Baadhi ya akina mama wanachama wa mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii wakifurahia baada ya kujifungua salama watoto wao kutoka katika
baadhi ya hospitali zilizoingia na mkataba na mfuko wa hifadhi ya jamii
Na christian
Gaya majira Januari 21 2014
Uzazi
salama kwa akina mama wanapojifungua ni sehemu muhimu sana kwa taiffa letu na kwa
maisha yao ya sasa na baadaye. Kwa nchi ya Tanzania kuwepo kwa kuborehesha kwa
kinga maalum ya uzazi ni kitu ambacho inatakiwa kuwekewa kipaumbele kama taifa
endelevu.
Hili ni jambo ambalo liko wazi kabisa ya kwamba kila
binadamu ana uhusiano mkubwa na hifadhi ya jamii iwe kinadharia au kivitendo
kutoka kuzaliwa kwake mpaka kufa, binadamu mwenyewe lazima ajishughulishe na
kazi hatarishi na kuugua magojwa mbalimbali
na kwa hiyo binadamu lazima akumbane na majanga mbalimbali kama vile
majanga ya kiuchumi na ya kijamii yanayosababishwa na kukoma au kupungua kipato
kutokana na maradhi, kujifungua mtoto, ajari za kuumia kazini, ukosefu wa
ajira, ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa gharama za matibabu haya majanga
yote ni matukio ya kila siku kwa binadamu ambayo hayatabiriki na yote
yanaaangukia kwenye mpango wa hifadhi ya jamii. Hivyo ni kitu cha asili ya
kwamba kila mtu lazima ajue hifadhi ya jamii ni nini kwa sababu ni sehemu ya
maisha ya mwanadamu
Kutokana
na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa shirika la kazi duniani (ILO) lengo
la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni kuhakikisha kuwa kazi za wanamke hawaingiliwi
na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za
kuzaa hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama wa
kazi zao iwe ya kujiajiri au kuajiriwa.
Mpaka sasa hapa nchini kuna
mifuko sita ya hifadhi ya jamii ambayo imeanzishwa kwa sheria za bunge mifuko
ambayo ni: Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa pensheni wa
wafanyakaziwa serikali za mitaa(LAPF), Mfuko wa akiba wa wafanyakazi wa
serikali (GEPF), Mfuko wa pensheni wa watumishi wa serikali (PSPF), Mfuko wa
pensheni wa PPF, Mfuko wa taifa wa bima
ya afya (NHIF).
Lakini
kati ya mifuko hii ni mifuko miwili tu ambayo ni NSSF na LAPF ndiyo inayotoa
fao hili la uzazi kwa wamama na hutolewa kwa wamama ambao ni wanachama tu na
wala siyo hata kwa mke wa mwanaume ambaye ni mwanachama wa mchangiaji wa mifuko
hii. Fao hili ni la muhimu sana kwa upande wamama kwani husaidia kupunguza vifo
vya watoto na wamama wenyewe. Kwa sababu utafiti unaonesha ya kuwa idadi kubwa
ya wamama wanaokufa kwa sababu ya kukosa huduma wakati wa kujifungua
inaongezeka kila siku hasa kwa nchi zinazoendelea kama vile Tanzania. Na kwamba
kati ya wajawazito kumi wanajifungua akina mama wanne hupoteza maisha pamoja na
watoto wao. Na matukio haya yote hutokea nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania
Na
elementi kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao
taslimu ya kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake
wakati akiwa wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu,
kuhakikisha ya kuwa mama mjamzito anapatiwa kinga ya afya ya ujauzito pamoja na
mama anayeyonyesha bila kumsahau mtoto wake kupatiwa kinga kutokana na hali
hatarishi zinazoweza kusababishwa na sehemu za kazi zenyewe. Mama mjamzito au
anayeyonyesha ana haki kupewa kinga ya kutofukuzwa na kubaguliwa na kupewa
kinga ya kwenda kunyonyesha mara tu baada ya kurudi kazini au mara tu baada ya
kutoka rikizo ya uzazi.
