Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAFANYABIASHARA nchini wameshauriwa kujenga utamaduni wa kusajili Alama za biashara zao pamoja na huduma ili ziweze kujulikana kwa urahisi.
Kwa mujibu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni kwamba wafanyabiashara wengi wamekuwa wakisajili majina ya biashara na Kampuni pamoja na huduma nyingine lakini wamekosa elimu inayohusu kutambua umuhimu wa Alama za biashara( Nembo au Logo).
Akizungumza na Michuzi Blog kwenye Kampeni ya Utoaji huduma na Elimu kwa Wananchi wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mliman City ,Msajili Msaidizi BRELA Vyonne Masele amesema mbali ya kutoa huduma wameamua kutoa elimu kuhusu umuhimu wa mfanyabishara kusajili Alama ya biashara kwani kuna faida nyingi.
Katika Kampeni hiyo ya utoaji elimu katika Viwanja hivyo BRELA inakwenda sambamba na kauli mbiu ya "Kamilika 2022" wakiwa na maana ya kwamba wafanyabiashara kuhakikisha kupitia Wakala huo wanakuwa wamekamilika katika shughuli zao kama kusajili jina la biashara, kusajili Kampuni, kurasimisha biashara,kusajili Alama ya biashara na pamoja na kukamilisha nyaraka zote muhimu.
Kuhusu kusajili Alama za Alama za biashara, Vyonne Masele amesema Wananchi wengi ambao wamefika katika Viwanja hivyo wamekuwa wakisajili majina ya biashara na wengine wanasajili Kampuni,hivyo moja ya elimu wanayoitoa ni kuhusu faida za kusajili Alama za Biashara ambazo zenyewe zinafanyiwa usajili wake tofauti na kusajili jina la biashara.
"Wengi wanaokuja BRELA wamekuwa wakisajili jina tu la biashara badala ya kusajili vyote pamoja na hii inatokana na kutokuwa na uelewa kuhusu kusajili Alama za biashara ( Logo).Kusajii Alama kuna faida nyingi ukiwemo ya kufanya kutambulika,kwa mfano Azam ukiona tu Alama unajua bidhaa husika inazalishwa hapo.
" Pia alama ya biashara inamwakilisha mteja kwenye biashara yake, inaonyesha utofauti wa kipekee kati ya biashara moja na nyingine na kwa wanaojua umuhimu wa Alama ya biashara wamekuwa wakisajili haraka ,hivyo tunatoa elimu kwa Wananchi...
"Na bahati nzuri tukiwaeleza wanatuelewa, hivyo tutaendelea kuwaelimisha,"amesema Maselle alipokuwa kwenye viwanja vya Mliman City ambako BRELA wamekuwa wakitoa huduma kuanzia Januari 26 hadi Januari 30 na baadae wakaongeza siku tatu baada ya wingi wa watu waliokuwa wakihitaji kuhudumiwa.
Katika kueleza zaidi Alama ya biashara,amesema ni Ile alama ambayo mfanyabiashara anaibuni kwa ajili ya kuwakilisha biashara yake, hivyo ametumia nafasi kuwahamasisha Wananchi kuhakikisha wajenge utamaduni wa kusajili alama za biashara zao ni muhimu kama ilivyo kusajili jina la biashara au kusajili Kampuni.
“Tunawakaribisha kusajili alama za biashara na huduma kwa kuwa faida zake ni kujulikana kisheria, mmiliki anaweza kuuza kwa mtu mwingine ili aweze kuitumia, ama kukodisha kwa mtu akaitumia kwa muda, Pia inawezesha kupata zabuni serikalini kwa sababu inajulikana kisheria,” amesisitiza Masele.
sema.
Kuhusu siku tatu ambazo zimeongezwa baada ya kumalizika siku tano,amesema kumekuwepo na mwamko mkubwa na watu wengi wamejitokeza kupata huduma, na hata baada ya siku tatu kuongezwa watu wameendelea kujitokeza kwa wingi na hiyo inatokana na eneo hilo liko katika mzunguko mkubwa wa watu ambao wanakwenda kupata mahitaji mbalimbali Mliman City.
No comments:
Post a Comment