Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
maalum za SMZ Haji Omar Kheir akizungumza na waandishi wa habari juu ya
kuanzishwa Mamlaka za Serikali za Mitaa Zanzibar katika Ukumbi wa Wizara
ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Kikwajuni.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Haji Omar Kheir alipokuwa akitangaza kuanzishwa Mamlaka za Serikali za Mitaa Zanzibar.
——————————————————————————–
Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
Maalum za SMZ Haji Omar Kheir ametangaza rasmi kuanzishwa Mamlaka
za Serikali za Mitaa na kuwateua Madiwani 56 kwa mujibu wa sheria Namba
7 ya mwaka 2014.
Akitangaza
Mamlaka hizo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na
Michezo, Waziri Haji Omar Kheir alisema lengo la kuanzishwa Mamlaka
hizo ni kuimarisha misingi ya Utawala bora Zanzibar.
Alisema
katika Mkoa wa Mjini Magharibi kutakuwa na Mabaraza matatu ya
Manispaa ambayo ni Baraza la Manispaa la Mjini, Baraza la Manispaa la
Magharibi ‘A’ na Baraza la Manispaa la Magharibi ‘B’.
Katika
Mkoa Kaskazini Unguja kutakuwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini
‘A’ na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Wakati Mkoa wa Kusini
Unguja kutakuwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kati na Halmashauri ya
Wilaya ya Kusini.
Alisema
Pemba kutakuwa na Baraza la Mji Mkoani na Baraza la Mji Chake chake
kwa Mkoa wa Kusini na Mkoa wa Kaskazini kutakuwa na Baraza la Mji Wete
na Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni.
Aidhaa
Waziri Kheir amefuta baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
zilizokuwepo awali ambazo ni Halmashauri ya Wilaya Magharibi,
Halmashauri ya Wilaya ya Wete, Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani na
Halmashasuri ya Chake chake.
Amesema
hatua ya kuunda Mabaraza zaidi ya moja ndani ya Mkoa wa Mjini
Magharibi ni moja ya maandalizi ya Serikali ya kuanzisha Jiji la
Zanzibar katika siku za baadae.
Aliwataka
wananchi kuendelea kupata huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
kwa kushiriki kikamilifu katika vyombo vya maamuzi kwa lengo la kukuza
ustawi wa Zanzibar.
Wakati
huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa
na Idara maalum za SMZ ametangaza majina ya Madiwani 56 aliowateua
kuungana na Madiwani waliochaguliwa na wananchi kuzitumikia Mamlaka
hizo.
Kwa mujibu wa uteuzi huo madiwani 36 ni wanawake ambao ni sawa na asilimia 64 na madiwani 20 ni wanaume.
Ameyaagiza
Mabaraza yote kuwaapisha madiwani kuyatumika mabaraza yao na kuandaa
taratibu za uchaguzi na kufanya uchaguzi wa viongozi kwa Mabaraza ya
Miji na Halmsahauri kabla ya tarehe 20 Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment