Monday, March 30, 2015

ZOEZI LA KUHESABU KURA NIGERIA LINAENDELEA HUKO RAIS JONATHAN AKIKABILIWA NA USHINDANI

Zoezi la kuhesabu kura nchini Nigeria linaendelea huku rais aliyemadarakani Goodluck Jonathan akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari.

Tume ya uchaguzi ya Nigeria imesema kuwa inatarajia kumtangaza mshindi wa urais hii leo, katika uchaguzi huo ambao wapigakura walipiga kura kwa siku mbili kutokana na hitilafu.

Umoja wa Mataifa umepongeza uchaguzi huo licha ya kuwepo kwa hitilafu za kiufundi, maandamano ya kupinga na vurugu zinazohusishwa na kundi la Boko Haram.

MAWAZIRI WA MATAIFA YENYE NGUVU WAKUTANA NA WAZIRI WA IRAN LEO

Mawaziri kutoka nchi sita zenye nguvu duniani wanatarajiwa kukutana hii leo kwa siku nzima na waziri wa mambo ya nje wa Iran kuhusiana na mpango wake wa kurutubisha nishati ya nyuklia.

Siku ya mwisho ya kufikia makubaliano ya Iran kusitisha mpango huo, imepangwa kuwa ni jumanne.

Lengo la makubaliano hayo ni kuifanya Iran, kuwa mwaka mmoja nyuma kabla ya kuweza kutengeneza mafuta ya kutosha ya nyuklia yatakayoiwezesha kutengeneza silaha ya nyuklia.

Wawakilishi kutoka Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Urusi wanashiriki mazungumzo hayo yanayofanyika katika Jiji la Lausanne nchini Switzerland.

SHOW YA LADY JAY DEE NA ALI KIBA ILIVYOBAMBA KIOTA CHA M.O.G BAR & RESTAURANT

DSC_0035
Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
DSC_0033
DSC_0058
Vijana watanashati wenye vipaji vya aina yake wa Machozi Band wakipiga Back Vocal kumpa sapoti Lady Jay Dee a.k.a Komando Binti Machozi. Kutoka kushoto ni Faraja, Omirady pamoja na Chiqitita.
DSC_0089
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Machozi Band wakimtunza manoti Lady Jay Dee.
DSC_0083
DSC_0078
DSC_0046
Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.
DSC_0048
DSC_0065
DSC_0066
DSC_0204
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.
DSC_0217
               Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.

UN KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUTANZUA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO

DSC_0065
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.
DSC_0207
Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0209
Meza kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
DSC_0131
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Maendele0 ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
DSC_0223
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0228
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia htouba ya mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.
DSC_0233
DSC_0241
DSC_0201
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma risala kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.

TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA HABARI ZANZIBAR MABINGWA WA NSSF MEDIA CUP 2015

Mgeni rasmi katika mashindano hayo Prof. Herman Mwansoko akikabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha wa Timu ya Habari Zanzibar baada ya kuibuka mabingwa wa Mashindano ya NSSF Media cup 2015. Wapili kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NSSF  Ludovick Mrosso, na wa kwanza Kulia ni Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Bi Eunice Chiume.
 
Mgeni rasmi katika mashinado hayo Prof. Herman Mwansoko akikabidhi zawadi kwa Mshindi wa pili kwa kwa Nahodha wa Timu ya IPP Media baada ya kuwa washindi wa pili kwa mpira wa miguu wa Mashindano ya NSSF Media cup 2015. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NSSF  Ludovick
Mrosso, na wa kwanza Kulia ni Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Bi Eunice Chiume.
Mgeni rasmi katika mashinado hayo Prof. Herman akikabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha wa Timu ya NSSF ya Mpira wa Pete Bi Nora Mwidunda baada ya kuwa washindi wa pili wa Mashindano ya NSSF Media cup 2015. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ludovick Mrosso, na wa kwanza Kulia ni Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Huduma kwa
Wateja Bi Eunice Chiume.
Mgeni rasmi katika mashinado hayo Prof. Herman Mwansoko akikabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha wa Timu ya Uhuru Queens ya Mpira wa Pete baada ya kuibuka mabingwa wa Mashindano ya NSSF Media cup 2015.
Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ludovick Mrosso, na wa kwanza Kulia ni Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Bi Eunice Chiume.

No comments :

Post a Comment