Thursday, April 30, 2015

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 100 KWA SACCOS YA WALIMU WILAYANI RUANGWA MKOANI LINDI

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Mashariki, Yessaya
Mwakifulefule akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa,
Nicholous Kombe,  mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi millioni 100 ikiwa ni mkopo uliotolewa na mfuko huo kwa
wanachama wa SACCOS ya waalimu wilayani Ruangwa..Hafla hiyo ilifanyika
Wiyani Ruangwa hivi karibuni.

Wanachamawa  Walimu Saccos wa Wilaya  ya Ruangwa mkoani
Lindi wakifurahia   mkopo wenye thamaniya shilingi Milioni 100 uliotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa wanachama wa Saccos hiyo. Anaeshuhudia wa pili kulia ni Meneja wa LAPF,  Kanda ya Mashariki,
Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Wilayani Ruangwa hivi
karibuni.

 
Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe: William Lukuvi katika ziara yake Mkoni Mwanza.

1
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana Bw Baraka Konisaga (Kulia),ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakimkaribisha Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi muda mfupi kabla ya Mheshimiwa Lukuvi kupoekea ripoti ya awali ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza
2
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw Baraka Konisaga akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi wakati wa kupokea taarifa ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza ambayo imekuwa kero kwa wananchi wa jiji hilo katika
ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo
3
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akijadiliana jambo na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya
Kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza kufuatia tume iliyoundwa na Mheshimiwa Waziri mwezi uliyopita.
5
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na watendaji wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) mara baada ya kupokea ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wataalamu wa kujitolea wakikaribishwa nchini

1
Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Shota Yanagisawa (aliyesimama) akijitambulisha kwa Kaimu Katibu Mkuu – Utumishi Bw. HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kukaribishwa nchini iliyofanyika Utumishi mapema leo.
2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akiwakaribisha wataalamu wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kuja kujitambulisha Utumishi.
3
Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani wakishukuru baada ya kukaribishwa.
4
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akiagana na Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha iliyofanyika Utumishi.

Fight of the Century’ to air ONLY on DStv in Sub-Saharan Africa

New Picture (4)29 April 2015: MultiChoice Africa would like to inform the general public and all television broadcasters that ONLY SuperSport International has rights to air the ‘Fight of the Century’ bout taking place this weekend between Floyd Mayweather and Manny Pacquiao in Sub-Saharan Africa.
From this Saturday, 2nd of May, DStv will air the super-fight on SS6 and SS6 HD to enable all DStv Premium viewers to watch the action in High Definition. The build-up to the live event will begin at 8pm and headed by former boxer, Brian Mitchell, with a professional record of 45-1-3 and a panel that includes Phillip Ndou, who fought Mayweather in 2003, and legendary referee Stan Christodoulou. Viewers will also be treated to breaking news, extensive behind-the-scenes coverage, documentaries, one-on-ones with Mayweather and Pacquiao, plus past fight highlights involving the pair.
The rights also include live streaming, which is available to Premium subscribers on the SuperSport app. The build-up will culminate in The Fight of the Century which will air from the early hours of Sunday on May 3rd.
No other television station/event organiser or entity shall screen this boxing match on any other programme or channel in a public place or free-to-air, live or repeated, without the authorisation of MultiChoice since this will be in violation of the directives governing the distribution of programmes and television channels. It furthermore interferes with and infringes upon the programme and channel distribution rights and arrangements of third parties.
SuperSport’s knock-out build-up programming to ‘The Fight of the Century’ includes:
• Studio analysis headed by former boxer, Brian Mitchell and a panel that includes Phillip Ndou and legendary referee Stan Christodoulou on SS6 from 10pm CAT on Saturday.
• Updates on the biggest fight in boxing history plus “Big Fight Special” on SuperSport Blitz at 7am, 1pm and 7pm CAT daily.
• Wall-to-wall big-fight programming on Friday, 1st May on SS6 from 6am to 5.30pm CAT.
• SS6 will cross live to the MGM Grand Garden Arena in Las Vegas at midnight on Friday for the pre-fight weigh-in.
• After the weigh-in, Pacquiao’s six-knockdown defeat of Chris Algieri will be broadcast on SS6 to remind fans of his power and excitement.
• SS6 will cross to Las Vegas for the tournament at 3am CAT on Sunday morning. The undercard features WBC super-bantamweight champion Leo Santa Cruz against Jose Cayetano, plus WBO featherweight champion Vasyl Lomachenko against Gamalier Rodriguez.
• In the unfathomable possibility of missing the live fight action, DStv subscribers can catch the repeat the fight on SS6 at 7am CAT on Sunday and again on SS5 from 9pm CAT. Repeats will continue throughout the week.
• The bulk of the programming will also be available on the Video on Demand service.
PLEASE NOTE: SuperSport advises fight fans to set their alarm clocks for 4:30am CAT as the big Las Vegas bouts typically start at any time between 5:15am and 6am CAT.
For more information about this much-anticipated #MayPac bout, please visit www.dstv.com.

CHAWAKAMA yafanya ziara Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA, hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo
2
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA) wakisikiliza kwa makini walipofanya ziara katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam.
3
Mkurugenzi Msaidizi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wanne kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
 

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.

 Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.

Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

Anti poaching efforts lower elephant poaching in Ruaha

TANZANIA NATIONAL PARKS
images
On 23rd April, 2015, the ITV News network of UK ran an article with a title “Exposed: Tanzania’s elephant killing fields”. The article cited a decrease of elephants in Ruaha National Park from 8,500 in 2014 to just over 4,200 now. The article further pointed out that the main reason for the decline is “poaching and claimed that these findings are part of the Great Elephant Census, an ambitious two year project to conduct an aerial survey of elephant numbers and distribution across Africa”.
Tanzania National Parks would like to categorically deny the above accusations and is hereby giving clarification on the same for the interest of the general public:
• Tanzania National Parks is not informed of the release of any official census results indicating the decrease of elephants in Ruaha National Park.
• The practice of conducting census in the protected areas including National Parks is done on the basis of ecosystems as animals do migrate from one area to the other. Therefore, it is expected that any official release of the census results should have included the whole ecosystem of Ruaha-Rungwa and not Ruaha alone.
• Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) is an authority mandated to conduct wildlife census in all protected areas in Tanzania. Therefore as of now they have not released any official results regarding the census.
• As pointed out in our regular news releases, there have been significant improvement in efforts to fight poaching in Ruaha National Park that has resulted to a significant decline of elephant poaching incidences inside the park from 82 in 2012/2013 to only 36 in 2013/2014 and only 12 incidences between July 2014 and March 2015. These efforts will eventually lead to further decline and/or halting of elephant poaching in all National Parks.
In view of the above, Tanzania National Parks would like to assure the public that once the official results of the census are out, the public will be officially informed.
Issued by Corporate Communication Department
Tanzania National Parks
30th April, 2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com

