Wednesday, May 6, 2015

MGOMO WA MADEREVA, DAR


 Mabasi yakiwa yameegeshwa Kituo cha Mabasi Ubungo baada ya madereva kuwa katika mgomo wa kimasilahi Dar es Salaam jana. Mgoma huo umefanyika nchi nzima ukihusisha na daladala hivyo kuleta adha kwa wananchi.


 Wananchi wakitembea maeneo ya Jangwani kutokana 
na mgomo huo.
 Wanafunzi na watu wengine wakitembea maeneo ya chuo cha maji Ubungo wakielekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
 Hali ilivyokuwa stendi ya Ubungo.
 Baadhi ya madereva, wapiga debe na makondakta wakikimbia huku wakiimba wanaonewa na wanataka mikataba ya kazi zao .
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi maeneo yanayozunguka kituo hicho cha mabasi cha ubungo.
 Wananchi wakisubiri mabasi kwenye kituo cha Makumbusho
 Kituo cha mabasi cha Makumbusho kikiwa hakina mabasi kutokana na mgomo huo.
 Askari wa FFU wakiwa doria maeneo ya Ubungo Mataa.
Madereva, wapiga debe na makondakata wakishangilia jambo wakati wakiongea na viongozi wao kuhusu mgomo huo.
Dotto Mwaibale

MADEREVA wa mabasi na daladala wamesema wapo tayari kula biskuti wakati wakiendelea na mgomo wao ulianza rasmi jana mpaka  hapo serikali itakapokaa nao ili kuumaliza mgpmo huo.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo asubuhi na  Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Madereva, Shabani Mdemu kati akizungumza na wanachama wa umoja huo na wadau wengine.

"Tupo katika wakati mgumu sana lakini tupo tayari kula biskuti lakini hatuta rudi nyuma ni vema tukae katika hali hii kwa siku mbili na zaidi mpaka tupate majibu ya kueleweka" alisema Mdemu.

Mdemu alisema haoni kwanini viongozi wenye dhamana wanashindwa kufika kuzungumza hana hana na wanachama hao badala ya kwenda maofisi kwao baadhi ya viongozi tu.

"Wanapotafuta kura huwa wanaenda vijijini kuomba sasa wanashindwa nini leo hii kutufuata hapa tulipo kuja kusikiliza kilio chetu" alisisitiza Mdemu huku akishangiliwa na wanaumoja hao.


Akizungumzia kuhusu kutatua mgogoro huo Mdemu alisema walimuomba waziri mkuu afike za kufika kutokana na hali ya usalama katika eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo madereva hao walipinga vikali kitendo cha waziri kuwataka wamfuate hivyo waliamua kuendelea kugoma hadi hapo Waziri atakapoamua kufika.

"Tumemuomba Waziri aje kusikiliza kilio chetu lakini amesema hawezi kuja kutokana na hali ya kiusalama hivyo sisi tunaenelea kugoma hadi atakapoamua kuja kutusikiliza.

"Kuna mambo mengi ambayo Waziri alituahidi atatutekelezea kipindi kile cha mgomo wa mwanzo lakini hadi sasa hayajatekelezeka na ndiyo maana leo hii tunagoma," alisema

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, aliwasili eneo la tukio tangu majira ya saa 12 asubuhi akiwa na kikosi chake kwaajili ya kuangalia usalama katika eneo hilo.

Lakini ilipofika majira ya saa 3:30 asubuhi aliamua kuondoka huku akidai kuwa hana chochote ambacho angeweza kuzungumza kwani viongozi wapo katika mazungumzo.

Kamanda Mpinga alisema kuwa hana chochote cha kusema kwani atarudia yale yale na kuwataka madereva wamsubiri Waziri Mkuu Mizengo Pinda hadi majira ya saa sita kwaajili ya mazungumzo na madereva hao.

Kadri muda ulivozidi kwenda hali ilizidi kuwa tete kutokana jambo ambalo lilipelekea kuongezeka kwa vikosi vya jeshi la polisi huku wakitumia mabomu ya machozi na mbwa.

Lakini hadi kufikia majira ya saa sita mchana hakuna kiongozi wowote wa serikali waliofika eneo hilo, huku madereva wakiwa wameegesha mabasi yao na wasafiri wakiwa hawafahamu hatima yao.

Hata hivyo mmoja wa askari polisi ambaye ni trafiki aliyejulikana kwa jina la Solomon Mwangamilo alizua taharuki katika eneo hilo alipotaka kutoa Bus lililokuwa likielea mwanza lijulikanalo Lucky Star.

Hali hiyo lisababisha madereva kumzomea na kutanda mbele ya gari huku na kulizuia gari hiyo kutoka , madereva hao walifanikiwa na gari hilo liliridishwa ndani ya stebi ya Ubungo.

Aidha moja ya madereva wa magari hayo Ngonyani Gervas alisema wamechoka kunyanyaswa tunataka haki zetu kama madereva pia tunataka wawakilishi wetu bungeni.

