Pages

Wednesday, June 22, 2016

SAGCOT WASAINI MKATABA NA MAKAMPUNI YALIYOOMBA UFADHILI KWA AJILI YA UKUZAJI KILIMO NA VIWANDA

01 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
1 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akishuhudia  wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo. wanaosaini hati hizo kutoka kulia ni Mkulima wa miwa Dk George Mlingwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Germao Cane Estate, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe, Roy Omulo kutoka kiwanda cha Maziwa cha Asas Dairies Iringa  na Lutengano Peter Mwenyekiti wa MUWAMARU Tukuyu mkoani Mbeya.
02Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa  kwa miradi kupitia madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto za wakulima na masoko yao.
2
Baadhi ya viongozi hao wakiwa katika mkutano huo leo
3
Baadhi ya wafadhili wakiwa katika mkutano huo
4
Washiriki wa mkutano huo kutoka makampuni mbalimbali na serikali
5 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe wakati wa mkutano huo.

Waziri mwijage azindua siku ya viwango barani Afrika

index 
Arusha
Waziri wa Viwanda  Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja  wanamaliza bidhaa zote bandia na  zilizo chini ya  viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo kuteketezwa.
Tamko hilo amelitoa waziri Charles Mwijage leo hii wakati alipokuwa anatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya Dangote afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wakati huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao akiwemo Maofisa masoko  afisa mkuu wa masoko wa AZANIA  Naifa Abubakari pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM  wamemuhakikishia waziri wa viwanda biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa bidhaa zinazokidhi viwango  bora na zenye ushindani na masoko kote duniani
Aidha kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL  wataakikisha wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.

Pombe za asili zatamba soko la vinywaji nchini

CHIB1
Wafanyakazi wa DarBrew wakionyesha kinywaji cha Chibuku kwenye chupa ndogo wakati wa kuizindua hivi karibuni CHIB2 
Kikosi kazi cha menejimenti  na wafanyakazi wa DarBrew wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kusherehekea kupata tuzo ya SABMiller ya kuendeleza vinywaji vya asili nchini hivi karibuni.
…………………………………………………………………………………………………………..
-TBL Group yajipanga kuziboresha kulinda afya za watumiaji na kuchangia pato la Taifa
 
Licha ya kuwepo na viwanda mbalimbali vya kutengeneza bia na vinywaji vingine vya kisasa ikiwemo uingizwaji wa vinywaji  hivyo kutoka nje ya nchi bado idadi kubwa ya watanzania wanatumia pombe za asili na sababu kubwa inabainishwa kuwa hali hiyo inatokana na vinywaji vya kisasa kuuzwa kwa bei ya juu.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya  pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni asilimia 50% ambapo kati ya asilimia  hizo vinywaji vya asili vinavyototengenezwa kisasa viwandani vinatawala kwa asilimia  8% .
Sababu kubwa ya watumiaji wa vinywaji vya asili ambavyo vingi vinatengenezwa kwenye mazingira yasiyo salama na vinaendelea kuleta athari kwenye jamii ni kutokana  na bei kubwa ya  bia ,wine na vinywaji vinginevyo vya kisasa ambapo idadi kubwa ya wananchi hawana uwezo wa kumudu kuvinunua na kuvitumia.
Akitoa  ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari hivi karibuni,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin alisema kuwa kampuni  yake tayari imeanza kutekeleza mkakati wa kuboresha vinywaji vya asili na kuhakikisha vinaingia katika mfumo rasmi unaotambulika kwa kuviwezesha kuchangia pato la taifa kwa njia ya kodi ikiwemo kulinda afya za wananchi.
Jarrin  alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na  katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.
Alisema kuwa akina mama wakiendelea kujiunga na mpango huu wataweza kujikwamua kimapato na  kulinda afya zao na wanywaji pia kupunguza uharibifu wa  mazingira kwa  kutumia kuni kwa ajili ya kupikia pombe za asili ambazo zimekuwa zikiuzwa katika vilabu mbalimbali.”Tunawasihi watumiaji wa vinywaji vya asili kujenga mazoea ya kutumia vinywaji vyenye ubora na vilivyotengenezwa kwenye mazingira mazuri kwa ajili ya kulinda afya zao”.Alisema
Katika kuhakikisha  watumiaji wanamudu vinywaji vya asili vya Chibuku na Nzagamba  alisema kampuni imeanza kusambaza vinywaji hivi vikiwa kwenye ujazo wa chupa za ukubwa wa aina mbalimbali ili wanywaji wote waweze kuvipata kulingana na vipato vyao.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza  kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili  ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha  vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin

Wakala ya serikali mtandao kufanya ziara ya kutembelea taasisi za serikali.

EG1 
Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Wakala wa Serikali Mtandao Bi Suzan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa taasisi yake kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
……………………………………………………………………………………
Na Eliphace Marwa – Maelezo            
Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) imeandaa utaratibu wa kutembelea wateja wake ambao  ni taasisi za umma ili kusikiliza na kutatua   changamoto  zinazo tokana na huduma wanazotoa,huduma hizo ni pamoja na mfumo wa barua pepe unaorahisisha mawasiliano  serikalini.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wataasisi hiyo Bi Suzan Mshakangoto, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salam na kutaja baadhi ya taasisi 34 zitakazoanza kutembelewa kuanzia tarehe 22 Juni hadi Juni 23.
Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari,utamaduni Sanaa na  Michezo, Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika  Mashariki Kikanda na Kimataifa.       
Aidha aliongeza kuwa huduma nyingine zinazotolewa  na wakala wa serikali ni pamoja na uhifadhi wa mifumo ya tovuti  za serikalini, utoaji huduma za simu za mikononi, Uratibu wa  mitandao serikalini, Ugawaji wa masafa ya internet, huduma za ujumbe mfupi wa maandishi (sms) pamoja na utengenezaji wa mifumo ya tovuti na usajili anuani  za tovuti.  
Hiyo ni kutimiza Agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Angela Kairuki la kutaka kila Wizara, wakala na Taasisi za Serikali katika kipindi cha Wiki ya Utumishi wa Umma kukutana na wateja wao na kusikiliza kero walizonazo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi, aidha kauli mbiu ya mwaka huu ni, “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.
Kila taasisi itatembelewa na wataalam  wawili wa wakala wa serikali watakao sikiliza maoni na kutoa  msaada wa kiufundi na ushauri wa kitaalamu katika kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeza juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na wakala.    

