Mkurugenzi
Mkuu wa VISA Tanzania, Bi. Olive Njoroge (kushoto), akipeana mikono na
Mkurugenzi Mkuu wa Engen Tanzania, Bw. Paul Muhato wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya miezi miwili ya kuhamasisha watumiaji wa mfumo wa kufanya
malipo kupitia simu ya mkononi (Visa-on-mobile) na malipo mengine ya
kidijitali ambapo kampuni hizo mbili zimeanzisha ushirikiano ili
kuendeleza matumizi ya malipo kwa njia hiyo. Kampeni hiyo ilizinduliwa
kwenye kituo chga mafuta Engen kilichoko eneo la Msasani jijini Dar es
Salaam Julai 26, 2019.
Bi.
Olive Njoroge (kushoto) na Bw. Paul Muhato, wakiwa katika mkutano na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Julai 26, 2019.
Bw. Paul Muhato(kulia) na Bi. Olive Njoroge, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Julai 26, 2019.
Kampeni
hiyo imeanza leo Ijumaa Julai 26, 2019 na wateja ambao watanunua mafuta
yenye thamani ya shilingi elfu 50,000/= siku za Ijumaa na Jumapili
wakitumia Visa on mobile au kutumia kadi za benki yenye nembo ya VISA
wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ushirikiano huu baina ya VISA
na Engen Petrol Stations.
Bi.
Olive Njoroge (wapili kushoto) na Bw. Paul Muhato, wakimzawadia mteja
vocha ya manunuzi kwenye kituo cha Engen Msasani Julai 26, 2019.
KAMPUNI
ya malipo ya kidigitali VISA na ile ya kuuza mafuta, Engen Tanzania wamezindua kampeni ya miezi
miwili kuanzia leo Ijumaa Julai 26, 2019 yenye lengo la kuhamasisha utumiaji wa... mfumo wa kufanya malipo kupitia
simu ya mkononi (Visa-on-mobile), na malipo mengine ya kidijitali wakati wa
malipo wakiwa kwenye vituo vya Engine
nchi nzima.
Wateja
ambao watanunua mafuta yenye thamani ya shilingi elfu 50,000/= siku za Ijumaa
na Jumapili wakitumia Visa on mobile au kutumia kadi za benki yenye nembo ya
VISA wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ushirikiano huu baina ya VISA na
Engen Petrol Stations.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi humo Mkurugenzi Mkuu wa VISA nchini Tanzania, Bi. Olive
Njoroge amesema “Promosheni hii ni nzuri kwa wateja ambao wataweza kufurahia
usalama na uzuri wakitumia mfumo wa Visa on mobile na pia wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ubia wetu na Engen
Tanzania.” Alisema Bi. Njoroge wakati w amkutano w apamoja na waandishi wa
habari akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Engen Tanzania Bw. Paul Muhato.
Kwa
upande wake Mkuurgenzi Mkuu wa Engen Tanzania, Bw. Paul Muhato alisema mara
nyngi madereva wa vyombo vya moto hufanya malipo kwa pesa taslimu (cash),
wakinunua mafuta ya petrol na dizeli na wakati mwingine mteja anahitaji kwenda
kwenye ATM, mchakato ambao huchukua muda mrefu, lakini ukitumia mfumo huu wa
Visa on mobile (kufanya malipo kupitia simu ya mkononi (Visa on mobile) ni salama zaidi na huokoa
muda, tumefurahi kushirikiana na Visa tukiwahamasisha wateja wetu kutumia mfumo
wa malipo kwa njia ya kidijitali na pia kuwapatia zawadi.” Alifafanua Bw. Muhato.

Excellent article. Very interesting to read. I really love to read such a nice article. Thanks! keep rocking. visto per il canada
ReplyDelete