"Mbona fani nyingine zina  wawakilishi bungeni na sisi madereva tumechoka tunataka wawakilishi bungeni kama ilivyo kwa vyama vingine kama albino kwani hii fani haitambuliki kitaifa?  "

Aliongeza kuwa Kama viongozi wameshindwa kuwasaidia  katika fani yao taaluma hiyo ifutwe.

Kwa upande wake Msemaji wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Gervas Rutavunzinda, alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kusafiri kutoka sehemu moja kenda nyingine, na huu mgomo umevunja katiba kwani ni kuwakosesha abiria haki yao ya kusafiri.

Alisema abiria anakuwa amekidhi vigezo anapokata tiketi lakini akishindwa kusafiri inakuwa ni tatizo la mmiliki na serikali hivyo tatizo hilo linatakiwa kuingiliwa kati na serikali ili kuondokana na mgogoro.

"Kitendo cha kumrudishia abiria nauli kunakuwa umemnyima haki kwasababu abiria wengi wamekuwa wamejiandaa halafu anashangaa anafika sehemu husika kwa ajili ya safari unamwambia ahirishe safari jambo ambalo si zuri.

"Hili tatizo ni la wamiliki na madereva haliwahusu abiria, serikali inapaswa kuangalia tatizo lilipo na kuhakikisha halitokei tena pia mamlaka husika zihakikishe zinatatua matatizo kama hayo kutokana na madhara kuwa makubwa," alisema.

Katika hali isiyo ya kawaida kulitangazwa kurudishwa nauli kwa abiria ambao wapo hiari kuahirisha safari zao lakini madereva hao walishindwa kufanya hivyo kutokana na fedha hizo kupelekwa kwa wamiliki na kufanyiwa manunuzi ya mafuta ya magari hayo kwa kuanza safari.

Mmoja wa Utingo wa Basi la Majinja Express linalofanya safari zake Dar Mbeya Sumbawanga Flora Ngailo alisema kitendo cha kurudisha nauli kwa abilria hao hakitawezekana kutokana na fedha hizo wameshamkabidhi mmiliki na tayari zimeshanunuliwa mafuta.

"Hatuwezi kurudisha fedha za nauli hizo kwasababu tayari mahesabu yameshaenda kwa bosi na zimeshanunuliwa mafuta, labda wasubiri hadi hapo tutakapopewa taarifa za kuondoka au waahirishe hadi kesho asubuhi," alisema Ngailo.

Kwanyakati tofauti abiria waliokuwa wakitaka kusafiri kituoni hapo Rehema Obadia na Issa Jafari, walisema mgomo huo umewaathiri kwa kiasi kikubwa kwani mamlaka ilitakiwa kutoa taarifa kwa wananchi kama kutatokea kwa mgomo huo.

"Mamlaka husika walitakiwa kutoa taarifa kwa wananchi kuwa kutatokea hali kama hii, sasa hivi hatujui tutasafiri au hatutasafiri kwani hakuna lolote yunaloambiwa,

"Hatuna taarifa zozote hadi sasa hatujala tuna watoto, wagonjwa na hutujanywa chai na wengine wamefiwa hadi sasa hali hii inasababisha kuingia gharama upya na hatujui hatma yetu," alisema.

"Huu ni uzembe wa serikali kwani walipaswa wasikatishe tiketi kwasababu mgomo huu wanaujua na hii ni sanaa ya wanafanya, serikali watatue migogoro kama hii kwa wakati ili kuepusha adha kama hizi," walisema.

Vituo vya daladala

Katika kituo cha daladala Makumbusho hapakua na gari ya abiria bali kulikuwa na magari binafsi, Bajaji na Pikipiki zilizokuwa zikitumika kubebea abiria.

Kituoni hapo palikuwa na abiria ambao walikuwa hawajui hatma ya safari yao na ni namna gani wataenda makazini wengine wakilalamika kuchelewa vipindi vyuoni kutokana na kutokuwepo kwa usafiri eneo hilo.

Mmoja wa abiria, Diana Bernard alisema mgomo huo umemuathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli zake kukwama ikiwa ni pamoja na kushindwa kuelekea chuoni.

Hadi waandishi wa gazeti hili wanaondoka eneo la ubungo bado hakukua na dalili yoyote ya ujio wa Waziri Mkuu badala yake madereva hao walikuwa mameshikilia kuwa msimamo wao kuwa mgomo upo palepale.

Waziri wa Kazi na Ajira.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka aliwataka madereva kuachana na migomo hiyo kwani serikali inafanyia kazi madai  yao hivyo wawe wavumilivu.