Serikali yadhamiria kukamilisha Miradi ya Kitaifa ya Kimkakati

01
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
02
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
03 04
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya  uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
07
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
08
Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
09
Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiongea na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila (Kulia) mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima. Anayewasikiliza ni Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy.
010
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiongea na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
011
viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 uliokuwa ukifanywa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
……………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli
Serikali imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miradi ya kitaifa ya kimkakati iliyoibuliwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo unaofikia kikomo mwaka ujao wa fedha wa serikali.
Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nagu alisema kuwa mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kutandika reli za uzito wa ratili 56.12 kwa yadi kwa umbali wa km 9 kati ya stesheni za Lumbe, Mto Ugalla na Katumba; kukamilisha malipo ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo ambapo mabehewa yameshaanza kupokelewa Novemba 2014; kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli iliyoharibiwa na mafuriko katika maeneo ya Ruvu – njia panda ya Mruazi.
Waziri Nagu aliongeza kuwa kwa upande wa Barabara hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa kilometa 502.6 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kilomita 560, na ukarabati wa kilomita 78.8 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kukarabati kilomita 131.5. Kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madaraja ambapo daraja la Kigamboni limefikia asilimia 75, Sibiti asilimia 22, Kilombero asilimia 26, Mbutu asilimia 99, Lukuledi II asilimia 25 na Kavuu asilimia 36.
Katika sekta ya Uchukuzi, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa shehena iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 14.3 Machi 2015 dhidi ya lengo la tani milioni 13.0 kwa mwaka 2014/15; kuongezeka kwa ufanisi wa bandari katika kupakua magari kwa kila shifti moja ya saa 8 kufikia magari 886 kwa shifti kufikia Machi 2015 ikilinganishwa na lengo la magari 600 kwa shifti katika mwaka 2014/15; kupungua kwa muda wa meli kupakia na kupakua mizigo bandarini kutoka lengo la wastani wa siku 5 mwaka 2013/14 hadi wastani wa siku 3.7 kufikia Machi 2015; kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa malipo kwa njia ya mtandao mwezi Julai, 2014; na kuanza  kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa masaa 24 kwa siku zote za juma. Aidha, kwa upande wa bandari ya Bagamoyo, hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ujenzi wa bandari; na kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kupata wawekezaji katika bandari za Mtwara na Mwambani -Tanga.
“Katika sekta ya nishati, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542) Machi 2015, na ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) umefikia asilimia 86.9 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 2015. Kwa upande wa usambazaji wa umeme vijijini, wateja wapya 2,602 wameunganishiwa umeme katika mikoa ya Simiyu, Singida, Kagera, Tanga, Ruvuma, na Iringa,” alisema Dkt. Nagu.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, shughuli nyingine zilizotekelezwa nia katika sekta ya nishati, ni pamoja na kukamilika kwa usimikaji wa mitambo 4 ya kufua umeme yenye uwezo wa jumla ya MW 150, kuendelea na ujenzi  wa vituo vya kupoza na njia za kusafirisha umeme, na kuendelea na ujenzi wa  karakana, majengo ya utawala, na barabara za ndani katika mradi wa Kinyerezi I; kukamilisha ulipaji fidia kwa eneo la Makambako katika mradi wa usafirishaji umeme wa Makambako – Songea;  na kuanza ujenzi wa nguzo za njia ya umeme katika mradi wa msongo wa kV 400 wa Iringa – Shinyanga.
Akiwasilisha kazi zilizotekelezwa katika sekta  ya Maji, Dkt. Nagu alisema kuwa  ulazaji wa mabomba katika mradi wa maji Ruvu Chini kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam kazi ambayo imekamilika kwa kilomita 52.43 kati ya kilomita 55.93 za mradi sawa na asilimia 93.8; kwa upande wa mradi wa maji Ruvu Juu: mkandarasi amekamilisha utafiti wa udongo na uchunguzi wa awali wa mahali yatakapojengwa matanki Kibamba na Kimara; na kwa upande wa mradi wa Bwawa la Kidunda,  wananchi wamelipwa fidia ya shilingi bilioni 7 kupisha ujenzi wa barabara na eneo litakapojengwa bwawa.
“Kwa upande wa miradi ya maji vijijini, jumla ya miradi 123 ya maji ilijengwa na kukamilika. Idadi hii imenufaisha wananchi wapatao 463,750 na kuongezeka kwa ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma katika mikataba kutoka siku 265 hadi siku 90. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo bwawa la Iguluba (Iringa) na Wegero (Mara) yamekamilika. Vile vile, ujenzi wa bwawa la Kawa (Rukwa) umefikia asilimia 95, bwawa la Sasajila (Dodoma) asilimia 66.09 na Mwanjoro (Shinyanga) asilimia 45.4,” aliongeza Waziri Nagu.
Katika sekta ya kilimo, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kupatikana kwa hati za mashamba mawili ya Bagamoyo na Mkulazi; maghala 30 yamekarabatiwa na kupatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbozi na Momba.  Vile vile, skimu 30 za umwagiliaji zimepatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbarali, Kyela na Iringa; na mafunzo juu ya kubaini na kudhibiti visumbufu, matumizi bora ya maji, utunzaji na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji na kutumia mwongozo wa uendeshaji skimu za umwagiliaji yametolewa.  Aidha, ujenzi wa maghala 2 katika Wilaya ya Mlele umekamilika.
Vile vile katika sekta ya viwanda, Waziri Nagu alizitaja kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Itoni – Mkiu – Liganga na Mchuchuma kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha mitambo kufika maeneo ya Mchuchuma na Liganga; na kuanza uthamini wa mali za wananchi watakaohama eneo la Mchuchuma. Vile vile, fidia shilingi bilioni 53 imelipwa katika eneo la kujenga kituo cha Biashara na Huduma Kurasini; na fidia ya shilingi bilioni 7 imelipwa katika eneo la uwekezaji Bagamoyo na Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Mechants Holding International kwa ajili ya kujenga bandari na eneo la viwanda. Aidha, katika kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua viluwiluwi wa mbu, Kibaha, kazi ya ufungaji wa mitambo na ujenzi wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2015.
Akizungumzia upande wa maendeleo ya rasilimali watu, Dkt. Nagu alisema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na kuendelea kugharamia wanafunzi 159 wanaoendelea na mafunzo katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya nchi ambapo wanafunzi 124 wanagharamiwa na Serikali na wanafunzi 35 wanagharamiwa na nchi wahisani; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, ufundi na ustawi wa jamii.
Kwa upande wa utafutaji wa rasilimali fedha, Waziri Nagu alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inatumia kanzidata bora inayohifadhi taarifa inayoweza kuthaminisha bidhaa na hivyo kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Vilevile, alisema kuwa tozo kwa ajili ya uwekezaji katika elimu umeanza Julai 2013 ikiwa asilimia 2.5 ya mapato ghafi ya kampuni za simu.
“Katika sekta ya fedha, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuongezea Benki ya Maendeleo ya Kilimo mtaji wa shilingi bilioni 60; kuendelea kuongeza mtaji wa Benki ya Rasilimali kufikia shilingi bilioni 212 ambapo mtaji kutoka Serikalini ni shilingi bilioni 152.2 na shilingi bilioni 59.8 zimetokana na malimbikizo ya faida; na  mali za Benki ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 26.5 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 34.8 mwaka 2014,” alisema Dk. Nagu.
Kuhusu eneo la huduma za utalii, Dkt. Nagu aliongeza kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na usanifu wa ujenzi wa Utalii House awamu ya pili na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji mapato (utalii, uwindaji na upigaji picha). Aidha, idadi ya watalii kutoka nje iliongezeka kutoka watalii 1,090,905 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014. Vile vile mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.81 mwaka 2013 hadi dola za Marekani bilioni 1.98 mwaka 2014.
“Kwa upande wa Biashara, hatua iliyofikiwa ni kurekebisha sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa  elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo; kuanzishwa kwa kampuni ijulikanayo kama Tanzania Mechantile Exchange plc kusimamia na kuendesha soko la mazao ya bidhaa na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya mipakani, Kikanda na Kimataifa,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Dkt. Nagu maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/16 yamezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16). Aidha, Mpango huu umezingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini – MKUKUTA II (2010/11 – 2014/15), Malengo ya Milenia, Mwongozo wa Mpango na Bajeti  kwa mwaka 2014/15; Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2014/15 yaliyojadiliwa na Bunge Novemba, 2014; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010 – 2015); na sera na mikakati ya kisekta.

