia, Tecno na Samsung. Kamanda Sabas alisema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliofanikiwa kukimbia na kubaini mtandao mzima wa kundi hilo.
Kamanda Sabas alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushirikiana na Jeshi hilo juu ya utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuonya yoyote ambaye atajiingiza katika matukio ya kufanya uhalifu Jeshi hilo litamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA HUDUMA ZA “DUTY FREE SHOP” MAGEREZA MKOANI ARUSHA

1
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil (wa pili kushoto) , akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Huduma za Magereza Duty free shop Mkoani Arusha leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha (wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Smart LTD, Bw. Mohamed Panjwani.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
2
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil (kulia), akisoma jiwe la Msingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
3
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha.
4
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Magereza mbalimbali yaliyopo Mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbaraka Abdulwakil(hayupo pichani).
5
Bidhaa za majumbani zinazopatikana katika Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha.
6
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha waliosimama mara tu baada ya kuzindua Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, SACP. Hamis Nkubasi(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, SACP. Venant Kayombo(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Mart LTD, Bw. Mohamed Panjwani.
………………………………………………………..
 Na Lucas Mboje, Arusha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil  amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja  pamoja na Uongozi wote wa Jeshi hilo kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao ya  kazi hususani huduma za  “Duty free shops”.
  Mhe. Mbarak Abdulwakil  ameyasema hayo wakati wa  uzinduzi rasmi wa “Duty free shop”ya Magereza Mkoani Arusha iliyofanyika leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Binafsi wa Mkoa wa Arusha walihudhuria hafla hiyo.
  “Nampongeza kwa dhati Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kwa jitihada hizi ambapo matunda yake yanaonekana na amethibitisha kwamba azma ya kusambaza huduma hii nchi nzima ipo pale pale na jitihada zinaonekana”. Alisema Abdulwakil.
  Ameongeza kuwa lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama unatekelezwa ipasavyo kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
  Aidha, Mhe. Abdulwakil  amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha  Maafisa, askari  pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.
  Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja  alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar Mart LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.
Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za “Duty Free Shop” na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenda kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.
Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya “Duty Free Shops” tisa(09) ikiwemo Gereza Kuu Ukonga na Keko – Dar es Salaam, Gereza Isanga – Dodoma,  Gereza Kuu Karanga – Moshi, Gereza Butimba – Mwanza, Gereza Ruanda – Mbeya, Gereza Lilungu – Mtwara, Gereza Uyui – Tabora, Chuo KPF – Morogoro na duka la tisa(09) ni Gereza Kuu Arusha.

MANJI AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA VIONGOZI WA BIASHARA AFRIKA

unnamedBMwenyekiti  wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji.
……………………………………………………..
NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI  wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji
amenyakua tuzo ya kielelezo cha viongozi wa biashara wa Afrika kwa
mwaka 2015.
Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, aliwapiku
wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo bilionea namba moja Afrika,
 Aliko Dangote.
 Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi Quality Group,
ilisema  tuzo hiyo ilimshtua ‘bosi’ wao kwani hakutarajia na kwamba
itasaidia kuvutia wawekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii
nchini.
 Tuzo hizo zilitolewa Septemba 16 mwaka huu.
Taarifa hiyo iliongeza  Manji ni chachu kwa vijana kufanya vizuri
kwenye sekta zao na  itasaidia nchi kusonga mbele katika kujikwamua na
umasikini.
 Tanzania inaendelea kujukulikana kimataifa na itasawaidia watanzania
kwa ujumla kufanya kazi ama biashara katika nchi nyingine bila ya
vikwazo visivyo na msingi kupitia tuzo hiyo.
Baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Emirates Group,
Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege ya
Emirates inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na
nyingine kubwa.
Wengine ni Mwenyekiti wa Emmar Properties, Mohammed Alabbar pia
bilionea kutoka India, Ratan Tata anayemiliki kampuni kubwa ya
Emeritus of Tata Sons Ltd.
Pia bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri, Mukesh Ambani ambaye
ni mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni Yingluck
Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Manji, pia kampuni yake ya
Quality Group imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa
uhakika kwa bara la Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”