"Wao wanasema kuwa wanadharauriwa lakini si kweli kwani tulikaa pamoja tukaelewana na hivyo tunayafanyia kazi madai yao na mambo yatakuwa mazuri tu"alisema


i
Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji.
Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya (Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo athirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo wananchi walilazimika kuibomoa kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha TPC ili kuruhusu maji kupita.
Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita.
Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje.
Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya mabanda ya kuku.
Baada ya maji kujaa wengine walilazimika kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo.
Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na maji vilianikwa juu ya paa.
Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya paa.
Mifugo pia liathirika na mafuriko hayo.
Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo
Mbunge Lucy Owenya akimfariji mmoja ya waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo vyeti vya taaluma ya utabibu.
Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.
Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada huo.
Afisa mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC ,Jafary Ally akizungumza kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo athiri kiwanda hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Meneja Unendelezaji wa Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, Asa Mwaipopo, (katikati), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), wakati wa ziara yake ya kutembelea mgodi wa North Mara na maeneo yanayozunguka mgodi huo, Jumatatu Mei 4, 2015 ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Kulia ni Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo

Wananchi wakiendelea na ujenzi kwa mtindo wa “Tegesha” mita chache kutoka eneo la machimbo (pit), la mgodi wa dhahabu wa North Mara, huko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara jana. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga, amesikitishwa na mtindo huo wa “Tegesha”, ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa awali. Naibu huyo wa waziri yuko ziarani kutembelea maeneo ya mgodi huo ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, akizungumza na mama huyu mkazi wa kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na eeno la mgodi wa North Mara, huko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara, wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo Jumatatu Mei 5, 2015 ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (Wapili kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa nyumba moja kwa mtindo unaoitwa na wakazi wa Nyamongo “Tegesha”, mita chache kutoka uzio wa mgodi wa North Mara, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Naibu waziri amesikitishwa na mtindo huo ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa awali


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), akisalimiana na Meneja Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, wakati alipofika kwenye kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na mgodi wa North Mara, Mara ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,(Watatu kulia), Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jimmy Ijumba, (Wapili kulia) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo

Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara, Abel Yiga, (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga wakati waziri huyo alipotembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, (Watatu kulia), na kaimu kiongozi wa kitengo cha mahusiano ya kijamii ya mgodi wa North Mara, Zakayo Kalebo. (kushoto

Naibu Wazirti Kitwanga, akitembelea moja ya Guest House ZMB iliyoko kijiji cha Nyakunguru, ambayo imejengwa kwa mtindo wa "Tegesha"

Naibu Wazirti Kitwanga, viongozi wa mgodi wa North Mara, na mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, wakitembelea moja ya Guest House ZMB iliyoko kijiji cha Nyakunguru, ambayo imejengwa kwa mtindo wa "Tegesha"

Mzee Maswi, akisikiliza kwa makini ushauri anaopewa na Naibu Waziri, kuhusu fidia ya eneo lake

Viongozi wa Mgodi wa North Mara, Abel Yiga, (kulia) na Jommy Ijumba, (wapili kulia), na Kamanda wa polisi wakiongoza ujumbe wa naibu waziri mara baada ya kutembelea Nyumba nyingine iliyojengwa kwa mtindo wa Tegesha jirani kabisa na eneo la uchimbaji la mgodi wa North Mara

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Jimmy Ijumba, (kushoto), Meneja wa Uendelezaji wa Kampuni ya Acacia

Asa Mwaipopo, (kulia) na Mkuu wa mahusiano ya serikali wa Acacia, Alex Lugendo, wakimsindikiza Naibu Waziri wa Madini, Charles Kitwanga, mara baada ya ziara yake ya kutembelea mgodi huo Jumatatu Mei 4, 2015. Ziara ya Naibu huyo wa waziri inakamilika leo Jumanne Mei 5

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (katikati), akizungumza mwishoni mwa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (Kuli), aliyoifanya kutembelea maeneo yanayozunguka Mgodi wa North Mara, Jumatatu Mei 4, 2015. Kushoto ni Meneja Uendelezaji wa Kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo

BAADA ya kusubiri kwa mika mitano, Vijana wa mtaa wa Stanford Bridge, CHEALSE,wametwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza  mapema, baada ya kuifunga Crystle Palace bao 1-0, bao lililofungwa kwa kichwa na Mbelgiji Eden Hazard, baada ya kipa wa Crystal Palace, Julian Speroni kupangua mkwaju wa penati uliopigwa na Hazard mwenyewe.

Chelsea imetwaa ubingwa huo wa mapema, huku ikiwa imebakiza michezo mitatu kibindoni, na katika ujumbe wake kabla ya mchezo huo, kocha mbwatukaji, Jose Morinho, aliandika maneno mafupi tu kwenye mtandao wa klabu hiyo akisema “Three more points let’s do it together” kwa kibongo, “Pointi tatu zaidi, tufanye kazi pamoja”

Ushindi huo umeifanya Chelsea kutwaa kombe hilo baada ya kujikusanyia pointi 83 baada ya michezo 35, ikifuatiwa na Manchester city yenye pointi 70 na ikicheza michezo 35. Arsenal iko nafasi ya tatu kwa kujikusanyia pointi 67 wakiwa wamecheza michezo 33, huku mashetani wekundu, Manchester United wao wako nafasi ya nne wakiwa na pointi 65, wakati Liverpoool, wako nafasi ya tano na pointi zao 61 na michezo 35.




No comments :

Post a Comment