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
 
…………………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
 
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad
Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya
kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza
makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
 
Utafiti
huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini
Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni
ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI

Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingiJaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
……………………………………….
Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria vipo.
Dk Bana alisema kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.
Alisema watu kama wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.
Katika shauri hilo la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning) ili iweze kukabiliana navyo mapema.
Akizungumzia kama Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23 iliyopita.
Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahaloMkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.
Aidha alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.
Alisema mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.
Pia alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk bana akizungumza katika mdahaloDk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.
Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Alisema kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa vyama vingi.
Alisema pia kuna haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu yanayostahili katika maeneo yao.
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP PoinsotJaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .
Alizungumzia pia haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.
Katika mdahalo huo ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa changamoto za siasa za vyama vingi.
Profesa Rugumamu alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
IMG_4917Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Miongoni mwa changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi, wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.
Pia alizungumza uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.
Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Awali akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na kutokuelewana.
Alisema mkutano huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.
Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.
Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingiProfesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumzaProfesa Rugumamu akizungumza.
IMG_4861Baadhi ya washiriki wakijadiliana.
IMG_4879Washiriki wa mkutano wakijadiliana.
wanamdahalo wakiwa makiniWanamdahalo wakiwa makini.

SIMU ZA MKONONI ZINAWEZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

indexMahmoud Ahmad Arusha
………………………………..
Imeelezwa kuwa elimu ya juu inaweza kuchangia watu wote kupata elimu hapa nchini ikiwemo matumizi ya simu za mkononi na utandawazi kama matumizi sahihi ya teknolojia na kuwafikia wananchi wengi hata vijijini.
Kauli hiyo imetolewa na makamu mkuu wa Taasisi ya Nelson Mandela Prof.Botrun Mwamila wakati wa hitimisho la mkutano uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na serikali ya Sweden na vyuo vikuu vya nchi hiyo uliofanyika chuoni hapa kwa siku tatu kujadili teknolojia inavyoweza kusaidia kuweza kupata elimu.
Prof.Mwamila alisema kuwa elimu ya vyuo vikuu kama itatumiwa vizuri na wasomi wetu hapa nchini inaweza kuwasaidia wananchi wengi wa madaraja yote kuweza kupata elimu kusudiwa na hivyo kuweza kurahisisha maendeleo na ukuaji wa kiuchumi.
Alisema kuwa katika mkutano huo wamejadili mambo mbali mbali yatakayosaidia kuweza kutoa elimu kwa urahisi kuwafikia wananchi  kwa kutumia teknolojia ya simu za mkanoni ambazo wananchi wengi wanazo hata vijijini.
“Teknolojia na utandawazi ukitumiwa vizuri unaweza kusaidia katika ukuaji na upatikana wa elimu hivyo kuondoa matatizo yatokanayo na wananchi kutoweza kupata elimu na kushindwa kuchangia shemu ya maendeleo”alisema Prof.Mwamila.
Aidha alisema kuwa  maazimo yaliotokana na mkuatano huo  yatakuwa ni sehemu ya Agenda ya mkutano utakaofanyika nchini Korea Kusini ambapo suala la elimu kwa wote bila ya kujali jinsia litapewa kipaumbele katika majadiliano ya mkutano huo.
Akatanabaisha kuwa ukuaji wa elimu na matumizi ya utandawazi ikiwemo simu za mkononi na matumizi ya mtandao wananchi wakiacha kutumia kwa matumizi yasiofaa na wakageukia kutumia kwa kujipatia elimu maendeleo ya haraka yatapatikana hapa nchini na hivyo kila mwananchi kwa daraja lake atasogea kiufahamu.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 50 KUTOKA KAMPUNI YA TSN NA MIPIRA 50 KUTOKA KAMPUNI YA SMART SPORTS KWA AJILI YA MASHINDANO YA KINONDONI CUP

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda ‘Kaka Bonda’
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.
…………………………………………………………………..
 