MKUU WA WILAYA YA MAGHARIB B AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UCHAGUZI MKUU UJAO

x1
MKUU WA WILAYA YA MAGHARIBI ( B), AYOUB MOHD MAHAMOUD AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI  KUHUSIANA NA NAMNA WALIVYOJIPANGA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA HARAKATI ZINAZOEENDELEA ZA KUELEKEKEA UCHAGUZI MKUU  NCHNI. MAZUNGUMZO HAYO YALIFANYIKA OFISINI KWAKE MWERA ZANZIBAR.
x2……………………………………………………………….
Na Rahma Khamis  na Takdir Ali Maelezo Zanzibar    
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi  B Unguja Ayoub Mohd Mahamoud  amewataka wanasiasa, viongozi wa dini  na taasisi  za kiraia kuzungumza na kuhimiza amani wakati huu wa kampeni ili  Zanzibar iendelee kuwa nchi yenye utulivu.
Hayo ameyaeleza  Ofisini kwake Mwera  wakati akizunumza  na waandishi wa habari kuhusu  kampeni za Uchaguzi  zinavyoendelea baada ya wananchi wengi  kuhamasika  na kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo.
Amesema katika kuendeleza amani Serekali inaendelea na jitihada za  kuweka walinzi katika mikutano ya kampeni  na kujaribu kutenganisha mikutano maeneo  mbalimbali  ili wasikutane.
Akizugumzia  suala la amani Ayoub amefahamisha kuwa  sio suala linaloihusu  Serekali pekee  bali ni la  kila mwananchi hivyo  amewanasihi  waendelee kuienzi  kwani kutoweka  kwa amani iliyopo haitakuwa kazi rahisi kuirejesha.
 Kwa upande wa wanasiasa  Mkuu wa Wilaya  amesema  wanachohitaji ni uongozi hivyo hawanabudi kuwa waangalifu katika kaulizao  ili zisijenge hamasa kwa  vijana wao kuvunja amani iliyopo.
“Kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa wakati huu  wa kampeni Serekali itakua haishughulikii nawambia Serekali ipo haijenda likizo  hivyo atakaekwenda kinyume hatutomuachia”.
Amesema changamoto zinazoikabili Wilaya yamagharibi ni kuwa na mikutano mingi katika kwa wakati mmoja jambo ambalo linaweza kupelekea kutokea kwa ugomvi hasa wakati  wanachama wanaporudi mikutanoni kutokana na hamasa wanazokuwa kuwa nazo.
Aidha amewanasihi wananchi wasikubali  kutumiwa na wanasiasa kwa kuanza  kufanya fujo na kuvunja  amani ya nchi kwa wale wenye vyama na wasio na vyama kwani hakuna mbadala wa amani .
“Jitihada za Serekali kuhamasisha amani  zinaonekana  kuzaa   matunda hivyo tuendelee kuhamasishana  na kunasihiana  kwani siku 30 za kampeni zilizobaki zisipelekee amani kutoweka kw siku nyingi zinazokuja.” Alsisitiza Mkuu wa Wilaya.    

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA BAADHI YA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015.
2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015. 
3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi    
4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. 
(Picha zote na OMR) 

viingilio Tamasha la Amani hadharani

imagesNa Mwandishi Wetu
………………………………….
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imetangaza kiingilio kwa VIP ni shilingi 5000 kwa watakaohudhuria katika tamasha hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama viti vya kawaida watalipa shilingi 3000.
Msama alisema watoto watachangia shilingi 1000 ambako alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani katika nchi yetu.
Msama alisema katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagiza maombi hayo kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
Aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
Alisema baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA) yadhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri

indexvNa Mwandishi Wetu
……………………….
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA),  imetoa Sh. 10, 486,000 kwa ajili ya kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA zinatarajiwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa sekta ya michezo katika uongozi wake.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo, alisema wameamua kusaidiana na TASWA kwa sababu Rais Kikwete ni mdau mkubwa wa michezo na pia wa masuala ya utalii.
‘’Dk. Kikwete ni mdau mkubwa  wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa kipindi chote ambacho amekuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ametembelea hifadhi hii  mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa letu waliomtangulia.
‘’Pia amekuwa mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika  kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya Ngorongoro katika mataifa mbalimbali duniani alikokwenda kwa ziara za kikazi.
‘’Jambo hili limeleta watalii wengi nchini kutoka mataifa  mbalimbali dunini. Vile vile ziara zake za mapumziko hifadhini wakati wa sikukuu mbalimbali zimewahamasisha sana  Watanzania walio  wengi kutembelea  hifadhi hii kutoka kote nchini na hata nchi jirani,’’ alisema Akyoo.
Pia alisema waandishi wa habari ni wadau wakubwa na muhimu katika harakati za utalii na ndiyo sababu wameamua kuisaidia TASWA ifanikishe shughuli yake.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru mamlaka ya hifadhi hiyo na kusema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuomba wadau wengine waungane nao kufanikisha jambo hilo.
‘’Kama tulivyosema bajeti yetu ni Sh milioni 130, juzi (Jumatano) tulipata watu wa GSM Foundation waliotupa Sh. Milioni 50, tunaomba na wengine tushirikiane nao katika hili,’’ alisema Mhando.
Alisema TASWA imeamua kuandaa hafla ya wanamichezo kumuaga Rais na pia kumpa tuzo kwa vile wakati wa uongozi wake amefanya mambo makubwa katika sekta ya michezo.
Kwa mujibu wa Mhando, wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na TASWA kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.

