Pages

Thursday, January 23, 2014

Mafao ya uzazi na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii



 

Baadhi ya akina mama wanachama wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii wakifurahia baada ya kujifungua salama watoto wao kutoka katika baadhi ya hospitali zilizoingia na mkataba na mfuko wa hifadhi ya jamii

Na christian Gaya majira  Januari 21 2014

Uzazi salama kwa akina mama wanapojifungua ni sehemu muhimu sana kwa taiffa letu na kwa maisha yao ya sasa na baadaye. Kwa nchi ya Tanzania kuwepo kwa kuborehesha kwa kinga maalum ya uzazi ni kitu ambacho inatakiwa kuwekewa kipaumbele kama taifa endelevu.



Hili ni jambo ambalo liko wazi kabisa ya kwamba kila binadamu ana uhusiano mkubwa na hifadhi ya jamii iwe kinadharia au kivitendo kutoka kuzaliwa kwake mpaka kufa, binadamu mwenyewe lazima ajishughulishe na kazi hatarishi na kuugua magojwa mbalimbali  na kwa hiyo binadamu lazima akumbane na majanga mbalimbali kama vile majanga ya kiuchumi na ya kijamii yanayosababishwa na kukoma au kupungua kipato kutokana na maradhi, kujifungua mtoto, ajari za kuumia kazini, ukosefu wa ajira, ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa gharama za matibabu haya majanga yote ni matukio ya kila siku kwa binadamu ambayo hayatabiriki na yote yanaaangukia kwenye mpango wa hifadhi ya jamii. Hivyo ni kitu cha asili ya kwamba kila mtu lazima ajue hifadhi ya jamii ni nini kwa sababu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu


Kutokana na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa shirika la kazi duniani (ILO) lengo la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni kuhakikisha kuwa kazi za wanamke hawaingiliwi na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za kuzaa hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama wa kazi zao iwe ya kujiajiri au kuajiriwa. 


Mpaka sasa hapa nchini kuna mifuko sita ya hifadhi ya jamii ambayo imeanzishwa kwa sheria za bunge mifuko ambayo ni: Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa pensheni wa wafanyakaziwa serikali za mitaa(LAPF), Mfuko wa akiba wa wafanyakazi wa serikali (GEPF), Mfuko wa pensheni wa watumishi wa serikali (PSPF), Mfuko wa pensheni  wa PPF, Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF).


Lakini kati ya mifuko hii ni mifuko miwili tu ambayo ni NSSF na LAPF ndiyo inayotoa fao hili la uzazi kwa wamama na hutolewa kwa wamama ambao ni wanachama tu na wala siyo hata kwa mke wa mwanaume ambaye ni mwanachama wa mchangiaji wa mifuko hii. Fao hili ni la muhimu sana kwa upande wamama kwani husaidia kupunguza vifo vya watoto na wamama wenyewe. Kwa sababu utafiti unaonesha ya kuwa idadi kubwa ya wamama wanaokufa kwa sababu ya kukosa huduma wakati wa kujifungua inaongezeka kila siku hasa kwa nchi zinazoendelea kama vile Tanzania. Na kwamba kati ya wajawazito kumi wanajifungua akina mama wanne hupoteza maisha pamoja na watoto wao. Na matukio haya yote hutokea nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania 


Na elementi kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao taslimu ya kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake wakati akiwa wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu, kuhakikisha ya kuwa mama mjamzito anapatiwa kinga ya afya ya ujauzito pamoja na mama anayeyonyesha bila kumsahau mtoto wake kupatiwa kinga kutokana na hali hatarishi zinazoweza kusababishwa na sehemu za kazi zenyewe. Mama mjamzito au anayeyonyesha ana haki kupewa kinga ya kutofukuzwa na kubaguliwa na kupewa kinga ya kwenda kunyonyesha mara tu baada ya kurudi kazini au mara tu baada ya kutoka rikizo ya uzazi.


Kwa hiyo kinga ya uzazi kwa akina mama lazima ichangie afya na ustawi wa wamama pamoja na watoto wao na hivyo kutimiza malengo ya namba 4 na 5 ya maendeleo ya millennia ya Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa, yanayotaka kupunguza vifo vya watoto na kuboresha afya za wamama. Na kwa kuhakikisha ya kuwa kazi zao wanawake za kuajiriwa pamoja na usalama wa mapato yao yanalindwa kama inavyotakiwa wakati na hata baada ya kutoka likizo ya uzazi. Kinga ya uzazi kwa  mwanamke ambaye ni mjamzito kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua  vile vile ni muhimu kuhakikisha ya kuwa mwanamke mzazi anapewa fursa sawa na matibabu katika sehemu za kazi ili kuhamasisha usawa wa jinsia na madaraka kwa wanawake. 


Lakini pamoja na haya yote ingawa kinga ya uzazi imewekwa kama sehemu ya mila na desturi zetu ndani ya familia zetu, lakini mpaka leo wanawake kwenye sekta iliyorasmi na ile isiyorasmi bado wanawake wanaishi kwenye mazingira yanahusiana na uzazi wa kutishiwa kwa ajili kupata afya na usalama wa kiuchumi na kijamii.


Wanawake wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi na hata kubaguliwa eti kwa sababu ni mjamzito au atakuja apate mimba. Lakini pamoja na hayo mazingira ya kazi, biolojia na kifizikia na kemia mbalimbali za madawa zinazosaidia kuzalishia kazi zinaweza kuleta hali hatarishi zaidi kwa upande wa uzazi na watoto wanaozaliwa hasa kwa kukosa mikakati ya uhamasishaji wa elimu ya umma, miongozo na thathimini.


Uwezo wa wanawake wanaoanza kunyonyesha watoto kulingana na utaratibu uliowekwa na shirika la afya la dunia unaingiliwa na kazi za uzalishaji hasa za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe kutokana na ukosefu wa kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha watoto. Kulea watoto bila ya kuwaharibia wanawake fursa zao za haki za kushirikishwa kwenye kazi za maendeleo ya kiuchumi inabaki kuwa ni changa moto kubwa wakati ubora na uwezo nafuu wa mipangilio ya uangalizi wa mtoto haupo kwa mpana mkubwa kabisa. 

 
Kwa hapa nchini wanawake wengi si wanachama wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii lakini kwa sababu ya kukosa elimu juu ya mafao yanayotolewa na mifuko hii hata wale wachache ambao ambao ni wanachama hai wa mifuko hii wanakosa huduma hizi za kinga ya uzazi. 


Na tunaona mara nyingi idadi kubwa ya mama kufa kabla au mara tu ya kujifungua. Hivyo hizi mimba nyingi zimekuwa zikitishia wamama na mara nyingi hufa mama au mtoto kama siyo wote. Na inasekama karibu asilimia 70 ya wamama duniani wanaopoteza maisha yao wakati wa kujifungua hutokea afrika na Tanzania ikiwa mojawapo. Na watoto wengi huzaliwa wakiwa wemekufa au mara tu mama kujifungua. 


Ni kweli ya kuwa idadi kubwa ya akina mama hawako katika mpango wa hifadhi ya jamii hivyo wengi wamejiajiri wenyewe. Lakini hata idadi ndogo ya wanawake  walioajiriwa na kuwa wanachama wa mifuko hii ya pensheni hawajaweza kutumia nafasi ya fao la uzazi kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua. 


Na kwa upande wa fao hili la uzazi mara nyingi wazazi wengi hawapata taarifa ya kuwa anastahili kupata kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua na kupita muda wa grace period ambao ni miezi mitabu (3) au ndani ya siku tisini (90). Tumeona mara kwa mara wamama waliojifungua wakifuatilia bila mafanikio kwa sababu wanachelewa kufungua madai kwa wakati muafaka. 