Na Suleiman Msuya
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.“Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao,” alisema. Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.
Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU KIJIJINI KISANGA.

 
 Mgeni Rasmi katika Sherehe za uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akiongea na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula
Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica
Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na
kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo
Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa
Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia
kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi
na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua
Mama kiuchumi.
 Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia
kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na
kumkwamua kiuchumi.
 
Akizungumza katika Sherehe hizo Mh.
Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia
wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi
kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe
sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa
kwanza atokee katika wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa
mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na
kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa
mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za
kisasa za kilimo bora.
 
Nae Mwakilishi kutoka Oxfam
Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa
wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi
mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha
Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni
Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa
vifaa na zana za Kilimo.
 
Eluka  alizungumzia historia fupi
ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza
kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao
wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na
kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za
kuendesha Kilimo.
 
Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh.
Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na
watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano
hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano
la  Mama Shujaa wa Chakula.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AKUTANA NA BIONGOZI WA BRITISH AMERICAN TOBACCO

1
PRIME MINISTER MIZENGO PINDA SPEAKING TO BRITISH AMERICAN TOBACCO OFFICIALS IN HIS OFFICE, DAR ES SALAAM, APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS  JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA, ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA
(PMO PHOTO)
2
PRIME MINISTER, MIZENGO PINDA POSES FOR A GROUP PHOTO WITH BRITISH AMETICAN TOBACCO OFFICIALS AT HIS OFFICE IN DAR ES SALAAM ON APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA- BAT AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA, PM, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO AND TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA

TASWIRA ZA SUNDAY CELEBRATION SEASON 6 YA GWT

Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakilishambulia jukwaa katika Sunday Celebration Season 6.
Kiongozi wa Bendi ya The Jordan, Daniel Mbepera, akiimba kwa hisia sambamba na bendi yake.
Wageni waliohudhuria wakisifu na kuabudu sambamba na GWT.
Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.
KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la ‘Sunday Celebration’ ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.
Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.
(PICHA ZOTE NA GWT)

MATUKIO YA UZINDUZI WA mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Ruvuma April 29, 2015.

1
Muasisi wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Wilaya wa Kwanza mwafrika kuteuliwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Alhaj Mustafa Mohamed Songambele(90  ) akiongea na mwakishi wa Channel ten mkoani Ruvuma Marietha Msembele (kushoto) leo mjini Songea wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein.
2
Baadhi ya umati wa wananchi wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein leo mjini Songea.
3
Baadhi ya umati wa watumishi wa umma na sekta binafsi wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein leo mjini Songea.
Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent-Songea.

BENKI YA POSTA YAJIVUNIA UTENDAJI BORA KWA MWAKA 2014 ULIYOIPA FAIDA NONO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia , Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo leo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

Timu ya Soka ya Nyota Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden Fc kwa Magoli Sita kwa Matano

222
Naibu Meya wa Jiji la Arusha Prosper  Msofe akiwa na watangazaji wa Redio 5 arusha,wa kwanza kushoto Hilda Kinabo,Mwangaza Jumanne na Akida Kilango wakifuatilia mashindano ya ndondo Cup yaliyoandaliwa na kampuni ya tan communication media
005
Mlinda mlango wa timu ya Nyota Fc Hamis maarufu kama Dida akiwa anatizama mpira wavuni.
001
Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1.
002
Mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penati katika lango la Umbrela Garden.
003
Mashabiki waliojitokeza Uwanjani hapo wakifuatilia mechi hiyo.
004
Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5.
 Habari picha -na Ashura mohamed.arusha
…………………………………….
Timu ya  Soka ya Nyota  Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden Fc  kwa  Magoli  Sita kwa Matano na kufanikiwa kuondoka na kombe la Ndondo Cup  Sambamba na Kitita cha Shilingi  Laki  Tano Taslimu  katika fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc vilivyopo Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup  yamewakutananisha vijana wengi ambao wamepata fursa ya kuonesha vipaji  vyao.
Prosper Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi lakini katika upande wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao  inafanya vizuri katika ligi mbali mbali hapa nchini.
Aidha Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji zaidi na kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua eneo la kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za kuonesha vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja ambayo itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa nchini.
Kwa sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu vijana wetu wana vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua viwanja na kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema Msofe
Kwa upande wake waandaaji wa  Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa redio 5, Mathew Philip alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani kwa wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa soka.
Mathew alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani mbali mbali kwa wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha  kwa muda mrefu hakukuwa na Soka la Mchangani ambalo lina vijana wengi ambao wana vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.
Timu zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka washindi,Ambrella Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia shilingi  laki tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,

BASATA, TCRA WAWATAKA WASANII KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO

01
1. Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika Jumanne ya wiki hii makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala, Sharif Shamba. Kushoto ni Mwanasheria wa BASATA Deogratius Nchimbi.
02
2. Mwanasheria wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Deogratius Nchimbi (Kushoto) akiongea jambo na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii wakati akihitimisha mjadala kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii uliowasilishwa na Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
03
3. Mmoja wa wadau wa Jukwaa la Sanaa akiuliza swali kwa Meneja mawasiliano wa TCRA juu ya athari za sheria mpya ya mitandao ya kijamii kwa wasanii na waandishi wa habari.
04
3. Mmoja wa wadau wa Jukwaa la Sanaa akiuliza swali kwa Meneja mawasiliano wa TCRA juu ya athari za sheria mpya ya mitandao ya kijamii kwa wasanii na waandishi wa habari.
05
 Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa mapema wiki hii.