Kwa
hiyo kinga ya uzazi kwa akina mama lazima ichangie afya na ustawi wa wamama
pamoja na watoto wao na hivyo kutimiza malengo ya namba 4 na 5 ya maendeleo ya
millennia ya Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa, yanayotaka kupunguza
vifo vya watoto na kuboresha afya za wamama. Na kwa kuhakikisha ya kuwa kazi
zao wanawake za kuajiriwa pamoja na usalama wa mapato yao yanalindwa kama inavyotakiwa
wakati na hata baada ya kutoka likizo ya uzazi. Kinga ya uzazi kwa mwanamke ambaye ni mjamzito kabla ya
kujifungua na baada ya kujifungua vile
vile ni muhimu kuhakikisha ya kuwa mwanamke mzazi anapewa fursa sawa na
matibabu katika sehemu za kazi ili kuhamasisha usawa wa jinsia na madaraka kwa
wanawake.
Lakini
pamoja na haya yote ingawa kinga ya uzazi imewekwa kama sehemu ya mila na
desturi zetu ndani ya familia zetu, lakini mpaka leo wanawake kwenye sekta
iliyorasmi na ile isiyorasmi bado wanawake wanaishi kwenye mazingira
yanahusiana na uzazi wa kutishiwa kwa ajili kupata afya na usalama wa kiuchumi
na kijamii.
Wanawake
wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata
baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi na hata
kubaguliwa eti kwa sababu ni mjamzito au atakuja apate mimba. Lakini pamoja na
hayo mazingira ya kazi, biolojia na kifizikia na kemia mbalimbali za madawa
zinazosaidia kuzalishia kazi zinaweza kuleta hali hatarishi zaidi kwa upande wa
uzazi na watoto wanaozaliwa hasa kwa kukosa mikakati ya uhamasishaji wa elimu
ya umma, miongozo na thathimini.
Uwezo
wa wanawake wanaoanza kunyonyesha watoto kulingana na utaratibu uliowekwa na
shirika la afya la dunia unaingiliwa na kazi za uzalishaji hasa za kuajiriwa na
kujiajiri wenyewe kutokana na ukosefu wa kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha
watoto. Kulea watoto bila ya kuwaharibia wanawake fursa zao za haki za
kushirikishwa kwenye kazi za maendeleo ya kiuchumi inabaki kuwa ni changa moto kubwa
wakati ubora na uwezo nafuu wa mipangilio ya uangalizi wa mtoto haupo kwa mpana
mkubwa kabisa.
Kwa
hapa nchini wanawake wengi si wanachama wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya
jamii lakini kwa sababu ya kukosa elimu juu ya mafao yanayotolewa na mifuko hii
hata wale wachache ambao ambao ni wanachama hai wa mifuko hii wanakosa huduma
hizi za kinga ya uzazi.
Na
tunaona mara nyingi idadi kubwa ya mama kufa kabla au mara tu ya kujifungua.
Hivyo hizi mimba nyingi zimekuwa zikitishia wamama na mara nyingi hufa mama au
mtoto kama siyo wote. Na inasekama karibu asilimia 70 ya wamama duniani
wanaopoteza maisha yao wakati wa kujifungua hutokea afrika na Tanzania ikiwa
mojawapo. Na watoto wengi huzaliwa wakiwa wemekufa au mara tu mama kujifungua.
Ni
kweli ya kuwa idadi kubwa ya akina mama hawako katika mpango wa hifadhi ya
jamii hivyo wengi wamejiajiri wenyewe. Lakini hata idadi ndogo ya wanawake walioajiriwa na kuwa wanachama wa mifuko hii
ya pensheni hawajaweza kutumia nafasi ya fao la uzazi kabla ya kujifungua na
baada ya kujifungua.
Na
kwa upande wa fao hili la uzazi mara nyingi wazazi wengi hawapata taarifa ya
kuwa anastahili kupata kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua na kupita
muda wa grace period ambao ni miezi mitabu (3) au ndani ya siku tisini (90).
Tumeona mara kwa mara wamama waliojifungua wakifuatilia bila mafanikio kwa
sababu wanachelewa kufungua madai kwa wakati muafaka.