Ni kweli kwamba nchi kadhaa, zikiwemo Brazil na Tanzania, zimeanza kuwahusisha wafanyakazi wanawake katika sheria za kazi ili kuwapatia kinga au haki za msingi kama vile likizo ya uzazi, likizo ya ugonjwa na ruzuku ya serikali pindi wanapokuwa hawana kazi.Hata hivyo, inaweza kuwa vigumu sana kutekeleza sheria hii katika nchi ambazo wasimamiaji wa sheria za kazi hawana vitendea kazi au rasilimali za kutosha za kufanyia kazi zao na mifumo ya


taarifa/habari ni duni. Aidha, utafiti unaonesha wafanyakazi wengi wa hasa  wanawake hawajui haki zao, hivyo hawawezi kudai ulinzi au haki za kupatia huduma za uzazi kabla na baada ya kujifungua kutoka katika mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii na hata baadhi ya haki zao kutoka kwa waajiri wao.



Hivyo malengo ya makusudi yanahitajika ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuja na mikakati ya kuandaa elimu ya fao la uzazi kwa kutumia njia za mbalimbali za kufundishia au kuelemisha jamii sehemu za kazi na kwa kutumia vipindi maalumu vya redio, runinga, mabango, vipeperushi na kwa njia ya maigizo ili kuwaelemisha juu faida zinazopatikana kwa kufungua fao la uzazi kwa mwanamke aliyejiari au aliyeajiriwa na kuwa mwanachama wa mfuko hii ya hifadhi ya jamii. Lakini hata kwa Yule ambaye ni mwanachama wa mfuko ambao huuna fao anaruhusiwa kujiunga na mifuko inayotoa fao hili kwa njia ya hiyari. Kumekuwepo na dhana potofu kwa wanawake wanachama wa mifuko hi ya hifadhi ya jamii inayotoa fao hili kuogopa kufungua fao hili wakidai ya kuwa wakifungua na kupata mafao ya uzazi, itakapofikia siku anataka kujitoa hataruhusiwa kufungua madai ili kupata michango yake ya pensheni kabla ya muda wake wa kustaafu ambapo imewafanya wengi wa wanachama wanawake wasiweza kunufaidika na fao hili na hii yote ni kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya hifadhi ya jamii miongoni mwa wanachama  na kwa umma kwa ujumla.


Kulingana na mkataba wa shirika la kazi duniani yaani ILO ibara ya 102 ya mwaka 1952 unaainisha mafao ambayo inatakiwa kupewa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua kwa mwanachama mwanamke anayetegemewa kujifungua au ameshajifungua tayari, ingawa baadhi ya nchi ziliendelea kama vile Sweden na Canada fao hili hata wanaume nao hunufaika nalo. Sifa au masharti yake ya kupata fao hili ni rahisi. Mkataba wa ILO unasema wazi ya mafao ya uzazi hulipwa kwa mwanachama ambaye amechangia angalau michango ya miezi 36 kati ya hiyo michango ya miezi 12 iwe imechangiwa  karibu na wiki ya kujifungua.


Mwanachama awe anategemea kujifungua au ameshajifungua mtoto.  Na kwamba mafao haya ya uzazi hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokuwa ikiwa mtoto atafariki ndani ya miezi 12 baada ya kuzaliwa. Madai yanatakiwa yafanyike kabla ya kujifungua au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua. Hii sheria inasaidia kutekeleza malengo na mikakati ya taifa ya mpango wa uzazi wa kuzaa watoto wanne wanatambuliwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaotoa mafao ya uzazi kwa kujifungua mtoto kila baada ya miaka minne
Mwanachama mwanamke anayetegemewa kujifungua au amejifungua anatakiwa kupewa kwanza mafao ya fedha taslimu ya asilimia 100 ya wastani wa mapato ya siku ya mwanachama kwa kipindi cha miezi sita kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito. Na mafao hayo yanatakiwa  kulipwa kwa muda wa wiki 12


Kwa upande malipo inatakiwa kufanyika kwa awamu mbili yaani wiki 4 kabla ya kujifungua na wiki 8 baada ya kujifungua. Mwanachama anaweza kuamua kulipwa kwa wiki zote 12 baada ya kujifungua.