KITABU KIPYA CHA MHAMASISHAJI MAHIRI ZAIDI AFRIKA, ERIC SHIGONGO KUZINDULIWA MEI 30, 2015 ALISA HOTEL, ACCRA


Dk.Shein azindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Ruvuma April 29, 2015.

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015.
3
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
4
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
 Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent, Songea

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE.

AD1 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD2 AD3 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD4Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia mkutano huo. AD5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR
AD7 AD8 AD9Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania, waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR/
………………………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Aprili 29, 2015, ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa dharura wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Harare, chini ya Uenyekiti wa Rais Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, Mwenyekiti wa sasa wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mkutano huo wa siku moja pia umehudhuriwa na Rais Seretse Ian Khama, Rais wa Botswana na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mfalme Muswati III wa Swaziland, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Namibia Hage Geingob, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Awali akifungua mkutano huo Rais Mugabe alisisitiza umuhimu wa nchi za SADC kuwa na mpango madhubuti wa Viwanda kwa kuwa uwepo wa viwanda utasaidia kupunguza tatizo kubwa linalozikabili nchi hizi hasa ajira, pamoja na uchumi duni unaotokana na ukosefu wa viwanda vya kuboresha bidhaa zinazozalishwa katika nchi za ukanda huu. Mkakati huu uliopitishwa na Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaanza mwaka huu 2015 hadi mwaka 2063. Katika mkakati huu nchi za SADC zinalenga kutanua uhuru wa soko katika utatu wa kanda za Kibiashara yaani SADC, EAC na COMESA ikiwa ni pamoja na kutenga eneo huru la ukanda wa kiuchumi wa nchi za kanda hizi, huku lengo likiwa kufanikiwa upatikanaji wa eneo huru la ukanda wa biashara kwa nchi za Afrika. Masuala mengine ni pamoja na kukuza bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizi katika masoko ya Asia ambao ni walaji na watumaji wakubwa wa malighafi zinazozalishwa katika nchi hizi.
Rais Mugabe alifafanua pia kuwa, nchi hizi kwa umoja wake zikiunganishwa utakuta ndizo zina rasimali kubwa ya madini ya Dhahabu, Almasi na hata Gesi na kwamba kama mtengamano huu utakamilika nguvu ya pamoja inaweza kugeuza hali ya maisha ya wananchi wa nchi hizi sambamba na maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo.
Awali akizungumza kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Mugabe, Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Lawrence Tax aliishukuru serikali ya Zimbabwe kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu ambao ulikuwa ni mwendelezo wa ule uliofanyika Victoria Falls, Zimbabwe Agosti 17, 2014 mkutano uliotaka nchi wanachama wa SADC pamoja na kupitisha mkakati wake wa Kimaendeleo, upange dira ya utanuaji na uendedlezaji viwanda katika ukanda huu.
Matukio mengine katika mkutano huu ni pamoja na makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, makabidhiano yaliyofanywa na nchi ya Zimbabwe chini ya Rais wake Robert Mugabe kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Pia Rais Mugabe alitumia muda huo kuutaka Mkutano huu wa Dharura kutoa heshima zao kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi kwa kutambua mchango wake katika uhuru wa nchi zilizomo SADC na pia mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi. Raia Mugabe alimtaja Hayati Brigedia Mbita kama mpiganaji mahiri na kiongozi aliyefanya kazi kwa maslahi ya watu wengi bila kuchoka na kwamba Afrika na SADC vitamkumbuka daima kwa mchango wake huo.
Imetolewa na:    Ofisi ya Makamu wa Rais
                                 Harare, Zimbabwe
                                       Aprili 29, 2015

WATUHUMIWA WA KESI ZA UGAIDI ARUSHA WAIBUA MAMBO MAHAKAMANI

imagesMahmoud Ahmad,Arusha
…………………………………………
 
Watuhumiwa 60 wa kesi za ugaidi jijini Arusha wamemuomba Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Nestory Barro kuchukua uamuzi mgumu wa kufanyia kazi kwa vitendo makosa yaliyomo kwenye Sheria dhidi ya tuhuma zinazowakabili.
 