Ni kweli kwamba nchi
kadhaa, zikiwemo Brazil na Tanzania, zimeanza kuwahusisha wafanyakazi wanawake
katika sheria za kazi ili kuwapatia kinga au haki za msingi kama vile likizo ya
uzazi, likizo ya ugonjwa na ruzuku ya serikali pindi wanapokuwa hawana
kazi.Hata hivyo, inaweza kuwa vigumu sana kutekeleza sheria hii katika nchi
ambazo wasimamiaji wa sheria za kazi hawana vitendea kazi au rasilimali za
kutosha za kufanyia kazi zao na mifumo ya
taarifa/habari ni
duni. Aidha, utafiti unaonesha wafanyakazi wengi wa hasa wanawake hawajui haki zao, hivyo hawawezi
kudai ulinzi au haki za kupatia huduma za uzazi kabla na baada ya kujifungua
kutoka katika mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii na hata baadhi ya haki zao
kutoka kwa waajiri wao.
Hivyo malengo ya
makusudi yanahitajika ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuja na mikakati ya kuandaa
elimu ya fao la uzazi kwa kutumia njia za mbalimbali za kufundishia au
kuelemisha jamii sehemu za kazi na kwa kutumia vipindi maalumu vya redio,
runinga, mabango, vipeperushi na kwa njia ya maigizo ili kuwaelemisha juu faida
zinazopatikana kwa kufungua fao la uzazi kwa mwanamke aliyejiari au
aliyeajiriwa na kuwa mwanachama wa mfuko hii ya hifadhi ya jamii. Lakini hata
kwa Yule ambaye ni mwanachama wa mfuko ambao huuna fao anaruhusiwa kujiunga na
mifuko inayotoa fao hili kwa njia ya hiyari. Kumekuwepo na dhana potofu kwa
wanawake wanachama wa mifuko hi ya hifadhi ya jamii inayotoa fao hili kuogopa
kufungua fao hili wakidai ya kuwa wakifungua na kupata mafao ya uzazi,
itakapofikia siku anataka kujitoa hataruhusiwa kufungua madai ili kupata
michango yake ya pensheni kabla ya muda wake wa kustaafu ambapo imewafanya
wengi wa wanachama wanawake wasiweza kunufaidika na fao hili na hii yote ni kwa
sababu ya ukosefu wa elimu ya hifadhi ya jamii miongoni mwa wanachama na kwa umma kwa ujumla.
Kulingana na mkataba wa shirika la kazi
duniani yaani ILO ibara ya 102 ya mwaka 1952 unaainisha mafao ambayo inatakiwa
kupewa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua kwa mwanachama mwanamke
anayetegemewa kujifungua au ameshajifungua tayari, ingawa baadhi ya nchi
ziliendelea kama vile Sweden na Canada fao hili hata wanaume nao hunufaika
nalo. Sifa au masharti yake ya kupata fao hili ni rahisi. Mkataba wa ILO
unasema wazi ya mafao ya uzazi hulipwa kwa mwanachama ambaye amechangia angalau
michango ya miezi 36 kati ya hiyo michango ya miezi 12 iwe imechangiwa karibu na wiki ya kujifungua.
Mwanachama awe anategemea kujifungua au
ameshajifungua mtoto. Na kwamba mafao
haya ya uzazi hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokuwa ikiwa mtoto
atafariki ndani ya miezi 12 baada ya kuzaliwa. Madai yanatakiwa yafanyike kabla
ya kujifungua au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua. Hii sheria inasaidia
kutekeleza malengo na mikakati ya taifa ya mpango wa uzazi wa kuzaa watoto
wanne wanatambuliwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaotoa mafao ya
uzazi kwa kujifungua mtoto kila baada ya miaka minne
Mwanachama mwanamke anayetegemewa kujifungua
au amejifungua anatakiwa kupewa kwanza mafao ya fedha taslimu ya asilimia 100
ya wastani wa mapato ya siku ya mwanachama kwa kipindi cha miezi sita kabla ya
wiki ya 20 ya ujauzito. Na mafao hayo yanatakiwa kulipwa kwa muda wa wiki 12
Kwa
upande malipo inatakiwa kufanyika kwa awamu mbili yaani wiki 4 kabla ya
kujifungua na wiki 8 baada ya kujifungua. Mwanachama anaweza kuamua kulipwa kwa
wiki zote 12 baada ya kujifungua.
