Pages

Sunday, April 3, 2022

NIC Yatoa Zawadi Kwa Washindi Wa Kilomita 21 Bima Marathon

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule akimpongeza mshindi wa kwanza wa kilomita 21 wa Bima Marathon  Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule akimpongeza mshindi wa kwanza wa kilomita 21 upande wa wanawake  wa Bima Marathon  Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
 *Yaahidi kujenga uchumi ni pamoja na kujenga uchumi wa afya


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 

Shirika la Bima la Taifa NIC limedhamini mbio za Bima Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam, ambapo NIC iliweza kutoa zawadi kwa washindi wa mbio za Kilomita 21 kwa

wanawake na wanaume wa kwanza hadi watano.

Aidha kupitia mbio hizo NIC wametoa elimu ya bima kwa kueleza umuhimu wa kuwa na Bima kama NIC ili kuweza kujilinda na majanga ya moto na maafa mengine ya mali.

Akizungumza katika mbio Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC)Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa ushiriki umekuwa wa kuvutia kwani washiriki wameweza kujiunga na mbio hizo wakitoka katika maeneo mbalimbali .

Amesema kuwa mshindi wa pili wa Kilomita 21 ametokea Zanzibar inaonyesha vipaji vipo kila kona.

Mwakifulefule amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi hasa ya mbio kwani yanasaidia kuuweka mwili vizuri na kujiepusha na magonjwa yasioambukiza ambayo yanatokana na usugu wa mwili wa kutofanya mazoezi.

No comments:

Post a Comment