Madai hayo waliyatoa mwishoni mwa wiki iliyopita  wakati kesi zao zilipokuwa zimepangwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo Mwendesha Mashitaka wa Serikali Augustine Kombe aliziahirisha hadi Mei 8, Mwaka huu kutokana upelelezi wa polisi kutokamilika.
 
Akizungumza mahakamani hapo kwa niaba ya wenzake mara baada ya kunyoosha mkono na kupewa nafasi na Hakimu Barro, mtuhumiwa Jafar Lema aliyeomba kujulishwa wanapokuwa mahakamani hapo wanakuwa chini ya mamlaka ipi.
 
Hatua ya kuuliza swali ilikuja baada ya mtuhumiwa mwenzake kutaka kujua suala la dhamana dhidi ya mashitaka yanayowakabili ilihali akidai wapo watuhumiwa wenzao waliopewa dhamana wakiwa polisi na wanaendelea kuripoti kituoni hadi leo.
Akitoa ufafanuzi kwa mtuhumiwa na wenzake Hakimu alisema, kosa waliloshitakiwa nalo halina dhamana, kwani hata hao aliodai walipewa dhamana polisi na kutakiwa kuripoti wanaweza kuwa wana mambo yao na ndio maana hawapo mahakamani.
“Unajua sheria yetu hii bado ina makosa kwasababu mtuhumiwa unatakiwa uwe mahabusu wakati kesi yako ikiwa imeanza kusikilizwa na si wakati wa upelelezi,” alisema Hakimu Mkazi Baro.
 
Hata hivyo majibu hayo yalimpa fursa mtuhumiwa Lema kuomba kufahamishwa kwamba wanapokuwa mahakamani hapo wanakuwa chini ya nani, Polisi au Mahakama, ambapo Hakimu Mkazi Barro alimueleza kuwa ni Mahakama.
“Mheshimiwa Hakimu, sasa nakuomba usiogope, hakuna mtu atakayekufunga kwani Taifa litakuona wewe ni shujaa, nakuomba na wenzangu ufanyie kazi kwa vitendo makosa hayo yaliyopo kwenye sheria,”alidai mtuhumiwa Lema na kuongeza:
“Nakuomba umwambie Mwendesha Mashitaka wa Serikali Kombe ayarudishe majalada yote ya kesi hizi hadi hapo upelelezi utakapokamilika, kama watakusumbua nipo tayari mimi na wewe tushirikiane kufungua kesi ya Kikatiba,”alidai Lema
Hata hivyo Hakimu Mkazi Barro alilazimika tena kutoa ufafanuzi kwa mtuhumiwa huyo na wenzake akieleza kwamba alichokuwa akikisema mtuhumiwa kina ukweli kwamba sheria ina makosa lakini kwa shauri hilo yeye hana mamlaka yoyote.
“Katika mashitaka haya ya PI aisee sina mamlaka nayo, labda kama ingekuwa na makosa ya wizi wa kuku na mengine kama hayo huku nina mamlaka napo, sio katika hili,” alisema Hakimu Mkazi Barro.
Kwa upande wake Mwendesha Mashitaka Kombe akijibu maadhi ya madai ya watuhumiwa hao  aliwashauri kuandika barua kwa Mkurugenzi Mashitaka nchini (DPP), kuelezea kuhusu kuchelewa kukamilika kwa upelelezi wa kesi zao.
 
Watuhumiwa hao wameshitakiwa kwa makosa yaliyo chini ya Sheria ya kuzuia ugaidi, ambapo Sheria namba 22  ya Mwaka 2002 inasema upelelezi wa shauri hilo ukishakamilika, Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi. Watuhumiwa hao 60  waliopo katika kesi mbalimbali wanakabiliwa na mashitaka ya kuua, kujaribu kuua, kusajili na kusafirisha vijana kujiunga na kikundi cha ugaidi cha Al-Shabaab.
 
 Mbali na mashitaka hayo wanahusishwa na  tukio la  milipuko ya mabomu Bar ya  Arusha Night Park, mlipuko wa Bomu Viwanja vya Soweto na mlipuko uliotokea Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasite  jijini Arusha ambapo ilisababisha vifo na majeruhi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AAGANA NA BALOZI WA BRAZIL NCHINI

1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco  Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco  Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.
Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.
Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.
“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.
Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, APRILI 29, 2015.

Dk.Shein azindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Ruvuma April 29, 2015.

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwasha mwenge wa Uhuru Kitaifa katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma leo(kushoto) Waziri wa Vijana Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa jamii vijana wanawwake na watoto Bi Zainab Mohammed.
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa  Juma Khatib Chum baada ya kuuwasha leo katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma,
{Picha na IKulu.]

Rais Kikwete atoa heshima za Mwisho kwa Brigedia Jenerali Hashim Mbita

1
2Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika(OAU) marehemu  Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
2
3 4Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho.
(picha na Freddy Maro)

WAZIRI WA MEMBE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Membe akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 28, 2015. Rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinton Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).

