Na Julius Mtatiro
Kwa ufupi
- Profesa Muhongo amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Tume ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW), Mhariri Mkuu wa Jarida la Afrika la Sayansi za Miamba na Madini (The Journal of African Earth Sciences, Elsevier) na hadi sasa ni mjumbe wa bodi kadhaa za uhariri wa majarida ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Historia yake
Profesa Sospeter Muhongo alizaliwa katika Wilaya
ya Musoma Mjini, mkoani Mara Juni 25, 1954 (atatimiza miaka 61 Juni
mwaka huu). Alianza shule ya msingi mkoani Mara na kuendelea na masomo
ya sekondari (kidato cha I – VI) katika shule mbalimbali hapa nchini.
Alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kuhitimu Shahada ya Jiolojia. Kwa sababu ya ufaulu wa hali ya
juu, alipata ufadhili kirahisi, kwenda kusoma shahada ya Uzamili katika
Chuo Kikuu cha Gӧttingen, Ujerumani na baada ya kuihitimu, aliendelea na
Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Berlin
akibobea katika eneo hilohilo la jiolojia ambako alihitimu.
Katika maisha yake ya kitaaluma, amewahi kupokea
na kutunukiwa tuzo nyingi, achilia mbali ushiriki wake katika mambo
mengi ya kitafiti. Serikali ya Ufaransa ilimtunukia Cheo cha Ofisa
Mwenye tunu ya Kitaaluma Iliyotukuka - Ordre des Palmes Académiques
(Iliyoanzishwa na Mfalme Napoleon Mwaka 1808).
Mwaka 2004, alipokea tuzo inayoheshimika kwa jamii
ya wanajiolojia wa Afrika ya Profesa Robert Shackleton (UK) (Geological
Society of Africa’s prestigious Professor Robert Shackleton Award), kwa
ajili ya utafiti wa kipekee kuhusu jiolojia ya Afrika ya miamba yenye
umri wa zaidi ya miaka milioni 500 (Precambrian Geology of Africa).
Amekuwa Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa
Akademia ya Sayansi ya Nchi zinazoendelea (FTWAS), Chama cha
Wanajiolojia wa Afrika (FGSAf), Akademia ya Sayansi ya Afrika (FAAS) na
Akademia ya Sayansi ya Tanzania (FTAAS).
Profesa Muhongo amewahi kuwa Makamu wa Rais wa
Tume ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW), Mhariri Mkuu wa Jarida la
Afrika la Sayansi za Miamba na Madini (The Journal of African Earth
Sciences, Elsevier) na hadi sasa ni mjumbe wa bodi kadhaa za uhariri wa
majarida ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Pia, Profesa Muhongo amewahi kuwa Rais wa Chama
cha Wanajiolojia wa Afrika (1995-2001), Mkurugenzi Mwanzilishi
(2005-2010) wa Ofisi ya Sayansi ya Kanda ya Afrika (ICSU) yenye Makao
Mkuu yake Pretoria, Afrika Kusini, Mwenyekiti wa Bodi ya
Unesco-IUGS-IGCP Programu ya Kimataifa ya Sayansi ya Jiolojia (2004 -
2008) na Mwenyekiti wa Kamati ya Programu ya Kisayansi (SPC) ya Mwaka wa
Kimataifa wa Sayari ya Dunia uliotangazwa na Umoja wa Mataifa (UN-IYPE)
mwaka 2007-2010.
Mwaka 2009, Profesa Muhongo aliteuliwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi
Mkuu wa Unesco na alikuwa miongoni mwa wasomi mashuhuri wanne
walioingia kwenye mchujo wa mwisho, japokuwa hakupewa wadhifa huo.
Mwaka 2014, alishinda tuzo ya Heshima ya Jamii ya
Wanasayansi wa Jiolojia na Uchimbaji Petroli na Gesi Asilia ya Nigeria
(NMGS)/AMNI ya Profesa M.O. Oyawaye.
Nguli huyu anazungumza lugha nne kubwa, Kiswahili,
Kiingereza, Kijerumani na Kifaransa na amemuoa Bertha Mamuya - wana
kijana aitwaye Rukonge na wanawalea watoto yatima watatu.
Mbio za ubunge
No comments :
Post a Comment