Wanachama SHIWATA kunufaika na viwanja bure

indexcNa Mwandishi Wetu
…………………………
MAKUNDI ya wasanii, wanamichezo na waabdishi wa habari wanaendelea kumiminika kulipia nyumba za bei nafuu baada ya Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kutoa viwanja bure katika kijiji cha Wasanii Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa ofa hiyo inamhusu kila mwanachama ambaye atapata nusu hekari miguu (25kwa 25)kama atakuwa amelipa sh. 200,000 za kujengewa msingi wa nyumba ya chuma kimoja kutumia matofali ya saruji.
“Tumeanzisha ofa maalum kwa wanachama wetu kupata kiwanja bure kama atakuwa amelipia benki sh. 200,000 za kumjengea msingi wa nyumba yake katika kijiji chetu Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa kati ya hekari 300 tulizonazo za makazi ni hekari kumi tu zimejengwa nyumba 120,.” alisema Taalib.
Alisema katika misingi hiyo wanaotaka kumaliza nyumba zao gharama yake jumla itakuwa sh. 850,000 kwa nyumba ya chumba kimoja, sh. 3,800.000 kwa nyumba ya vyumba viwili na sh. 6,400,000 kwa nyumba vya vyumba vitatu na sebule.
Mwenyekiti Taalib alisema bado nafasi iko wazi kwa wasanii wanaotaka kuwekeza kwa kujenga shule, hospitali, kumbi za starehe na viwanja vya nmichezo wanakaribishwa.
Alisema makundi ya wasanii ambao bado hawajajiunga na mtandao huo watapewa ofa ya kulipa sh. 70,000 kwa mtu mmoja katika vikundi na mmoja mmoja atajiunga kwa sh. 120,000 ambapo atapewa pia katiba ya mtandao huo.
Alisema wanachama wanaotaka kutembelea kijijini kumeandaliwa usafiri wa kila Jumamosi kwa nauli ya kwenda na kurudi ya sh. 10,000 kwenda kujionea maendelea ya kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
index
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WATU TISA WAFUASI WA CCM NA CHADEMA WAJERUHIWA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA MAENEO YA MBATA BUCHANI JIJINI MBEYA.
WATU WAWILI RAIA WA KIGENI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MBATA – BUCHANI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CCM BW. SHAMBWE SHITAMBALA AKIWA NA WAFUASI WAKE, WAPENZI WA CHAMA HICHO ALIKUWA AKIFANYA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA ENEO HILO KWA MUJIBU WA RATIBA YAKE.
MGOMBEA HUYO AKIWA KATIKA MKUTANO HUO, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW. JOSEPH MBILINYI ALIKUWA AKIPITA ENEO HILO AKIWA NA MSAFARA WAKE KUELEKEA MAENEO YA NSOHO KWENYE MKUTANO WA KAMPENI. KUTOKANA NA KITENDO HICHO WAFUASI WA CCM AMBAO WALIONEKANA KUWA WENGI HADI ENEO LA BARABARA HIVYO KUPELEKEA MSAFARA WA BW. MBILINYI KUTOWEZA KUPITA ENEO HILO HALI ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU ZILIZOPELEKEA KUJERUHIWA KWA WATU NA UHARIBIFU WA MALI.
KUTOKANA NA VURUGU HIZO, WAFUASI TISA WA VYAMA HIVYO VYA SIASA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. ROBERT KERENGE (58) KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA 2. SALUM MWANSASU (35) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 3. ATUPELE BROWN (39) MKAZI WA GHANA [CCM] 4. ROSE NELSON (30) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 5. SAKINA SALUM (25) MKAZI WA GHANA [CCM] 6. MALANYINGI MATUKUTA (31) MKAZI WA FOREST [CCM] 7. AGABO MWAKATOBE (44) MKAZI WA GHANA [CHADEMA] 8. JAILOS MWAIJANDE (23) MKAZI WA ITIJI [CHADEMA] NA 9. GABRIEL MWAIJANDE, DEREVA WA MGOMBEA UBUNGE [CHADEMA].
AIDHA KATIKA VURUGU HIZO GARI LA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW.JODEPH MBILINYI AINA YA TOYOTA LAND CRUISER YENYE NAMBA ZA USAJILI T.161 CPP LILIHARIBIWA KIOO CHA MBELE, TAA MOJA YA NYUMA UPANDE WA KUSHOTO NA KIOO CHA UPANDE WA DEREVA KWA KUPIGWA MAWE. PIA PIKIPIKI ZENYE NAMBA ZA USAJILI T.332 CHV AINA YA T-BETTER NA T.383 CSE AINA YA SKYMARK ZILIHARIBIWA KWA KUVUNJWA SIDE MIRROR ZA UPANDE WA KUSHOTO NA ZIPO KITUO CHA POLISI KATI.
KWA MUJIBU WA RATIBA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA KWA TAREHE 17.09.2015, ILIKUWA IKIONYESHA CHADEMA SAA 10:00 ASUBUHI HADI SAA 15:00 ALASIRI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA NSOHO NA SAA 15:00 ALASIRI HADI 18:00 JIONI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA MAENDELEO WAKATI CCM KWA MUJIBU WA RATIBA WALITAKIWA KUFANYA KAMPENI KATA YA ITENDE SAA 08:00 ASUBUHI HADI SAA 13:00 MCHANA NA SAA 13:00 MCHANA HADI SAA 18:00 JIONI MTAA WA MBATA, KATA YA GHANA AMBAPO NIPO TUKIO HILI LILIPOTOKEA.
UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUPELEKA JALADA LA UCHUNGUZI KWA MWANASHERIA WA SERIKALI ILI WALIOHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA IDARA NYINGINE, LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI MSUMBIJI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ARQUEMIDES JOAO MAHANJANE (40) NA 2. HENRIQUES BENDITO ASSUBA (36) WOTE WAKAZI WA MAPUTO WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI VIPANDE 2 VINAVYODHANIWA KUWA NI PEMBE ZA FARU ZENYE UZITO WA KILO 5 ½, VIPANDE 4 VYA MAWE YADHANIWAYO KUWA NI MADINI YENYE UZITO WA KILO 1 ½ NA MZANI 01 [PORTABLE ELECTRONIC SCALE].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KASUMULU MPAKANI, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA WAKIWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI ABL 860 MC AINA YA TOYOTA HILLUX VIGO D/CABIN WAKITOKEA NCHINI MALAWI KUINGIA NCHINI. NYARA HIZO PAMOJA NA VITU HIVYO VILIKUWA VIMEFICHA CHINI YA CHASES YA GARI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA MAENEO YA MIPAKANI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAKABIDHIWA PIKIPIKI TANO KWA AJILI YA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO KUAKABILIANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WATOTO.