Mkataba
wa shirika la kazi duniani yaani ILO ibara ya 102 ya mwaka 1952 unaendelea
kunaainisha ya kwamba mafao ya matibabu lazima yatolewe kwa magonjwa
yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama. Matibabu yanatakiwa kuanza kutolewa
baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku
7 ikiwa mama mwanachama amejifungua kwa upasuaji. Matibabu haya hufanywa na
hospitali ambazo zimeingia mkataba na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii ambazo
huwa zinatakiwa mwanachama mwenyewe achangua hospitali anayoitaka kulingana na
unafuu wa ukaribu na huduma bora inayotolewa. Mwanachama anaruhusiwa
kubadilisha hospitali ya kujifungulia kila baada ya mwaka mmoja kama ataona
kuna umuhimu wa kubadilisha. Na gharama zote hulipwa na mfuko wa pensheni wa
hifadhi ya jamii na hivyo mwanachama mwanamke anatarajia kujifungua au
aliyejifungua haruhusiwi kubughuziwa juu ya ulipwaji wa gharama za matibabu ya
magonjwa yatokanayo na ujauzito au kufanyiwa upasuaji kwa mama huyo mjamzito.
Nawezaje kujiunga na bima ya afya ya nssf
ReplyDeleteHI ZENA!
ReplyDeleteNDIYO UNAWEZA KAMA UPO DSM NENDA MAKAO MAKUU BENJAMINI MKAPA PENSION TOWERS POSTA MPYA AU OFISI ZA MKOA ILALA BOMANI KWA MAELEZO ZAID.
AHSANTE KAZI NJEMA
Nitawezaje pata stahiki zangu endapo mwajiri hakutuma michango yangu kwenye mfuko husika na Mimi nimejifungua?maana naona inatakiwa kufungua madai ya stahiki ndani ya siku 90.
ReplyDeleteNakuomba nipigie kwa simu namba 0655131341 ili nikujibu maswali yako kwa ufasaha zaidi. Samahani kwa usumbufu
DeleteHabari... Ninataka kujiunga na anachama was hiari yaani kuendeleza pale mwajiri wangu alipoishia baada ya mm kuacha kazi je.. nitapata fao la uzazi na bima? Na ni kwa muda gani?
ReplyDeleteNakuomba nipigie kwa simu namba 0655131341 ili nikujibu maswali yako kwa ufasaha. Samahani kwa usumbufu
DeleteMimi sijapata mafao yangu ya uzazi awamu ya pili kwasababu sikufanikiwa kupata kizazi hai kwa wakati na nilipeleka barua kutoka hospitali niliyojifungulia lakini walinirudisha sasa ni mwaka sijapata mafao yangu lakini juz wamenitumia meseji nipeleke kizazi hai cha mtoto ili nipate malipo yangu je nitapewa kwel ikiwa nilisikia mafao hayo ni ndani ya siku tisini tu au utaratibu umebadilika????
ReplyDeleteHivi kweli psspf mlianzisha fao la uzazi mkubwa hamjajipanga maana mpaka leo hamlipi
ReplyDeleteKwa kweli hawakujipanga ingekuwa vyema watoe tamko walifute.Maana usumbufu wansoupata wazazi sijawshi ona na majibu kamili hamna mpaka sasa wazazi wengi hawajalipwa fao linakuwa halina maana.
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletemtoto wangu wa kwanza nilijifungua 2017 mwezi wa 9 wapili natarajia kujifungua mwezi wa 7 mwakaa huu je nikifuatilia mafao ya uzazi na weza kupata
ReplyDeleteNdiyo unaweza kupata
ReplyDeletemimi ni mwanachama wa NSSF na ninatarajia kujifungua mwezi wa nane , je fao langu la uzazi nitalipataje awamu ya kwanza?
ReplyDeletepili njia ipi rahisi kuhudumiwa kulingana na hali ya ujauzito ukizingatia nakaribia kujifungua ?
ikiwa mimi ni mwanachama hai wa NSSF lakini bado sijatimiza miezi 36,je,naweza kupata FAO la uzazi?
ReplyDeleteHutaweza kupata fao la uzazi mpaka utakapotimiza miezi 36 kisheria
ReplyDeleteKwani psssf hulipa sh kiasi gani fao la uzazi mana mm nimejaza fomu mtoto anakaribia miaka2 hakuna kitu
ReplyDeleteKwa sasa PSSSF wamesha anza kulipa fao la uzazi Fao la uzazi ni mshahara mmoja wa mfanyakazi usiozidi milioni moja, na kama ni zaidi ya milioni moja basi atalipwa hiyo milioni moja tu.
ReplyDelete