Nyumba ina
mchango mkubwa kwa upande wa uchumi, kijamii na kisiasa, na alama au muonyesho
wa maendeleo na ustawi wa jamii katika nchi yeyote ile. Hivyo basi ni kitega
uchumi ambacho kinachangia katika kupunguza kama siyo kuondoa umaskini kabisa, nyumba ni kitega uchumi ambacho kinachangia kuongezea
ajira, kinaongezea mapato, kinaboresha afya na kuongeza ufanisi kwa nguvu kazi
Nyumba kwa
mwenye nayo au anaye miliki ni rasilimali ambayo inawezekana kubadilishana na
kitu chochote kwa vile kina thamani yake na ikatumika kwa vile ina thamani yake
inayotambulika. Kijamii nyumba inachangia kuhamasisha na kuboresha nafsi ya
mtu, utu, usalama na kutambuliwa mbele za watu. Kisiasa, nyumba bora inapunguza
vitishia vya kisiasa vinavyotokana na kugandamizwa na kuchanganyikiwa hasa kwa
watu wanaoishi kwa mazingira hatarishi na makazi yasiyokuwa rasmi
Kutokana na upeo
wa michango au mafao ya pensheni, umilikaji wa nyumba ni sehemu ya upangaji mzuri
wa jinsi ya kustaafu. Kumiliki nyumba wakati wa kustaafu inawalinda wastaafu
kutokana na mahitaji ya mtiririko wa fedha mkononi-mahitaji ya mapato au fedha
mkononi kwa ajili ya kuitumia kwa kulipia kodi ya nyumba inakuwa tayari
imeshapungua.
Pamoja na hayo
tena inawalinda wastaafu kutokana na maamuzi mabaya ya uwekezaji, na faida
mbaya inayotokana na uwekezaji ikiwemo na mfumuko wa bei ambao hauendi na ukali
wa maisha wa wakati huo. Vile vile inamwandaa mstaafu na maisha yenye heshima
usoni mwa jamii na yenye utu mzuri wa hali ya maisha. Umilikaji wa nyumbani kwa
kweli huchangia kiasi kikubwa kwa wastaafu kwa ajili ya kuwaandaa maisha ya
ulimwengu wa kustaafu na katika kuwatengenezea staili ya miaka yao ya mwanzoni
kabla hawajastaafu.
Kuna haja kubwa kabisa msimamizi
na mdhibiti wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii yaani (SSRA) kubuni
mikakati ya kuhamasisha uhitaji wa nyumba ili kuwezesha wanachama wa mifuko hii
ya hifadhi ya jamii kununua nyumba za gharama nafuu. Kwa mfano Singapore
wanachama wa hifadhi ya jamii wanaruhusiwa kutumia asilimia 75 ya akiba yao ya
michango ya pensheni kwa ajili kukopeshewa nyumba au kwa ajili ya kununulia
nyumba maalumu anayohitaji.
Wakati Mauritius na Africa kusini mifuko ya
pensheni ya hifadhi za jamii kama vile Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Pensheni kwa ajili ya Mashirika ya
Umma (PPF), Mfuko wa Pensheni wa Hifadhi ya jamii kwa ajili ya Watumishi wa
Umma (PSPF) na Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi wa Serikali (GEPF), Mfuko
wa Bima wa Taifa yaani (NHIF), mfuko wa pensheni ya Hifadhi ya jamii kwa ajili
ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa yaani (LAPF). Pamoja na Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF) yanaruhusu kutoa mikopo moja kwa moja kwa
wanachama na hata vilevile wanachama wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii
kutumia sehemu ya theruthi mbili (2/3) ya mafao yao ya baadaye kama amana ya kumpatia
mikopo benki na kupata mkopo wa nyumba kutoka taasisi za nyumba au mashirika ya
nyumba ya nchi hizo kama vile Shirika la Nyumba la Taifa (THC) la Tanzania.
Na mafao yaliyosalia yanaachwa
kama yalivyo bila kuguswa mpaka wanachama atakapofikia wakati wa kustaafu kwa
hiyari au kwa lazima. Wanachama waliokopa wanalipa riba kwa muda wote na
kuhurusiwa kuingilia mafao kulipa deni halisi alilokopa wakati utakapofika muda
wake wa kawaida wa kustaafu. Kwa Afrika kusini viongozi wa hifadhi ya jamii
wanapandisha mkopo wa nyumba kwa kutumia soko la mtaji kwa kutoa amana ya
pensheni ili kumwezesha mwanachama wa hifadhi ya jamii kumiliki nyumba
Tanzania hairuhusu wanachama wa
mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii kuingilia michango yao ya akiba ya
pensheni kwa ajili amana ya kujipatia nyumba ya mkopo. Kwa maana hiyo kuna
baadhi ya taasisi au mashirika ambayo yafanya kuwa siyo ya ushindani hasa pale
yanapokuja na masharti magumu yanayofanya kwa mtu asisitahili kabisa kupata
nyumba ya mkopo. Pamoja na hayo idadi kubwa ya wanachama wa mifuko hii ya
hifadhi ya jamii wanakopo kutoka katika taasisi hizo bado idadi kubwa ya
wanachama mpaka sasa hawafikiwi. Wakati njia ya kutumia akiba ya michango ya
pensheni ambayo huchangiwa na mwanachama na mwajiri wake ilikuwa ndiyo njia
pekee ya mbadala ya kumwezesha mwanachama kupata mkopo wa nyumba.
Katika kutambua
umuhimu wa ungezeko wa uzalishaji nyumba kwa ajili ya kuhudumia watu
wanaongezeka kila siku, serikali mara kwa mara
imekuwa ikiaangalia uwezekano wa kuwa na ufumbuzi wa aina mbalimbali na hata vilevile
kushawishi ushiriki wa sekta za watu binafsi ili kufikia lengo hili la nyumba.
Uwezekano wa kupata mikopo ya fedha kwa waendelezaji na wanunuzi kumekuwa ni
mojawapo ya sababu zilizochangia kuwa na uhaba wa nyumba.
Baada ya
kutambua kwa thamani ya uchumi ya sekta hii muhimu ya pensheni ya hifadhi ya
jamii iliyokuwa nayo mpaka sasa, mwaka 2008 serikali iliunda chombo cha
kusimamia na kuthibiti mifumo hii ya hifadhi ya jamii. Muda umefika sasa kwa
serikali kuchukua maamuzi ya makusudi ya kuchukulia sekta hii ya hifadhi ya
jamii kama chombo ambacho kinachoweza
kuwa na mchango mkubwa wa kutoa mikopo kwa ajili sekta
ya nyumba
Chombo cha
kusimamia na kuthibiti sekta ya pensheni ya hifadhi ya jamii yaani SSRA kimetoa
miongozo ya uwekezaji pamoja na kuruhusiwa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya
jamii kujihusisha na uwekezaji wa rasilimali pamoja na nyumba/makazi mpaka kikomo
cha asilimia 30% ya jumla ya fedha zote za mfuko. Na mifuko inaweza kujenga au
kununua rasilimali isiyohamishika. Isipokuwa
michango au mafao ya pensheni haiwezi kutolewa kwa ajili ya kumwezesha
mwanachama kupat mikopo ya nyumba au haiwezi kutumika kama amana ya kupata
nyumba ya mkopo au dhamana ya kupata mkopo wa nyumba kwa ajili ya faida au
manufaa ya mwanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii
No comments :
Post a Comment