Mkataba wa shirika la kazi duniani yaani ILO ibara ya 102 ya mwaka 1952 unaendelea kunaainisha ya kwamba mafao ya matibabu lazima yatolewe kwa magonjwa yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama. Matibabu yanatakiwa kuanza kutolewa baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa mama mwanachama amejifungua kwa upasuaji. Matibabu haya hufanywa na hospitali ambazo zimeingia mkataba na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii ambazo huwa zinatakiwa mwanachama mwenyewe achangua hospitali anayoitaka kulingana na unafuu wa ukaribu na huduma bora inayotolewa. Mwanachama anaruhusiwa kubadilisha hospitali ya kujifungulia kila baada ya mwaka mmoja kama ataona kuna umuhimu wa kubadilisha. Na gharama zote hulipwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii na hivyo mwanachama mwanamke anatarajia kujifungua au aliyejifungua haruhusiwi kubughuziwa juu ya ulipwaji wa gharama za matibabu ya magonjwa yatokanayo na ujauzito au kufanyiwa upasuaji kwa mama huyo mjamzito.

17 comments:

  1. Nawezaje kujiunga na bima ya afya ya nssf

    ReplyDelete
  2. HI ZENA!
    NDIYO UNAWEZA KAMA UPO DSM NENDA MAKAO MAKUU BENJAMINI MKAPA PENSION TOWERS POSTA MPYA AU OFISI ZA MKOA ILALA BOMANI KWA MAELEZO ZAID.

    AHSANTE KAZI NJEMA

    ReplyDelete
  3. Nitawezaje pata stahiki zangu endapo mwajiri hakutuma michango yangu kwenye mfuko husika na Mimi nimejifungua?maana naona inatakiwa kufungua madai ya stahiki ndani ya siku 90.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuomba nipigie kwa simu namba 0655131341 ili nikujibu maswali yako kwa ufasaha zaidi. Samahani kwa usumbufu

      Delete
  4. Habari... Ninataka kujiunga na anachama was hiari yaani kuendeleza pale mwajiri wangu alipoishia baada ya mm kuacha kazi je.. nitapata fao la uzazi na bima? Na ni kwa muda gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuomba nipigie kwa simu namba 0655131341 ili nikujibu maswali yako kwa ufasaha. Samahani kwa usumbufu


      Delete
  5. Mimi sijapata mafao yangu ya uzazi awamu ya pili kwasababu sikufanikiwa kupata kizazi hai kwa wakati na nilipeleka barua kutoka hospitali niliyojifungulia lakini walinirudisha sasa ni mwaka sijapata mafao yangu lakini juz wamenitumia meseji nipeleke kizazi hai cha mtoto ili nipate malipo yangu je nitapewa kwel ikiwa nilisikia mafao hayo ni ndani ya siku tisini tu au utaratibu umebadilika????

    ReplyDelete
  6. Hivi kweli psspf mlianzisha fao la uzazi mkubwa hamjajipanga maana mpaka leo hamlipi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kweli hawakujipanga ingekuwa vyema watoe tamko walifute.Maana usumbufu wansoupata wazazi sijawshi ona na majibu kamili hamna mpaka sasa wazazi wengi hawajalipwa fao linakuwa halina maana.

      Delete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. mtoto wangu wa kwanza nilijifungua 2017 mwezi wa 9 wapili natarajia kujifungua mwezi wa 7 mwakaa huu je nikifuatilia mafao ya uzazi na weza kupata

    ReplyDelete
  9. mimi ni mwanachama wa NSSF na ninatarajia kujifungua mwezi wa nane , je fao langu la uzazi nitalipataje awamu ya kwanza?

    pili njia ipi rahisi kuhudumiwa kulingana na hali ya ujauzito ukizingatia nakaribia kujifungua ?

    ReplyDelete
  10. ikiwa mimi ni mwanachama hai wa NSSF lakini bado sijatimiza miezi 36,je,naweza kupata FAO la uzazi?

    ReplyDelete
  11. Hutaweza kupata fao la uzazi mpaka utakapotimiza miezi 36 kisheria

    ReplyDelete
  12. Kwani psssf hulipa sh kiasi gani fao la uzazi mana mm nimejaza fomu mtoto anakaribia miaka2 hakuna kitu

    ReplyDelete
  13. Kwa sasa PSSSF wamesha anza kulipa fao la uzazi Fao la uzazi ni mshahara mmoja wa mfanyakazi usiozidi milioni moja, na kama ni zaidi ya milioni moja basi atalipwa hiyo milioni moja tu.

    ReplyDelete