WAMILIKI wa redio za jamii watakiwa kujenga taswira njema za redio zao

DSC_0088
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
……………………………………..
Na Mwandishi wetu, Mwanza
WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu.
Akizungumzia malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake alisema kwamba kuwapo kwa mpango wa biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa na maana kama wasipozingatia ujenzi wa taswira utakaowafanya wadau kuvutiwa na redio hizo.
Alisema kuna umuhimu wa suala hilo kwani kusipojengeka kwa mahusiano bora kati yake na jamii, watu binafsi na taasisi za kiraia zenye malengo tofauti katika kuhudumia wananchi, redio hizo hazitakuwa na biashara ya kufanya.
Ahungu pamoja na kusifia mtindo uliotumika kuwezesha redio hizo kuandaa mipango kazi ya biashara yenye lengo la kusimamia masoko na fedha alisema warsha imefanikiwa kuwaweka karibu zaidi na wadau wamiliki wa vyombo hivyo.
Warsha hiyo ni hitimisho ya awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo redio za jamii katika matumizi ya Tehama na mawasiliano inayoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO iliyofanyika katika kituo redio cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema katika warsha hiyo wamiliki hao walijifunza uandaaji wa mipango ya biashara, kutunza fedha, utafutaji masoko, uhakiki wa mipango ya biashara na vipindi vya redio kwa lengo la kuona namna ya kuvifanya kuleta biashara.
Naye Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemsaidia sana katika kuhakikisha kwamba kituo chake kinakuwa bora na kinachovutia watangazaji.
Alisema mafunzo hayo yamewafanya wajitambue kwani yamefanyika mfululizo kwa mara 5 na kuwafanya wabadilike.
Aidha Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula alisema kwamba anashukuru mafunzo kwa kuwa yamewafanya kuondoa mawazo vichwani na kuweka mipango kazi katika karatasi na kuwezesha wafanyakazi nao kufuatilia.
DSC_0219Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0229Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0067Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0064
DSC_0082Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu akiendelea kuwapiga msasa viongozi hao namna ya kutafuta masoko na kuboresha mpango biashara.
DSC_0236Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa pili kulia) wakati wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja. Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vituo vya Redio Jamii nchini.
DSC_0246
Picha ya pamoja ya Wakufunzi na washiriki wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.

TANZANITE YAKOSA SOKO HAPA NCHINI KUTOKANA NA WATANZANIA KUTOKUVAA MADINI HAYO

SAM_2162
Kulia Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine  Gibson A.Kilala akitoa maelezo kwa Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene hivikaribuni jijini Arusha mara baada ya Waziri huyo kutembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya madini na vito yaliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2156
Baadhi ya madini
SAM_2163
Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine  Gibson A.Kilala akimuonyesha Waziri baadhi ya madini yanayopatikana katika kampuni yao
SAM_2160
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene kushoto akipata maelezo mafupi kutoka kwa mfanyakazi wa Moreshine Bw.William Simba
SAM_2161
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene akiangalia madini.
SAM_2159
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana katika banda la Moreshine kushoto ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Gibson A.Kilala na kulia ni William Simba mfanyakazi wa Moreshine
SAM_2166
Bango la Kampuni ya Moreshine.
SAM_2164
Mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu  Gibson A.Kilala akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
……………………………………………………..
Changamoto ya Watanzania kutokuvaa vito vya thamani vinavyotengenezwa na mawe mbali mbali yanayopatikana hapa nchini  imepelekea madini yakiwamo Tanzanite kukosa soko hapa nchini,Soko la madini haswa tanzanite limekuwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa watanzania hawana desturi ya kuvaa madini hayo
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala alisema kuwa kutokuwepo kwa utamaduni huo miongoni mwa watanzania kumepelekea soko la madini kupatikana nje ya nchi badala ya hapa nchini ambapo yanapatikana.
Aidha ameiomba serikali kuweza kusajili kampuni ambayo itasaidia kusafirisha madini kama zilizo kampuni nyingine za kusafirishia mizigo hapa nchini kama {DHL)ili kuwawezesha wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa usalama zaidi kama zilivyo nchi za jirani kama Kenya.
Hata hivyo ameiomba serikali kuondoa changamoto ya mipaka kwa wafanyabiashara wa madini kwa kuwaruhusu kufuata madini yalipo badala ya kusubiria brokers hali ambayo inawagharimu muda mwingi lakini pia gharama kuongezeka.
Amesema ni vyema wafanyabiashara wakaruhusiwa kwa leseni zao kufuata madini yalipo ili kuwawezesha kufikia migodini tofauti na sasa ambapo leseni zao haziruhusu kufuata madini yanapopatikana badala yake kusubiria broker wawaletee.

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI- ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

Balozi Amina Salum Ali
 …………………………………………
Na mwandishi wetu Washington, DC
Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.
Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.
Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.
 
Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania

No comments :

Post a Comment