Kwa ufupi
“NSSF mmekuwa mkiendesha miradi mkubwa ambayo ni
mizuri, lakini mmeweka wazi kwa wanachama wenu jinsi wanavyonufaika na
miradi hii mnayoianzisha kupitia fedha zao?” alihoji Mbunge wa Ileje,
Aliko Kibona
Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wamechachamaa na kuhoji faida wanazozipata wanachama wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutokana na uwekezaji unaofanya kwenye miradi mikubwa.
Pia, wabunge hao wameichachamalia Serikali kwa kuendelea kuwalipa fidia kidogo kwa kutumia Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, wananchi wanaohamishwa kwenye makazi yao kupisha ujenzi.
Hayo yalijiri jana wakati kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miundombinu mbalimbali, likiwamo daraja kubwa la kisasa linalojengwa eneo la Kigamboni na Kurasini.
“NSSF mmekuwa mkiendesha miradi mkubwa ambayo ni mizuri, lakini mmeweka wazi kwa wanachama wenu jinsi wanavyonufaika na miradi hii mnayoianzisha kupitia fedha zao?” alihoji Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona na kuongeza:
“Daraja kubwa kama hili linalokatiza baharini, kuna miradi ya nyumba, je wananufaika vipi?”.
Mkurugenzi wa NSSF, Ramadhan Dau alisema wanachama wananufaika khasa kupitia mafao saba ambayo hulipwa, ikiwamo matibabu, pensheni kwa wastaafu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alisema kuna haja NSSF ikawaelimisha wanachama wake jinsi wanavyonufaika na miradi hiyo.
No comments :
Post a Comment