Kuna njia nyingi za kujifunza
kama vile kusoma vitabu, kujifunza kutoka kwa watu waliokutangulia, wenye
uzoefu, mahiri na wenye mafanikio katika katika mfuko unaotaka kujiunga nao.
Utahitaji kujifunza zaidi utendaji wa mifuko ya pensheni kutoka kwa wataalamu
na mamlaka inayohusika kama vile mdhibiti na msimamizi wa mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii (SSRA)
Sawa umepewa uhuru huo wa kuchagua
kujiunga na mifuko hii ya pensheni, hivyo ningependa kukuuliza wewe mfanyakazi
uliyeajiriwa leo je unajua mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaotoa mafao
bora zaidi ya kulingana na kiwango cha shirika la kazi duniani ILO? yaani kwa
idadi ya mafao, ubora wa mafao, na kulipwa pensheni kulingana na ukali wa
maisha ya kila siku.
Mfanyakazi unahitaji kujua
kiundani zaidi juu ya ubora wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii,
lazima ujue hata viwango vya ubora huduma zao, mazingira ya sehemu unapopatiwa
huduma kuanzia getini kwa askari mpaka
unapofungulia madai ambapo yanahitaji kuwa sehemu za kuvutia zaidi. Je huchukua
siku ngapi kupata hundi yako ya pensheni au ya mafao ya kujitoa, je ahadi zako
zinatekelezwa kama walivyokuahidi, na anayekuhudumia anakuchagamukia na
kukuhudumia kama ndiye mfalme wa mfuko huo wa pensheni. Je hao wafanyakazi wa
mifuko ya pensheni wanajua ya kuwa wewe ndiye mwajiri wao.
Wanaandaa pensheni yako ya
kustaafu baada ya mwezi mmoja kama walivyokuahidi. Kuna mambo mengi ya
kuchunguza kwanza kabla ya kujiunga hasa kama mwanachama mchangiaji utahitaji
kujua kwanza utaratibu wa kujisajiri kiwango cha kuchangia ni asilimia ngapi ya
kipato chako cha mwezi, mchango huo unakatwa kwenye mshahara kabla ya marupurupu
mengine au baada ya kuchanganya na marupurupu mengine yaani kwenye basic salary
au kwenye gross salary. Je mafao yako ya pensheni yanakatwa kodi au hayakatwi.
Na lazima ujue ni kwa sababu
gani ukate kwenye basic au gross salary.
Na ni nani anayetakiwa kukuandikisha wewe kwenye mfuko huo wa pensheni. Na
kiwango gani mwajiri naye inatakiwa akuchangie ili ichanganye pamoja na
kupelekwa kwenye mfuko wa pensheni. Na hiyo michango inatakiwa ipelekwa kwenye
huo mfuko kwa wakati gani wa muafaka. Je ni wajibu wa nani kuhakikisha kuwa
michango hiyo inapelekwa kwenye mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Na chama
cha wafanyakazi kina wajibu gani juu ya michango hii ya pensheni kazini.
Je mfumo gani wa hifadhi ya
jamii ni wa pensheni au wa akiba ya wafanyakazi. Ni aina gani ya mafao
yanayotolewa na mfuko huo wa hifadhi ya jamii. Je kuna mafao ambayo unaweza
kunufaika wakati unapoendelea kufanya kazi yaani ya muda mfupi na ya yale
ambayo utanufaika baada ya kustaafu yaani ya muda mrefu. Je familia yako
unawezaje naye kunufaika na mafao hayo ya muda mrefu na ya muda mfupi. Je
ukusanyaji wa michango ya pensheni una urasimu mwingi na usio na uwazi na
ukweli kwa mchangiaji.
Je mipango ya malipo ya mafao
kwa mwanachama inalipwa kwa wakati muafaka na kwa usahihi wa uhakika kabisa
bila ya mapunjo au kuzidishiwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Je wanachama
anaweza kutegemea kupata habari zote na ushauri na zilizokamilika karibu na
mahali karibu anapoishi. Mwanachama anaweza kupata habari na ushauri wowote
hata bila ya kuanza yeye kudai huduma hiyo. Je muda unaotumika kukokotoa mafao
yake ya pensheni ni mfupi au ni wa muda mrefu.
Je maamuzi yeyote juu ya huduma
za mwanachama zinahudumiwa kirafiki. Ni muhimu vile vile kama mwanachama kujua
wewe kama mchangiaji pamoja na mwajiri wako kila mmoja ana wajibu gani kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii. Mfuko
wa pensheni wa hifadhi ya jamii lazima uweke wazi juu ya haki za wanachama hasa
zile za kumruhusu mwanachama kukata rufaa kwenye bodi ya sheria au mahakamani
atakapoona kwamba pale hajatendelewa haki inavyotakiwa na mfuko wa pensheni wa
hifadhi ya jamii. Kama wanachama mchangiaji wa mfuko wa pensheni je
utashirikishwaje kwenye maamuzi na uendeshaji wa mfuko huo na kwa faida ya
nani. Sasa ni juu ya mfanyakazi mwenyewe kuchagua kwa kutumia vigezo vya
kitaalamu
No comments :
Post a Comment