1MWAKILISHI  WA WASHIRIKA LA KUHUDUMIA WATOTO  ZANZIBAR  (SAVE THE CHILDREN), BI  MALI LISSON AKITOA MAELEZO KABLA  YA KUKABIDHI PIKIPIKI ZA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO  KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA  WIZARA YA  AFYA  MNAZIMMOJA MJINI ZAZNIBAR.
2
MWAKILISHI  WA SHIRIKA LA KUHUDUMIA WATOTO ZANZIBAR (SAVE THE CHILDREN), BI MALI LISSON AKIMKABIDHI FUNGUO, ZA PIKIPIKI TANO,  NAIBU WAZIRI  WA  AFYA  MAHMOUD THABIT KOMBO  KWA AJILI YA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO  WA WILAYA KATIKA HAFLA  ILIYOFANYIKA  WIZARA YA AFYA  MNAZIMMOJA  MJINI ZANZIBAR.
3
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAHMOUD THABIT  KOMBO AKITIA SAINI  BAADA YA KUPOKEA PIKIPIKI TANO KWA AJILI YA KUWARAHISISHIA KAZI  WAKUU WA VITENGO VYA   HUDUMA YA MKONO KWA MKONO WA WILAYA.
4
NAIBU WAZIRI  WA AFYA  MAHMOUD THABIT KOMBA AKIZUNGUMZA NA  WAFANYAKAZI NA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO WALIOKABIDHIWA PIKIPIKI HIZO.
5
PIKIPIKI WALIZO KABIDHIWA WAKUU WA VITENGO  VYA MKONO KWA MKONO KWA AJILI YA KUWASAIDIA SHUGHULI ZA KUFUATILIA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA KWA WATOTO.
PICHA ZOTE NA MIZA OTHMAN –MAELEZO ZANZIBAR.

