Baadhi ya wadau wa Kiswahli wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Samwel W. Shelukindo,Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, aliyevalia suti na shati jeupe.

Na Mwandishi Wetu,Paris
UBALOZI wa Tanzania mjini Paris kwa kushirikiana na Chama cha Watanzania wa Ufaransa (CCWU), wamewakutanisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vinavyofundisha lugha ya Kiswahili katika jiji la Paris kwa ajili ya maandalizi ya kusherehekea siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani ( World Kiswahili Language Day) ambayo itasheherekewa rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka.
Kwa mara ya kwanza lugha ya Kiswahili imeingia katika lugha za kimataifa sambamba na Kingereza, Kifaransa, Kireno, Kiarabu, Kichina, Kirusi ambazo zinazotambulika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Ubalozi na kuhudhuriwa na wanafunzi wanaosoma Kiswahili katika jiji la Paris kutoka katika vyuo vikuu vya Inalco, Chuo cha Sayansi ya Siasa (Political Science), Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ufaransa na wanafunzi wa Kituo cha Lugha na Utamaduni Tanzania (CCLT).
Akifungua mkutano, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel W. Shelukindo aliwaeleza washiriki kuwa Kiswahili kimeendelea kukua kwa kasi hadi kutambulikana kimataifa, ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na UNESCO, Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Aliwatia moyo kujifunza zaidi na pia kuwakaribisha kutembelea Tanzania.Aidha Wadau hao wa Kiswahili walifurahia sana kuweza kusheherekea hafla hiyo iliyopewa jina la Jioni ya Kiswahili na kuahidi kutembelea Tanzania kuendelea kujifunza mila na desturi za Kiswahili.
No comments:
Post a Comment