Mkurugenzi Muhimbili Akutana na Madaktari, Aongeza Posho

MSE1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru LEO amekutana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwasikiliza na kujibu kero mbalimbali. MSE2 
Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru baada ya kukutana nao LEO kwenye ukumbi wa CPL katika hospitali hiyo. MSE3 
Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo. MSE4Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo LEO.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Neema Mwangomo, Dar es salaam          
                                                                                                                                                                             
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na Madaktari  wa MNH  ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza  madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali  na kufikia Shingili Bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
Amesema kutokana na mafanikio hayo,  MNH imewaongezea madaktari  wake posho mbalimbali  ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali  imeamua  kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake  jambo ambalo awali halikuwapo.
Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia  MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki  za wafanyakazi wake ikiwamo  pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.
“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
Akielezea mipango ya MNH  Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH kesho Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.

PROF. MAKAME MBARAWA AZINDUA BODI YA TPA

TPA1Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
TPA2 
Wajumbe wa Bodi mpya ya Bandari Nchini (TPA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
TPA3Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo.
TPA4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alipokagua eneo la kupakulia makontena bandarini hapo.
TPA5 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Aloyce Matei (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), alipokagua miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.
TPA6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia  magari katika bandari ya Dar es Salaam.
Habari Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

Messi aitanguliza Argentina fainali za Copa America na rekodi juu!

index 
Alfajiri ya kuamkia Jumatano hii kupitia king’amuzi cha StarTimes watanzania wapenda soka walishuhudia muendelezo wa burudani ya soka kupitia kwa nyota wa dunia Lionel Messi akiiongoza Argentina kutinga fainali ya Copa America kwa kipigo cha magoli 4 – 0 dhidi ya Marekani ambapo alifunga goli safi kwa mkwaju wa mpira wa adhabu na kutoa pasi za magoli yaliyosalia kwa Ezequiel Lavezzi (1) na Gonzalo Higuan (2).
Katika mechi hiyo ambayo Messi ameisaidia kuingia fainali za kombe hilo pia ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kuifungia timu ya taifa ya Argentina kwa kufikisha magoli 55 moja zaidi ya Gabriel Batistuta aliyekuwa akiishikilia kwa muda wa miaka 14.
Kwa ushindi huo timu ya taifa ya Argentina ambayo ina kiu kali ya muda wa miaka 23 tangu iuchukue ubingwa huo sasa inasubiria mshindi wa nusu fainali ya mechi ya pili kati ya Chile na Colombia itakayochezwa saa 9 alfajiri ya tarehe 23 katika uwanja wa Soldier Field, Chicago – Illinois nchini Marekani.
Chile ambao ndio mabingwa watetezi wanatarajia kutetea vema nafasi ya kwenda hatua ya fainali baada ya kutinga hatua hii kwa kuibamiza timu ya taifa ya Mexico kwa magoli 7 – 0. Timu hiyo inayoongozwa na nyota wake Alexis Sanchez na Arturo Vidal mwaka jana ilichukua kombe hilo baada ya kuwafunga timu ya taifa ya Argentina kwa mikwaju ya penati baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 za mchezo.
Hivyo basi mashabiki wa soka ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla ambao kwa mara ya kwanza wamepata fursa ya kujionea michezo yote moja kwa moja kupitia chaneli za Sports Focus na World Football za StarTimes wanatarajia kushuhudia aidha fainali ya mwaka jana inajirudia au Colombia kufanikiwa kufikia hatua hiyo.
Wateja wa StarTimes Tanzania mbali na kufurahia mechi hizo pia wanazo fursa kabambe za kushiriki kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni na kushinda zawadi kupitia kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook na instagram.
Wateja wanaombwa kushiriki kampeni za ‘tabiri na ushinde’ pamoja na hash tag ya #CopaAmericaonStarTimes ambazo wanaweza kujishindia fedha taslimu, tiketi ya ndege kwenda Ujerumani kushuhudia ligi ya Bundesliga msimu ujao pamoja na simu za mkononi za kisasa.
Wateja wa StarTimes wanashinda kila siku kutokana kufuatilia kwa makani kampeni hizo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii, lakini ile zawadi kubwa itatangazwa baada ya mashindano kuisha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukabidhi Ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kesho.

index 
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakabidhi Ripoti ya Uchaguzi mkuu uliofanyika October 2015 kwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Mhe.John Pombe Magufuli kesho tarehe 23 Juni, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw.Ramadhani Kailima kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.
Ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mwaka 2015 itafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo Tume imepewa majukumu ya kuendesha Uchaguzi wa Rais na wabunge  katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uchaguzi wa Madiwani kwa upande wa Tanzania bara.
Kukamilika kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakamilisha mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuashiria kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment