By NATION TEAM newsdesk@ke.nationmedia.com
na Christian Gaya majira Machi 05,2013
Zaidi ya asilimia hamsini ya milioni mbili
ya watoto yatima na watoto wanaishi kwenye mazingira hatarishi wanategemea
wazee kupata mahitaji muhimu kama vile
chakula, tiba na mahitaji muhimu ya elimu. Kwa maana hiyo wazee ni msingi wa
muhimu sana kwa
makuzi ya mamilioni ya watoto kwa sasa na siku zijazo. Pamoja na hayo ingawa
mtandao usio rasmi wa hifadhi ya jamii unaendelea kubadilika lakini unazidi
kumwachia akina bibi wazee kuwa ndiyo wanatunza watoto ambao hata shule
hawajaanza hata madarasa ya awali au darasa la kwanza.
Uchumi wa kizazi cha vijana wa sasa
unawafanya vigumu kufanya maamuzi ya
kujikimu wenyewe na familia zao kwa vile kwa sababu kila siku jamii ya
kitanzania inazidi kuongezeka kumomonyoka na kutawanyika, mwongezeko wa idadi
ya wazee inafanya kuwa ni msingi imara wa familia pana.
Wazee wanaume kwa wanawake wametoa mchango
mkubwa kwa jamii ya kitanzania kwenye mabadiliko mbalimbali katika ngazi ya
kanya, jumuia na kitaifa. Wazee wameweza kuchangia katika uchumi wa taifa moja
kwa moja au kupitia katika maisha yao yote waliyokuwa wakifanyia kazi
serikalini, kwenye makampuni ya watu binafsi, kazi za kilimo na ufugaji na
madini lakini pamoja na hayo karibu asilimia sabini na tano ya wazee
wanaendelea kuchapa kazi vizuri kabisa pamoja na umri w a uzee waliokuwa
nao.
Kipato cha wazee mara nyingi imekuwa ikiwekezwa kwa ajili ya maendeleo ya vizazi vya vijana. Ingawa wazee wengi wanaishi maeneo ya vijijini na kufanya kazi sehemu za sekta zisizo rasmi ni muhimu kutambuliwa kuwa wengi wao bado wanaendelea kuchangia kwenye pato la taifa kwa njia ya kutoa kodi za aina mbalimbali kama vile kwa njia ya bidhaa zenye kodi ambazo wazee wanazinunuliwa sokoni kila siku.
Katika ngazi ya kaya wazee wanaume kwa
wanawake wanatoa mchango mkubwa kwa ajili ya mtaji na rasilimali ya maendeleo
watu katika nchi. Mara nyingi wazee wamejishughulisha katika kazi zisizo na
malipo yeyote hasa zile za kuangalia watoto kwa ajili ya familia zao, kwa
kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia kaya nyingi kuongeza uzalishaji na ufanisi wa
kazi pamoja na kuongeza maendeleo ya rasilimali mtu. Ingawa hivi karibuni wazee
wameonekana kwa muda wote wamekuwa wakiongezeka wakishushughulika na uangalizi
wa kulea watoto.
Watoto na wajukuu wanaweza kwenda mijini
kutafuta kazi za kujiajiri au kuajiriwa, lakini mara nyingi wanarudi tena kwa
wazee. Na mchango mkubwa wa wazee umekuwa ukionekana kwenye ngazi ya jumuia.
Hesabu nyingi zinaonekana kutoka kwa madiwani na wajumbe wa jumuiya zinaeleza
ni jinsi gani wazee wanavyochangia kutoa elimu muhimu ya malezi inayojenga misingi
imara ya kukuza vijana kwa njia iliyokuwa rasmi na ile isiyokuwa rasmi.
Vilevile wanasifiwa kwa kutunza mila na
desturi za urithi kutoka kwa mababu na bibi zetu na kwa mchango mkubwa kwa
kuhamasisha mshikamano ndani ya jamii katika kutatua migongana. Wazee hasa
wanaume wana uzoefu mkubwa wa kutoa upatanisho kati ya mivutano au mgogoro ya
kaya na kaya. Kumbukumbu zao za madeni na malipo na ugumu
wa uhusiano wa kiuukoo ni mambo muhimu sana
kwa jumuia na ambayo inategemea zaidi makubaliano yaliyokuwa sawa sawa kijamii
Akina bibi wazee wanasaidia kaya
mabalimbali zisizo kuwa rasmi na zingine zilizoko kwenye jumuia mbalimbali kwa
kuwajali na kuwatunza vitoto vichanga na watoto kuwawezesha wanawake wengine
wenye nguvu kufanya kazi za uzalishaji mali. Kwa kufanya hivyo rasilimali
za kaya zinaweza kuelekezwa kwenye huduma ya matibabu au kulipa gharama za
matibabu kuliko kuwekeza kwa watoto.
Utafiti
uliofanywa huko vijijini nchini Tanzania
inaeleza kuwa watoto wenye wazazi ambao ni dhaifu kiakiri, na kimawazo ni
rahisi sana kusababisha hao watoto kuacha shule
na kutumia masaa machache sana
kwa ajili ya shule. Lakini ni vizuri kutambua ya kuwa ni mara nyingi hawa wazee
ya kwamba wanatunzwa na watoto
No comments :
Post a Comment