Na Christian Gaya: Majira 29 Januari 2013
Changamoto kubwa ya nchi
yetu ya Tanzania ni kudidimia kwa mfumo wetu wa hifadhi ya jamii usio kuwa
rasmi hasa kwa njia ya kutoa fedha taslimu na kujikimu au kusaidia kwa pande
zote za familia zaidi ya moja na kama chanzo cha jumuiya. Na mwongezeko zaidi
wa changamoto ni kutokana na mabadiliko ya muundo wa familia na kudidimia kwa
mitandao ya kusaidiana kijamii.
Tangia enzi za zamani hifadhi
ya jamii isiyo rasmi ilinajulikana kuwa ndiyo inayofaa kutoka vizazi kimoja
hadi kingine kuwa ndiyo chombo au mtandao maalum kwa kutoa michango mikubwa wa
kusaidia wazee na kwa wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi. Na kutokana kwa
kuongezeka kwa miji na madhara ya mlipuko wa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS)
mtandao huu muhimu wa kusaidiana umekuwa unaendelea kubomoka na kuporomoka
zaidi hasa kwa upande wa baadhi ya makundi ya kijamii hasa yale yaliyoguswa na
madhara ya mlipuko wa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS). Dhima na wajibu wa jamii
umekuwa kinyume kabisa na inavyotakiwa iwajibike kwa wazee, watoto, wamama,
vilema na wale ambao wanaishi kwenye mazingira hatarishi.
Kwa upande mwingine utafiti
unaonyesha ya kuwa wazee yaani akina babu na bibi ndio wanatunza watoto yatima
na kutoa hata faraja kwa wajane, ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila siku.
Na takwimu vil;e vile zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 (hamsini) ya watoto
yatima hapa Tanzania wanaishi na babu au bibi zao. Kwa upande mwingine ni
kwamba kutokea na kuongezeka zaidi kwa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS)
kumesababisha kutokea haraka kwa kundi la hili la wazee wanaoishi peke yao ambalo
hawatambuliwi na jamii wala jumuiya na hata na serikali yao, na bila kunufaika
na mwangalizi yeyote. Utafiti uliofanywa kutoka katika nchi sita za Kiafrika
unaonyesha kuwa idadi ya asilimia zaidi ya 4 (nne) ya wazee wanasumbuliwa na
magonjwa sugu ya moyo na kisukari hasa pale wanapofikisha umri wa miaka zaidi
ya sitini ukilinganisha na wale ambao wako chini ya umri wa miaka sitini.
Utawala na menejimenti wa
magonjwa ya sugu na ya muda mrefu na yale mengine ya ulemavu yanatakiwa kuwa na
idadi kubwa ya rasilimali watu yaani wataalam na fedha kutoka serikalini,
jumuia mbalimbali, na hata kwenye familia. Pamoja na hayo bado serikali kama ya
Tanzania, inatumia kiwango kidogo sana cha kipato kwa kichwa cha mtu kwa
matumizi ya afya ukiachilia mbali mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hayagusi
kabisa makundi haya yanayoishi kwenye mazingira hatarishi ukilinganisha na nchi
zilizoendelea.
Kwa mfano halisi ni kwamba Tanzania
haina mpango wa kutoa huduma ya jamii kwa wote au mpango rasmi wa kuwatunza na kuwajali
wazee, kwa kweli bado hawa wazee wanategemea mfumo usio rasmi wa hifadhi ya
jamii unaotegemea zaidi muundo wa familia na wala siyo serikali. Kwa hiyo
gharama hasa ya matibabu mara nyingi anaachiwa mwananchi ambaye hana uwezo wa
kubeba mzigo bila msaada wowote kutoka serikalini au jumuia yeyote au asasi.
Utafiti kutoka nchi kumi na
tano za Kiafrika ikiwemo Tanzania unaonyesha idadi kubwa ya watu wa kipato cha
chini wanakimbilia au wanaishia kukopa au kuuza rasilimali zao ili kuweza
kwenda pamoja na gharama za matibabu. Hali hii imepelekea familia nyingi
kuingia kwenye janga la umasikini zaidi na afya zao kuwa mbaya zaidi na
zaidi
Licha ya mapadiliko haya ya
demografia muhimu ya takwimu ya kima cha uzazi, uzee, vifo, maradhi yanaonyesha
hali halisi ya jamii yetu, demografia ya uzee haionekani hata kidogo
kuzungumziwa kwenye midaharo na mihadhara ya sera mbalimbali. Kutoonekana kwa
mazingira hatarisha ya wazee kwenye makaratasi ya sera muhimu za nchi inaletwa
na msukumu wa kutoonekano kwao hata kwenye mipango ya maendeleo ya taifa.
Wakati malengo ya maendeleo ya milinea yaani millinium development goals (MDGs)
inatoa malengo maalumu ya watoto, vijana na akina mama, hawakumbushii wala kuzungumzia
ya kwamba nao wazee ni kundi muhimu.
Matokeo yake hili kundi la
wazee halinufaiki na mipango hii maalum ya misaada ya maendeleo. Kukosekana kwa
kutotambuliwa hili kundi la wazee hata kwenye ajenda za MDGs ajenda ambayo ni
mipango iliyopewa kipa umbele na mipango ya maendeleo ya kimataifa umechangia
kwa kudidimiza zaidi hali ya kundi muhimu la wazee ambao ndio wachangiaji
wakubwa wa uchumi wa taifa hili la Tanzania.
No comments :
Post a Comment