NHC ina mpango wa kujenga nyumba zipatazo 200 na NSSF ina mpango wa
kujenga nyumba 300 katika awamu kwa kwanza. Nyumba hizi ni za aina
tofauti na zina vyumba kati ya 2-4.
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko toka kwa wananchi kuwa nyumba za
bei nafuu (affordable houses) bado si rahisi kwa mwananchi wa kipato
cha kati na chini. Bei ya nyumba mpya za NHC hivi karibuni zimekuwa ni
zaidi ya TSh 100 millioni kila moja. Bei hii inalalamikiwa kuwa ni kubwa
sana kwa mlalahoi.
Katika mradi huu wa Kigamboni, NHC ina mpango wa kuuza nyumba zake
kati ya TSh 30-40 millioni kutegemea na ukubwa. Sikuweza kupata bei za
nyumba za NSSF.
Pamoja na miradi hii mizuri itakayopendezesha Jimbo la Kigamboni,
nyumba hizi zinaweza kununuliwa kwa matajiri wachache kutokana na bei
kuwa kubwa. Kuna umuhimu wa kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini
na kati kupata mikopo ya muda mrefu itakayowawezesha kununua nyumba
hizi.
Kwa watanzania walio nje ya nchi, hii ni fursa nzuri ya kununua nyumba, itumieni.
No comments :
Post a Comment