Dk Mauwa Daftari -wakinamama tushikamane kuhakikisha tunamuunga Mkono Samiya Suluhu Hassan

indexNa Masanja Mabula –Pemba
……………………………………..
MJUMBE wa Kamati  Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa  Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Dk Mauwa Abeid Daftari amewataka wanawake kuondoa tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na wawe kitu kimoja kwa kuhakikisha wanamuunga Mkono Mgombea mwenza wa Chama hicho Samiya Suluhu Hassan  .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  Dk Mauwa amewataka wanawake kuweka kando tofauti zao na  wadumishe ushirikiano kwa kumuunga Mkono Mgombea mwenza kwa kuwa ni suluhisho la changamoto zinazowakabili akinamama .
Amefahamisha kwamba ukombozi wa mwanamke umewadia na kueleza kuwa hayo yatatimia iwapo wanawake watashikamana kwani kilio cha kundi hilo cha siku nyingi kimepata wa kukinyamazisha kwani Samiya ndiyo ukombozi wa mwanamke.
“Mwaka huu ndiyo wa ukombozi kwa akinamama , napenda kuwaomba tushikamane kuhakikisha tunamuunga Mkono Samiya Suluhu Hassan kwani anafahamu changamoto zinatukubili ili kufanikisha hilo lazima tuondoe tofauti zetu za kisiasa ”alisisitiza .
Aidha ameeleza kwamba kumchagua Samiya kuwa makamu wa Rais ni mikakati ya kufikia usawa katika vyombo vya maamuzi ikiwemo Bunge na Baraza la Wawakilishi (hamsini kwa hamsini) hivyo ni vyema wanawake kokote nchini kulitambua hilo .
“Ni wakati wa wanawake kufikia nusu kwa nusu katika vyombo vya maamuzi , na hili limeanza kuchomoza kwani tumekuwa tukihitaji kwa muda mrefu hatimaye limetimia ”alieleza Dk Mauwa .
Naye Mjumbe wa Halmashauri ya Chama Hicho Asiya Sharif amesema kuwa kitendo cha CCM kumpendekeza Samiya  Saluhu Hassan ni hatua za kuutokomeza  mfumo dume ambao unaendelea kuwakandamiza wanawake kwa muda mrefu .
Amesema kuwa wanawake wamekuwa wakikosa haki zao za msingi  ikiwemo kutoshiriki vyema katika vikao vya maamuzi kutokana  na kuwepo na mfumo dume hali ambayo kwa sasa imeanza kupatiwa ufumbuzi wake .
“Tujiandaeni kuutokomeza mfumo dume ili tuweze kushiriki ipasavyo kwenye vyombo vya maamuzi , kwani kuna haki nyingi zimekosekana kutokana na baadhi ya wanaume kuwazuia akinamama kushiriki katika kufanya maamuzi ”alifahamisha .
Kwa upande wake Khadija SKibano  amesema ukombozi wa mwanawake umefika na kuelezea haja kwa wananchi wa Tanzania kushikamana pamoja na kumtetea mwanamke na kuongeza kwamba bado wananchi ni watumwa wa siasa .
“Bado wananchi tunasumbuliwa na mapenzi ya chama , lakini kusema kweli mwaka huu ni lazima tushikamane pamoja na tuachane na ushabiki wa vyama vyetu kwani ukombozi wa mwanamke umewaidia ”alieleza Khaadija .
Hivyo wameshauri wanawake kuwashawishi waume zao pamoja na ndugu na jamaa zao kila mmoja kuhakikisha kwamba wanaunga mkono juhudi za ukombozi wa akinamama .

No comments :

Post a Comment